Image

Maambukizi ya njia ya mkojo (UTI) husababishwa na vimelea kitaalamu hujulikana E. Coli. Vimelea hawa huishi huishi kwenye mfumo wa chakula bila kuleta madhara yoyote wawapo humo, ila wakiingia kwenye njia ya mkojo huleta maambukizi na kusababishwa ugonjwa wa UTI.

Kutokana na sababu za kimaumbile, Wanawake huathirika zaidi na ugonjwa wa UTI kuliko wanamume, hii ni kwa kwasababu kuna ukaribu zaidi katika njia hizi mbili za chakula na mkojo. Na pale mtu anaponawa baada ya haja kubwa ni rahisi zaidi kuhamisha vimelea hivi vya E. Coli  kwenye njia ya mkojo pale ambapo hujifuta kuelekea mbele.  Na ndiyo sababu, kwa wanawake, hushauriwa kunawa kuanzia mbele kuja nyuma. Endapo utanawa kuanzia nyuma kuja mbele, kuna uwezekano wa kuhamisha vimelea hivi ambavyo husambaa hadi kwenye kibofu, na endapo hautotibiwa vyema, basi hupanda hadi kwenye figo.

Pia, Wanawake huathiriwa sana na UTI kwa sababu wana njia fupi ya mirija ya mkojo (urethra) ambayo, inawapa bakteria wa UTI urahisi wa kusafiri hadi kwenye kibofu cha mkojo. Kujamiiana pia kunaweza kunaweza kupelekea kupata bakteria wanaosababisha UTI. Matumizi ya vipandikizi vya kuzuia mimba vinavyowekwa kwenye shingo ya uzazi huongeza hatari ya kupata UTI. Magonjwa kama kisukari na matatizo ya kimaumbile katika mfumo wa mkojo huongeza asilimia za kupata UTI.

Dalili za maambukizi ya njia ya mkojo

  • Maumivu wakati wa haja ndogo, na hisia ya mkojo kuchoma choma
  • Kubanwa na mkojo mara kwa mara
  • Maumivu ya kiuno na maumivu ya chini ya kitovu
  • Mkojo wa njano sana, na muda mwingine unatoa harufu
  • Uchovu
  • Homa
  • Kuna baadhi ya watu hawawi na dalili yoyote (asymptomatic bacteriuria)
  • Kukosa hamu ya kula,Kichefuchefu na kutapika.

Miongoni mwa magonjwa sugu yanayoendelea kuathiri afya za mamilioni ya watu wa nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania ni ugonjwa wa kisukari. Ugonjwa huu hutokea pale ambapo tezi kongosho linaposhindwa kutengeneza kichocheo aina ya Insulin au pale mwili unaposhindwa kutumia vizuri kichocheo hicho cha insulin na kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha sukari kwenye damu au hyperglycemia.

Aina za Kisukari

Kisukari kimeanishwa katika makundi yafuatayo

Aina ya kwanza ya Kisukari au Type 1 Diabetes Mellitus

Hii ni aina ya kisukari inayowaathiri zaidi watoto na vijana (young adults).

Aina hii hutokea iwapo seli maalum zinazotengeneza homoni ya insulin zijulikanazo kama beta cells of Islet of Langerhans katika tezi kongosho zitakosekana au zitaharibika kwa sababu yeyote ile, na hivyo kusababisha ukosefu kabisa au upungufu wa kichocheo hicho kwenye damu.

 Upungufu wa akili ni tatizo ambalo kwa ujumla hutokea kabla ya mtu kuwa mkubwa (adulthood) na huambatana na dalili za kupunguwa uwezo wa akili ya  utambuzi na kutafakari  (cognitive functions) pamoja na kushindwa kukua kwa tabia za kuendana na mazingira yanayomzunguka mtu (adaptive behavior). Pia kitaalamu, upungufu wa akili hujulikana kama mtu yoyote mwenye IQ (Intelligence Quotient) chini ya 70.
Upungufu wa akili ni hali ya kuwa na mapungufu katika ukuaji (development deficit) yanayoanza utotoni ambayo husababisha kupungua uwezo wa kusoma (intellect), kutafakari, utambuzi na kutoweza kuendana na majukumu ya kila siku ya maisha.
 
