Jinsi wanavyoambukiza
Ndani ya jamii ya wadudu hawa ziko jamii zingine ndogondogo ambazo zinatofautiana kwa uwezo wa kuchachua vyakula na kutoa tindikali na hata uwezo wa kujishikiza kwenye meno. Kwa mtu mwenye wadudu wasio wakali anaweza kuambukizwa na mwenzake mwenye wadudu wakali na hivyo kuingia kwenye hatari zaidi ya kuoza meno. Tafiti zimeonesha wapenzi/wanandoa wanaweza kuambukizana kwa njia ya kubusiana. Watoto wanaochangia ice cream/ice water mashuleni pia wanaambukizana kwa njia hii. Tafiti pia zimeonesha wazazi wanaotafunia vyakula watoto wao kama sehemu ya kuvilainisha wanaweza kuwambukiza pia watoto wao.
Njia nyingine ni jino lililooza kuambukiza mengine yanayogusana nayo, tindikali inayozalishwa na wadudu katika jino lililooza inaweza kuathiri jino lililo jirani. Ndiyo maana inashauriwa ukiona jino limeanza kuoza muone mtaalamu akalitibu au akaling’oe kama halitibiki ili lisiambukize mengine.
Namna ya kujikinga
- Njia muhimu ni kutembelea cliniki za meno angalau kila baada ya miezi sita
- Kuzuia watoto kuchangia vyakula mudomoni
- Kupima kuangalia kiwango na aina za bakiteria zilizi kwenye mate yake na kupata dawa ikibidi.
- Kuhusu kubusiana sina la kusema