Image

Assalamu’alaikum Warahmutullahi Wabarakatuh. Natumai mu wazima wa afya na mnaendelea vyema na majukumu ya kila siku.

Waumini wa dini ya Kiislam duniani kote wameingia katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Hivyo,katika muendelezo wa makala zinazohusu kisukari, tunaoenda tujikumbushe au tujifunze mambo machache ya kufanya kabla, wakati na baada ya kipindi takatifu cha mfungo wa Ramadhani.

Tukiwa tuna amini kuwa watu wengi wanaoishi na tatizo la Kisukari hasa aina ya pili ya kisukari wanatamani sana kufunga Ramadhani katika kutimiza moja ya nguzo za imani ya dini ya Kiislam, na kwa imani Funga ni dawa kiroho na kimwili pia.

Jambo la kwanza kwa mtu mwenye kisukari ni kujiweka tayari kwa funga miezi mitatu au minne kabla, kuitayarisha akili na nafsi,hii itakusaidia kuwa mwangalifu sana katika ulaji wako na mfumo mzima wa ulaji.

Kufanya kipimo cha hba1c ni muhimu kwa sababu inaonesha kiwango cha sukari miezi mitatu na hii inakufanya ujue kama utaweza kufunga ramadhan bila kuwa tatizo lolote au hutaweza kufunga. Kupima sukari kabla na baada ya kula kabla ya mfungo wa ramadhani pia ni muhimu,kabla ya kula ni lazima sukari iwe chini ya sita(6) na masaa mawili baada ya kula iwe chini ya nane (8) na kama majibu yatakuwa hivyo kila mara hii itakuonesha kuwa unaweza kufunga bila tatizo.

Jambo la pili ni kuhakikisha unapata ushauri kutoka kwaa daktari wako wa kisukari, Shauriana naye, usiamue kufunga Ramadhani bila ya kushauriana na daktari wako, hii ni muhimu kwa sababu anaweza kukupa ushauri kulingana na kiwango chako cha sukari kwa miezi mitatu nyuma.(hba1c) na kipimo cha sukari cha kila siku unachopima kabla na masaa mawili baada ya kula.

Wakati wa mfungo ni lazima mtu mwenye kisukari atambue kuwa anaweza kufunga baada ya ushauri na ruhusa dakitari wake,na endapo akifunga, ni lazima pia awe anapima kiwango cha sukar kabla ya kuanza ,mfungo,kwa mfano, kabla ya kula daku ni lazima apima,hii itamsaidia kujua kama ataweza kufunga kwa siku hiyo ama Lah, kama akipima na kiwango cha sukari kikiwa sita (6) au saba(7) anaweza kufunga lakini indapo akipima akikuta kwango cha sukar iki chini ya sita (6), labda ni tano(5) au nne (4) hatoweza kufunga kwa sababu moja ya kisababisho cha sukari kushuka ni kukaa bila kula kwa muda mrefu.

Kutokupata choo au kuhisi kwenda kujisaidia haja kubwa na kutofanikiwa kutoa choo au mtu kupata choo chini ya mara tatu kwa wiki hujulikana kitaalamu kama constipation.Mtu mwenye tatizo hili la kufunga choo hupata choo kigumu,kikavu na chenye kupita kwa taabu kwenye njia ya haja kubwa

Tafiti nyingi zinaonyesha kwamba angalau kila mtu katika maisha yake huwa anapata tatizo hili la kufunga choo. Kufunga choo ni tatizo ambalo watu wengi  bado huhisi ni jambo la aibu sana hata kulizungumzia na hubaki na tatizo kwa muda mrefu  mpaka pale wanapopata madhara ya kiafya ndio hutafuta msaada wa kitabibu.

Dalili  zifuatazo zinaweza kutumika kuelezea tatizo la choo kufunga;

 1. Kupata choo kigumu na kinachoambatana na maumivu makali wakati wa kwenda haja kubwa
 2. Kutokupata choo kwa muda mrefu (infrequent bowel movements)
 3. Mtu kuhisi kama hajamaliza haja kubwa licha ya kupata choo

Tafiti nyingi zilizowahi kufayika zinaonyesha kwamba takribani asilimia 16 (16%) ya watu wazima hupata tatizo hili la kufunga choo,waathirika wengi wakiwa ni watu wenye umri kati  ya 60-110 (asilimia 35%).