Ukubwa wa Tatizo (Epidemiology)

Upungufu wa akili ni tatizo kubwa sana duniani.Huathiri asilimia 1-2 ya watu wote duniani.Huonekana sana kwa wanaume kuliko wanawake (inakisiwa huonekana mara mbili zaidi kwa wanaume kuliko wanawake). Upungufu wa akili wa kati (mild mental retardation) huonekana sana kwa watu wa kipato cha chini lakini upungufu wa akili wa kiwango cha juu hutokea uwiano sawa katika jamii ya matabaka yote na huonekana sana katika umri kati ya miaka 10 hadi 14.
Upungufu wa akili sio ugonjwa (axis II disorder in DSM-IV)  kutokana na dalili na viashiria vyake bali ni tatizo la mfumo wa utambuzi wa watu wenye kuhitaji huduma za kijamii na elimu maalum ili kuweza kumudu majukumu yao ya kila siku. Mara nyingi upungufu wa akili hutokea kabla ya mtu kufikisha umri wa miaka 18. Tungependa kwa yoyote mwenye takwimu kutoka afrika mashariki za tatizo hili la upungufu wa akili kutoka katika hospitali za magonjwa ya akili za Butabika National Referral and Teaching  Mental Hospital (Kampala, Uganda), Port Reitz District Hospital (Mombasa, Kenya), Mathare  Mental Hospital (Nairobi, Kenya), Lutindi Mental Hospital (Tanga, Tanzania) na Mirembe Psychiatric Referral Hospital (Dodoma, Tanzania).
 
Tabia za Kuendana na Mazingira (Adaptive behavior) ni Nini? 

Tabia za kuendana na mazingira ni jinsi mtu anavyoweza kumudu matakwa ya kujihudumia mwenyewe kila siku pasi na kumtegemea mtu yoyote kutokana na umri wake, tabaka lake, utamaduni pamoja na jamii inayomzunguka  kutokana  na vipengele viwili kati ya hivi vifuatavyo;

  • Mawasiliano (Kuweza kuwasiliana na watu)
  • Kuweza kujihudumia  katika shughuli zinazohitaji kutumia akili (functional academic skills)
  • Kuweza kuishi mazingira ya nyumbani na kazini
  • Kuwa na uwezo wa kuchanganyikana na jamii katika masuala ya afya na usalama wake
  • Kuweza kutumia huduma za jamii ambazo zitamfanya kuishi maisha ya furaha 


Ni vizuri kutambua ya kwamba tabia hizi hutegemea sana elimu, uhamasishaji, tabia za mtu binafsi, kupewa fursa za kijamii na za kiufundi (vocational skills), matatizo ya akili na magonjwa mbalimbali ya akili.
Intelligence kitaalamu ni uwezo wa ubongo katika kufikiri, kutatua matatizo, kuchagua au kuwa na busara (reason), na kuelimika.
 
IQ= Mental age (Umri wa akili)                                             ×  100

Chronological age (Umri wa kawaida wa binadamu)
 
Makundi ya Upungufu wa Akili                                                            Kundi Kipimo cha IQ

Upungufu wa akili uliopitiliza kabisa (Profound Mental Retardation)         Chini ya 20

Upungufu wa akili mkubwa (Severe Mental Retardation)                          20-34

Upungufu wa akili wa kati (Moderate Mental Retardation)                        35-49

Upungufu wa akili  (Mild Mental Retardation)                                            50-69

Upungufu wa akili wa kawaida (Borderline Intellectual  Functioning)         70-84
 
Mtu aliye kwenye kundi la upungufu wa akili (Mild Mental Retardation) anaweza kuelimika, na Yule aliye na upungufu wa akili wa kati, mtu huyu anaweza kufunzwa kazi za kumuwezesha kumudu maisha yake ya kila siku. Wale walio na upungufu wa akili mkubwa (Severe MR) na kundi la waliopitiliza (Profound MR) hawawezi kufunzwa chochote na kufundishika.
Kwa hiyo mtoto aliye na umri sawa wa akili na umri sawa wa kibinadamu atakuwa na kipimo cha akili 100 (yaani IQ=100). Kwa wale watoto wenye vipaji maalum, kipimo cha akili yao huwa zaidi ya 100 (IQ>100), na kwa wale wenye akili ya kawaida kipimo cha akili huwa chini ya 100 lakini hakishuki chini ya 85.
 
Upungufu wa Akili wa Kawaida (Borderline Mental Retardation)

Huwa na akili yakipimo cha IQ= 70-85%. Wanauelewa mdogo shuleni (Slow learners) lakini wanaishi maisha ya kawaida yaani bila kupata taabu yoyote katika maisha yao ya kila siku na wanaweza kuajiriwa.
 
Upungufu wa akili (Mild Mental Retardation)

Huwa na akili ya kipimo cha IQ=50-70. Asilimia kubwa ya watu wenye upungufu wa akili huwa kwenye kundi hili (asilimia 85-95). Wanatambulika kama wanaoweza kuelimika. Wanaweza kujifunza kusoma, kuandika, na kufanya hesabu rahisi rahisi (simple arithmetic calculations). Hawa wanahitaji shule maalum ili waje kuweza kumudu majukumu yao ya maisha ya kila siku baada ya muda mrefu.Wanakuwa na upungufu mdogo katika uwezo wao wa kuhisi na utambuzi wa vitu (minimal sensorimotor deficits) na ni vigumu kutambua kwamba wanaupungufu wa akili mpaka baadae maishani. Katika ujana wao wanaweza kupata elimu hadi darasa la sita.Ukubwani, hupata uwezo wa kujihudumia wenyewe katika mahitaji yao ya kila siku lakini wanahitaji uangalizi, ushauri, kupewa mwongozo katika majukumu yao ya kifamilia na hasa wanapopata msongo wa mawazo au wakati wamepata matatizo ya kiuchumi.
 
