Pakua TanzMED App?

Bima kwa Ujumla

Bima ni mfumo wa kumwahidi kumrejeshea mwanachama hali ya afya, kipato, maisha na ustawi pindi anapopata janga au anapopoteza kitu chake cha thamani hasa ikiwa amelipia michango ya marejesho (premiums).

Bima hulenga kumkinga mwanachama dhidi ya janga lisilotegemewa, kwa mfano kinga dhidi ya Ajali, Kulazwa Hospitalini, Moto, Mafuriko, Wizi, nk. Aghalabu, matukio hayo yasipokingwa, hurudisha nyuma maendeleo ya mtu au familia nzima.

Kwa kawaida kuna aina mbili za mfumo wa Bima

 • Huduma za Bima zilizo Rasmi – (Formal) kama Bima ya Afya, Bima ya Majengo, Bima ya Gari, Bima ya Maisha
 • Bima zisizo rasmi – kama Bima za Mazishi, Bima za makundi ya kuweka na kukopa, Bima ya Mfuko wa Afya ya Jamii n.k.

Tunavyofahamu

Tofauti na nchi nyingine za Afrika Mashariki kama Rwanda na Kenya, Watanzania wengi hawana huduma ya bima na wengi hawafahamu faida za kuwa na utaratibu wa bima. Wengi hawana huduma yoyote ya bima (92%) na huku asilimia ya Bima Rasmi ikiwa 6.4% na isiyo rasmi ikiwa asilimia 1.9% . (1) (FSDT/Finscope Survey 2009)

Pia, utafiti uliofanywa mwaka 2009 na The First Microinsurance Agency Limited iliyopo Dar es Salaam ikiwahusisha watu 600 na ikifanywa na kundi la Steadman ulionesha kuwa walio wengi wanapendelea sana kuwa na Bima ya Afya. Hii inafuatiwa na Bima ya Elimu na Bima ya Maisha. (2) (Market Research on the Demand for Health and Life Insurance in Tanzania. Steadman Group, 2008).

Mifumo iliyopo nchini

Kwa sasa, Bima zilizopo nchini Tanzania ni zifuatazo:

 • Bima za Afya
 • Bima za Ajali
 • Bima za Mali
 • Bima za Ajali
 • Bima za Majengo

Bima ya Afya

Kinga kulipia gharama za matibabu

 • Bima ya Kulipia Kulazwa tu (Inpatient-only Insurance Cover)
 • Bima ya Kulipia Kulazwa na Magonjwa yasiyo ya Kulazwa (Outpatient & Inpatient Cover)
 • Bima ya Kulipia Magonjwa yasiyo ya Kulazwa tu (Outpatient Cover)
 • Bima ya Kulipia gharama za Vipimo tu
 • Bima inayomlipa mgonjwa pesa taslimu

Mlengwa hupataje Bima?(Mchakato wa Kujiunga)

Mara nyingi Bima hutolewa kwa kikundi kizima (mfano: wafanyakazi wote wa kampuni fulani, au wanafunzi wote) ili kuepusha uwezekano wa kuwapa Bima wale tu ambao wana uwezekano wa kuugua au kuathirika na janga linalokingwa. Kiutaalamu hii huitwa Anti-Selection.

Kunakuwa na mipango inayofanywa na maafisa wa kampuni ya Bima ya Afya na Uongozi wa Kikundi kama vile

 • Kujadili Mafao, Kusainiana mikataba
 • Kuwafahamisha na kuwafundisha wafanyakazi au wana-kikundi
 • Kulipia na Kushughulikia madai pindi yanapotokea.

Mambo muhimu

Kila Bima inakuwa na mambo muhimu ambayo inayaondoa katika malipo. Kwa mfano, Bima inaweza kusema kuwa mgonjwa atakayelazwa hospitali na kuzidi kiasi fulani, hatalipiwa tena, au magonjwa kadhaa hayatalipiwa. Hii inatokana na makubaliano yaliyofikiwa mwanzo kati ya kampuni/kikundi walimo na kampuni ya Bima.