Kwa nini wazee hupata tatizo hili la kufunga choo?

Sababu zifuatazo huchangia wazee kutokupata choo au kufunga choo;

 1. Hali ya uzee husababisha mmeng’enyo wa chakula kufanyika taratibu (slow metabolism) 
 2. Ukosefu wa lishe bora
 3. Kutokunywa maji ya kutosha
 4. Kutofanya mazoezi
 5. Magonjwa ya uzee kama pelvic floor prolapse na utumiaji wa dawa aina ya antacids na dawa za kupunguza maumivu
 6. Pia uzee husababisha meno kung’oka hivyo wazee huchagua vyakula laini na vyenye ufumwele (fiber) kidogo

Wanawake wajawazito ni miongoni mwa watu wanaopata tatizo hili la kufunga choo mara kwa mara.

Visababishi vya choo kufunga (constipation) ni kama ifuatavyo;

 1. Kutokula mlo wenye ufumwele (fiber) wa kutosha
 2. Kutokunywa maji ya kutosha
 3. Kutumia sana dawa za kulainisha choo
 4. Kutokufanya mazoezi au
 5. kuishi maisha ya unyongovu (stressful life)
 6. Madawa kama aspirin (NSAID), morphine, dawa za presha(thiazides, verapamil, furosemide), dawa za sonono (antidpressants), madawa ya saratani n.k
 7. Magonjwa ya  mfumo wa mmengenyo wa chakula  au  vichocheo vya mwili (hormonal disorders) kama hypothyroidism
 8. Ujauzito- Mama mjamzito yupo kwenye hatari zaidi ya kupata choo kigumu au constipation hasa katika miezi ya mwisho ya ujauzaito wake kwa sababu ya kuongezeka kwa vichocheo mwili aina ya sex hormones, kupungua kwa mmeng’enyo kwenye tumbo na kuchelewa kwa tumbo kupitisha chakula (delayed interstinal emptying)
 9. Magonjwa ya tumbo kama colorectal dysfunction, diverticulitis, irritable bowel syndrome, saratani za matumbo hasa utumbo mkubwa
 10. Chronic Idiopathic constipation- Sababu zisizojulikana

Kama ambavyo tumejifunza sababu na makundi wa watu ambao wapo kwenye hatari zaidi. Tatizo hili linaweza kumpata mtu yoyote wa rika lolote hata watoto wachanga. Hivyo fuatilia makala zetu zijazo ili kujua uchunguzi,matibabu na jinsi ya kuepukana na tatizo hili la kufunga choo.Kama tayari una tatizo hili  tafadhali fika kituo cha afya kilichokaribu nawe kwa ajili ya uchunguzi, matibabu na ushauri wa kitaalamu.

Watoto wanapozaliwa, tayari wanakuwa na meno ambayo  yamefunikiwa kwa fizi. Meno huanza kutoka kwa mara ya kwanza mtoto akiwa na umri wa miezi sita ( 6) japo umri huu unaweza tofautiana kutoka kwa mtoto mmoja hadi mwingine.

Meno mawili ya kwanza yanayoonekana mara nyingi ni yale ya kinywa cha chini katikati yakifuatiwa na ya kinywa cha  juu katikati. Watoto wengi hufikisha meno yote 20 ya kwanza wakiwa na umri wa miaka 3.

Baadhi ya watoto hawaoti meno kama watoto wengine, yao huchelewa au kutokuota kabisa. Hii husababishwa na vitu mbalimbali. Kama mtoto wako hajaota jino hata moja hadi umri wa miezi 18 basi ni muhimu umpeleke hospitali aonane na daktari wa kinywa na meno kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Sababu za meno kuchelewa kuota

Zipo sababu nyingi za meno kuchelewa kuota. Wakati mwingine tatizo la meno kuchelewa kuota huwa ni tatizo la kwenye familia  hivyo linaweza kurithishwa kwa vizazi vinavyokuja. Mzazi pia ujiulize kama meno yako yalichelewa kuota, kama ni ndio basi tambua kwamba hata ya mwanao yataota tu japo kwa kuchelewa.

