Karibu

Karibu Jukwaa la Afya. Jukwaa linakuwezesha kuuliza au kujibu maswali ya Afya. Sasa unaweza kuuliza kwa Faragha (Private)
  1. Kiluilui
  2. Magonjwa ya Wanawake
  3. Jumanne, 17 Oktoba 2017
Je, kukosa nguvu kwenye miguu kwa mwanamke kipindi cha ujauzito inasababishwa na nini?, pia tiba yake ni ipi?
Dr.Henry Mayala Jibu Sahihi Pending Moderation
Mtaalamu
0
Votes
Undo
Kuishiwa nguvu kipindi cha ujauzito au uchovu uliopitiliza na dalili ambazo hutokea kipindi cha ujauzito. Wengine huwa na dalili hizi kipindi chote cha ujauzito, na kwa wengine miezi mitatu ya mwanzo na hurudi mizezi mitatu ya mwisho.

Miezi mitatu ya mwanzo dalili hizi huweza kusababishwa na mabadiliko ya vichocheo, na mtoto huwa nakuwa kipindi hiki damu ya mama huongezeka ili kubeba virutubisho kupeleka kwa mtoto. Shiniko hushuka na sukari hushuka mwilini. Kuongezeka kwa kichocheo aina ya progesterone husababisha hali ya kuwa na usingizi muda mwingi.

Miezi mitatu ya mwisho hali hii husababishwa na uzito kuongezeka usabishwao na uzito wa mtoto, kusindwa kulala vizuri usiku kwasababu ya kwenda haja ndogo mara kwa mara.
Unaweza kupambana na hali hii kwa
1. Kupumzika zaidi pale unajisikia mchovu au kuishiwa nguvu. Hupunguzwa kwa kulala mapema, au kupata muda wa kupumzika mchana. Na punguza kunywa maji usiku, au muda mfupi kbala ya kulala, ila kunywa maji muda wa mchana
2. Kuweka sawa ratiba, kama mtu wa shughuli sana ni vyema kuomba msaada au kupunguza shughuli kwa kipindi hiki
3. Kula chakula bora chenye protini, vitamin, madini chuma, na vyenye kuongezea mwili nguvu
4. Fanya mazoezi japo matembezi madogo madogo ya nusu saa.
  • Kurasa :
  • 1


Hakuna mtu aliyejibu bado
Kuwa wa kwanza kujibu swali hili!
Mgeni
Tuma majibu yako...
Unaweza ambatanisha swali lako na kipachiko (Attachment). Picha au faili. Vikoo vinavyokubalika gif,jpg,png,jpeg,zip,rar,pdf,doc,docx
• COM_EASYDISCUSS_INSERT • Remove Kizio cha kupandisha (Mwisho: 4 MB)
Namba za usalama
Ili kuwalinda watumiaji pamoja na Website yetu. Unatakiwa kuingiza namba ya usalama kabla haujatuma swali.