Image

Kwa muda mrefu sana wanawake wamekuwa wakitumia parachichi kama nyenzo mojawapo ya urembo ima kwa kupaka kwenye uso au nywele bila kuwa na uhakika kama kweli parachichi husaidia katika kurutubisha nywele na ngozi ya kwenye uso.

Swali ni je ni wangapi wanajua faida za parachichi kiafya, hususani faida ya kuukinga mwili dhidhi ya kemikali hatari pamoja na kumfanya mtu kuonekana kijana?

Wanasayansi wa chuo kikuu cha Michoacana de San Nicolas de Hidalgo cha nchini Mexico wamesema ya kwamba parachichi husaidia katika kuukinga mwili dhidhi ya kemikali hatari (free radicals) na hivyo kuweka kinga dhidhi ya magonjwa mengi pamoja na kumfanya mtu kuonekana kijana (fight against ageing). Wanasayansi hao wamesema kwamba mafuta yanayopatikana katika parachichi yanauwezo wa kupenya hadi ndani ya injini inayotengeneza nishati mwilini inayopatikana katika seli inayojulikana kama mitochondria.

Free radicals ni kemikali zinazosababisha magonjwa mengi yakiwemo baadhi ya saratani, huharibu mishipa ya damu ya ateri (arteries), pamoja na kumfanya mtu kuzeeka haraka. Mafuta yanayopatikana katika baadhi ya mboga za majani, matunda na nyanya/tungule (tomatoes) yanauwezo wa kupambana na kemikali hizi hatari lakini mafuta haya hushindwa kuingia ndani ya mitochondria ambapo ndio kuna kemikali hizi hatari kwa wingi.

Mtafiti Christian Cortes-Rojo kutoka chuo kikuu hicho cha Mexico ambaye ndiye alifanya utafiti huu, alisema ‘’Anti-oxidants zinazopatikana katika mboga za majani na matunda mengi haziwezi kupenya ndani ya mitochondria na hivyo kushindwa kudhibiti kemikali hatari ndani ya mitochondria hizo. Hivyo kusababisha kemikali hizo hatari kuendelea kushambulia mitochondria na kuziharibu, matokeo yake ni kuwa nishati haitolewi tena kutoka kwenye mitochondria na seli hushindwa kufanya kazi na kufa.”

Avocado Mask

Kwa muda mrefu sana wanawake wamekuwa wakitumia parachichi kama nyenzo mojawapo ya urembo ima kwa kupaka kwenye uso au  nywele bila kuwa na uhakika kama kweli parachichi husaidia katika kurutubisha nywele na ngozi ya kwenye uso, swali ni je ni wangapi wanajua faida za parachichi kiafya, hususani faida ya kuukinga mwili dhidhi ya kemikali hatari pamoja na kumfanya mtu kuonekana kijana?

Wanasayansi wa chuo kikuu cha Michoacana de San Nicolas de Hidalgo cha nchini Mexico wamesema ya kwamba parachichi husaidia katika kuukinga mwili dhidhi ya kemikali hatari (free radicals) na hivyo kuweka kinga dhidhi ya magonjwa mengi pamoja na kumfanya mtu kuonekana kijana (fight against ageing). Wanasayansi hao wamesema kwamba mafuta yanayopatikana katika parachichi yanauwezo wa kupenya hadi ndani ya injini inayotengeneza nishati mwilini inayopatikana katika seli inayojulikana kama mitochondria.

Utangulizi

Saratani ya koo ni miongoni mwa magonjwa ya kutisha. Ingawa baadhi ya wagonjwa wa saratani ya koo wanaweza kutibiwa na kupona kabisa, kuna mjadala miongoni mwa matabibu juu ya tiba sahihi ya ugonjwa huu. Bila kujali ni aina gani inayotumika, karibu aina zote za tiba za saratani hii huwa na madhara kwa mgonjwa na wakati mwingine kusababisha kifo badala ya kuponya.

