Pakua TanzMED App?

Hongera kama wewe ni mama mjauzito, baaada ya kupata ujauzito, wazazi wengi wamekuwa wakipenda kujua hatua atakazopitia mama mjamzito  mpaka kujifungua kwake. Hatua hizi siyo tuu zitamsaidia mwanamke au ni maalumu kwa ajili ya wanawake pekee, bali hata wanamume kwa sababu kwa kujua hatua anazopitia mwenza wako, zitakusaidia kwenye kumsaidia pindi kunapotokea uhitaji. Makala hii itakufafanulia hatua hizo mwezi hadi mwezi na nini kinatokea kuanzia uchavushaji unapotokea, mtoto akiwa tumboni mpaka siku ya kujifungua. Kuna wakati, mwanamke hutoa mayai zaidi ya moja kwa mkupuo na yote yakaruhusu mbegu moja moja kuingia, na hapo ndipo kutatokea mapacha wasiofanana (dizygotic twins).

Kutunga kwa ujauzito.

Uchavushaji hutokea pindi mbegu za kiume zinapofanikiwa kupenya kwenye yai la mwanamke. Wakati wa tendo la ndoa, manii ya mwanamume hutoka ikiwa na mamilioni ya mbegu, ila ni mbegu moja tuu itakayofanikiwa kupenya kwenye yai la mwanamke na kusababisha ujauzito. Baada ya kupenya, yai hujifunga na kukamilisha kitendo cha uchavushaji na hapo mimba huwa imeshatungwa (Conception). Pindi tuu mbegu ya mwanamume inapofanikiwa kuingia kwenye yai la mwanamke, jinsia ya mtoto huwa tayari imeshakamilika . Ikumbukwe kuwa, kwenye manii, kunakuwa na mbegu za kike na za kiume, na ni mbegu moja tuu ndiyo itakayofanikiwa kuingia kwenye yai, ama ya kike ama ya kiume. Hivyo, ni mbegu za mwanamume ndizo zinazoamua jinsia ya mtoto. Na 

Siku tatu za mwanzo baada ya utungaji wa mimba, yai lililochavushwa hujigawa kwenye chembe hai nyingi. Hupita kwenye mirija ya fallopian (fallopian tube) na kupanda hadi kwenye mfuko wa uzazi (Uterus) na hujibadika hapo. Wakati huu, planseta au mji wa uzazi huanza kutengenezwa.

 

Maendeleo wiki ya 4

Wakati huu, mtoto anaanza kutengeneza umbo la muonekano wa sura pamoja na shingo. Moyo na misuli ya damu huanza kujengwa wiki hii. Kwa sasa, unaweza kutumia vipimo vya nyumbani kujipima na kupata matokeo halisi.

Maendeleo wiki ya 8

Hadi wiki hii, mtoto huwa na ukubwa wa nusu inchi (1.27cm). Pia, ngozi inayofunika macho (eyelid ) na masikio sasa yanaanza kutengenezwa, pia alama ya pua huanza kutokea kwa mbali. Mikono na miguuu tayari inakuwa  imeshatengenezwa hadi sasa. Vidole navyo vinaanza kukua na kuonekana vyema.

Maendeleo wiki ya 12

Mtoto sasa anakaribia 5cm, na anaanza kuzunguka. Unaweza kuanza kuhisi juu ya mji wa uzazi (uterus). Kwa sasa, daktari anaweza kuanza kusikia mapigo ya moyo ya mtoto kwa kutumia kifaa maalumu. Hadi sasa, sehemu za siri za mtoto huwa zimeshajijenga vyema.

Maendeleo wiki ya 16

Ukubwa wa mtoto kwa wiki hii huwa kati ya 11cm hadi 12cm na uzito wa gram 100. Kwa wiki hii, mtoto anao uwezo wa kuchezesha macho, pia, moyo na mishipa ya damu inakuwe imeshakamilika. Vidole vyake sasa vinakuwa tayari vimeshatengeneza michirizi (fingerprints).

Meaendeleo wiki ya 20

Uzito wa mtoto sasa hufikia gram 285 na urefu wake huwa zaidi ya nusu rurla (15cm). Mtoto ana uwezo wa kunyonya vidole, kujinyoosha, muda si mrefu (kama bado haujaanza kusikia) utaanza kusikia akicheza "quickening."

Mara nyingi, ultrasound hufanyika wiki hii. Daktari atahakikisha kuwa mji wa uzazi (placenta) lipo salama na lina afya njema, pia atahakikisha kuwa mtoto wako anakua vyema. Kwa kutumia ultrasound, utaweza pia kuona mapigo ya moyo ya mtoto na baadhi ya viungo kama mikono, miguu na hata muenendo wa mwili wake.

