Image

Ushauri

Je una tatizo la kitabibu linalohitaji ushauri wa daktari? TanzMED inakuletea nyenzo ya ushauri. Kwa kutumia simu yako, unaweza kuwasiliana na kupata ushauri wa kitabibu moja kwa moja kutoka kwa madaktari bingwa waliopo pande mbalimbali za nchi na dunia nzima.

Nyenzo hii ina hatua mbili, kabla ya kuunganishwa na daktari, utakutana na Dokta Kiteko, hii inatumia technolojia ya Artificial Intelligency (AI) kwa kupitia taarifa zako na taarifa nyingine nyingi zenye kuendana na wewe ili kutengeneza muelekeo (patern) ambayo itaweza kubashiri nini kinachokusumbua na machine (Dr Kiteko) itakushauri.

Baada ya kutumia Dokta Kiteko na kama imeshindwa kutatua tatizo lako, basi utaunganishwa moja kwa moja na daktari wa ukweli (Human Doctor).

Ikumbukwe kuwa, TanzMED haitibii kwa njia ya mtandao bali tinakupa ufafanuzi au muongozo utakaokuwezesha kufanya maamuzi sahihi kama; sayansi ya magonjwa, uende hospitali gani yenye uwezo wa kukusaidia tatizo lako, ukaonane na daktari wa kitengo kipi, dalili gani ukiziona inabidi uchukue hatua, jinsi ya kupata huduma ya kwanza kabla haujaenda hospitali nk.