Muundo wa Koo

Ili tuweze kujadili vizuri ugonjwa huu, ni vema kwanza tuangalie muundo wa koo. Koo ni sehemu mojawapo ya mfumo wa chakula likiwa na urefu wa takribani sentimita 25 kuanzia mdomoni mpaka kwenye mfuko wa tumbo yaani stomach.

Ukuta wa koo unajengwa na tando (layers). Tando hizi zimetengenezwa kwa aina tofauti ya chembe hai au seli ambazo kila moja ina kazi zake maalum. Sehemu ya ndani kabisa ya ukuta wa koo huitwa mucosa ambayo hufanya kazi ya kulowanisha chakula ili kiweze kupita vizuri kuelekea kwenye mfuko wa chakula.

Chini ya utando huu, kuna utando mwingine unaoitwa submucosa ambao umejaa tezi zenye kuzalisha ute unaoitwa mucus ulio na kazi ya kulainisha koo na kulifanya liwe na hali ya umajimaji muda wote. Utando wa tatu unajulikana kama muscle layer. Utando huu umejaa misuli inayosaidia koo kusukuma chakula kuelekea tumboni. Utando wa juu kabisa unaolizunguka koo huitwa outer layer ambao una kazi ya kulinda koo kwa ujumla.

Tunashukuru kwa mtandao kwani habari zinasambaa haraka kama mwanga. Hata hivyo, uvumi, imani potofu vinasambaa kwa kasi ile ile pia. Hii inahusisha imani potofu kuhusu afya ya kinywa na meno. Kwa hiyo,

Nafikiri ni bora kuchukua muda kidogo kuweka baadhi mambo sawa kuhusu afya ya kinywa na meno.

Baadhi ya imani potofu ni kama ifuatavyo

POTOFU: Kupiga mswaki mara nyingi na kwa nguvu huzuia kuoza kwa meno

UKWELI: Si mara ngapi unapiga mswaki na nguvu gani inatumika, suala ni unapigaje mswaki. Kupiga mswaki mara nyingi na kwa maguvu kunaweza kupelekea kukwangua sehemu ngumu ya nje ya jino, kulifanya laini na hatimaye kuuma au hata kuvunjika. Kupiga mswaki mara mbili, taratibu na kwa njia sahihi ndicho kinachosaidia meno kuwa na afya

POTOFU: Huna haja ya kumuona tabibu wa meno kama hujaona au kuhisi una tatizo la meno.

UKWELI: Kila mtu anatakiwa kumuona tabibu wa meno angalau mara mbili kwa mwaka bila kujali meno yake yanaonekana vizuri au imara kiasi gani.Si meno yote yanayoonekana mazuri na imara ni mazima, mengine yanaweza kuwa yameoza katika maeneo usiyoweza ona kama chini ya fizi na kwenye mizizi, si hivyo tu hata uoto mpya (neoplasm) uweza kugundulika mapema kabla ya kufanya uaribifu mkubwa kama utachunguzwa na wataalamu. Kumbuka pia mangonjwa ya mifumo mingine kama ukimwi, kisukari na mengine mengi hujidhihirisha mapema kinywani kabla mgonjwa hajapata dalili zingine.

Neno syndrome humaanisha mkusanyiko wa dalili au magonjwa kadhaa ili kufanya ugonjwa mmoja.

Ugonjwa wa Nephrotic syndrome ni hali ya maradhi inayokumba figo na kusababisha kupoteza kiasi kingi cha protini kutoka kwenye damu kuingia kwenye mkojo. Kiasi cha protini kinachopotea ni wastani wa gram 3.5 kwa siku kwa kila mita za mraba 1.73 za mwili.

Chujio za figo (glomeruli) huwa na vitundu vidogo vidogo viitwavyo podocytes ambavyo hufanya kazi ya kuchuja uchafu na sumu nyingine kutoka mwilini na kuzitoa nje. Vitundu hivi vina uwezo wa kuzuia protini isichujwe kuingia kwenye mkojo. Hata hivyo, figo zenye Nephrotic syndrome huwa na podocytes kubwa kiasi cha kuweza kupitisha protini za ukubwa mbalimbali (zikiwepo albumin ambazo ni protini zenye kipenyo kikubwa zaidi). Pamoja na kuharibika huku kwa chujio, podocytes bado hazina ukubwa wa kuweza kupitisha seli nyekundu za damu ndiyo maana mkojo wa mgonjwa wa Nephrotic syndrome hauna damu ndani yake.

