Pia katika utaifiti huu wanawake waliambiwa waaandike kiwango cha chai ya kijani (green tea) au chai ya tiba (herbal tea) wanayokunywa kwa siku na hakuna uhusiano wowote ulionekana kati ya chai ya kijani au chai ya tiba na kuongeza uwezo wa kushika mimba kwa mwanamke.
Tafiti zaidi zinahitajika ili kuweza kujua kama chai ya kijani husaidia wanawake kupata ujauzito au la.
Ufuatiliaji zaidi utaweza kujua afya na saizi ya watoto wataokaozaliwa na kina mama hawa wanaokunywa chai vikombe viwili kwa siku na kama hawa wanawake waliweza kubeba mimba hizo kwa muda mrefu/mfupi au kama mimba hizo ziliharibika.
Maha Ragunath, bingwa wa tiba ya uzazi katika kituo cha care fertility center cha Nottingham amesema “Kuna virutubisho maalum kwenye chai vinavyosaidia katika utungaji mimba. Chai huwa na kemikali nyingi aina ya anti-oxidants ambazo ni nzuri kwa uzazi kwa wanaume na wanawake lakini nadhani kwa wanawake wanaohitaji mtoto ni vizuri kunywa chai kwa kiwango cha wastani”.
Laurence Shaw mkurugenzi katika kituo cha uzazi cha Bridge Fertility Centre jijini London amesema “Wanawake walio na umri zaidi ya miaka 35 wanaojaribu kushika mimba ni bora watafute ushauri kutoka kwa madaktari na si kunywa vikombe 10 vya chai eti kwa sababu wanataka mtoto”.
Ni bora tusubiri matokeo zaidi ya wanawake ambao wamepata ujauzito wakati wa utafiti huu ili tupate majibu ya uhakika kuhusu maendeleo yao baada ya kushika ujauzito huo.