Image

Ugonjwa Wa Kupooza (Poliomyelitis)

Polio ni ugonjwa wa kuambukiza usababishwao na virusi, huathiri neva na kusababisha ulemavu.

Kutokana na taarifa za shirika la afya duniani:

  • Polio huathiri zaidi watoto wa umri wa chini ya miaka mitano
  • Ulemavu hutokea kwa mmoja kati ya maambukizi 200
  • Mpaka 2013 ni nchi tatu ambazo bado kuna mlipuko wa ugonjwa huu wa kupooza Afghanistan, Pakistan na Nigeria. Ila kutokana na Taarifa kutoka wizara ya afya ya Tanzania ilipokea taarifa kutoka shirika la afya duniani kuwa kuna mlipuko katika nji jirani ya Kenya, wilaya ya Fafi.

Je ni zipi dalili za ugonjwa huu?

Dalili hizi hudumu kwa kati ya siku 1 hadi 10

  • Homa
  • Maumivu ya kichwa
  • Kutapika
  • Uchovu
  • Maumivu ya shingo
  • Maumivu ya mgongo
  • Maumivu ya mikono na miguu
  • Misuli kukakamaa

Je ni matatizo gani mtu huweza kupata baada ya maambukizi haya?

  • Kupooza misuli
  • Ulemavu wa miguu

Vipimo:

  • virusi vya polio huweza kuonekana katika makohozi, kinyesi na maji maji ya uti wa mgongo.

Matibabu

Hamna matibabu ya maambukizi haya, kwahiyo ni tiba ya dalili ambayo hutolewa:

  • Kupumzika
  • Dawa za kutuliza maumivu na kushusha homa
  • Antibiotiki kuzuia maambukizi nyemelezi
  • Mazoezi kiasi kwaajili ya kuzuia kukakamaa
  • Na kula chakula bora

Kinga

Ni chanjo ya Polio ambayo hutolewa pamoja na chanjo nyingine kwa watoto baada tu ya kuzaliwa, na kurudiwa tena katika wiki ya nne, ya nane na mwisho ya kumi na mbili.

 

Picha kwa hisani ya https://www.passporthealthglobal.com/

Imesomwa mara 29594 Imehaririwa Alhamisi, 15 Agosti 2019 08:54
Dr.Mayala

Dr.Henry A Mayala ni daktari bingwa Wa Tiba ya moyo katika taasisi ya Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI), ambaye kwasasa anasomea shahada ya uzamivu (PhD) ya Tiba ya Moyo katika Chuo Kikuu cha Tongji  nchini China.

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.