Ukubwa wa tatizo

Nephrotic syndrome huathiri karibu watu wa rika zote. Hata hivyo watoto walio katika umri wa miaka 2 mpaka sita ndiyo waathirika wakuu wa ugonjwa huu. Ugonjwa huu umeonekana kuwapata zaidi watoto wa kiume kuliko wa kike.

Visababishi vya Nephrotic syndrome

Visababishi vya Nephrotic syndrome vimegawanyika katika makundi mawili; yale yanayosababishwa na magonjwa yaliyo ndani ya figo zenyewe (primary nephrotic syndrome), au yale yanayosababishwa na magonjwa yaliyo nje ya figo (secondary nephotic syndrome).

Raia mmoja nchini Italia mwenye umri wa miaka 71 alipata mishtuko ya mioyo yake yote miwili na kupoteza fahamu kwa sekunde kadhaa lakini hatimaye aliweza kuokolewa maisha yake. Mtu huyo alikimbizwa katika hospitali ya Verona nchini Italia baada ya kupata maumivu ya kifua na mapigo ya mioyo yake kuwa si ya kawaida.

Taarifa kutoka jarida la American Emergency Medical Journal inaeleza kuwa mtu huyo aliwahi kufanyiwa upasuaji wa moyo na kupandikizwa moyo mwingine miaka kadhaa iliyopita katika upasuaji unaojulikana kama double heart transplant (heterotopic heart transplantation).

Hii ni aina ya upasuaji ambapo moyo hupandikizwa na kufanya kazi sambamba na moyo wa awali (wa mgonjwa mwenyewe) ambao huwa umeadhirika kutokana na maradhi. Chemba za damu za kwenye mioyo hiyo huunganishwa ili moyo uliopandikizwa uweze kusaidia moyo wa mgonjwa.

Ripoti zinasema kuwa moyo mmoja ulianza kuwa na nguvu zaidi kuliko mwingine na hivyo kusababisha mapigo yake kutofautiana na mwingine. Madaktari walijaribu kurekebisha mapigo ya mioyo hiyo ili yaendane sawa kwa kutumia dawa lakini mioyo hiyo iliacha kupiga kabisa na mtu huyo kuacha kupumua.

Hata hivyo, waliweza kumrejesha katika hali ya kupumua kwa kutumia kifaa maalum cha Defibrillator kabla ya kumfanyia upasuaji na kubadilisha kifaa kinachosaidia kuweka sawa mapigo ya moyo kinachojulikana kama pacemaker.

 

