Image

Shahawa Humuongezea Mwanamke Uwezo wa Kushika Mimba?

 Wanasanyansi katika chuo kikuu cha Saskatchewan cha nchini Canada wamesema ya kwamba manii(semen) yanayotolewa na mwanamume wakati wa kujamiana na mwanamke yanasaidia mwanamke kuwa na uwezo wa kushika mimba. Kulingana na utafiti mpya uliofanywa na watafiti wa kimataifa chini ya Gregg Adams na kuchapishwa katika jarida la proceedings of the National Academy of Sciences, umesema ya kwamba manii sio tu hubeba shahawa (sperm) za mwanamume kwenda kwa mwanamke bali pia huchochea mayai ya mwanamke (ovaries) kutoa mayai ya uzazi.

Protini inayopatikana katika shahawa inayojulikana kama Ovulation-Inducing Factor au IFO, ndio hasa huchochea sehemu ya ubongo inayojulikana kama hypothalamus kwenye ubongo wa mwanamke kutoa homoni ambazo hupelekwa moja kwa moja kwenye mfumo wa neva na kisha homoni hizo hupelekwa kwenye mfumo mwingine wa homoni unaojulikana kama endocrine system.

Homoni  hufika kwenye mfumo huu wa endocrine system kupitia sehemu ya ubongo inayojulikana kama pitituary gland na hivyo kuingia kwenye mzunguko wa damu.Baada ya kufika wenye mzunguko wa damu, homoni hizi huenda moja kwa moja mpaka kwenye mayai ya mwanamke (ovary) na  kuyachochea mayai haya  kutoa mayai ya uzazi(ovum) katika hatua inayojulikana kama ovulation.

Watafiti hao wamesema wamegundua protini hii aina ya IFO katika shahawa za wanyama aina ya ilamas, sungura na hata kwa binadamu. Wanyama wengi wana viungo vya ziada vya kujamiana ambavyo hutoa manii kwenda kwenye shahawa lakini umuhimu wa manii hayo bado haujagundulika. “Wazo la kuwa kuna chembechembe katika manii ya wanyama na binadamu ambayo huchochea ubongo wa mwanamke ni wazo geni kabisa, alisema Gregg Adams”.
Wanasayansi hao wameweza kugundua ya kwamba ni chembechembe hizi ndizo pia husaidia katika ukuaji, urekebishaji na ustawishaji wa seli za neva.
 
Katika utafiti huu ambao wanasayansi walitumia ngombe, ilamas na binadamu, wanasayansi hao waliweza kugundua protini aina ya Ovulation-Induced-Factor kutoka katika manii ya wanyama hawa pamoja na binadamu waliohusika katika utafiti huu. Wanasayansi hao waliwachoma sindano yenye protini hii wanyama aina ya ilamas na kuwafanya wanyama hao kupata ovulation wakati walipowachoma ngombe sindano yenye protini hii aina ya IFO, ngombe hao walishindwa kuingia katika ovulation lakini protini hiyo iliweza kuwafanya ngombe kutengeza mifuko kwenye mayai yao ambayo ndio hasa hubeba mayai ya uzazi na hivyo kuwafanya ngome kuwa tayari kwa kushika mimba.Pia ilionekana ya kwamba protini hii (IFO) ina uwezo wa kustawisha mimba kwa ngombe hawa.
 
“Utafiti huu mpya unaongeza uelewa wetu wa mfumo wa ovulation lakini pia huongeza maswali mengi juu ya ovulation hiyo’, alisema Adams”
Tafiti zaidi zinahitajika ili kujua ni kazi gani ambayo protini hii aina ya IFO hufanya katika kumpa mtu uwezo wa kutunga au kushika mimba.Wanasayansi hao wanahisi uwepo wa protini hii kwa wingi kwa baadhi ya wanaume inawezekana ikawa ndio chanzo cha kuwafanya wanaume hao kuwa na uwezo mkubwa wa kutungisha  mimba mwanamke (fertile).
 
Ovulation ni hatua ambayo yai la uzazi hutolewa na kwenda katika mfuko wa uzazi (uterus) na kusubiri shahawa ili lirutubishwe na kuwa mimba.Ovulation hii hutokea siku ya 14 baada ya mwanamke ya  kuanza hedhi yake.Yai la uzazi ambalo hutolewa wakati huu hukaa kwa masaa 48 kusubiri kurutubishwa na kama halitarutubishwa na shahawa basi yai hili huharibika na kutolewa nje kama hedhi.Ni katika ovulation, ndio mwanamke huwa na uwezo/asilimia kubwa ya kushika ujauzito kama atajamiana na mwanamume.
 
Dalili za ovulation ni pamoja na kichwa kuuma, kizunguzungu, kichefuchefu, matiti kuuma, kuongezeka kwa kiwango cha joto mwilini, kutokwa jasho kwa wingi usiku, kubadilika  ladha ya ulimi, kuwa na hasira mara kwa mara, kupata hamu ya kujamiana, kutokwa na ute katika tupu ya mwanamke ,maumivu ya tumbo, maumivu ya mgongo na nk.
Imesomwa mara 40083 Imehaririwa Jumatatu, 12 Juni 2017 10:15
Dr Khamis

Dr. Khamis H.Bakari (MD PhD) ni daktari bingwa,mhadhiri katika chuo cha afya cha Chuo  Kikuu cha Dodoma,mtaalamu wa Tiba na Uchunguzi kwa kutumia mionzi ya nyuklia (Nuclear medicine).

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.