Image

Fahamu vihatarishi vinavyoweza kuchangia mimba kutunga nje ya kizazi

Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi wa mwanamke au ectopic pregnancy ni tatizo ambalo limetokea kuathiri wanawake mbalimbali. Kwa kawaida, isipokuwa mara chache sana, mimba zitungazo nje ya mfuko wa uzazi hazina uwezo wa kukua kuwa mtoto kamili. Aidha, mimba hizi ni hatari kwa afya ya mama mjamzito kwa vile humfanya kupoteza damu nyingi na hatimaye kusababisha kifo.

Nini husababisha mimba kutunga nje ya kizazi?

Katika mimba nyingi zinazotunga nje ya uterus, chanzo chake huwa hakijulikani. Hata hivyo kuna vihatarishi ambavyo humfanya mwanamke kuwa katika hatari ya kupata tatizo hili. Vihatarishi hivi ni pamoja na

Matatizo katika mirija ya fallopian

Magonjwa yanayoweza kusababisha hali hii ni pamoja na

  • Maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke (PID)
  • Matumizi ya vitanzi vya kuzuia mimba (Intra-uterine contraceptive devices)
  • Kuoteana kwa tishu za uterus kwenye viungo vingine vya uzazi au endometriosis.

Uvutaji sigara

Uvutaji sigara kwa mwanamke una uhusiano mkubwa na utungaji wa mimba nje ya kizazi. Imeonekana kwamba wanaowake wanaopendelea kuvuta sigara mara kwa mara wana hatari ya kupatwa na tatizo hili mara tano zaidi ya wale wasiovuta kabisa. Hali hii husababishwa na nicotini iliyomo ndani ya tumbaku. Kwa kawaida nicotini huchochea kusinyaa kwa mirija ya fallopian hali iletayo kuziba kwa mirija hiyo na hivyo kufanya kiinitete kushindwa kupita kwenye mirija kuingia kwenye uterus na kufanya mimba kutunga kwenye mirija ya fallopian.

Upasuaji wa tumbo uliofanyika zamani

Operesheni yeyote inayohusu mirija ya fallopian inaongeza uwezekano wa mwanamke kutunga mimba nje ya uterus kwa vile mirija ya fallopian huwa imesinyaa kutokana na operesheni hiyo.

Matumizi holela ya baadhi ya dawa

Matumizi ya baadhi ya dawa zenye homoni husababisha kupungua kwa uwezo wa mirija ya fallopian kusukuma kiinitete kuelekea kwenye uterus na hivyo kuleta uwezekano wa utungaji wa mimba nje ya kizazi. Dawa hizo ni kama dawa za kuzuia mimba zenye homoni za kike za progesterone, na dawa za kusaidia uzazi aina ya clomiphene...........

Tatizo la Mimba Kutunga Nje ya Mfuko wa Uzazi (Ectopic Pregnancy)

 

Imesomwa mara 4636 Imehaririwa Jumatano, 19 Desemba 2018 16:14
Sophia Mangapi

Web Developer

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.