Kuharibika kwa chujio ama Glomerulonephritis ni aina ya ugonjwa wa figo unaoathiri sehemu maalum ya figo (chujio) inayohusika na uchujaji wa maji pamoja na uchafu kutoka katika damu. Sehemu hii huitwa glomelurus au chujio kama tutakavyokuwa tukitumia katika mada hii.
Visababishi
Mara nyingi chanzo halisi cha kuharibika kwa chujio za figo (glomerulonephritis) huwa hakijulikani. Hata hivyo wakati mwingine uharibifu huu unaweza kusababishwa na kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili. Uharibifu katika chujio husababisha damu pamoja na protini kuingia katika mkojo.
Tatizo hili hukua kwa haraka na figo linaweza kupoteza uwezo wake wa kuchuja maji na uchafu kwa kasi ndani ya muda mfupi wa kati wiki chache mpaka miezi kadhaa. Aina hii ya kuharibika kwa chujio za figo kwa haraka hujulikana kitalaamu kama rapidly progressive glomerulonephritis.
Ukubwa wa tatizo na vihatarishi vyake
Takribani robo ya watu wanaopatwa na tatizo sugu la glomerulonephritis huwa hawana historia ya kuwa na ugonjwa wowote wa  figo hapo kabla.
Kuna mambo kadhaa yanayoweza kumfanya mtu awe katika hatari ya kupata glomerulonephritis. Mambo hayo ni pamoja na:
•Matatizo katika mfumo wake wa damu au lymph
•Kuwahi kutumia vimiminika vilivyotengenezwa kwa kemikali za hydrocarbon
•Wenye historia ya saratani
•Maambukizi ya bacteria aina ya streptococcus, virusi, majipu au maambukizi katika moyo 
Mambo mengine yanayoweza kuongeza hatari ya kupatwa na glomerulonephritis ni pamoja na:
•Magonjwa ya mishipa ya damu kama vile vasculitis au polyarteritis
•Matumizi yaliyopitiliza ya dawa za kutuliza maumivu za jamii ya Non steroidal anti-inflammatory drugs kama vile aspirin
•Magonjwa ya mfumo wa kinga ya mwili kama vile Anti-glomerular basement membrane antibody disease na IgA nephropathy
•Makovu katika chujio (Focal segmental glomerulosclerosis) au hali ya chujio kuwa na kuta nene kuliko kawaida (Membranoproliferative GN)
•Magonjwa yanayoathiri viungo mbalimbali vya mwili kama vile Henoch-Schonlein purpura, Goodpasture’s syndrome au Lupus nephritis 
•Ugonjwa wa kimetaboliki wa Amyloidosis
Dalili
Dalili kuu za glomerulonephritis ni kuwa na damu katika mkojo (hali inayoufanya mkojo kuwa na rangi kama nyeusi, kutu au samawati; mkojo kuwa kama wenye povu jingi (kwa sababu ya kuwa na protini nyingi kuliko kawaida) na kuvimba uso, macho, miguu au tumbo (hali inayojulikana kama edema)
Dalili nyingine ni pamoja na 
•Maumivu ya tumbo 
•Kutapika damu 
•Kuharisha au kupata choo kikubwa chenye kuchanganyika na damu 
•Kukohoa pamoja na kupumua kwa shida
•Kukojoa kupita kiasi 
•Homa
•Maumivu ya misuli na viungo, uchovu, maumivu ya mwili mzima pamoja na kukosa hamu ya kula 
•Kutokwa na damu puani
Baada ya muda, figo hushindwa kufanya kazi na mgonjwa huanza kuwa na dalili za mtu mwenye ugonjwa sugu wa figo.
Uchunguzi na vipimo
Kwa kawaida tatizo la uharibifu wa chujio za figo hutokea tatratibu sana hali inayoweza kufanya ugunduzi wake kuchelewa pia. Wengi wa wagonjwa wenye tatizo hili hugunduliwa pale wanapokwenda hospitali kwa ajili ya uchunguzi wa matatizo mengine. Mara nyingi hali hii hujifhihirisha kwa kuwepo na hitilafu katika kipimo cha urinalysis.  
Mambo makuu matatu yanaweza kuonesha kuwepo kwa uharibifu katika chujio za figo. Mambo hayo ni upungufu wa damu (anemia), shinikizo la damu kuwa juu na ishara za kupungua kwa utendaji kazi wa figo.
Vipimo vinavyoweza kufanywa hujumuisha vipimo vya mkojo, damu pamoja na picha kama vile Ultrasound, CT au SPECT/CT.
Vipimo vya mkojo kama vile urinalysis husaidia kuonesha:
•Utendaji kazi wa figo yaani Creatinine clearance pamoja na Urine creatinine
•Uchunguzi wa mkojo kwa kutumia hadubini