Upungufu wa Akili wa Kati (Moderate Mental Retardation)

Huwa na akili yakipimo cha IQ=35-50. Asilimia 10 tu ya watu wote wenye upungufu wa akili ndio huwa kwenye kundi hili.Wanatambulika kama wasioweza kufundishika (untrainable) ingawa wengi wao wanaweza kuelimika. Utotoni mwao wanakuwa na mawasiliano mabaya ya kijamii, lakini wanaweza kujifunza kuzungumza, kutambua majina yao na baadhi ya maneno rahisi ambapo kutokana na haya ambayo nimeelezea hapo juu, kwa sasa wanatambulika kama kundi linaloweza kufundishika.Kawaida, huacha shule baada ya kufika darasa la pili (Standard 2). Wanaweza kufundishika katika kazi ambazo hazihitaji kutumia akili ama kazi za mikono.Msongo wa mawazo huathiri mafunzo yao hivyo ni muhimu kuboresha  mazingira yao na kuwahudumia vizuri ili wasipate msongo wa mawazo. 


Mara nyingi, uwezo wao wa kuelewa watu wanapozungumza ni mzuri kuliko uwezo wao wa kuzungumza na hii huwafanya kupata msongo wa mawazo. Uzungumzaji wao ni wa kawaida na hueleweka vizuri na wale wanaoishi nao au wale wanaofahamiana nao vizuri. Vitendo kama uvaaji nguo, kula, na kujiweka msafi, huchukua muda mrefu kwao kujifunza. Wanahitaji msaada katika matumizi ya hela na hata kuvuka barabara.
 
Upungufu wa Akili Mkubwa (Severe Mental Retardation)

Huwa na akili ya kipimo cha IQ=20-35 na huonekana kwa watu wenye upungufu wa akili kwa asilimia 5 tu. Hutambulika mapema kwa kutokuwa na uwezo wa kutambua vitu mbalimbali (Poor motor development). Watu hawa hawana uwezo wa kuzungumza na kuwasiliana au hupata uwezo huo baadae maishani. Huitaji shule maalum pamoja na wataalamu wa tiba ya sauti ili waweze kujifunza kuzungumza.Chini ya uangalizi, huweza kujifunza shughuli ndogondogo.
 
Upungufu wa Akili Uliopitiliza (Profound Mental Retardation)

Huwa na akili ya kipimo cha chini ya 20 yaani IQ<20. Asilimia 1-2 ya watu wenye upungufu wa akili ndio walio kwenye kundi hili. Mara nyingi wanakuwa na ugonjwa au matatizo ya sehemu ya mishipa ya fahamu ambayo husababisha upungufu wa akili.Dalili za kuwa na uwezo finyu wa kutambua na kuhisi mambo mbalimbali, kushindwa kuelimika, kujihudumia, kufanya kazi, kujitunza huonekana mapema sana. Huitaji msaada wa kijamii pamoja na kuhudumiwa katika maisha yao ya kila siku.
 
Aina za Upungufu wa Akili

Kuna aina mbili za upungufu wa akili ambazo ni;
1.Syndromic  mental retardation – Hii ni upungufu wa akili (intellectual deficits)  unaoambatana na magonjwa mbalimbali  pamoja na  viashiria  na dalili za kitabia (behavioral signs).
2.Non syndromic mental retardation – Upungufu huu wa akili hausiani na magonjwa au ugonjwa wowote.
 
Pathofiziologia (Pathophysiology)

Upungufu wa akili ni mjumuiko wa matatizo katika mfumo wa fahamu (CNS functions) ambapo sehemu inayojulikana kama cortical structures (ambayo huusisha pamoja na sehemu zingine kama hippocampus na medial temporal cortex) ndio huathirika. Watu wengi wenye upungufu wa akili hawaonyeshi kuathirika katika mfumo wao wa fahamu. Ni aslimia 10-15 ya watu wote wenye upungufu wa akili ambao ndio wanaonyesha kuathirika katika mfumo wao wa fahamu.
Matatizo katika mfumo wa fahamu ambayo huonekana sana ni kichwa maji (hydrocephalus), neural tube defects, microcephaly na (disorders of migration- the lissencephalis na muunganiko wa mwatuko wa ubongo {agenesis of corpus carlosum} ambayo huonekana mara chache).


Watu wengi wenye upungufu wa akili aina ya mild mental retardation na wenye matatizo mengine ya ufahamu (other learning disorders), huwa hawana matatizo katika mfumo wao wa fahamu, madhara katika neva na dysmorphisms lakini wanauwezekano mkubwa wa kutoka katika familia zenye hali duni ya kiuchumi, familia yenye kipimo cha akili ndogo (low IQ), na elimu duni.
 
