Makala hii iliandikwa na Dada Subi wa tovuti ya wavuti.com akizungumzia kuhusu umuhimu wa kufanyika kwa utafiti juu ya dhana ya kuwepo kwa uwezo wa mafuta ya nazi katika kutibu na kuzuia ugonjwa wa kusahau wa Alzheimer's unaowaathiri zaidi wazee. Ungana naye katika maoni yake haya.
Baadhi ya watafiti wanasema kiwango fulani cha mafuta ya nazi ni muhimu kwenye chakula kwa kuwa husaidia kupunguza ugonjwa wa kusahau "Alzheimer's" ambao mara nyingi humjia mwanadamu kadiri umri unavyosogelea uzeeni.
Watafiti wanathubutu kusema, huenda mafuta haya ya nazi yakazuia kabisa kupata ugonjwa huo kwa baadhi ya watu.
Ingekuwa vyema na sisi Tanzania tukafanya utafiti kwa jamii ya watu wanaotumia kwa wingi mafuta ya nazi katika mapishi yao, hasa wale waishio mikoa ya mwambao wa pwani ambapo zao ma mnazi hustawi vizuri na kwa wingi.
Pengine hii ikawa pia sababu kujibu suala la kwa nini yapo matukio mengi ya Wazee na Vikongwe wengi kuuawa kikatili katika mikoa kadhaa nchini Tanzania ambayo zao la nazi ni nadra kuonekana sokoni, achilia mbali kutumika kama kiungo katika mapishi na/au matumizi ya kuchua na marashi.
Nimewaza hivyo kwa kuwa wazee wetu wanaouawa mara nyingi utetezi unaotolewa na wauaji ni kuwa mzee alikuwa na "dalili" za uchawi kwa kuwa pengine alikuwa akisema mwenyewe kama mwehu, akiondoka usiku na kutokomea pasikojulikana, alikuwa akivua nguo mbele ya kadamnasi, alikuwa mwoga au kuonekana mwenye wasiwasi wakati wote n.k., bila watu hao kufahamu kuwa kwa ujinga* wa masuala ya afya ya akili ya binadamu yatokanayo na umri, matukio mbalimbali maishani yaliyoathiri akili na fikira, pamoja na hofu ya uzee kwa vitendo walivyotendewa wengine, wanaweza kabisa kuwa sababu ya matatizo (dalili) na kuishia kuwawahukumu baadhi ya wazee hao kifo pasina hukumu ya haki. Ninaamini kuwa, kama ambavyo wapo waliofungwa jela kwa makosa ya kudhaniwa, kusingiziwa, wasiyoyatenda na visasi, vile vile wapo wanaouawa kwa sababu zizo hizo.
Niseme kuwa, zinazotajwa kuwa sababu (naita visingizio) za kumtuhumu mtu uchawi zinalandana na dalili za ugonjwa wa kusahau "Alzheimer's disease" ambazo niliwahi kuziandika wakati nikichangia makala za afya katika gazeti la KwanzaJamii (unaweza kuzisoma kwa lugha ya Kiingereza katika linki hii: alz.org).
Makala hii ni kwa hisani ya wavuti.com
Polio ni ugonjwa wa kuambukiza usababishwao na virusi, huathiri neva na kusababisha ulemavu.
Kutokana na taarifa za shirika la afya duniani:
- Polio huathiri zaidi watoto wa umri wa chini ya miaka mitano
- Ulemavu hutokea kwa mmoja kati ya maambukizi 200
- Mpaka 2013 ni nchi tatu ambazo bado kuna mlipuko wa ugonjwa huu wa kupooza Afghanistan, Pakistan na Nigeria. Ila kutokana na Taarifa kutoka wizara ya afya ya Tanzania ilipokea taarifa kutoka shirika la afya duniani kuwa kuna mlipuko katika nji jirani ya Kenya, wilaya ya Fafi.
Je ni zipi dalili za ugonjwa huu?
Dalili hizi hudumu kwa kati ya siku 1 hadi 10
- Homa
- Maumivu ya kichwa
- Kutapika
- Uchovu
- Maumivu ya shingo
- Maumivu ya mgongo
- Maumivu ya mikono na miguu
- Misuli kukakamaa
Je ni matatizo gani mtu huweza kupata baada ya maambukizi haya?