•Kiasi cha protini katika mkojo 
•Kiasi cha tindikali ya urea katika mkojo 
•Chembe nyekundu za damu (RBC) katika mkojo 
Specific gravity ya mkojo na kiasi cha chumvi kwenye mkojo (yaani urine osmolality)
Vipimo vingine ni pamoja na CT scan, ultrasound ya figo, X-ray ya kifua au Intravenous pyelogram (IVP)
Vipimo vya damu husaidia kuonesha:
•Kiasi cha protini ya albumin katika damu
•Utendaji kazi figo kuchunguza kiasi cha BUN na creatinine katika damu
•Viasili vinavyohusika katika mfumo wa kinga ya mwili kama vile Anti-glomerular basement membrane antibody, Anti-neutrophil cytoplasmic antibodies (ANCAs), Anti-nuclear antibodies au Complement levels.
Ili kuthibitisha uwepo wa tatizo hili na aina yake, kipimo cha biopsy (renal biopsy) hutumika. 
Matibabu
Matibabu ya glomerulonephritis hutegemea sana na kisababishi cha tatizo hili, aina yake pamoja na ukubwa wa tatizo lenyewe yaani wingi wa dalili pamoja na uzito wake. Dalili ya muhimu sana kuithibiti ni ongezeko la shinikizo la damu ingawa kwa kawaida huwa ni ngumu sana kuthibiti shinikizo la damu kuwa katika kiwango cha kawaida.
Mgonjwa anashauriwa pia kupunguza kiasi cha chumvi katika chakula chake na pia kiasi cha protein na maji anayokunywa ili kusaidia utendaji kazi wa figo. 
Dawa zinazoweza kutumika kwa mgonjwa mwenye tatizo hili ni pamoja na:
•Zile za kushusha na kuthibiti shinikizo la damu hususani za jamii ya Angiotensin-converting enzyme (ACE) inhibitors kama vile captopril, Lisinopril au Enalapril; na zile za jamii ya Angiotensin receptor blockers kama vile losartan, Valsartan na Irbesartan.
•Zile za jamii ya Corticosteroids kwa ajili ya kupunguza na kuondoa mcharuko mwili
•Zile za kupunguza nguvu ya mfumo wa kinga ya mwili
Iwapo dawa za kupunguza nguvu ya kinga ya mwili zimeshindwa kufanya kazi na kuna uthibitisho kuwa glomerulonephritis imesababishwa na mashambulizi ya seli za kinga ya mwili katika figo, mgonjwa anaweza kufanyiwa tiba inayoitwa plasmapheresis. Katika tiba hii, sehemu ya damu yenye seli za kinga ya mwili zijulikanazo kama antibodies huondolewa kwa kubadilishwa na maji maji (plasma) yasiyo na antibodies zozote zile. Kuondoa antibodies husaidia kupunguza mcharuko mwili na uharibifu zaidi katika chujio za figo.
Iwapo figo zitashindwa kufanya kazi kabisa, mgonjwa anaweza kuhitaji kufanyiwa dialysis au kupandikizwa figo mpya.
Matarajio
Kuharibika kwa chujio za figo kunaweza kuwa ni tatizo la muda na lenye kurekebishika au linaweza kudorora na kuwa la kudumu. Kudorora kwa chujio za figo kunaweza kusababisha kupungua kwa utendaji kazi wa figo au ugonjwa sugu wa figo kushindwa kufanya kazi (chronic renal failure), au kufa kabisa kwa figo zote ( end-stage renal disease). 
Madhara
Pamoja na kusababisha shinikizo la damu kuwa juu, uharibifu katika chujio za figo unaweza pia kusababisha mlinganyo usio sawa wa madini katika damu (electrolytes imbalance) kama vile ongezeko la madini ya potassium (hyperkalemia); maambukizi yanayojirudia katika njia ya mkojo, uwezekano wa kupata maambukizi ya mwili, mrundikano wa maji mwilini hali inayoweza kusababisha moyo kushindwa kufanya kazi (congestive heart failure) au maji kujaa katika mapafu (pulmonary edema); au ugonjwa wa figo ujulikanao kama Nephrotic syndrome (utaelezwa katika makal zijazo). 
Kinga
Inawezekana kuzuia uharibifu wa chujio za figo kwa baadhi ya watu ingawa, kwa ujumla ni ngumu kufanya hivyo. Baadhi ya mambo ya kufanya ili kuepuka kupatwa na tatizo hili ni pamoja na kuepuka matumizi ya vimiminika vyenye kemikali za hydrocarbons, matumizi ya madini ya zebaki pamoja na matumizi ya muda mrefu ya dawa za jamii ya nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs) kama vile Aspirin.

