Image

Kukakamaa kwa mwili kutokanako na magonjwa ya Moyo

Hatari ya Kukakamaa kwa mwili  huongezeka kwa mtu mwenye kiharusi  au vihatarishi vya kiharusi kutokana na utafiti uliofanywa Rotterdam uholanzi.

Sehemu ya ubongo kitaalamu Cerebral cortex inapokandamizwa  aidha na kihararusi cha mishipa kuchanika na kuvujisha damu au mishipa inapoziba husababisha Kukakamaa kwa mwili. Hali yoyote isababishayo upungufu wa damu kufika katika sehemu za ubongo hupelekea Kukakamaa kwa mwili  kutokea, na moja wapo ya sababu hizo ni magonjwa ya moyo.

 Je ni magonjwa gani ya moyo husababisha Kukakamaa kwa mwili ?

  • Shambulizi la moyo
  • Moyo kushindwa kufanya kazi vizuri
  • Shida ya misuli ya moyo
  • Magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo
  • Upasuaji wa moyo
  • Magonjwa ya valvu za moyo
  • Moyo kupiga bila mpangilio
  • Dawa za magonjwa ya moyo

Kwa watoto kunatatizo la mapigo ya moyo kupiga kupungua na saa nyingine kuongezeka kitaalamu Bradycardia tachycardia syndrome (sick sinus syndrome) hufananishwa na kifafa. Na kunatatizo jingine la moyo liitwalo kitaalamu Long QT syndrome ambalo husababisha Kukakamaa kwa mwili  , kupoteza fahamu na hata kufa ghafla.

Ni vitu gani vinaweza kuwa vihatarishi vya kupelekea Kukakamaa kwa mwili?

  • Shinikizo la damu
  • Kisukari
  • Kuvuta sigara
  • Cholesterol kuwa nyingi mwilini
  • Historia ya familia kuwa na magonjwa ya moyo na mishipa ya damu kuziba

Vipimo gani vinashauriwa kufanywa japo mara mbili kwa mwaka?

  • ECG
  • Kipimo cha kujua wingi wa cholesterol mwilini
  • Kipimo cha kisukari
  • EEG
Imesomwa mara 28567 Imehaririwa Alhamisi, 29 Novemba 2018 08:28
Dr.Mayala

Dr.Henry A Mayala ni daktari bingwa Wa Tiba ya moyo katika taasisi ya Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI), ambaye kwasasa anasomea shahada ya uzamivu (PhD) ya Tiba ya Moyo katika Chuo Kikuu cha Tongji  nchini China.

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

Makala shabihana