- Kupooza misuli
- Ulemavu wa miguu
Kati ya maambukizi yanayowasumbua wanawake wengi duniani ni maambukizi ya fangasi. Inakisiwa asilimia 75 ya wanawake wote duniani hupata maambukizi haya katika kipindi cha uhai wao.
Maambukizi ya fangasi katika sehemu za siri za mwanamke husababishwa na uwepo wa fangasi wanaojulikana kitaalamu kama Candida albicans. Maambukizi haya pia hujulikana kama yeast infection au thrush. Fangasi hupatikana kama vimelea vya kawaida katika mdomo, mpira wa kupitisha chakula sehemu inayojulikana kama pharynx, katika kibofu cha mkojo, uume na hata kwenye uke.
Mfumo mzuri wa kinga wa mwili pamoja aina fulani za bakteria wanaoishi pamoja na fangasi hawa husaidia sana katika kuthibiti maambukizi yanayoyosababishwa na aina hi ya fangasi.
Nini hutokea?
Kwa kawaida, Candida albicans huishi kwenye uke na sehemu nyingine (kama zilivyoelezewa hapo juu) bila kusababisha madhara yoyote yale isipokuwa pale mazingira ya eneo husika yanapobadilika kama vile mabadiliko katika hali ya pH ya eneo husika (ifahamike ya kwamba pH ya kawaida ndani ya uke ni 4.0 - 4.5) au uwiano wake na vimelea (microorganisms) wengine unapoharibiwa kutokana na sababu mbalimbali kama vile matumizi ya madawa aina ya antibiotics, kupungua kwa kinga mwilini kutokana na magonjwa mbalimbali n.k.
Maambukizi haya ya fangasi yanaweza kugawanywa katika sehemu kuu mbili
- Maambukizi yasiyo makali yaani uncomplicated thrush: Katika kundi hili, mgonjwa hupatwa na maambukizi mara moja hadi nne kwa mwaka na dalili zake huwa si mbaya sana na maambukizi haya husababishwa na fangasi wa jamii hii ya Candida albicans.
- Maambukizi makali yaani complicated thrush: Katika kundi hili, mgonjwa hupatwa na maambukizi zaidi ya mara nne kwa mwaka, dalili zake kuwa mbaya zaidi au kama maambukizi yatakuwa yametokea kipindi cha ujauzito, ugonjwa wa kisukari, upungufu wa kinga mwilini. Aina hii kusababishwa na vimelea vya aina nyingine tofauti na Candida albicans.
Vihatarishi
Watu walio katika hatari ya kupata maambukizi ya fangasi hawa ni wale wenye
Ugumba ni hali inayotokea iwapo watu wawili, mwanaume na mwanamke wanapokutana kimwili (au kujamiana) bila kutumia njia yoyote ile ya upangaji uzazi kwa muda wa miezi 12 na kutoweza kushika mimba au kupata ujauzito.
Aina za Ugumba
Ugumba wa asili (Primary infertility) - Hii ni pale ambapo mwanaume na mwanamke hawajawahi kutunguisha mimba kabisa maishani mwao hata baada ya kujamiana au kukutana kimwili kwa muda wa mwaka mmoja bila kutumia njia yoyote ile ya kuzuia kupata mimba.
Ugumba unaotokea baadaye maishani (Secondary infertility) - Hii ni pale ambapo wote wawili, mwanamke na mwanaume wameshawahi kupata ujauzito au kutungisha mimba angalau mara moja maishani mwao na baada ya hapo hawajafanikiwa kupata au kutungisha mimba tena.
Asilimia 30-40 ya tatizo la ugumba huwakumba wanaume na asilimia 40-50 ya tatizo hili huwakumba wanawake, wakati asilimia 10-30 zilizobakia ya tatizo hili husababishwa kwa pamoja na matatizo kati ya wanaume na wanawake, hapa sababu halisi hazijulikani.