Huu ni ugonjwa unaoathiri zaidi ndege wa jamii mbalimbali. Hata hivyo virusi wanaosababisha ugonjwa huu, wana uwezo wa kujibadilisha umbo na tabia zake (mutation) na kisha kumuathiri mwanadamu. Mabadiliko haya ya kimaumbile na kitabia husababisha kutokea kwa milipuko (epidemic) ya mafua ya ndege sehemu mbalimbali duniani hali ambayo isipothibitiwa inaweza kusambaa na kuathiri sehemu kubwa ya dunia kwa wakati mmoja (pandemic).

Visababishi vya mafua ya ndege

Mafua ya ndege husababishwa na jamii ya virus wajulikanao kama Avian Influenza virus. Virusi vya kwanza kabisa kumuathiri binadamu na kumsababishia mafua ya ndege vilihusishwa na kuku na viligunduliwa mwaka 1997 huko nchini Hong Kong na kupewa jina la avian influenza A (H5N1). Huu ulikuwa ni mlipuko wa kwanza wa ugonjwa huu kuwahi kuripotiwa. Kuna matukio machache sana ya maambukizi kutoka kwa binadamu kwenda binadamu yaliyowahi kuripotiwa mpaka sasa.

Influenza virus ni nini?

Kuna aina kuu tatu za virusi wa influenza, A, B na C. Mafua ya ndege husababishwa na jamii ya influenza A ambao wana uwezo wa kuingia na kuishi katika seli za ndege. Umbo la kinasaba la virusi hawa wa influenza A limeundwa na kamba nane za protein aina ya RNA.

Aidha virus wa Influenza wanaweza pia kuainishwa kulingana na aina ya protein inayounda maumbo yao. Protini hizo zipo katika aina mbili nazo ni hemagglutinin (H) pamoja na neuraminidase (N). Protini hizi zina kazi mbalimbali katika umbo la virusi. Kadhalika protini hizi nao pia zimeganyika katika aina mbali, ambapo virusi hatari wa mafua ya ndege wanaundwa na aina ya 5 ya protin ya hemagglutinin na aina ya 1 ya protini ya neuraminidase na hivyo ndiyo maana hujulikana kama H5N1 influenza A virus.

Hii ni aina ya saratani inayokumba tezi ya thyroid. Ikumbukwe kuwa tezi ya thyroid ipo sehemu ya mbele ya shingo ya mwanadamu ikiwa na sehemu mbili (lobes) moja kila upande wa shingo.

Visababishi na ukubwa tatizo

Saratani ya thyroid huwapata watu wa umri mbalimbali, kuanzia watoto mpaka watu wazima. Watu waliowahi kupigwa mionzi sehemu ya mbele ya shingo wapo katika hatari kubwa ya kupata aina hii ya saratani. Kadhalika watu wazima ambao waliwahi kupigwa mionzi kipindi cha utotoni nao pia wana hatari kubwa zaidi ya kupata saratani ya thyroid hata kama hawakuwahi kupata tatizo hilo wakati wanakua.

Tiba ya mionzi maeneo ya shingoni ilikuwa ikitumika sana zamani kwenye miaka ya 50 mpaka 60 kwa ajili ya matibabu ya uvimbe wa tezi ya thymus, mafindofindo (tonsils), au baadhi ya magonjwa ya ngozi. Hata hivyo ni nadra sana kwa tiba hii kutumika katika zama hizi.

Vihatarishi vingine vya saratani ya tezi ya thyroid ni pamoja na kuwepo kwa historia ya tatizo hili miongoni mwa wanafamilia na kuwa na goita iliyodumu muda mrefu bila kutibiwa.