Pia, wiki hii unaweza pia kutambua jinsia ya mtoto kama ni wa kike au wa kiume.

Maendeleo wiki ya 24

Sasa mtoto atakuwa na uzito zaidi ya nusu kilo, pia, anao uwezo wa kufuata sauti, unaweza kumsikia akizunguka kufuata sauti inapotokea. Jenga mazoea ya kuongea naye kuanzia sasa maana watoto hujenga mazoea na sauti wanazozisikia kila siku na huzitambua (kuonesha kuwazoea watu wenye sauti hizo) pindi wanapozaliwa. Wiki hii, sehemu za ndani za masikio (mfumo wa masikio) unakuwa umekamilika. Pia, anao uwezo wa kuhisi uelekeo wake ndani ya tumbo placenta. 

Maendeleo wiki ya 28

Uzito wa mtoto kwa wiki hii unakaribia kilo moja, na huendelea kukua kwa haraka kwa wiki zijazo, mtoto hubadilisha sana uelekeo akiwa kwenye wiki hii. Kwa wale waliojifungua mtoto kabla ya muda, watoto waliozaliwa kwenye wiki hii, wana nafasi kubwa ya kuishi. Tafadhali ongea na daktari wako juu ya dalili za kujifungua kabla ya muda (preterm labor warning signs). Sasa, unatakiwa kuanza maandalizi ya kujifungua, maandalizi haya ni juu ya nini unatakiwa kufanya ukiwa leba, jinsi ya kumuhudumia mtoto mchanga nk. Pia, hakikisha unatembea na vifaa/taarifa muhimu popote unapoenda.

Maendeleo wiki ya 32

Wiki hizi, utamsikia sana mtoto akiwa anazunguka, na uzito wake hufikia hadi 1.8kg. Ngozi ya mtoto kwa wiki hii huonekana kama imejikunja kunja, kwa sababu, tabaka la fati huanza kutengenezwa. Kuanzia sasa mpaka unapojifungua, mtoto huongezeka uzito mpaka nusu ya uzito atakaozaliwa nao. Unaweza kuanza kuona majimaji ya njano yakitoka kwenye chuchu. Hii inaitwa colostrum, ni matayarisho ya kuanza kutenegeneza maziwa. Kuanzia wiki hii, ratiba ya kliniki hubadilika na sasa huwa kila baada ya wiki mbili.

Maendeleo wiki ya 36

uzito wa mtoto sasa hutofautiana, kuna sababu nyingi sana zinazopelekea utofauti huo kama jinsia ya mtoto (watoto wa kike huzaliwa na uzito mdogo kuliko wa kiume), idadi ya watoto (kama una mapacha, uzito hupungua) na pia maumbile ya wazazi. Hivyo, kitu cha msingi kuzingatia hapa ni uwiano wa ukuaji na siyo uzito halisi. Mtoto anaweza kuwa na uzito mdogo lakini amekuwa akiongezeka katika uwiano mzuri. Kwa wastani, watoto wengi huwa na urefu wa 47cm na uzito wa kilo mbili na zaidi katika wiki hizi. Ubongo sasa unajengeka kwa haraka zaidi. Mapafu nayo yanaelekea kukamilika na sasa mtoto anakuwa amegeuka na kichwa huwa kinaelekewa chini kwenye njia (pelvis).

Wiki ya 37 huchukuliwa kama ndiyo muhula wa kujifungua (term). Endapo utajifungua wiki ya 37-39 huchukulia kuwa umejifungua mapema, 39-40 huchukuliwa kama umejifungua katika muhula na wiki ya 41-42 huchukuliwa kama umechelewa. Watoto wengi waliozaliwa kabla ya wiki 39 huwa na nafasi kubwa ya kuwa na matatizo ya upumuaji na mengineyo, na kuna wakati wanahitaji uangalizi maalumu. 

Kujifungua

Safari ya ujauzito huitimishwa wiki ya 40. tarehe ya kujifungua hukokotolewa kutokea siku ya kwanza ya hedhi ya mwisho. Kulingana na mahesabu hayo, mwanamke kwa wastani hukaa na ujauzito kwa wiki 38 hadi 42, na muhula wenyewe hukamilika wiki ya 40 kwa sababu, inakadiriwa kuwa utapata ujauzito siku ya 14 baada ya hedhi yako ya mwisho. Mahebau haya huwa ni makadirio, hivyo kuna baadhi ya watoto huzaliwa wiki ya 42 na huchukuliwa kama ndani ya muhula.