Nini husababisha upungufu wa akili?

Zipo sababu nyingi ambazo husababisha upungufu wa akili ambazo ni kama ifuatavyo;

  • Matatizo ya kurithi (genetic factors)
  • Antenatal factors
  • Postnatal factors
  • Matatizo ya kijamii na kitamaduni (socio-cultural factors)

Magonjwa ya akili (psychiatry disorders)
 
Thuluthi moja (1/3) ya watu wenye upungufu wa akili chanzo hasa hakijulikani.
 
Matatizo ya viashiria vya urithi (genetic factors)

  • Chromosal abnormalities kama down syndrome, fragile X syndrome (mgonjwa anakuwa na kichwa kikubwa, masikio makubwa kama ya popo, uso mrefu, korodani kubwa kupitiliza na nyayo zinakuwa bapa {flat feet},huwa na matatizo ya lugha na sauti, hii husababishwa na matatizo katika ncha ya mkono mrefu wa chromosome)
  • Metabolic disorders kama phenylketonuria, homocystinuri, galactosemia nk.
  • Magonjwa kwenye ubongo (Gross disease of the brain) kama cerebral dysgenesis, tuberose sclerosis, neurofibrosis nk.

Madhara ya kwenye ubongo (brain malformations) kama  nueral tube defects, kichwa maji na microcephalus
 
Antenatal factors

  • Matatizo ambayo hutokea wakati mtoto bado hajazaliwa (yaani yanayompata mtoto wakati bado yupo tumboni mwa mama yake). Haya yanaweza kuwa;
  • Magonjwa kama ugonjwa wa kaswende (syphilis), TORCH
  • Sumu (intoxications) kama madini ya risasi (lead), madawa ya kulevya, unywaji pombe wakati wa ujauzito nk.
  • Physical damage – Tiba ya mionzi au vipimo vya mionzi, injury, ukosefu wa hewa ya oksijeni kwa mtoto (hypoxia).
  • Matatizo ya kondo la uzazi (Placental dysfunctions) – Toxaemia, ukosefu wa virutubisho sahihi katika ukuaji wa kondo (Nutritional growth retardation).
  • Matatizo katika mfumo wa vichocheo mwilini (Endocrine disorders) – Hypothyroidism (ugonjwa wa tezi la koo), ugonjwa wa kisukari kwa mama mjazito, hypoparathyroidism.

 
Perinatal factors

  • Matatizo yanayotokea wakati mtoto anazaliwa (wakati wa kujifungua kwa mama mjazito)
  • Ukosefu wa hewa ya oksijeni (Birth asphyxia), cerebral palsy nk
  • Madhara ya mtoto kuzaliwa njiti (complications of prematurity) kama uvujaji damu ndani ya ubongo (intraventricular haemorrhage).
  • Hypoxic Ischemic encephalopathy
     


Post-natal factors

  • Matatizo yanayotokea baada ya mtoto kuzaliwa
  • Injury – Head injury (kuumia kichwa)
  • Sumu (Intoxication) kutokana na madini ya risasi, mercury nk.

Magonjwa kama ugonjwa wa uti wa mgongo (meningitis), encephalitis (maambukizi kwenye ubongo)
 
Socio-cultural factors (Matatizo ya kijamii na kitamaduni)

Kutokuwa na uwezo wa kujumuika na jamii huchochewa na ukosefu wa elimu, kiwango duni cha uhamasishaji, tabia ya mtu, ucheshi wa mtu,utapia mlo, mimba za utotoni (kwani huleta umaskini, utapia mlo, afya duni, kuathirika kwa mama na hivyo kumuathiri mtoto), vocational opportunities pamoja na magonjwa ya akili na magonjwa mbalimbali.

Kukosekana kwa vichocheo hivyo au kuwepo kwa magonjwa ya akili na baadhi ya magonjwa mbalimbali huweza kusababisha upungufu wa akili. Ikumbukwe ya kwamba akili ya mtoto huwa inakuwa kwa hiyo ni muhimu apewe fursa ya kuweza kukuza akili yake.
 
Magonjwa ya akili (Psychiatric disorders)

  • Pervasive developmental disorders (Autistic spectrum disorders). 

 

Image Source: https://newrepublic.com

Baadhi ya watu hukumbwa na tatizo la kuwa na vijiwe katika figo na mfumo wa mkojo kwa ujumla. Mawe haya hutokana na ama madini chumvi au tindikali mbalimbali zinazotolewa mwilini.

Aina za mawe katika figo

Aina za vijiwe katika figo ni pamoja na

  • vijiwe vya calcium oxalate
  • vijiwe vya tindikali ya uric (uric acid)
  • Vijiwe vya struvite (magnesium, ammonium na phosphate)

Vijiwe katika figo husababishwa na nini?

Kwa kiasi kikubwa, vijiwe husababishwa na kukosekana kwa usawa wa maji, madini na tindikali mwilini yaani electrolyte imbalance.