Aina za saratani ya tezi ya thyroid

Kulingana na aina ya seli zinazounda tezi ya thyroid zinazoshambuliwa, saratani ya thyroid inaweza kugawanywa katika aina zifuatazo

Gauti (Gout) ni aina ya ugonjwa unaoathiri viungo vya mwili unaosababishwa na kuwepo kwa kiasi kikubwa kuliko kawaida cha tindikali ya Urea (uric acid) katika damu.

Ongezeko la uric acid husababisha madhara katika jointi (joint) (joint ni sehemu ya mwili inapokutana/ inapoungana mifupa miwili). Gauti inaweza kutokea ghafla (acute gout) au ikawa sugu (chronic gout). Gauti inayotokea ghafla huwa na maumivu makali na mara nyingi huathiri jointi moja tu wakati gauti sugu inaweza kuathiri jointi zaidi ya moja na huambatana na hali ya kujirudia ya maumivu na uvimbe kwenye jointi.

Visababishi

Gauti husababishwa na kuwepo kwa kiwango kikubwa kuliko kawaida cha uric acid katika damu. Hali hutokea iwapo mwili  wa mgonjwa unatengeneza uric acid nyingi kuliko kawaida au unashindwa kutoa uric acid mwilini kama inavyotakiwa.

Ongezeko hili husababisha mrundikano wa uric acid katika maji maji yanayozunguka jointi yanayoitwa synovial fluid na hatimaye kutengeneza vijiwe vidogo vidogo vya tindikali ya urea yaani uric acid crystals ambavyo husababisha jointi kuvimba na hatimaye kuathirika.

Vihatarishi (risk factors)

Ingawa chanzo hakieleweki vema, ugonjwa wa gauti hutokea kuwapata baadhi ya watu walio katika familia moja. Wanaume huathiriwa zaidi kuliko wanawake ingawa wanawake waliokoma kupata hedhi huathiriwa zaidi kuliko wale wanaoendelea kupata hedhi.

Aidha unywaji pombe unachangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa ugonjwa huu pamoja na matumizi ya baadhi ya madawa kama vile dawa za kutoa maji mwilini ambazo kwa ujumla husababisha ongezeko la kiwango cha uric acid katika damu.

Vihatarishi vingine vya gauti ni pamoja na kuwa na ugonjwa wa kisukari, magonjwa ya figo, unene uliopitiliza, ugonjwa wa sickle cell anemia au aina nyingine za upungufu wa damu, pamoja na saratani ya damu (leukemia).

Hali kadhalika, gauti inaweza kusababishwa na matumizi ya dawa ambazo utendaji wake kazi huingiliana na utoaji wa uric acid mwilini.

Dalili

  • Dalili za gauti kwa kawaida uhusisha jointi moja au joint chache. Jointi zinazoathiriwa zaidi ni pamoja na kidole kikubwa ha mguuni, magoti, au kiwiko cha mguu.
  • Wagonjwa huwa na maumivu yanayoanza kwa ghafla hususani nyakati za usiku. Mara nyingi mgonjwa hudai anasikia maumivu makali kama kitu kinachokata, kupwita au mifupa inayosagana.
  • Jointi hubadilika na kuwa na joto, kuvimba na kuwa na nyekundu (hujionesha zaidi kwa watu wenye ngozi nyeupe). Kwa kawaida mgonjwa hulalamika maumivu makali ikiwa ataguswa kwenye jointi yenye matatizo.
  • Shambulio linaweza kudumu kwa siku kadhaa kabla mgonjwa hajapata nafuu, lakini pia laweza kujirudia mara kwa mara.
  • Pia mgonjwa anaweza kujihisi homa.

Baadhi ya wagonjwa hupata gauti sugu ambayo huwaletea madhara sugu katika jointi (chronic arthritis) hali ambayo husababisha mgonjwa kujihisi maumivu na muda mwingi kushindwa vizuri kutumia jointi zake. Wagonjwa wenye gauti kwa muda mrefu huwa pia na vinundu chini ya ngozi inayozunguka jointi zilizoathirika. Vinundu hivi kwa kitaalamu huitwa trophy na ni ishara ya muhimu kwa madaktari.

