Pakua TanzMED App?

Upungufu wa akili ni tatizo ambalo kwa ujumla hutokea kabla ya mtu kuwa mkubwa (adulthood) na huambatana na dalili za kupunguwa uwezo wa akili ya utambuzi na kutafakari (cognitive functions) pamoja na kushindwa kukua kwa tabia za kuendana na mazingira yanayomzunguka mtu (adaptive behavior). Pia kitaalamu, upungufu wa akili hujulikana kama mtu yoyote mwenye IQ (Intelligence Quotient) chini ya 70.

Upungufu wa akili ni hali ya kuwa na mapungufu katika ukuaji (development deficit) yanayoanza utotoni ambayo husababisha kupungua uwezo wa kusoma (intellect), kutafakari, utambuzi na kutoweza kuendana na majukumu ya kila siku ya maisha.

Ukubwa wa Tatizo (Epidemiology)

Upungufu wa akili ni tatizo kubwa sana duniani.Huathiri asilimia 1-2 ya watu wote duniani.Huonekana sana kwa wanaume kuliko wanawake (inakisiwa huonekana mara mbili zaidi kwa wanaume kuliko wanawake). Upungufu wa akili wa kati (mild mental retardation) huonekana sana kwa watu wa kipato cha chini lakini upungufu wa akili wa kiwango cha juu hutokea uwiano sawa katika jamii ya matabaka yote na huonekana sana katika umri kati ya miaka 10 hadi 14.

Upungufu wa akili sio ugonjwa (axis II disorder in DSM-IV) kutokana na dalili na viashiria vyake bali ni tatizo la mfumo wa utambuzi wa watu wenye kuhitaji huduma za kijamii na elimu maalum ili kuweza kumudu majukumu yao ya kila siku. Mara nyingi upungufu wa akili hutokea kabla ya mtu kufikisha umri wa miaka 18.

Tungependa kwa yoyote mwenye takwimu kutoka afrika mashariki za tatizo hili la upungufu wa akili kutoka katika hospitali za magonjwa ya akili za Butabika National Referral and Teaching Mental Hospital (Kampala, Uganda), Port Reitz District Hospital (Mombasa, Kenya), Mathare Mental Hospital (Nairobi, Kenya), Lutindi Mental Hospital (Tanga, Tanzania) na Mirembe Psychiatric Referral Hospital (Dodoma, Tanzania).

Tabia za Kuendana na Mazingira (Adaptive behavior) ni nini?

Tatizo la kiakili la kujihisi mnene na kupoteza hamu ya kula au Anorexia nervosa ni tatizo linawaathiri watu wengi na kuwafanya kupoteza uzito zaidi ya ule unaokubalika kulingana na umri na urefu wa muhusika.

Watu wenye tatizo hili wana hali ya kuwa na hofu isiyo kifani ya kuongezeka uzito hata kama, kiukweli, wana uzito mdogo (wamekonda) kuliko kawaida. Wanaweza kujinyima au kupunguza kula makusudi (dieting), kufanya mazoezi ya kupunguza uzito kuliko kawaida au hata kufanya njia nyingine zozote ilimradi wapungue uzito.

Chanzo na vihatarishi vya tatizo hili

Chanzo halisi cha tatizo hili bado hakifahamiki rasmi. Hata hivyo, mambo kadhaa yanahusishwa na kutokea kwake. Mambo hayo yanajumuisha sababu za kinasaba (genetic factors) na vichocheo mwili (hormones). Aidha masuala ya kijamii yenye kuchochea wana jamii kama vile baadhi ya wasichana kupenda maumbo madogo (vimodo) nayo pia yanahusishwa.

Kipindi cha nyuma, masuala kama matatizo katika familia yalikuwa yakihusishwa na uwepo wa tatizo hili pamoja na matatizo mengine yanahusiana na ulaji wa muhusika ingawa kwa sasa uhusiano wake unaonekana kuwa si wa nguvu sana.

