Kujilinda na Corona Virus

Epuka kujishika usoni
Pindi mtu mwenye virusi vya Corona atatoa matone (kwa kukohoa au kupiga chafya) Virusi vya Corona hukaa kwenye vitu (surface), hivyo kama utashika na ukajishika mdomoni, puani au machoni basi utajiambukiza virusi vya Corona. Kuepuka kushika uso ni moja ya njia thabiti ya kuepuka virusi hivi.

Epuka kusogeleana umbali wa mita 2
Kwakuwa ni ngumu kumjua mtu mwenye maambukizi ya vorusi vya Corona. Hivyo inashauriwa kukaa umbali wa mita 2 pindi unapoongea na mtu. Hii itasaidia pindi akikohoa au kupiga chavya basi virusi haviwezi kukufikia kiurahisi.

Epuka safari na mikusanyiko isiyo ya lazima
Moja ya njia thabiti ya kuzuia maambukizi ya Corona ni kuepuka mikuanyiko isiyo ya lazima kama sherehe, harusi,makanisani, misikitini nk. Hii itasaidia kuzuia maambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.

Osha mikono kwa maji yanayotiririka na sabuni
Hakikisha unaosha mikono mara kwa mara kwa kutumia maji yanayotiririka na sabuni kwa muda usiopungua sekunde ishirini na ujikaushe kwa tishu utakayoitupa na wala si nguo yako. Kama hauwezi kupata maji basi tumia viua bakteria (sanitizers).

Vaa Barakoa ikiwa Inapatikana
Tafiti zinaonyesha kuwa mask zina uwezowa kusaidia kupunguza maambukizi ya virusi vya Corona, hivyo inashauriwa utumie mask ili kuwalinda wengine haswa kwa wale wenye hofu ya kuwa na maambukizi.

Kinga pua na mdogo kwa tishu wakati wa kupiga chafya
Virusi vya Corona huweza kutoka na matone ya majimaji wakati unapopiga chafya, hivyo unashauriwa usipige chafya sehemu ya wazi au kwenye mikono, bali tumia tishu kavu kupigia chafya na uitupe sehemu husika baada ya hapo na unawe mikono kwa maji na sabuni au utumia sanitizers.