Katika sehemu ya kwanza ya makala ya upungufu wa akili tuliona makundi ya upungufu wa akili, ukubwa wa tatizo hili, visababishi na pathofiziolojia yake.
 
Sehemu hii ya pili tutaangalia dalili, vipimo vya uchunguzi, tiba yake pamoja na jinsi ya kujikinga na tatizo hili la upungufu wa akili.

Dalili na Viashiria vya Upungufu wa Akili

  • Kuchelewa katika ukuaji wa uwezo wa kuongea/kuzungumza
  • Upungufu wa kumbukumbu (deficits in memory skills)
  • Matatizo katika kufahamu mambo ya kijamii
  • Upungufu wa uwezo wa kutatua matatizo
  • Kuchelewa kukua kwa tabia za vitendo vya kujihudumia mwenyewe (kama kufunga vifungo vya shati nk)
  • Kuendelea kuwa na akili za kitoto
  • Kupungua uwezo wa kusoma

Ugonjwa wa kifua kikuu ni kati ya magonjwa matatu yanayotokea sana kwa watu masikini duniani (Disease of poverty). Magonjwa mengine katika jamii ya disease of poverty ni malaria na Ukimwi (AIDS). Ugonjwa wa kifua kikuu huathiri asilimia 98 ya watu katika nchi zinazoendelea, ukimwi asilimia 95 na malaria asilimia 90.

Magonjwa haya matatu husababisha vifo asilimia 10 ya idadi ya watu wote duniani kwa ujumla, ambapo inakisiwa watu wote duniani ni 6.91 bilioni kulingana na kituo cha kuhesabu watu cha Marekani ( US Census Bureau).

Kwa Tanzania, watu 120,191 hukisiwa kuwa na ugonjwa wa kifua kikuu kila mwaka, hii ni kutokana na taarifa ya shirika la USAID ya mwaka 2007. Kati ya watu hawa (120,191), 56,233 ni wale wanaogundulika kuwa na ugonjwa huu kupitia makohozi yaani sputum smear positive (SS+ ). Vifo vinavyotokana na ugonjwa wa kifua kikuu ni 32,000 kila mwaka nchini Tanzania.

Tanzania ni ya 15 kati ya nchi 22 ambazo zimeathiriwa sana na ugonjwa huu. Kati ya asilimia 50 ya wagonjwa wa kifua kikuu waliopimwa virusi vya ukimwi mwaka 2007, inakadiriwa ugonjwa wa ukimwi huathiri asilimia 47 ya wagonjwa wote wa kifua kikuu. Ugonjwa sugu wa kifua kikuu (Multidrug resistant tuberculosis) huathiri watu 1,300 nchini Tanzania kulingana na taarifa ya mwaka 2007.

Je, ugonjwa wa kifua kikuu husababishwa na nini?

Ugonjwa wa kifua kikuu, husababishwa na bakteria wanaojulikana kama Mycobacteria tuberculosis. Kuna aina nyingi za jamii ya Mycobacterium kama Mycobacteria tuberculosis (husababisha kifua kikuu), Mycobacteria leprae (husababisha ugonjwa wa ukoma), Mycobacteria bovis (huathiri ngombe na binadamu), Mycobacteria afrikanum na kadhalika.

Ugonjwa wa kifua kikuu unaweza kuathiri mapafu, mishipa ya fahamu, mifupa, mfumo wa mzunguko wa damu, ngozi, viunganishi vya mifupa (joints) na lymphatic system.

Mycobacteria bovis ambayo huathiri ngombe, inaweza kuambukiza binadamu kama atakula bidhaa zinazotokana na maziwa ya ngombe ambayo yameathirika na bakteria hawa kama vile siagi, mtindi, maziwa yenyewe, cheese, ice cream nk. Aina hii ya bakteria huathiri mapafu, tezi (lymph nodes), tumbo na sehemu nyingine za mwili.

Ni asilimia 10 tu ya watu walio na bakteria wa Mycobacteria tuberculosis ambao hawapati ugonjwa huu wa kifua kikuu.

Kati ya magonjwa yanayoathiri watu wengi sana duniani ni magonjwa ya zinaa. Haya ni magonjwa yanayoambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia vitendo vya ngono. Vitendo hivi vya ngono vinaweza kuwa kujamiana, kupiga denda (kissing), vitendo vya ngono kwa kutumia mdomo (oral genital sex), kujamiana kupitia njia ya haja kubwa (anal sex) iwe kwa mwanamume na mwanamke au kati ya wanaume wenyewe na hata wale wanaotumia vifaa vya kufanyia ngono (vibrators). Magonjwa ya zinaa huathiri sana watu walio katika umri wa miaka 15 – 24 lakini hata kwa watu wengine ambao wana umri chini au zaidi ya huu niliotaja pia yanaonekana kwa wingi.

