Image
Toto Clinic

Toto Clinic

kama wewe ni mzazi, utakuwa unajua kuwa moja ya changamoto na pia ni kitu cha muhimu ambacho wazazi hupitia ni kufuatilia kliniki ya mtoto. Na hata pale inapotokea mmoja wapo akaenda basi huwa ni ngumu kwa wote kuweza kuwa na taarifa sahihi kwa pamoja.

TanzMED Toto Kliniki ni moja ya nyenzo inayopatikana kwenye App ya TanzMED yenye kukuwezesha kufuatilia taarifa za ukuaji wa mtoto, taarifa za kliniki, ushauri wa daktari, siku za chanjo na mengine mengi yanayohusu mtoto.

Nyenzo hii, pia huwezesha wazazi wote wawili kwa pamoja kufuatilia, hii inamaanisha, mzazi mmoja ataweza kumuunga mwingine na wote wawili watafuatililia taarifa bila shida.

Na pindi mtoto anapofika umri wa miaka kumi na nane, TanzMED toto kliniki inaweza kubadilishwa na kuwa akaunti inayojisimamia yenyewe.