Sababu zinazochangia meno kuchelewa kuota kwa mtoto ni kama zifuatazo;

 1. Utapia mlo na upungufu wa madini na vitamini mwilini- Watoto wenye utapia mlo meno huchelewa kuota kwa sababu ya kukosa virutubisho muhimu vya ukuaji wa meno. Aidha madini ya calcium na vitamini  D ni muhimu sana katika ukuaji wa meno. Hivyo mtoto akipungukiwa na virutubisho hivi meno huchelewa kuota.
 2. Ugonjwa wa jeni unaofahamika kama Down Syndrome- Huu ni miongoni mwa mgonjwa wa kuzaliwa nayo (congenital).Ugonjwa huu unatokana na hitilafu kwenye kinasaba cha 21 (chromosome 21). Ugonjwa huu huambatana na tatizo la meno kuchelewa kuota.
 3. Magojwa ya yatokanayo na hitalifu kwenye chromosomes (chromosome anomalies)
 4. Mtoto kuzaliwa njiti-Kuzaliwa njiti au na kuzaliwa  na uzito mdogo kupita kawaida (chini ya 1.5kg) kunahusishwa na kuchelewa kuota kwa meno kwa mtoto. Watoto hawa wanaweza kuwa na matatizo ya meno yenyewe.
 5. Magonjwa kama Amelogenesis na Regional Odontodysplasia

Amelogenesis ni ugonjwa wa kuzaliwa nao (congenital disease) ambapo mtoto anazaliwa na hitilafu kwenye kwenye protini zinazotengeneza enameli (nyeupe ngumu ya jino) hii hupelekea kuwa  na enameli isiyo ya kawaida na meno yanakuwa ya njano. Hii huambatana na meno kuchelewa kuota.

Regional odondodysplasia ni hitilafu katika ukuaji inayohusisha mesodermal na ectoderm (hizi ndizo zinazotengeneza jino la ndani na nje) za meno. Ugonjwa huu huwa unaathiri sehemu moja tu ya kinywa (localized). Huu sio ugonjwa wa kurithi.

Kwanini uwe na wasiwasi kuhusu meno ya mtoto yanapochelewa kuota?

Watoto ambao hawajaota meno hadi umri wa miezi 18 wapelekwe kumuona daktari wa meno. Watoto wengi huwa na meno manne wakifikia umri wa miezi 12 na huwa na yote 20 wakiwa na miezi 27.

Kama meno ya mtoto wako hayajaota kwa wakati inaweza kuwa ni ishara ya ugonjwa  au upungufu wa madini  au vitamini fulani mwilini.

Je, meno kuchelewa kutoa ni dalili mbaya?

Meno kuchelewa kuota sio jambo kubwa sana ila linaweza kuongeza uwezekano wa mtoto kupata matatizo ya meno ukubwani. Tafiti nyingi zinaonyesha kuwa watoto waliopata tatizo la meno kuchelewa kuota wana nafasi kubwa ya kuhitaji matibabu ya meno wakiwa na umri wa miaka 30.

Meno kuota kwa wakati kwa mtoto humsaidia kutafuna vizuri na husaidia meno ya pili kujipanga vizuri kwenye kinywa.

Meno yakichelewa kuota husababisha mtoto kukosa au kupata virutubisho vichache maana atakuwa hawezi kutafuna vizuri hivyo kupata shida ya kumeng’enya chakula.

Jinsi ya kutunza meno mapya ya mtoto wako

 1. Epuka vyakula na vinywaji vyenye sukari
 2. Safisha fizi kwa kutumia kutambaa kisafi mara mbili kwa siku
 3. Epuka kumlaza mtoto na chupa ya maziwa kitandani
 4. Kumbuka kuswaki na kusafisha meno yaliyoota

Utaanza kutumia dawa ya meno pindi mtoto akifikisha miaka 2.

 

Naweza Kunywa Pombe kama nina Ugonjwa wa kisukari?