Kuna magonjwa ya zinaa zaidi ya ishirini yanayotambulika duniani, baadhi ya magonjwa ya zinaa ni

  • Kisonono (Gonorrhoea – “Gono” kama wengi wanavyopenda kuita kwa kifupi).
  • Chlamydia
  • Kaswende (Syphillis)
  • Human papilloma virus (HPV)
  • HIV/AIDS (Ukimwi/Upungufu wa kinga mwilini)
  • Hepatitis B, C, A
  • Herpes virus
  • Trichomoniasis
  • Bacteria Vaginosis
  • Pubic lice (chawa kwenye nywele za kinena)
  • Chancroid

Magonjwa mengi ya zinaa yanatibika lakini kuna baadhi ambayo hayana tiba ya uhakika kama HPV, Hepatitis B na C, na HIV. Mengine yameanza kuwa sugu kutokana na matumizi ya dawa za antibiotics bila mpangilio, magonjwa hayo ni kama gono (gonorrhoea) na nk.

Visababishi vya magonjwa ya zinaa

  • Vitendo vya ngono kama nilivyoeleza hapo awali
  • Kuanza vitendo vya ngono mapema au wakati wa umri mdogo
  • Kuwa na wapenzi wengi
  • Kufanya mapenzi ambao sio salama
  • Maambukizi kupitia michibuko au sehemu zilizokatika kwenye ngozi kwa kugusana na majimaji ya aina yoyote yanayotoka kwa mtu mwenye ugonjwa wa zinaa kama damu, shahawa nk. Hii inaweza kutokea bila mtu kujua kwani mara nyingi dalili za magonjwa ya zinaa zinakuwa hazionekani kwa wanawake na hata baadhi ya wanaume.

Watu wengi huhisi kitendo cha kula denda (kissing) ni salama lakini si kama wanavyofikiria kwani baadhi ya magonjwa kama kaswende, herpes nk, yanaweza kuambukizwa kupitia njia hii. Kondomu husaidia kupunguza maambukizi ya magonjwa ya zinaa kama gono, Chlamydia lakini sio kinga muafaka dhidhi ya magonjwa ya zinaa kama kaswende, genital herpes, genital warts, na magonjwa ya upungufu wa kinga mwilini (AIDS).

Nitaanza kuzungumzia ugonjwa wa gono (gonorrhea) kwa leo na makala zitakazofuata nitakuwa nazungumzia ugonjwa mmoja baada ya mwengine

Kisonono (gonorrhea) ni nini?

Kisonono ni ugonjwa kati ya magonjwa ya zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya Neisseria gonorrhoeae, bakteria ambao hukuwa na kuzaliana kwa haraka katika sehemu zenye unyevunyevu na joto mwilini kama kwenye shingo ya kizazi kwa wanawake (cervix), mirija ya kupitisha mkojo au shahawa (urethra), mdomoni na kwenye puru. Maambukizi mengi kwa wanawake hutokea kwenye shingo ya kizazi (cervix). Asilimia 75 ya ugonjwa wa gono hutokea kwa watu wenye umri wa miaka 15 – 29, wanawake walio katika umri wa miaka 15 -19 na wanaume walio katika umri wa miaka 20 – 24 wako kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu.

Ugonjwa huu huambukizwa vipi?

Ugonjwa huu huambukizwa kupitia vitendo vya ngono kupitia uke, njia ya haja kubwa (anus), kupitia mdomoni (oral sex). Ugonjwa unaweza kujitokeza kwenye sehemu za kujamiana, kwenye mdomo na kwenye puru (rectum). Ugonjwa wa gono huonekana sana kwa vijana, watu wenye maisha duni kiuchumi, watu wanaoishi mijini, watu weusi na watumiaji madawa ya kulevya.

Dalili za ugonjwa wa kisonono

Dalili za ugonjwa wa kisonono huanza kujitokeza kuanzia siku ya 2 hadi ya 7 baada ya mtu kupata maambukizi na huweza kuchelewa kwa wanawake. Dalili ni kama zifuatazo

Kwa wanaume

  • Kuhisi kama kichomi wakati wa kukojoa (burning sensation)
  • Kutokwa na majimaji ya njano au meupe au ya kijani kutoka kwenye uume yanayoambatana na maumivu makali sana
  • Wakati mwengine maumivu au kuvimba kwa korodani (swollen testicles)
  • Maambukizi yakiwa kwenye puru (rectum) huambatana na maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa, kuwashwa sehemu za haja kubwa, na hata haja kubwa inaweza kutoka ikiambatana na damu, hii inatokea kwa wanaume na wanawake.