Je upo katika harakati za kutafuta ujauzito? TanzMED inayo tool inayoweza kukusaidia kufuatilia siku zako, ipakue

 • Utafiti mpya unaonesha ya kwamba watoto wanaokunywa juisi au ambao mama zao walikunywa vitu vyenye sukari kipindi cha ujauzito wapo kwenye hatari kubwa ya kuugua ugonjwa wa Pumu
 • Wajawazito ambao walikunywa soda na vinywaji vyenye sukari (sugary beverages) wana asilimia 70 ya kuzaa watoto ambao baadae watapata ugonjwa wa Pumu

Matokeo ya utafiti kutoka Chuo Kikuu cha Harvard nchini Marekani yameonyesha ya kwamba, watoto wanaokunywa vinywaji vyenye sukari au juisi (artificial juice) na ambao mama zao walikunywa soda kipindi cha ujauzito wao wapo kwenye hatari kubwa ya kupata ugonjwa wa Pumu.

Watoto ambao waligundulika kuwa na kiwango kikubwa cha sukari aina ya fructose (ambayo hupatikana kwenye juisi au soda) kwenye milo yao kipindi cha ukuaji, walikuwa kwenye hatari ya asilimia 79 kupata ugonjwa wa Pumu ukilinganisha na watoto ambao hunywa vinywaji vyenye sukari kwa nadra au wale watoto ambao hawanywi kabisa vinywaji hivyo.

Kina mama ambao walitumia vinywaji vyenye sukari au soda kipindi cha ujauzito pia walikuwa kwenye hatari ya asilimia 70 kuzaa mtoto ambae baadae atagundulika kuwa na ugonjwa wa Pumu ikilinganishwa na kina mama ambao walitumia vinywaji vyenye sukari kwa nadra au ambao hawakutumia kabisa vinywaji hivyo kipindi cha ujauzito.

Homa ya kweli inasababisha wasiwasi hasa katika miezi michache ya kwanza ya maisha ya mtoto. Hii ni kwa sababu mfumo wa kinga kwa watoto huwa bado mchanga na hauna ufanisi sana katika kupambana na maambukizi kwa miezi mitatu au minne ya mwanzo baada ya mtoto kuzaliwa.

Hivyo ni muhimu kujifunza namna sahihi ipasayo kuchukua joto la mtoto wako na kuelewa nini kinaashiria homa ya kweli.

Homa kwa mtoto

Kwa kawaida madaktari husema mtoto ana homa iwapo kama joto la mwili wake litaongezeka na kufikia nyuzijoto 38?? (100.4F) au zaidi. Ni vizuri kujua joto la kawaida la mtoto wako kwa kuchukua vipimo mara chache wakati mtoto yupo katika hali ya kawaida ‘mzima wa afya’.

Nini husababisha homa kwa watoto?

Kuna sababu kadhaa ziletazo homa kwa watoto. Upungufu wa maji mwilini ni mojawapo ya sababu hizo. Aidha joto la watoto wachanga linaweza kuwa juu kufuatia nguo nyingi alizovaa katika mazingira ya joto kiasi. Kwa kawaida inashauriwa mtoto wako avae safu moja zaidi ya mavazi zaidi ya yale ambayo wewe mwenyewe ukivaa yanakufanya ujisikie vizuri, maana yake ni kwamba kama wewe umevaa nguo mbili juu, na ukajisikia vema, basi mtoto wako avae walau nguo tatu ili kulinda joto lake lisipungue wala kuongezeka sana.

Sababu nyingine iwezayo kuleta homa kwa watoto ni maambukizi. Mfumo wa kinga ya mwili wa mtoto unapohisi kuingiliwa na vimelea vya maradhi kama vile bacteria au virusi, hutoa taarifa kwenye ubongo ambao nao hutoa kemikali fulani zinazosababisha joto kupanda mwilini. Kupanda kwa joto huko ambako huitwa homa kunaweza kuwa na faida kadhaa katika mwilini wa mtoto zikiwemo;

 • Baadhi ya bakteria na virusi hawapendi hali ya joto la juu na hivyo basi ni rahisi zaidi kuharibiwa na mfumo wa kinga.
 • Joto la juu la mwili husaidia mwili kupambana na maambukizi.

Kucheua kwa mtoto ni hali ya mtoto kutoa chakula kupitia mdomoni muda mfupi baada ya kula/kunyonya.Kucheua kwa mtoto hupungua kadri mtoto anavyokuwa mkubwa na ni nadra sana kutokea baada ya mtoto kufikisha umri wa miezi 18.