Kwa wale wenye afya njema, uwezekano wa kupata au kutungisha mimba iwapo watajamiana mara kwa mara kwa mwezi ni asilimia 25-30. Wanawake hufikia kilele cha kupata ujauzito (peak fertility) wakiwa kwenye miaka ya ishirini. Mwanamke aliye na umri wa zaidi ya miaka 35 (au baada ya miaka 40) ana uwezekano wa kupata ujauzito kwa asilimia 10.
Je mimba hutungwa vipi?
Mimba hutungwa baada ya mwanamke kutoa yai kutoka katika moja ya viwanda vyake vya mayai ya kike yaani ovaries, kitendo hiki hujulikana kama ovulation. Yai husafiri hadi kwenye mfuko wa uzazi ujulikanao kama uterus (womb) kupitia kwenye mirija ya uzazi inayojulikana kama mirija ya fallopian.
Mbegu moja ya kiume (sperm) ni lazima itungishe au iungane (fertilize) na yai au mayai ya kike (ovum au ova) wakati yai likielekea kwenye uterus. Baada ya mbegu ya kiume na yai la kike kuungana, muunganiko uliotengenezwa yaani kiinitete (embryo) hushuka mpaka kwenye mfuko wa uzazi na kujiwekeza hapo ili kiendelee kuwa kiumbe.
Muundo ya moyo na mishipa ya damu ni mojawapo ya vinavyooathirika katika magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo. Vijusi(fetuses) kati ya 8 hadi 10 huathirika kwa kila 1000.
Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo huweza kutoa dalili mara tu baada ya kuzaliwa, utotoni na wakati mwingine husubiri mpaka ukubwani.
Magonjwa ya Moyo ya Kuzaliwa husababishwa na nini?
Kwa wengi sababu huwa haijulikani. Ila huwa kuna vitu hatarishi ambavyo hupelekea kuongezeka kwa uwezekano wa kupata magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo, vitu hivyo hatarishi ni:
- Matatizo ya kijenetekia utotoni kama Downs syndrome, Turner’s syndrome, Marfan syndrome,
- Matumizi ya dawa ya kutibu chunusi (acne) aina ya retinoic acid, madawa ya kulevya na unywaji wa pombe wakati wa ujauzito
- Maambukizi ya virusi vya Rubella (German measles) kipindi cha kwanza cha ujauzito (1st trimester)
Kuna aina mbili za magonjwa ya moyo ya kuzaliwa
- Cyanotic
- Non-cyanotic
Cyanosis ni hali ya kuwa na rangi ya samawati (katika midomo,ulimi, ganja za mikono na miguuni) kutokana na kukosa oksijeni ya kutosha mwilini.
Cyanotic
Magonjwa ya moyo ya asili ambayo yanaangukia katika kundi hili ni pamoja na
- Tetralogy of fallots
- Transposition of great vessels
- Tricuspid atresia
- Total anomalous pulmonary venous return
- Truncus arteriousus
- Hypoplastic left heart
- Pulmonary atresia
- Ebstein anomaly
Non-cyanotic
Magonjwa ya moyo ya asili yaliyo kwenye kundi hili hujumuisha
- Ventricular septal defect (tundu katika kuta za ventrikali)
- Atrial septal defect (tundu katika kuta za atria)
- Patents ductus arteriousus
- Aortic stenosis
- Pulmonic stenosis
- Coarctation of the aorta
- Atrioventricular canal (endocardial cushion defect)
Dalili za Magonjwa ya Moyo ya Kuzaliwa
Kwa ujumla, wagonjwa wa moyo wa asili huwa na dalili zifuatazo
- Kupumua kwa shida
- Kushindwa kula vizuri
- Matatizo ya ukuaji
- Matatizo ya ukuaji wa misuli ya mikono na miguu
- Maambukizi ya mfumo wa hewa
- Cyanosis kwa aina ya kwanza(rangi ya samawati katika midomo,ulimi, viganja vya mikono na miguuni)
- Ongezeko la sauti ya ziada katika sauti za moyo kutokana na tatizo (heart murmur)
- Mabadiliko kwenye kucha hasa za vidole vya mikononi (digital clubbing)
Vipimo na Uchunguzi
Baadhi ya vipimo vinavyotumika kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa haya ni
- Echocardiogram/transesophageal echocardiogram
- Cardiac catheterization
- Magnetic Resonance Imaging
- Electrocardiogram
- Chest x-ray
Matibabu
Matibabu hutegemea aina ya ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa nao, hivyo hapa nitaelezea kwa kifupi ila, maelezo zaidi nitatoa katika makala zinazokuja za ugonjwa mmoja mmoja.