Kwa wanawake

Dalili kwa wanawake huwa si nyingi lakini wanawake wengi hawaonyeshi dalili zozote

  • Maumivu au kuhisi kama kichomi wakati wa kukojoa
  • Kuongezeka kwa kutoka majimaji kutoka kwenye tupu ya mwanamke ambayo ni ya njano au yamechanganyika na damu
  • Kutokwa na damu kupitia tupu ya mwanamke kabla ya hedhi kufika.
  • Kutokwa na damu baada ya kujamiana au baada ya tendo la ndoa
  • Kichefuchefu
  • Homa (fever)
  • Kutapika

Vipimo vya ugonjwa wa kisonono

  • Swab for culture – Kipimo hiki hufanyika maabara kwa kupandikiza bakteria baada ya kufuta sehemu za siri kwa kutumia swab ili kuona kama kuna bakteria wanaosababisha gono.
  • Polymerase Chain Reaction (PCR) – Kipimo cha kuangalia vina saba (DNA) ya bakteria, ni ghali sana.

Tiba ya ugonjwa wa kisonono ni nini?

Tiba ya gono inahusisha na tiba ya ugonjwa wa Chlamydia kwani mara nyingi magonjwa haya huambatana kwa pamoja.Tiba hutegemea na umri wa mgonjwa na kama mtu ni mjamzito au la. Tiba ya gono ambayo sio sugu iliyo kwenye shingo ya kizazi (cervix), urethra na puru, dawa zinazotumika ni aina za cephalosporin dozi moja pamoja na dawa za aina ya macrolide antibiotics (mfano azithromycin) na za jamii ya penicillin (mfano doxycyclin) ili kutibu ugonjwa wa chlamydia. Mara nyingi kwa wale chini ya miaka 18 na wanawake wajawazito, hutibiwa kwa kuchomwa sindano.

Fuata ushauri wa daktari kabla ya kutumia dawa hizi kwani dawa nyingi zina madhara kwa wajawazito (mfano doxycyclin). Ushauri nasaha hutolewa kwa wapenzi wote wawili na ni vizuri wapenzi wote wawili kutibiwa hata kama mmoja hana dalili za ugonjwa huu.

Madhara ya ugonjwa wa kisonono

  • Kutoweza kuzaa kwa mwanamke (tasa) au kutoweza kutungisha mimba kwa mwanamume (infertility)
  • Huweza kuathiri moyo (heart valves), ubongo,ngozi nk ambayo ni hatari sana kwa mtu yoyote.
  • Madhara kwenye sehemu za maungio au jointi (joint inflammation)
  • Kwa wanawake wale ambao hawajatibiwa wanaweza kupata ugonjwa wa PID (Pelvic Inflammatory Disease) ambao huongeza asilimia ya mwanamke kuwa tasa.
  • Wale wanawake ambao ni wajawazito na wameambukizwa gono wako kwenye hatari ya mimba kutoka au kuzaa mapema kabla mimba haijatimiza umri wake (preterm labor).
  • Kwa wale wanaoambukizwa gono kipindi cha kukaribia kujifungua, wanaweza kuwaambukiza watoto wao na hivyo watoto kupata ugonjwa wa uti wa mgongo (meningitis), kuwa kipofu (blindness), homa ya mapafu (pneumonia) na ugonjwa wa mifupa (septic arthritis).

Kinga ya kisonono

  • Kutumia kondomu wakati wa kujamiana
  • Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu
  • Kuacha vitendo vya ngono kama matumizi ya vifaa vya ngono hasa kwa wanawake mfano vibrators nk.
  • Kwa wanawake wajawazito – Hakikisha unahudhuria kliniki mapema ili upate kuchunguzwa na kupatiwa tiba muafaka kama utagundulika na ugonjwa wa gono au ugonjwa mwengine wowote.
  • Wanawake wajawazito wanashauriwa kujifungulia hospitali ili kama mtoto ameathirika na gono apate matibabu ya haraka baada ya kuzaliwa kuepusha kuwa kipofu.
  • Epuka kufanya ngono na mtu aliyeambukizwa gono.

“Kumbuka ya kwamba hakuna kitu kama ngono salama kwani huwezi kujua kama wewe au mwenzako wakati wa kujamiana ameathirika au la, au una michibuko au umekatika kwenye ngozi au la kwani michibuko mengine inaweza isionekane au kugundulika kwa urahisi. Njia pekee na nzuri ni kuacha au kujikinga na vitendo vya ngono”. Mtu aliyepata gono awali anaweza kupata tena.

Usikose mwendelezo wa makala hii.........

 

Daktari mmoja aitwaye Mackod, alipitia makala nyingi za afya ili kuweza  kutambua visababishi vya vifo ambayo havitokani na umri au nasaba ya kiasili (Genetic), na akagundua mambo tisa ambayo yanasabisha vifo ambavyo vingeweza kuzuilika. Mambo hayo tisa ni; uvutaji wa sigara, unywaji wa pombe, kutofanya wa mazoezi, lishe duni, wadudu kama bakteria na virusi, ajali, tabia za ngono za kupita kiasi bila kinga,  vita na madawa ya kulevya.

Katika makala hii ningependa kuzungumzia juu ya ufanyaji wa wazoezi na hasa wakati bora wa kufanya mazoezi. Mazoezi ni muhimu sana kwa ajili ya kupunguza mafuta ya ziada mwilini, tafiti zinaonesha kuwa asiyefanya mazoezi, madhara anayopata ni sawa na mtu anayevuta tumbaku.