Wagonjwa wengi wa kisukari wameniuliza kuhusu swali hili.Aghalabu, hata wengine ambao wanasoma makala hii pia watakuwa na shauku ya kutaka kujua kama kweli wanaweza kunywa pombe ilihali wanaugua ugonjwa wa kisukari bila kupata madhara yoyote ya afya.Swali hili ni la msingi sana hasa unapokuwa kwenye matibabu ya ugonjwa wa kisukari.

Ugonjwa wa kisukari ni moja kati ya magonjwa mengi yasiyoambukiza (non-communicable diseases) ambayo yanongezeka kwa kasi na kusababisha vifo na ulemavu.

Taarifa ya International Diabetes Federation imesema watu millioni 463 duniani wanaishi na kisukari na millioni 19 ya hao wapo bara la Afrika pekee.

Shirika hili katika taarifa yake ya mwaka 2020 limesema kwamba uwezekano wa kupata ugonjwa wa kisukari  nchini Tanzania ni kwa asilimia 3.7 huku idadi ya wagonjwa wa kisukari watu wazima imefika takribani watu 997,400.

Unywaji wa pombe uliopitiliza kwa watu wenye kisukari husababisha madhara makubwa ikiwemo kuongeza hatari ya kupata shinikizo la damu, magonjwa ya moyo,macho na kuharibika kwa mishipa ya fahamu.

Aidha Pombe au vileo vingi vina idadi kubwa ya wanga na sukari hivyo husababisha kupanda kwa haraka kwa sukari kwenye damu. Pia vina kalori nyingi hii upelekea kuwepo hatari ya kuongezeka uzito uliopitiliza ambapo hupunguza unyeti (sensitivity) na utolewaji wa kichocheo aina ya insulin  mwishowe husababisha ugumu wa kudhibiti sukari yako mwilini.

Sasa je naweza kunywa pombe kama ni ugonjwa wa kisukari?

jibu ni NDIO japo inabidi ujenge tabia ya kuwa na tahadhari pindi unapokunywa pombe.

Utatumia pombe pale tu ambapo sukari yako imedhibitiwa vizuri na kwa hali yoyote epuka unywaji pombe kupitiliza.

Najua kuna swali unaliwaza kuwa nisinywe kupitiliza unaamanisha nini?

Hili ni swali zuri na la msingi.Kulingana na shirika la ugonjwa wa kisukari la marekani (American Dabetes Association), imetoa vipimo vifuatavyo vya unywaji wa pombe kwa watu wenye kisukari.

Mwanamke mwenye kisukari asinywe zaidi ya chupa moja ya bia  sawa na 350mls, au 147 mls za wine na 44 mls za pombe kali kwa siku.

Kwa mwanamume, asinywe zaidi ya bia mbili sawa na 700mls, au 294 mls za wine au  88 mls za pombe kali.

USHAURI

Kabla ya kunywa pombe hebu jiulize masawali yafuatayo;

Je sukari yangu imedhibitiwa?

Je daktari wangu anakubali nitumie pombe au kilevi cha aina yoyote ile?

Je najua jinsi pombe inaweza kuniathiri mimi pamoja na sukari yangu?

Kama majibu yako yote ni ndio basi waweza kunywa pombe. Ila kumbuka pombe pia husababisha sukari kushuka. Ni vizuri kufahamu kiwango cha sukari yako mwilini kabla, wakati na baada ya kunywa pombe angalau kwa kipindi cha masaa 12.

Usikose kutembelea TanZMED kwa makala zaidi za afya kwa lugha ya kiswahili.

 

 

Ni moja kati ya magonjwa sugu yahusuyo mfumo wa kinga ya mwili kushambulia mwili wako na huwa na mtindo wa kuwa na kipindi cha kupata nafuu na kuwa kama umepona na kipindi cha kushambulia na kuwa hoi.

Huathiri zaidi wanawake, hadi asilimia 90 ya wagonjwa huwa wanawake. Na mara nyingi huanza kwenye umri wa uwezo wa ubebaji mimba.