Aina nyingi za magonjwa haya huwa na madhara makubwa hivyo huhitaji upasuaji kurekebisha kasoro hizo, pamoja na matibabu ya dawa (diuretics ambazo husaidia kupunguza maji na chumvi mwilini, digoxin ambayo husaidia kuongeza nguvu katika mapigo ya moyo).
Vilevile kuna tiba nyengine ambayo badala ya upasuaji kitaalamu Transcatheter ambapo kifaa cha kufunga au kupachika huwekwa kwenye catheter maalumu ambayo hupita kwenye mishipa ya damu mpaka kwenye kasoro na kurekebisha kwa kuziba tundu nakadhalika.
Kuna aina mbili kuu za hiatus hernia
- Sliding type : Kama jina lake linavyomaanisha, aina hii hutokea iwapo sehemu ya juu ya utumbo inaposukumwa juu na kuingia kwenye upenyo wa esophagus hiatus baada ya kutokea kwa ongezeko la presha katika maeneo ya tumbo (increased pressure in the abdominal cavity) na kurudi kama kawaida wakati presha inapopungua.
- Fixing type: Aina hii hutokea iwapo sehemu ya juu ya utumbo inapokuwa kwenye maeneo ya kifua na haishuki chini.
Vihatarishi vya Ugonjwa huu
- Kunyanyua vitu vizito au kuinama sana
- Kukohoa sana au kukohoa mara kwa mara kutokana na sababu mbalimbali
- Kutapika sana (violent vomiting)
- Kupiga chafya sana (Hard sneezing)
- Ujauzito -Kutokana na mfuko wa uzazi (uterus) kusukuma viungo kwenda juu kutokana na kuongezeka ukubwa wake.
- Wakati wa kujifungua- Kutokana na kuongezeka kwa presha ndani ya tumbo wakati mama anajitahidi kusukuma mtoto. Si wanawake wote wanaopata tatizo hili.
- Kujikamua wakati wa kwenda haja kubwa (straining during constipation)
- Uzito uliopitiliza -Kutokana na kuongezeka uzito ambao unasukuma viungo kwenye maeneo ya kifua kwenda chini na hivyo kuongeza presha tumboni.
- Kujisaidia haja kubwa wakati mtu amekaa - Kutokana na maendeleo ya binadamu, watu wengi sasa hivi wameanza utamaduni wa kutumia vyoo vya kukaa wakati wa kujisaidia haja kubwa, katika tafiti iliyofanywa na Dr Denis Burkitt (1), imeonekana ya kwamba kujisaidia wakati mtu amekaa hufanya mtu kujikamua zaidi na hivyo kuongeza presha ndani ya utumbo (Increased intraabdominal pressure) na hivyo kusukuma mfuko wa kuhifadhia chakula (utumbo) kupitia kwenye upenyo wa esophagus hiatus na hivyo kusababisha hiatus hernia.
Tatizo la kurithi (Heredity)
- Uvutaji sigara
- Matumizi ya madawa ya kulevya kama cocaine
- Kuwa na kiwambo hewa (diaghram) dhaifu
- Msongo wa mawazo (depression)
- Matatizo ya kuzaliwa (congenital defects).
Dalili na Viashiria
- Maumivu ya kifua
- Kichomi (pleurisy) ambacho kinakuwa kikali sana wakati wa kuinama au mtu anapolala chini
- Matatizo katika kumeza chakula
- Kupumua kwa shida Kutokana na hiatus hernia kupunguza uwezo wa ufanyaji kazi wa kiwambo hewa (diaphragm).
- Mapigo ya moyo kwenda kasi Kutokana na mkwaruzo wa neva inayojulikana kama vagus nerve.