Utafiti uliofanywa na Dr. Jason na Nor Farah (2004) wa Chuo kikuu cha Glasgow, umeonesha kuwa unapofanya mazoezi kabla ya kifungua kinywa, wakati tumbo likiwa tupu, ni bora zaidi kuliko unapoweza kufanya mazoezi baada ya mlo wowote. Kufanya mazoezi ni jambo la maana kwa afya kuliko kutokufanya mazoezi ya mwili, lakini unaweza kupata  faida zaidi kama unaweza kufanya kabla hujala chochote.

Mazoezi kwa ujumla wake yana umuhimu mkubwa kwa afya ya binadamu, hasa kama yakiambatana na lishe bora. Mazoezi huweza kuzuia magonjwa sugu kama kisukari, magonjwa ya moyo, kansa na shinikizo la damu, pia kwa kufanya mazoezi unaweza kuongeza kipato kwa kuwa unaweza kufanya kazi muda mrefu kuliko asiyefanya mazoezi.

Familia ambazo hufanya mazoezi huwa na afya bora na kipato kikubwa kwa kuwa fedha kidogo wanazopata hutumika kwenye maendeleo tofauti na familia zisizofanya mazoezi ambazo hujikuta wakitumia kipato hicho kidogo kwa ajili ya kutibu  magonjwa ambayo yangeepukika kwa kufanya mazoezi.

 

Utangulizi

Surua ni mojawapo ya magonjwa ya kuambukiza yanayotisha kwa binadamu. Huu ni ugonjwa ulio na kiwango cha juu cha karibu asilimia 100 cha mashambulizi pindi mtu apatapo vimelea vya ugonjwa huu.

Pamoja na kuwepo chanjo ya ugonjwa huu, bado surua ni miongoni mwa magonjwa yanayosababisha vifo vingi vya watoto walio chini ya umri wa miaka 5 katika baadhi ya maeneo duniani hasa kwa nchi zinazoendelea. Ugonjwa huu ambao ulitoweka katika baadhi ya nchi, umeanza kuonekana tena hivi karibuni miongoni mwa watu ambao hawakupata chanjo katika nchi za Uingereza na nyingine za Ulaya.

Surua husababishwa na nini?

Surua huenezwa na aina ya virusi jamii ya paramyxovirus. Jamii hii ya virusi hupatikana katika mfumo wa njia ya hewa. Hukaa katika kamasi na majimaji yaliyopo katika mfumo wa hewa. Kwa sababu hii basi virusi hawa huenezwa kwa njia ya upumuaji. Virusi hawa wanaweza kuishi hewani kwa muda wa hadi saa moja baada ya kutolewa kwa kupiga chafya au kukohoa au hata mazungumzo na mgonjwa. Hii ina maana kuwa, ili kuambukizwa surua, si lazima mtu akutane uso kwa uso na mgonjwa. Baada ya kuingia ndani ya mfumo wa hewa virusi hushambulia seli za utando wa nje wa njia ya hewa (respiratory tract epithelium) na kuingia katika mzunguko wa wa limfu na kufika kwenye tezi zilizo karibu. Katika tezi huzaliana zaidi na kusambaa mwilini.

Utangulizi

Mada hii ina lengo la kuzungumzia tatizo la kuwa na hofu au wasiwasi uliopita kiasi au kwa kitaalamu Generalized anxiety disorder (GAD). Kwa ajili ya kutofautisha kati ya hofu iliyopitiliza na hofu ya kawaida ambayo yaweza kumkumba mwanadamu yeyote, wakati fulani fulani mwandishi atatumia maneno anxiety au GAD katika kuwasilisha ujumbe wake.

Hofu iliyopitiliza au au anxiety au GAD huambatana na hali ya kuwa na wasiwasi kupita kiasi juu ya maisha ya kila siku pamoja na matukio yake bila hata muhusika kuwa na sababu maalum ya kuwa na hofu hiyo. Kwa maneno mengine ni kuwa, watu wenye anxiety hujihisi hofu kubwa bila ya kuwa na sababu yeyote ya msingi ya kuwafanya wawe hivyo. Mara nyingi watu wenye tatizo hili huwa na tabia ya kuhisi kwamba janga kubwa litawatokea karibuni au maafa yatamkumba katika maisha yake na daima hawaachi kuwa na hofu isiyo na sababu juu ya familia zao, pesa, afya, ajira, masomo au hata biashara zao.

Maisha yao ya kila siku huwa na mchanganyiko wa hofu, wasiwasi na huzuni, kiasi kwamba hatimaye hofu hutawala mawazo  ya muhusika kiasi cha kuingilia utendaji wake wa kila siku ikiwemo kazi, masomo, shughuli zake za kijamii, na hata mahusiano na mwenza wake wa ndoa.

Dalili za hofu iliyopitiliza (anxiety) ni nini?

Ukurasa 4 ya 11