Mapya katika Bima Tanzania

Mifumo mipya ya Bima

 • Bima ya Mazao mashambani
 • Bima ya Mazao Ghalani
 • Bima ya Simu za Mkononi – kukinga simu ikiibiwa au kupotea
 • Bima za Mifugo

Kulipia Bima Kwa njia ya simu

Mobile Money Transfer

Asilimia kubwa ya familia nchini Tanzania zinamiliki simu ya mkononi. Kwa hivyo, makampuni mengi ya Bima yanaandaa mipango ya kuanzisha huduma ya kupokea michango moja kwa moja kutoka kwa wanachama wake bila na kupunguza ucheleweshwaji wa malipo hayo, au hata upotevu wake na gharama za kiuendeshaji kwenye vikundi vyao.

Claims Payment

Pia, kuna uwezekano mkubwa wa kufanya malipo ya madai ya Bima kupitia mfumo huu

Mobile Banking

Vilevile, simu za mkononi zitaweza kufanywa benkindogo, kwa maana kuwa, mwenye simu ya mkononi anaweza kufungua akaunti ya akiba, na hivyo kurahisisha kuweka akiba na kuzitumia mahali na kipindi zinapohitajika.

Microinsurance: Bima kwa wenye kipato Kidogo

CGAP Consultative Group to Assist the Poor www.cgap.org inapendekeza kuwa kwa watu wenye kipato kidogo wanatakiwa wapate huduma za Bima zenye mfumo mbadala:

Bima maalum (Microinsurance)

 • Iwe Bima kwa wengi / wote
 • Bima iliyo rahisi kujiunga na kuendesha, iliyo nafuu (yenye michango wanayoweza kumudu).
 • Bima inayotolewa kulingana na mazingira waliyomo
 • Madai yalipwe haraka
 • Watu wapewe mafunzo ili kuelewa bima, nini wanalipia, wanapata faida gani na utaratibu wa kufuata pindi madai yanapotokea.

Ingawa Watanzania walio wengi (iwe mijini au vijijini), hawana huduma za bima, lakini walio na kipato kidogo hutaabika zaidi pindi linapotokea janga linalotingisha familia kiuchumi.

Aghlabu, hawa ni watu wenye kipato kisicho cha uhakika, wana uwezo mdogo wa kujiwekea akiba na pengine kuna ukosefu wa huduma za mikopo kwa majanga ya dharura, watu hawa hutumbukia katika mtego mkubwa.

Majanga huzifanya familia zenye kipato kidogo kutumia akiba yao yote, kuuza mali au mashamba yao, kukopa kwa marafiki, au hata kukopa mahali ambapo wanatozwa riba kubwa sana.

Changamoto katika kutoa huduma ya Bima Tanzania

 • Uelewa mdogo na uhaba wa elimu juu ya Bima kwa walenga – hivyo wanashindwa kupanga kwa ajili ya baadaye.
 • Uhaba wa Masoko Mapya (hasa kama ni Bima za Makundi)
 • Mfumo mgumu wa kutolea maamuzi – mfano, maamuzi ya kukinga kikundi chote hutegemea mikutano mikuu ya kikundi, ambayo inaweza kusubiri kipindi kirefu, na baadae ndio mazungumzo ya ziada hufuata.
 • Kutokuwa na Njia nyepesi ya Kukusanya Michango ya Marejesho na kulipa Madai
 • Kwa Bima Ndogo (microinsurance), kukosekana kwa uzoefu na takwimu au taarifa za kutosha maana ni mifumo mipya ambayo haijawahi kujaribiwa kokote.
 • Mfumo wa kutoamini Bima inaweza kusaidia, na pengine kutokuwa na imani na makampuni ya Bima ambayo
 • Uthibiti – kukosekana kwa utashi wa kisiasa au hata sheria mwongozo wa Sera kuhusiana na bima kadhaa
Imesomwa mara 6359 Imehaririwa Jumatano, 17 Oktoba 2018 16:18
Facebook Google Plus Twitter LinkedIn
No Internet Connection