Vipele ambavyo hutokea kipindi cha jua huathiri Ngozi (picha kwa hisani ya Dr. Erik Stratman, Marshfield Clinic)

 

Dalili

Ugonjwa huu huathiri karibu kila kiungo kwenye mwili

Dalili 3 kubwa ambazo hutokea ni:

 • Homa
 • Maumivu ya viungo
 • Vipele

Picha  inaonyesha vipele usoni hasa kwenye mashavu na pua kitalaamu Butterfly rash (Picha Kwa hisani ya affordablehealthinsurance.org)

Dalili nyingine ni:

 • Uchovu
 • Kupungua uzito
 • Figo kushindwa kufanya kazi vizuri
 • Dege dege
 • Maji kujaa kwenye mapafu, shinikizo la mapafu
 • Maumivu ya tumbo, kichefu chefu
 • Upungu wa damu, upungufu wa chembe chembe sahani

Vipimo:

Vipimo vya uhakika kuthibitisha ugonjwa huu ni;

 • Kipimo cha vinasaba kitaalamu double strand DNA antibodies na
 • Kingine kitaalamu Antinuclear antibody (ANA)

Vipimo vingine ni:

 • CBC- kujua wingi wa damu, na chembe chembe sahani
 • Kipimo cha damu kujua uwezo wa figo kufanya kazi (RFT)
 • Kipimo cha damu cha kujua uwezo wa ini kufanya kazi (LFT)

Matibabu:

Ugonjwa huu hauna tiba ziaidi ni kutibu dalili na kupunguza makali yake

Moja kati ya dawa ambazo hutumika ni:

 • Dawa za malaria - ambazo husaidia kupunguza makali yak inga kuushambulia mwili bila kuishusha kinga ya mwili. Dawa hizi pia huzuia na kutibu vipele ambavyo husababishwa na ugonjwa huu. Mfano wa dawa hizi ni: Hydroxychloroquine sulfate (Plaquenil)
 • Dawa za maumivu- ambazo husaidia kupunguza homa, maumivu ya kichwa na maumivu ya viungo. Mfano wa dawa hizi ni: Ibuprofen (advil, motrin)
 • Dawa za kupunguza kinga ya mwili- dawa hizi hupunguza kinga ya mwili hivyo kupunguza makali ya kushambulia mwili hivyo kupunguza makali ya ugonjwa, mfano wa dawa hizi ni: cyclophosphamide na methotrexate
 • Na kutibu kila dalili zitakazo jitokeza ipasavyo

 

 

Moja ya matatizo yanayoathiri sana jamii kubwa ya watanzania hususani watoto ni ugonjwa wa sickle cell. Ugonjwa huu wa kinasaba huathiri hemoglobin, sehemu iliyo muhimu sana katika muundo na ufanisi wa chembe nyekundu za damu.

Kazi kuu ya hemoglobin katika chembe nyekundu za damu ni kubeba, kusafirisha na kusambaza wa hewa ya oksijeni katika mwilini.

Watu wenye ugonjwa huu, hupata mabadiliko ya vinasaba ambayo hutokea katika nafasi ya sita ya mnyororo wa beta globin (beta chain) katika hemoglobin ambapo kiasili cha valine ambacho ni mojawapo ya tindikali muhimu za amino (amino acid) huchukua nafasi ya kiasili cha glutamate na hivyo kubadili kabisa umbo la chembechembe nyekundu za damu na kuzifanya zishindwe kufanya kazi zake vile inavyopaswa.

Kuna aina mbali mbali za sickle cell, nazo ni HbSS, HbAS, HbSC, HbSD na HbSO. HbSS huwaathiri watu wengi zaidi wakati wenye HbAS huitwa carriers au sickle cell traits kwa vile ndiyo wanaobeba tatizo hili la kijenetekia na kueneza kwa wengine ingawa wao mara nyingi kama siyo zote hawaoneshi dalili zozote za ugonjwa huu.

Dalili za ugonjwa wa sickle cell ni zipi?

Dalili za ugonjwa wa sickle cell hutegemea sana na kiwango cha uathirikaji wa chembe nyekundu za damu.

