Kidokezo
Unapomaliza kuzipika kila moja, zitandaze kwanza chapati katika sahani (au sinia) kubwa zipate kupoa ziwe kavu ili zisinyonye mafuta. Kisha tena ziweke katika sahani yako ya kawaida.
Ni nzuri kutolea na jam au asali
Unaweza ku freeze chapati katika Freezer bags. Kunja chapati moja moja ziwe nusu. Zifunike na Wax paper, kisha zitie kwenye freezer bags na uzihifadhi katika freezer. Unapotaka kula, toa kwenye freezer na upashe moto katika Microwave. Unaweza kula kwa mbaazi za mchicha, mbaazi za nazi, maharage ya nazi au ya samli/mafuta, choroko za nazi, kunde za nazi, au mboga yoyote ile upendayo.
Mbaazi za Mchicha kwa Chapati
Vipimo
Mchicha uliokatwa katwa (chopped) 400 gm au vikombe 3
Mbaazi mbichi au kavu 1 kikopo au vikombe 2
Kitunguu Kimoja
Nyanya kopo ½ kijiko cha chai
Tui la nazi zito 1 kikombe
Chumvi Kiasi
Pilipili mbichi nzima 2
Namna ya Kutayarisha na Kupika
- Ikiwa mbaazi sio za tayari, loweka uchemshe hadi ziive.
- Osha vizuri mchicha kisha, katakata mdogo mdogo (chopped) au tumia ulio tayari wa barafu (frozen chopped spinach)
- Katika sufuria, tia mchicha pamoja na mbaazi zilizokwisha iva.
- Katakata kitunguu, utie humo, tia nyanya kopo, tia chumvi na pilipili mbichi nzima .
- Tia tui upike katika moto mdogo mdogo hadi zitokote na kuiva mchicha, usiache zikauke sana. Tayari kuliwa na chapati, maandazi au wali.
Mbaazi za Nazi
Vipimo
Mbaazi za kopo 2 au nusu kilo
Kitunguu 1
Chumvi Kiasi
Manjano (curry powder ) ½ Kijiko cha chai
Kidonge cha supu (curry cube) Kipande kidogo
Mafuta 1 Kijiko cha chai
Pilipili mbichi 2 Nzima
Nazi 3 ½ Vikombe
Namna ya Kutayarisha na Kupika
- Osha mbaazi kwenye chungio na ziache zitoke maji.
- Kaanga kitunguu kidogo tu kisha tia mbaazi na majano.
- Tia kidonge cha supu na chumvi pilipili mbichi na nazi
- vikombe vitatu, utabakisha nusu kikombe.
- Ikisha kauka kidogo changanya nazi ya unga kama
- Vijiko 4 vya supu kwenye nazi uliobakisha, mimina kwenye mbaazi
- Iache motoni kidogo hadi iwe nzito na itakuwa tayari kuliwa kwa maandazi au chapati.
Uji wa Kunde
Vipimo
Kunde Kavu 2 Vikombe
Tui 1 Kikombe
Sukari 1 Kikombe
Maji 7 Vikombe
Garam masala ½ Kijiko cha chai
Hiliki Kiasi
Karafuu 3-4 Chembe
Pilipili manga ½ Kijiko cha chai
Chumvi Kiasi
Namna ya Kutayarisha na Kupika
- Chemsha kunde kavu bila ya kuloweka kwa maji vikombe 4 na sukari kikombe kimoja kwa moto kiasi mpaka ziive
- Kisha mimina vitu vyote vilivyobakia pamoja na maji vikombe 3 vilivyobaki na acha ichemke taratibu mpaka maji yapunguke uji uwe mzito.
- Epua mimina kwenye bakuli na tayari kwa kuliwa.
Juisi ya Kuondoa Sumu Mwilini (Detoxifying Juice)
Vipimo
Majani ya Kale (kale leaves) 3
Brokoli pamoja na miche yake ½ msongo
Kabeji iliyokatwa pamoja na zizi lake ½
Nyasi majani (fennel) 1
Tufaha (apples) 2
Namna ya kutayarisha
- Katakata vitu vyote vipande weka katika bakuli
- Tia katika mashine ya kukamua juisi, washa mashine ikamue juisi.
- Mimina katika gilasi ikiwa tayari kunyiwa
Kidokezo
Juisi hii ni ya kuondosha athari za sumu (toxins) zinazokusanyika mwilini na kusababisha maradhi mbali mali. Kutumia kwake kila baada ya muda kunasaidia kusafisha damu na kumuhifadhi mtu na athari za sumu.
Shukrani kwa tovuti ya www.alhidaaya.com kwa makala hii.