Image

Je, wajua viashiria vya baadhi ya wanaume walio katika hatari ya kuota matiti?

Kuongezeka ukubwa wa matiti kwa wanaume hutokana na kuharibika kwa mfumo wa vichocheo unaojulikana kama estrogen-androgen balance na hivyo kusababisha estrogen kutolewa kwa wingi ama kuongezeka kwa msisimko (sensitivity) wa matiti kwa kiwango cha zaidi ya kawaida kwa kichocheo aina ya estrogen kilicho kwenye mzunguko wa damu. Tatizo hili huonekana sana kwa watoto wachanga na  wanaume waliokatika umri wa kubaleghe, lakini pia huonekana kwa watu wazima na wazee.

Ni nani aliyekatika hatari ya kupata tatizo hili?

.Wanaume walio na umri zaidi ya miaka 50.

.Wenye uzito uliopitiliza (Obesity)

.Unywaji pombe kupindukia

.Magonjwa sugu ya figo au ya Ini

.Kuwepo kwa historia ya tatizo hili katika familia.

.Soma hapa kupata maarifa zaidi Tatizo la Kuota Matiti kwa Wanaume na Watoto (Gynecomastia)

Imesomwa mara 2419 Imehaririwa Alhamisi, 07 Novemba 2019 17:14
Sophia Mangapi

Web Developer

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.