Vihatarishi vya anorexia nervosa vinajumuisha

Utangulizi

Mada hii ina lengo la kuzungumzia tatizo la kuwa na hofu au wasiwasi uliopita kiasi au kwa kitaalamu Generalized anxiety disorder (GAD). Kwa ajili ya kutofautisha kati ya hofu iliyopitiliza na hofu ya kawaida ambayo yaweza kumkumba mwanadamu yeyote, wakati fulani fulani mwandishi atatumia maneno anxiety au GAD katika kuwasilisha ujumbe wake.

Hofu iliyopitiliza au au anxiety au GAD huambatana na hali ya kuwa na wasiwasi kupita kiasi juu ya maisha ya kila siku pamoja na matukio yake bila hata muhusika kuwa na sababu maalum ya kuwa na hofu hiyo. Kwa maneno mengine ni kuwa, watu wenye anxiety hujihisi hofu kubwa bila ya kuwa na sababu yeyote ya msingi ya kuwafanya wawe hivyo. Mara nyingi watu wenye tatizo hili huwa na tabia ya kuhisi kwamba janga kubwa litawatokea karibuni au maafa yatamkumba katika maisha yake na daima hawaachi kuwa na hofu isiyo na sababu juu ya familia zao, pesa, afya, ajira, masomo au hata biashara zao.

Maisha yao ya kila siku huwa na mchanganyiko wa hofu, wasiwasi na huzuni, kiasi kwamba hatimaye hofu hutawala mawazo  ya muhusika kiasi cha kuingilia utendaji wake wa kila siku ikiwemo kazi, masomo, shughuli zake za kijamii, na hata mahusiano na mwenza wake wa ndoa.

Dalili za hofu iliyopitiliza (anxiety) ni nini?

Utangulizi

Ugonjwa wa Alzheimer's ni miongoni mwa magonjwa ya ubongo yanayoathiri zaidi wazee au watu wa umri wa makamo. Ugonjwa huu ambao huanza polepole na kuchukua muda mrefu kujitokeza kwa kawaida hauoneshi dalili ya kupata nafuu mara unapoanza.

Ugonjwa wa Alzheimers’s ni miongoni mwa makundi ya magonjwa ya akili yanaitwa kitaalamu kama dementia na ambao huathiri zaidi watu wenye miaka 65 au zaidi.

Ugonjwa wa Alzheimer’s unasababishwa na nini?

Mpaka leo hii, chanzo halisi cha ugonjwa wa Alzheimer’s bado hakijajulikana. Hata hivyo, kuna nadharia kadhaa zilizoibuliwa na wanasayansi kuhusiana na baadhi ya visababishi vya ugonjwa huu. Nadharia inayoonekana kukubalika mpaka sasa ni ile ya uhusiano wa kuwepo kwa jamii ya protein inayoitwa amyloid na ugonjwa huu.

Wanasayansi wameonesha kuwa mabadiliko katika vinasaba vinavyodhibiti uzalishwaji wa protini hii ya amyloid ndiyo chanzo kikuu cha ugonjwa huu. Aidha ushahidi uliooneshwa na watafiti hao unasema kuwa mabadiliko haya ya vinasaba yamethibika kwa takribani zaidi ya nusu ya wagonjwa wote waliogunduliwa kuwa na ugonjwa huu.

Katika wagonjwa wote hawa waliofanyiwa utafiti imeonekana kwamba mabadiliko hayo ya vinasaba yamesababisha uzalishwaji uliopitiliza katika ubongo wa aina fulani ya vipande vya protini ijulikanayo kitaalamu kama ABeta (Aβ). Wataalamu wengi wanaamini kuwa, kukosekana kwa udhibiti wa uzalishaji wa aina hii ya protini kunakosababisha protini hii kuwa nyingi mno kwenye ubongo kuliko inavyoweza kuharibiwa ndiko kunakosababisha ugonjwa huu.