Mara nyingi sana hiatus hernia haioneshi dalili zozote zile isipokuwa inapokuwa kubwa sana. Maumivu na kichomi hutokana na kurudishwa kwa tindikali ya kwenye tumbo (gastric acid) kwenye kifua. Pia tindikali aina ya bile acid na hewa huwa inasukumwa juu kwenye kifua.
Vipimo vya Uchunguzi
- Barium Swallow X-ray – X-ray ya kuangalia viungo vya ndani, mgonjwa hupewa au huchomwa sindano yenye dawa maalum ambayo huonekana vizuri kwenye X-ray, na baada ya hapo hupigwa picha za X-ray akiwa amekaa au amesimama. Kawaida kipimo hiki huchukua masaa 3-6.
- Esophagogastroduodenoscopy (OGD) - Mpira maalum wenye taa na camera kwa mbele unaoingizwa mdomoni kwenye mpira wa kupitisha chakula (esophagus) na hutazama kama kuna magonjwa yoyote kwenye esophagus hadi kwenye sehemu inayojulikana kama duodenum.
- Electrocardiography (ECG)- Kipimo cha kuangalia kama kuna matatizo katika jinsi moyo unavyopiga
- Chest X-ray- Kuangalia kama kuna magonjwa kama homa ya mapafu (Pneumonia), kama kuna pafu lolote ambalo halifanyi kazi, madhara kwenye moyo (injury to the heart) na pia kuangalia matatizo yoyote yale.
- Complete Blood Count- Kipimo cha kuangalia wingi wa damu, kuangalia aina mbalimbali za chembechembe za damu kama zipo katika maumbo yao ya kawaida, wingi wao kama ni wa kawaida.
Tiba ya Hiatus Hernia
- Dawa za kuyeyusha tindikali mwilini (antacids) hutumika kama Gelusil, Maalox nk.
- H2 receptor antagonist –Dawa zinazopunguza kiwango cha utolewaji wa tindikali kama cimetidine, ranitidine nk.
- Dawa ambazo huzuia utolewaji wa tindikali na kuponya tishu za esophagus (Proton Pump Inhibitors) dawa hizi ni omeprazole, lansoprazole nk.
Madhara ya Hiatus Hernia
- Kichomi
- Ugonjwa wa esophagitis
- Barretts esophagus
- Saratani ya kwenye mpira wa kupitisha chakula (esophageal cancer)
- Kuoza kwa meno (dental erosion)
- Strangulation of the stomach (kunyongwa kwa sehemu ya juu ya tumbo na hivyo kusababisha sehemu hii kukosa damu ya kutosha na hivyo tishu zake kufa na kuoza (ischemic and necrosis)
- Kuzuia pafu kujaa hewa na hivyo kushindwa kutanuka na kusababisha mtu kupumua kwa shida sana.
Jinsi ya kujikinga
- Kuacha kunywa pombe
- Kuacha matumizi ya madawa ya kulevya kama cocaine
- Kupunguza uzito uliopitiliza.
- Kula milo midogo mara nyingi kwa siku
- Epuka vyakula vinavyoongeza kichomi kama chocolate, vitunguu, vyakula vikali, vinywaji venye limau, ndimu nk.
- Kula chakula cha usiku masaa matatu kabla ya kwenda kulala
- Pumzika kwa kukaa baada ya kula usilale chini.
- Nyanyua sehemu unayoweka kichwa chako wakati wa kulala kwa angalau 15cm (6 inches)
- Punguza msongo wa mawazo
- Acha kuvuta sigara.
Marejeo
Hatari ya Kukakamaa kwa mwili huongezeka kwa mtu mwenye kiharusi au vihatarishi vya kiharusi kutokana na utafiti uliofanywa Rotterdam uholanzi.
Sehemu ya ubongo kitaalamu Cerebral cortex inapokandamizwa aidha na kihararusi cha mishipa kuchanika na kuvujisha damu au mishipa inapoziba husababisha Kukakamaa kwa mwili. Hali yoyote isababishayo upungufu wa damu kufika katika sehemu za ubongo hupelekea Kukakamaa kwa mwili kutokea, na moja wapo ya sababu hizo ni magonjwa ya moyo.
Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Marekani cha Boston umesema unywaji wa chai vikombe viwili kwa siku huongeza uwezekano wa mwanamke kupata ujauzito. Katika utafiti uliohusisha wanawake 3,600 umeonyesha ya kwamba wanawake wanaokunywa vikombe viwili vya chai kwa siku wana asilimia 27 ya kupata ujauzito ikilinganishwa na wanawake ambao hawanywi chai. Pia utafiti huo umeonyesha ya kwamba wanawake wanotumia vinywaji baridi viwili kwa siku kama coca cola, hupunguza uwezekano wao wa kushika mimba kwa asilimia 20 na haijalishi kama vinywaji hivyo vina sukari au la.
Mtafiti mkuu Profesa Elizabeth Hatch amesema alifanya utafiti huu ili kutaka kujua kama kuna uhusiano wowote wa kemikali aina ya caffeine inayopatikana kwenye chai, kahawa na uwezo wa kushika mimba kwa wanawake.Utafiti huu ulifanywa kwa kuwahusisha wanawake wa kutoka nchi ya Denmark kutokana na nchi hiyo kuwa na mfumo wa kuwapa raia wao namba za uraia wa kudumu wakati wa kuzaliwa na hivyo kuwa rahisi kwa Profesa Hatch kuwafuatilia kwa njia ya intaneti kwa muda wa mwaka mmoja.
Profesa Hatch amesema “Hatujui wanawake hawa walikuwa wakinywa chai ya aina gani, hatujui kama walikunywa chai bila kuongeza kitu chengine kwenye chai, kama waliongeza maziwa au limao kwenye chai, bali inaonekana kuna uhusiano wa caffeine na uwezo wa kushika mimba au uwezo huo umetokana na mfumo wa maisha wa wanawake hao au ni kutokana na virutubisho vya chai hiyo”.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wanaume wawili ambao walikuwa na maambukizi ya ugonjwa wa HIV huko nchini Marekani wameweza kuacha kabisa kutumia dawa za kurefusha maisha yaani ARV’S ambazo hupewa wagonjwa wa HIV baada ya kufanyiwa upandikizaji wa uboho (bone marrow transplant) katika mifupa yao.
Wanaume hao ambao walikuwa na ugonjwa wa HIV kwa miaka 30, walikuwa wakipewa tiba ya upandikizaji wa uboho kutokana kuugua saratani ya damu (Leukemia). Mmoja wa wanaume hao ameacha kutumia dawa hizo za kurefusha maisha miezi minne iliyopita na mwingine ameacha kuzitumia wiki saba zilizopita.
Wanasanyansi katika chuo kikuu cha Saskatchewan cha nchini Canada wamesema ya kwamba manii(semen) yanayotolewa na mwanamume wakati wa kujamiana na mwanamke yanasaidia mwanamke kuwa na uwezo wa kushika mimba. Kulingana na utafiti mpya uliofanywa na watafiti wa kimataifa chini ya Gregg Adams na kuchapishwa katika jarida la proceedings of the National Academy of Sciences, umesema ya kwamba manii sio tu hubeba shahawa (sperm) za mwanamume kwenda kwa mwanamke bali pia huchochea mayai ya mwanamke (ovaries) kutoa mayai ya uzazi.
Protini inayopatikana katika shahawa inayojulikana kama Ovulation-Inducing Factor au IFO, ndio hasa huchochea sehemu ya ubongo inayojulikana kama hypothalamus kwenye ubongo wa mwanamke kutoa homoni ambazo hupelekwa moja kwa moja kwenye mfumo wa neva na kisha homoni hizo hupelekwa kwenye mfumo mwingine wa homoni unaojulikana kama endocrine system.
Homoni hufika kwenye mfumo huu wa endocrine system kupitia sehemu ya ubongo inayojulikana kama pitituary gland na hivyo kuingia kwenye mzunguko wa damu.Baada ya kufika wenye mzunguko wa damu, homoni hizi huenda moja kwa moja mpaka kwenye mayai ya mwanamke (ovary) na kuyachochea mayai haya kutoa mayai ya uzazi(ovum) katika hatua inayojulikana kama ovulation.