Karibu

Karibu Jukwaa la Afya. Jukwaa linakuwezesha kuuliza au kujibu maswali ya Afya. Sasa unaweza kuuliza kwa Faragha (Private)
  1. Kiluilui
  2. Magonjwa
  3. Jumapili, 09 Julai 2017
Nina ugonjwa ambao nahis ni strock kwa dalili kwani nina mwaka wa tatu nashindwa kuongea vizur kama zamani nimejaribu kupima hadi mri nimeambiwa ninakama kidoa kwenye ubongo na nikapewa dawa na sindano kuyeyusha lakini bado cjapata nafuu.
kila kitu kinafanya kazi vzur shida ni kuongea tu.
naomba msaada
Dr.Henry Mayala Jibu Sahihi Pending Moderation
Mtaalamu
0
Votes
Undo
Kiharusi
Kuna aina mbili za kiharusi
 Kuziba kwa mishipa ya damu ya kwenye ubongo na kuathiri ufanyaji kazi wa ubongo na mishipa ya fahamu
 Kuvuilia damu kwenye ubongo kutokana na kuchanika mshipa wa damu wa kwenye ubongo na kuathiri ufanyaji kazi wa ubongo na mishipa ya fahamu
Visababishi
Kiharusi husababishwa na
• Shinikizo la damu
• Kisukari
• Moyo kupiga bila mpangilio(atrial fibrillation)
• Ongezeko kubwa la mafuta mabaya kwenye damu
• Utapia mlo (uzito uliopitiliza)
• Seli mundu
Dalili za kiharusi kisababishwacho na kuziba mishipa ya damu
o Kuishiwa nguvu upande mmoja wa mwili
o Kupoteza fahamu
o Matatizo wa kuona vizuri
o Kushindwa kuongea vizuri au ugumu wa kutengeneza maneno yanayo eleweka
o Kukosekana kwa uwiano wa uso
o Matatizo ya misuli na kusababisha kushindwa kutembea vizuri, kushindwa kumeza vizuri
Kinachoongezeka kwenye dalili za kiharusi kisababishwacho na Kuvuilia damu kwenye ubongo kutokana na kuchanika mshipa wa damu wa kwenye ubongo ni:
o Maumivu makali sana ya kichwa na
o Kutapika
Vipimo ambavyo hufanywa ni:
 CT –scan ya ubongo
 MRI ya ubongo
o Vyote husaidia kutambua aina ya kiharusi
Matibabu
Ni vyema kutibu na kudhibiti visababishi
Na kubadili mfumo wa maisha: kula vyakula vyenye lishe bora (epuka mafuta hasa mafuta mabaya (Bad cholesterol) na kupunguza chumvi nyingi hasa ya kuongeza (table added) na mazoezi, epuka pombe na sigara
Matibabu ya dawa ni muhimu sana kuonana na daktari bingwa wa mishipa ya fahamu hospitali maana kuna tofauti ya matibabu kati ya hizo aina za kiharusi na ni hatari kujitibu mwenyewe
Physiotherapy au mazoezi ya viungo ni muhimu sana kwenye kupata nafuu kwenye matibabu haya, na cha muhimu ni kuwa mvumilivu maana huweza kuchukua muda mrefu kidogo kupata nafuu, na kutokana na sehemu ya ubongo iliyoathirika
  1. zaidi ya mwezi
  2. Magonjwa
  3. # 1
  • Kurasa :
  • 1


Hakuna mtu aliyejibu bado
Kuwa wa kwanza kujibu swali hili!
Mgeni
Tuma majibu yako...
Unaweza ambatanisha swali lako na kipachiko (Attachment). Picha au faili. Vikoo vinavyokubalika gif,jpg,png,jpeg,zip,rar,pdf,doc,docx
• COM_EASYDISCUSS_INSERT • Remove Kizio cha kupandisha (Mwisho: 4 MB)
Namba za usalama
Ili kuwalinda watumiaji pamoja na Website yetu. Unatakiwa kuingiza namba ya usalama kabla haujatuma swali.