Image
×

Onyo

JUser: :_load: Haiwezi kupakia mtumiaji aliye na kitambulisho: 797

Kudhibiti Kisukari wakati wa mfungo wa Ramadhani

Assalamu’alaikum Warahmutullahi Wabarakatuh. Natumai mu wazima wa afya na mnaendelea vyema na majukumu ya kila siku.

Waumini wa dini ya Kiislam duniani kote wameingia katika mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani. Hivyo,katika muendelezo wa makala zinazohusu kisukari, tunaoenda tujikumbushe au tujifunze mambo machache ya kufanya kabla, wakati na baada ya kipindi takatifu cha mfungo wa Ramadhani.

Tukiwa tuna amini kuwa watu wengi wanaoishi na tatizo la Kisukari hasa aina ya pili ya kisukari wanatamani sana kufunga Ramadhani katika kutimiza moja ya nguzo za imani ya dini ya Kiislam, na kwa imani Funga ni dawa kiroho na kimwili pia.

Jambo la kwanza kwa mtu mwenye kisukari ni kujiweka tayari kwa funga miezi mitatu au minne kabla, kuitayarisha akili na nafsi,hii itakusaidia kuwa mwangalifu sana katika ulaji wako na mfumo mzima wa ulaji.

Kufanya kipimo cha hba1c ni muhimu kwa sababu inaonesha kiwango cha sukari miezi mitatu na hii inakufanya ujue kama utaweza kufunga ramadhan bila kuwa tatizo lolote au hutaweza kufunga. Kupima sukari kabla na baada ya kula kabla ya mfungo wa ramadhani pia ni muhimu,kabla ya kula ni lazima sukari iwe chini ya sita(6) na masaa mawili baada ya kula iwe chini ya nane (8) na kama majibu yatakuwa hivyo kila mara hii itakuonesha kuwa unaweza kufunga bila tatizo.

Jambo la pili ni kuhakikisha unapata ushauri kutoka kwaa daktari wako wa kisukari, Shauriana naye, usiamue kufunga Ramadhani bila ya kushauriana na daktari wako, hii ni muhimu kwa sababu anaweza kukupa ushauri kulingana na kiwango chako cha sukari kwa miezi mitatu nyuma.(hba1c) na kipimo cha sukari cha kila siku unachopima kabla na masaa mawili baada ya kula.

Wakati wa mfungo ni lazima mtu mwenye kisukari atambue kuwa anaweza kufunga baada ya ushauri na ruhusa dakitari wake,na endapo akifunga, ni lazima pia awe anapima kiwango cha sukar kabla ya kuanza ,mfungo,kwa mfano, kabla ya kula daku ni lazima apima,hii itamsaidia kujua kama ataweza kufunga kwa siku hiyo ama Lah, kama akipima na kiwango cha sukari kikiwa sita (6) au saba(7) anaweza kufunga lakini indapo akipima akikuta kwango cha sukar iki chini ya sita (6), labda ni tano(5) au nne (4) hatoweza kufunga kwa sababu moja ya kisababisho cha sukari kushuka ni kukaa bila kula kwa muda mrefu.

Endapo daktari wako wa kisukari amekuhakikishi kuwa unaweza kufunga Ramadhani, haya yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kuftari

  • Pima sukari kabla ya kuftari, hii inasaidia kujua kiwango cha sukari na pia itakusaida jnsi ya kula.  Kama utakuta sukari imeshuka ipo chini ya nne (4) unaweza kula chochote hata juisi ili tu kuipandisha. Na kama ipo juu ya 4,5,6,7 unaweza kumeza dawa kasha ukaftari kwa utaratibu wa kila siku.
  • Ulaji wa tende wakati wa kuftari

          Kwa mwenye kisukari anaruhusiwa kula tende endapo tu kiwango cha sukari kinamruhusu,kama sukari yake ipo 4 au 5 bado anaweza kula tende kwa kiasi kidogo, labda mbegu tatu au nne labda na maji au maziwa.

  • Ulaji wa Matunda
  • Utaratibu wa kuftari ufuate mpangilio wa kula,

Angalizo 1: Usifutari mchanganyiko wa wanga kwa wakati mmoja, mfano,muhogo,tambi, viazi,na uji, hivyo vyote ni wanga na kazi yake ni moja tu, na pia usifutari vyakula vilivyowekwa sukari,mfano, viazi vilivyowekwa sukari na  maharage yaliyowekwa sukari na uji ambayo pia umewekwa sukari. Unaweza kuftari, kama mihogo kidogo,au viazi kidogo,mahagare amabayo hayana sukari, mbogamboga au kachumbali, na kikombe cha chai au maziwa badala ya uji(uji pia ni wanga)

Kama kawada ya mpangilio wa mlo kwa wenye kisukari, tunda huliwa saa moja au masaa mawili baada ya chakula, na wakati wa mfungo pia,mpangilio huu lazima ufuate, futari ni saa kumi na mbili joini, tunda liliwe saa mbili au saa tatu ya usiku, na sio matunda, liliwe tunda ya aina moja tu,kama tunda la umbo dogo,chungwa, chenza, tufaa, peasi, ni moja tu na kwa matunda yenye maumbo makubwa, papai, nanasi, embe dodo, tikiti maji, ni kipande kidogo tu.

  • Pima masaa mawili baada ya kuftari au kabla hujalala
  • Pima kabla ya kula daku na kabla siku hajaanza(siku mpya ya kufunga)
  • Ulaji wa daku wa wenye kisukari usihusishe chakula kizito.

Angalizo 2: Makala hii sio tu kwa watu wenye Kisukari peke yao, Lah hasha. Hii ya kwa kila mmoja  katika jamii yetu, baada ya mfungo kwesha wengi huongezeka uzito wa miili yao, ukifikiria kwa kina mpangilio wa ulaji kipindi cha Ramadhan hubadilika sana,kipindi hiki ulaji wa vyakula vya wanga na sukari huliwa kwa wingi na bila mpangilio.Kuna athari moja kubwa ambayo hujitokeza baada ya mfungo kuisha ambayo ni:

  • Kuongezeka kwa uzito wa mwili kwa haraka ( ulaji wa vyakula vya wanga na sukar huongeza uzito kwa haraka na ni rahisi kupata maradhi ya moyo na kisukari)

kwa kumaliza, napenda kuwakumbusha kuwa kipindi cha mfungo ni kipindi takatifu kurudi kwa Allah basi ni lazima kufanya yale yote mema tuliyohusiwa na Allah na pia kuyaendeleza mara baada ya mfungo, Tumwombe Allah atufanyie wepesi katika kila jambo na aponye maradhi yanayotukabiri.

NAWATAKIA MFUNGO MWEMA WA MEZI MTUKUFU WA RAMADHANI.

 

Reviewed by Dr Khamis Bakari

Imesomwa mara 3873 Imehaririwa Jumatano, 14 Aprili 2021 11:14
Lucy Johnbosco

Diabetes Consciousness for Community is focusing on raising Diabetes awareness and healthy lifestyle

https://dicoco.or.tz | Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.