Image

Historia ya upasuaji wa moyo

Mapinduzi na maendeleo makubwa katika tiba ya upasuaji wa moyo duniani yanaanzia mwaka 1944 wakati kwa mara ya kwanza duniani katika Hospitali ya John Hopkins nchini Marekani ilifanyika operesheni ya kwanza ya upasuaji wa moyo na kufanikiwa kwa mtoto aliyekuwa na tatizo la moyo la kuzaliwa nalo lililokuwa linasababisha watoto watoto kufa kwa kukosa hewa safi ya oksijeni katika mzunguko wa damu mwilini.

Operesheni hii ilifanywa na Dkt. Alfred Blalock na wanafunzi wake wa upasuaji akiwemo Dkt. Denton A. Cooley (Mwalimu wangu na mwanzilishi wa Texas Heart Institute ya Marekani) baada ya kuombwa na daktari wa watoto, Dkt. Hellen Taussing kujaribu kuokoa maisha ya watoto hao waliokuwa wanakufa bila ya kujua jinsi ya kuwasaidia.

Lakini la muhimu kutambua ni kuwa, operesheni hii ya kwanza duniani ilifanikishwa na kijana Mmarekani mweusi (African-American), Vivien Thomas aliyekuwa msaidizi wa Dkt. Alfred Blalock kwa majaribio ya kisayansi aliyewezesha kufanyika kwa operesheni hii na akafikia kupewa Udaktari wa Heshima (Honorary Doctor of Medicine) na kufundisha madaktari wengi wa upasuaji wa moyo waliopitia katika Hospitali ya John Hopkins. Hivyo operesheni hii huitwa ‘Blalock-Taussing Shunt’. Lakini historia itamkumbuka Dkt. Vivien Thomas kwa mchango wake.

Operesheni hii ilikuwa ni ya kuunganisha baadhi ya mishipa ya damu ili kuwezesha mwili wa mtoto kupata hewa safi. Ingawa operesheni hii ilikuwa si ya kufungua moyo moja kwa moja lakini ilisaidia kutoa mwanga kuwa inawezekana kuufanyia moyo upasuaji na kurekebisha kasoro zilizo ndani ya moyo.

Hivyo madaktari na wanasayansi waliendelea na majaribio mbalimbali kwa kutumia wanyama na hadi baada ya vita ya Pili ya Dunia ambapo baadaye Dkt. John Gibbon na mkewe Mary Gibbon katika chuo kikuu cha Minnesota mjini Minneapolis nchini Marekani walipofanikiwa kugundua mashine ya

Ukurasa 2 ya 2