Karibu

Karibu Jukwaa la Afya. Jukwaa linakuwezesha kuuliza au kujibu maswali ya Afya. Sasa unaweza kuuliza kwa Faragha (Private)
  1. Kiluilui
  2. Afya ya Jamii
  3. Jumapili, 22 Oktoba 2017
Sawali langu je, kuna madhala yoyote kwa mama alie jifungua atakapo shiliki tendo ndoa
Dr.Henry Mayala Jibu Sahihi Pending Moderation
Mtaalamu
0
Votes
Undo
Kama umejifungua kwa njia ya kawaida na hukupata shida yoyote:
1. Kuna kipindi cha wiki sita kitalaamu Puerperium ambapo mama baada ya kujifungua mwili hurudi kwenye hali yake ya kawaida, huwa kuna ute na damu ambayo hutoka kitaalamu lochia.
2. Hivyo tendo la ndoa huweza kurudi mara damu hii inapokata, na pale mwanamke anapokuwa tayari kisaikolojia na kuwa na nguvu ya kuweza kumudu tendo la ndoa
3. Cha muhimu ni kuanza kuangalia njia za uzazi wa mpango maana ni rahisi sana kupata ujauzito mwingine kwenye kipindi hiki.

Kama umejifungua kwa njia ya kwaida na ukaongezwa njia, ni vyema kusubiri mpaka kidonda kitakapopona baada ya kushonwa, na kusubiri mpaka damu itakapo kata, na pale mwanamke anapokuwa tayari kisaikolojia na kuwa na nguvu ya kuweza kumudu tendo la ndoa.
Kama umejifungua kwa operesheni vilevile atahitaji muda wa kupona, na kipindi cha wiki sita kitaalamu puerperium, na vizuri kufuatilia kidonda kitakapo pona na kupata ushauri wa mtaalamu wa afya

Cha kuzingatia ni kuwa uchovu, msongo mawazo na wasiwasi wa maumivu ndio unaoweza kuchelewesha kurudi kwenye hamu ya tendo la ndoa, wengine husubiri wiki sita, wengine miezi miwili na wengine hadi miezi minne.
Cha kuzingatia ni mume na mke kuwa a mawasiliano mazuri na kujua kumpa mwenza muda wa kurudi kwenye hali yake maana huu huwa mtihani kwa wamama wengine huchukua muda mrefu kurudi kwenye hali ya kupata hamu ya tendo la ndoa, na mara nyingi ni sababu za kisaikolojia.
  1. zaidi ya mwezi
  2. Afya ya Jamii
  3. # 1
  • Kurasa :
  • 1


Hakuna mtu aliyejibu bado
Kuwa wa kwanza kujibu swali hili!
Mgeni
Tuma majibu yako...
Unaweza ambatanisha swali lako na kipachiko (Attachment). Picha au faili. Vikoo vinavyokubalika gif,jpg,png,jpeg,zip,rar,pdf,doc,docx
• COM_EASYDISCUSS_INSERT • Remove Kizio cha kupandisha (Mwisho: 4 MB)
Namba za usalama
Ili kuwalinda watumiaji pamoja na Website yetu. Unatakiwa kuingiza namba ya usalama kabla haujatuma swali.