Image

Je,Kujamiana Huondoa Msongo wa Mawazo kwa Wanawake?

Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha State University cha Jijini New York nchini Marekani umesema ya kwamba manii ni nzuri kwa wanawake kwani huwaondolea msongo wa mawazo.Pia watafiti hao wamesema wanawake wanaofanya tendo la ndoa mara kwa mara bila kutumia kinga (mapenzi salama) wanakuwa na kiwango idogo cha msongo wa mawazo na hufanya vizuri katika vipimo vya akili.

Hali hii wamesema inatokana na manii kuwa na kemikali ambazo humfanya mtu kuwa vizuri kihisia, huongeza upendo/unyenyekevu, huchochea mtu kupata usingizi na huwa na angalau aina tatu za kemikali za kuondoa msongo wa mawazo (anti-depressants).
Utafiti huo uliofanywa kwa kuwahoji wanawake 293 kwa kufuatilia maisha yao ya kujamiana dhidhi ya afya za akili zao (mental health).Manii huwa na mchanganyiko wa kemikali aina ya cortisol ambayo huongeza upendo, kemikali aina ya esterone na oxytocin ambazo zote humfanya mtu kuwa vizuri  kihisia (elevates mood).
Pia huwa na homoni aina za thyrotropin releasing hormone ambayo huondoa msongo wa mawazo, melatonin ambayo huchochea usingizi na serotonin homoni inayoondoa msongo wa mawazo.
Kutokana kuwepo kwa mchanganyiko wa kemikali na homoni hizo kwenye manii, watafiti  Gallup na Burch pamoja na mtaalamu wa saikolojia  Steven Platek wamesema ya kwamba wanawake ambao hujamiana na wanaume bila kinga yoyote (mapenzi salama) wana asilimia ndogo ya msongo wa mawazo tofauti na wale wasiojamiana.
Matokeo muhimu ya utafiti huu ambao umechapishwa katika jarida la Archives of Sexual Behavior ni kwamba hata baada ya baadhi ya watafitiwa kuongeza kiwango chao cha kujamiana, wale ambao walikuwa hawatumii kinga yoyote walikuwa na kiwango kidogo cha msongo wa mawazo tofauti na wale ambao walikuwa wakitumia kinga kama kondomu wakati wa kujamiana.Pia wanawake hawa ambao hawakutumia kinga walikuwa na kiwango kidogo cha msongo wa mawazo tofauti na wale ambao hawakushiriki tendo la ndoa kabisa.
Hata wale wanawake ambao ni wasagaji na wana wapenzi wengi pia wameonekana kuwa na kiwango kikubwa cha msongo wa mawazo  kama wale wanawake ambao hawakushiriki tendo la ndoa kabisa.
Watafiti hao wamesema sio tu kujamiana huongeza furaha kwa mwanamke na hivyo kumuondolea msongo wa mawazo bali kiwango cha furaha pia huendana na wingi wa manii katika mili yao.
Utafiti huu usiwe chanzo cha watu kufanya mapenzi bila kinga bali uwe chanzo cha ufanya mapenzi salama na mwenza unayemuamini.Pia tunakemea na kupinga wale wote wanaofanya vitendo vya usagaji kwani ni hatari kwa afya zao kwani ni chanzo kimojawapo cha magonjwa ya akili.Tutakuletea makala ya uhusiano kati ya usagaji na ugonjwa wa akili.
 
Imesomwa mara 33396 Imehaririwa Ijumaa, 25 Agosti 2017 07:19
Dr Khamis

Dr. Khamis H.Bakari (MD PhD) ni daktari bingwa,mhadhiri katika chuo cha afya cha Chuo  Kikuu cha Dodoma,mtaalamu wa Tiba na Uchunguzi kwa kutumia mionzi ya nyuklia (Nuclear medicine).

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

Makala shabihana