Kiujumla dalili zinaweza kuwa ni zile zinazohusiana na upungufu wa chembe nyekundu za damu mwilini yaani anemia, unaotokana na kuharibika kwa chembe hizo. Hizi ni pamoja na

 • Kushindwa kupumua vizuri
 • Kizunguzungu
 • Maumivu ya kichwa
 • Ubaridi katika viganja na miguuni
 • Unjano katika macho na ngozi au jaundice
 • Weupe katika viganja, na eneo la macho liitwalo conjuctiva, ulimi na midomo
 • Maumivu ya tumbo
 • Homa
 • Maumivu ya viungo (joint pains)
 • Maumivu ya kifua
 • Damu katika mkojo (hematuria)

Tatizo hili la kujikojolea bila sababu yoyote ya msingi ni tatizo linaloathiri watu wengi sana na ambalo huleta usumbufu  na aibu kubwa kama litampata mtu. Tatizo hili huwakumba sana wanawake kuliko wanaume  na inakisiwa kuwa asilimia 35 ya watu walio na umri zaidi ya miaka 60 wana tatizo hili, kati ya hawa wanawake ni mara mbili ya wanaume wanaopata tatizo hili.

Hakuna uhusiano wowote wa tatizo hili na vitendo vya kujaamiiana kinyume cha maumbile au ngono kwa njia ya haja kubwa (anal sex) au ushoga (homosexuality).
 
Miongoni mwa sababu zinazochangia kutokea kwa tatizo hili ni
 • Jinsia – Hutokea zaidi kwa wanawake kuliko wanaume (stress incontinence), kutokana na ujauzito, kujifungua, wanawake ambao wameacha kupata hedhi (menopausal women) na maumbile ya kawaida ya mwanamke (normal  female anatomy), hata hivyo, urinary incontinence huwa zaidi kwa wanaume wenye matatizo ya kwenye tezi dume (prostate) kama saratani ya tezi dume,  uvimbe katika tezi dume (BPH) nk.
 • Umri  – Kutokana na kuongeza umri, muscle za kwenye kibofu cha mkojo na kwenye mrija wa kupitisha mkojo yaani urethra, zinaanza kuwa legevu (weak) na hivyo kusababisha mtu kushindwa kuzuia mkojo au kujikojolea. Hii haimanishi ya kwamba kila mtu ambaye ana umri mkubwa hupata tatizo hili, la hasha, linaweza kuonekana kwa baadhi tu ya watu wenye umri mkubwa. Mara nyingi huonekana kwa watoto wadogo au wachanga kutokana na kutokukomaa kwa viungo vyao (kibofu cha mkojo na mrija wa kupitisha mkojo)
 • Uzito uliopitiliza – Kuwa na uzito uliopitiliza (obesity) ni moja ya chanzo kinachochangia kutokea kwa tatizo hili kwani uzito huu huongeza shinikizo katika kibofu cha mkojo na kufanya muscle zinazozunguka kibofu hiki kuwa legevu na matokeo yake ni mtu kujikojolea pindi anapopiga chafya au kukohoa

Upungufu wa akili ni tatizo ambalo kwa ujumla hutokea kabla ya mtu kuwa mkubwa (adulthood) na huambatana na dalili za kupunguwa uwezo wa akili ya utambuzi na kutafakari (cognitive functions) pamoja na kushindwa kukua kwa tabia za kuendana na mazingira yanayomzunguka mtu (adaptive behavior). Pia kitaalamu, upungufu wa akili hujulikana kama mtu yoyote mwenye IQ (Intelligence Quotient) chini ya 70.

Upungufu wa akili ni hali ya kuwa na mapungufu katika ukuaji (development deficit) yanayoanza utotoni ambayo husababisha kupungua uwezo wa kusoma (intellect), kutafakari, utambuzi na kutoweza kuendana na majukumu ya kila siku ya maisha.

Ukubwa wa Tatizo (Epidemiology)

Upungufu wa akili ni tatizo kubwa sana duniani.Huathiri asilimia 1-2 ya watu wote duniani.Huonekana sana kwa wanaume kuliko wanawake (inakisiwa huonekana mara mbili zaidi kwa wanaume kuliko wanawake). Upungufu wa akili wa kati (mild mental retardation) huonekana sana kwa watu wa kipato cha chini lakini upungufu wa akili wa kiwango cha juu hutokea uwiano sawa katika jamii ya matabaka yote na huonekana sana katika umri kati ya miaka 10 hadi 14.

