Image

Tohara kwa wanamume husaidia kupunguza maambukizi ya VVU

Tohara kwa wanaume ni oparesheni inayohusu kuondolewa kwa sehemu ya ngozi au ngozi yote inayofunika kichwa cha uume, na imekuwa ikifanywa na baadhi ya watu katika makabila na dini mbalimbali kwa zaidi ya maelfu ya miaka.
Kwa sasa tohara kwa wanaume imeamsha mvuto mkubwa wa kisayansi na uchunguzi kwa sababu utafiti umethibitisha kuwa wanaume waliotahiriwa wana viwango vidogo vya maambukizo ya virusi vya ukimwi (VVU) kuliko wasiotahiriwa.

Aidha ueneaji wa VVU ni mdogo kwa jumla katika jamii zinazotahiri wanaume kuliko zile ambazo wanaume hawatahiriwi. Kiasi cha asilimia 20 cha wanaume duniani kote inasemekana kuwa wametahiriwa, iwe mara baada ya kuzaliwa
au wakati wa balehe, kwa kawaida kutokana na sababu za kiutamaduni, kiafya au dini. Si nchi zote Barani Afrika zenye takwimu, kuhusu ushauri wa tohara kwa wanaume, hata hivyo kwa kawaida inakadiriwa kuwa chini ya
asilimia 20 ya wanaume kusini mwa Jangwa la Sahara wametahiriwa, kati ya asilimia 50 na 80 katika sehemu nyingi za Afrika ya Mashariki, na zaidi ya asilimia 80 au zaidi katika Bara la Afrika.


Kinachofahamika ni Nini?

Utafiti wa majaribio wa mara ya tatu Afrika Mashariki na Kusini ambao umefanywa, miaka ya hivi karibuni kupima kwa njia ya utafiti uliodhibitiwa, manufaa ya tohara kwa wanaume katika kuzuia maambukizi ya VVU. Utafiti uliofanywa katika Jimbo la Gauteng,Afrika Kusini, ulisimamishwa mapema zaidi kuliko ulivyopangwa kwa sababu matokeo yamethibitisha kuwa tohara ilikuwa kinga dhidi ya maambukizi ya VVU na wachunguzi wamependekeza kuwa utaratibu huo uendelee kwa watu zaidi ya 3,274 wanaoshiriki.

  •  Wanaume waliotahiriwa waliofanyiwa utafiti wameonekana kuwa ni asilimia 60 pungufu ya uwezekano wa kuambukizwa VVU kuliko wasiotahiriwa.
  •  Iwapo utafiti wa majaribio unaoendelea nchini Kenya na Uganda unaowahusisha wanaume 8,000 utatoa matokeo sawa na yale ya Afrika Kusini, tohara kwa wanaume itaungana na zana kama vile Kondomu za kiume na za kike kama njia kuu za kuzuia maambukizi ya VVU.
  •  Tayari msingi wa shauku umeonekana nchini Botswana na Swaziland, nchi mbili miongoni mwa nchi zilizoathiriwa sana na VVU/UKIMWI.
  •  Zaidi ya asilimia 80 ya wanaume waliofanyiwa utafiti Botswana wamesema kuwa wangependa kutahiriwa iwapo utaratibu huo ni salama na wenye gharama nafuu.
  •  Nchini Swaziland zile hospitali ambazo hazikuwa zikitahiri, sasa zimekuwa zikitahiri watu 10-15 kwa juma na zina orodha ndefu ya watu wanaosubiri huduma hiyo

 Hivyo basi kutokana na faida hizi, wanamume wanashauriwa sana kufanyiwa tohara, kwa kufanya tohara siyo tuu watakuwa wamepunguza uwezekano wa kuambukizwa VVU, bali pia watakuwa wamepunguza uwezekano wa kuwaambukiza wengine kama wao wanaishi na virusi vya ukimwi.

Ikumbukwe pia, kufanya tohara pekee hakukuondolei uwezekano wa kuambukizwa VVU, hivyo unashauriwa kuendelea kutumia njia nyingine zilizo salama za kujikinga na maambukizi ya VVU.

 

Credit: www.nacp.go.tz

Imesomwa mara 12758 Imehaririwa Jumatano, 09 Oktoba 2019 16:51
TanzMED Admin

TanzMED ni mjumuiko wa wataalamu wa fani mbalimbali za Afya na IT wa kitanzania ambao wamejitoa katika kuhakikisha kuwa jamii ya kitanzania na Afrika kwa ujumla inafaidika kwa kupata habari na ushauri juu ya masuala ya afya yanayozunguka jamii hizo.

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

Makala shabihana