Vipimo

Vipimo vya gauti hujumuisha

  • Kiwango cha uric acid katika damu. Hata hivyo, si kila aliye na kiwango kikubwa cha uric acid katika damu huwa na gauti.
  • Kiwango cha uric acid katika mkojo
  • Uchunguzi wa maji maji yanayozunguka jointi (synovial fluid) kuchunguza vijiwe katika jointi
  • X ray ya jointi iliyoathirika
  • Uchunguzi wa utando unaozunguka jointi (synovial biopsy)

Matibabu

Matibabu ya gauti hujumuisha matumizi ya dawa, lishe pamoja na mabadiliko katika mfumowa maisha wa mgonjwa.
Dawa hutumika mara tu mgonjwa anapopata shambulio la ghafla. Dawa hizo ni pamoja na

  • Dawa za kutuliza maumivu kama vile codeine, paracetamol
  • Dawa za kutuliza mcharuko mwili (nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs) kama vile ibuprofen (brufen), indomethacin (indocid), diclofenac n.k. Pia ni muhimu mgonjwa kumfahamisha daktari wake iwapo ana matatizo yasiyoendana na matumizi ya dawa hizi kama vile vidonda  vya tumbo au mzio.

Dawa hizo husaidia kupunguza maumivu, uvimbe, na mcharuko mwili (inflammation). Baadhi ya madaktari huchoma sindano dawa ya corticosteroids kwenye jointi iliyoathirika kwa ajili ya kupunguza maumivu na uvimbe. Kwa kawaida maumivu huondoka saa 12 baada ya kuanza matibabu, na mgonjwa hupata nafuu kamili baada ya saa angalau 48.

Ili kupunguza kiwango cha uric acid katika damu, mgonjwa hupewa dawa za allopurinol au probenecid kila siku. Wagonjwa wanaotumia dawa hizi ni wale ambao hupata mashambulizi ya mara kwa mara ndani ya mwaka au wale ambao hupata mashambulia makali, wagonjwa waliopata madhara mkubwa kwenye jointi, wagonjwa walio na vinundu (trophy) au wagonjwa wenye vijiwe vya uric katika figo.

Lishe na mabadiliko katika mfumo wa maisha husaidia pia kuthibiti na kumuepusha mgonjwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya gauti. Njia hizi ni pamoja na:

  • Kuacha kunywa pombe
  • Kupunguza ulaji wa vyakula vyenye viasili vya purine (aina ya protini) kama vile nyama ya mbuzi, samaki jamii ya sardines na herring, nyama ya maini au figo, mkate mtamu, maharage yaliyokaushwa, njegere, baadhi ya aina za uyoga, spinachi, n.k.
  • Thibiti pia ulaji wa nyama kwa kila mlo unaokula
  • Jiepushe na matumizi ya vyakula vya mafuta kama vile ice creams, mayonise au vyakula vya kuokwa
  • Kula kiasi kikubwa cha wanga
  • Iwapo utaamua kupunguza uzito, hakikisha unapunguza kidogo kidogo kwa sababu upunguzaji wa kasi unaweza kusababisha vijiwe vya uric kujitengeneza katika figo

Matarajio

Wagonjwa wanaofuata masharti na ushauri wa daktari huweza kuishi maisha ya kawaida. Hata hivyo, ni vema kufahamu kuwa mara nyingi gauti ya ghafla hatimaye huwa gauti sugu.

Madhara ya gauti

  • Gauti inaweza kusababisha matatizo sugu kwenye jointi (chronic gouty arthritis)
  • Vijiwe katika figo
  • Mrundikano wa uric acid unaoweza kusababisha ugonjwa sugu wa figo

Kinga

Kwa kawaida gauti haizuiliki, hata hivyo mgonjwa anashauriwa sana kujiepusha na vitu vinavyoweza kuchochea shambulizi na dalili za ugonjwa huu (rejea lishe na mabadiliko katika mfumo wa maisha hapo juu).

Ukurasa 9 ya 11