Upungufu wa akili sio ugonjwa (axis II disorder in DSM-IV) kutokana na dalili na viashiria vyake bali ni tatizo la mfumo wa utambuzi wa watu wenye kuhitaji huduma za kijamii na elimu maalum ili kuweza kumudu majukumu yao ya kila siku. Mara nyingi upungufu wa akili hutokea kabla ya mtu kufikisha umri wa miaka 18.

Tungependa kwa yoyote mwenye takwimu kutoka afrika mashariki za tatizo hili la upungufu wa akili kutoka katika hospitali za magonjwa ya akili za Butabika National Referral and Teaching Mental Hospital (Kampala, Uganda), Port Reitz District Hospital (Mombasa, Kenya), Mathare Mental Hospital (Nairobi, Kenya), Lutindi Mental Hospital (Tanga, Tanzania) na Mirembe Psychiatric Referral Hospital (Dodoma, Tanzania).

Tabia za Kuendana na Mazingira (Adaptive behavior) ni nini?

Utangulizi

Kibofu cha mkojo kinapatkana sehemu ya chini ya maeneo ya tumbo na ni kiungo ambacho kina uwazi/tundu ndani yake na kazi yake kubwa ni kukusanya na kuhifadhi mkojo unaotolewa na figo kabla ya kuutoa nje ya mwili wa binadamu. Kibofu cha mkojo kina kuta (layers) aina tatu za tishu ambazo ni;

1.Mucosa layer – Kuta ya ndani kabisa ambayo ndio inayokutana na mkojo wa binadamu. Kuta hii nayo inakuta nyingi sana za seli au chembechembe zinazojulikana kama transitional epithelium cells ambazo pia hupatikana kwenye sehemu ya mirija inayojulikana kama ureters, urethra na kwenye figo. Seli hizi zinazuia uvujaji wa mkojo kwenda kwenye sehemu nyengine ya mwili.

Ureter huingiza mkojo kutoka kwenye figo na urethra hutoa mkojo kutoka kwenye kibofu cha mkojo wakati wa kukojoa.

2.Lamina propia – Kuta ya katikati nyembamba sana kati ya kuta  hizi tatu na  ambayo mishipa ya damu na neva inapatikana hapa na ni muhimu sana  wakati wa kupanga makundi ya saratani ya kibofu cha mkojo wakati wa tiba.

3.Muscularis layer -  Kuta ya nje ambayo ndani yake kuna destrusor muscle na ndio kuta nene kati ya hizi tatu. Kazi yake kubwa ni kupumzisha kibofu cha mkojo ili mkojo uingie ndani na ukishajaa basi hukaza kibofu (contracts) na kufanya mkojo kutoka nje.

Nje ya hizi kuta tatu, kibofu cha mkojo kimezungukwa na  mafuta ambayo hukinga kibofu kutokana na mtikisiko wowote na kukitenganisha na viungo vengine. Kuna saratani aina tatu kutokana na kuta hizi tatu nilizotaja hapo juu za kibofu cha mkojo

Tatizo la kufunguka mlango wa kushoto wa moyo unaotenganisha chumba kidogo na kikubwa cha moyo na  kuzuia  kupita kwa damu ya kutosha kwenda kwenye mshipa mkubwa wa damu (Aorta) ambao huhusika kuzungusha damu ndani ya mwili hujulikana kama mitral stenosis

Visababishi

Tatizo hili la kufunguka mlango wa kushoto wa moyo unaotenganisha chumba kidogo na kikubwa husababishwa na;

 • Homa inayojulikana kama rheumatic fever
 • Mtu anaweza kuzaliwa na hali hii
 • Matibabu ya saratani za kifua kwa kutumia tiba ya mionzi
 • Mkusanyiko wa madini aina  calcium kwenye milango hiyo ya moyo

Kati ya hizi sababu hapo juu, inayosababisha kutokea kwa  tatizo hili kwa wakubwa ni homa ya rheumatic fever, ambayo hufuatia maambukizi ya vimelea vya bakteria aina ya  streptococci kwenye koo au ngozi ambayo hayakutibiwa kikamilifu

Page 1 of 10