Kucheua pia kunaweza kuashiria tatizo kubwa zaidi kwa mtoto kama ugonjwa wa Gastro-esophageal Reflux Disease (GERD), mzio (allergy) au kuziba kwa mrija wa kupitishia chakula.

Nini husababisha mtoto kucheua baada ya kula? 

Maumbile ya asili ya misuli ya mtoto (lower oesophageal sphincter)-Kwa watoto wachanga, misuli inayounganisha mrija wa kupitisha chakula na tumbo yaani lower oesophageal sphincter, huwa haijakomaa (immature),hivyo kuruhusu chakula (maziwa) kurudi juu yaani kuelekea mdomoni badala ya kwenda kwenye tumbo moja kwa moja.Kazi maalum ya misuli hii ni kufungua njia kuruhusu chakula kuingia kwenye tumbo na kufunga kuzuia chakula kurudi kilikotoka yaani mdomoni.Hivyo, kutokukomaa kwa misuli hii huchangia kucheua kwa watoto

Maziwa ya watoto pia huchangia kutokea kwa hali hii kwani maziwa yapo kwenye majimaji hivyo ni rahisi kurudi juu na kutolewa tena mdomoni.

Kuwepo kwa hewa kwenye tumbo ambayo hutokana na mtoto kunyonya haraka sana/kunyonya sana au mama kutojuwa jinsi ya kumnyonyesha mtoto wake kwa njia sahihi huchangia kutokea kwa hali hii ya kucheua.

Kwa kawaida mtoto hucheua baada ya kunyonya lakini mara nyingine kucheua kwa mtoto hutokana na

 • Allergic gastroenteritis- Mzio (Allergy) wa protini inayopatikana kwenye maziwa ya ng’ombe
 • Gastroesophageal reflux disease (GERD)-Huu ni ugonjwa unaosababishwa na kucheua kwa tindikali inayotoka tumboni ambayo pia huharibu kuta za mrija wa kupitisha chakula (oesophagus).Kitu chochote kile kinachoongeza presha (Intra-abdominal pressure) chini ya lower oesophageal sphincter kama uzito ulopitiliza (obesity), kutopata choo kwa muda (constipation), baadhi ya vyakula, vinywaji na baadhi ya dawa husababisha GERD.
 • Eosinophilic oesophagitis- Hali inayotokana na kukusanyika kwa wingi kwa chembechembe za damu aina ya eosinophils na hivyo kuharibu kuta za mrija wa kupitisha chakula.
 • Mrija wa chakula kuwa mwembamba/kuziba hali inayojulikana kitaalamu kama oesophageal stricture au sehemu ya misuli kati ya tumbo na mrija wa chakula kuwa nyembamba au kuziba nayo hujulikana kwa kitaalamu  kama pyloric stenosis

Dalili za Infant Reflux

Kucheua kwa mtoto ni hali ya mabaki ya chakula kutolewa kupitia mdomoni baada tu ya mtoto kunyonya.Mtoto pia anaweza kutapika. Ikiwa mtoto wako ana afya njema, hana tatizo basi huna haja ya kuwa na wasiwasi kama akicheua au kutapika baada ya kunyonya ingawa kabla ya kupata hali hii mtoto anakuwa anasumbuka sana au kulia, akiashiria kupata taabu tumboni kwa sababu hajacheua/kutapika, hivyo wewe kama mama au baba hutakiwi kuwa na hofu.

Ni wakati gani wa kumpeleka mtoto kwa daktari?

Mpeleke mtoto kwa daktari kama

 • Haongezeki uzito 
 • Anacheua kwa nguvu mpaka macheuo au matapishi yakaruka nje kwa nguvu sana (projectile vomiting)
 • Anajikamua sana kabla ya kucheua/kutapika na kupata maumivu
 • Anacheua macheuo ya rangi ya kijani au ya njano
 • Anacheua macheuo yaliyochanganyika na damu au yenye rangi ya kahawia
 • Anakataa kunyonya
 • Anapata choo kilichoambatana na damu
 • Anapumua kwa shida
 • Anatapika baada ya kufikisha miezi sita
 • Anapata taabu ya kumeza chakula,kunguruma kwa sauti yake (hoarseness of voice),ana maumivu ya koo (sore throat), pua zimeziba kwa muda mrefu, maambukizi kwenye pua/masikio

Kama mzazi tambua ya kwamba

 • Baadhi ya watoto huanza kucheua wakati meno yanapoanza kuota, wakati wanaanza kutambaa,au wakati wanaanza kula vyakula vigumu (solid foods).
 • Baadhi ya watoto wakati wa kunyonya hutoa titi la mama ili waangalie mazingira yanayowazunguka/au wale wanaopenda kucheza na titi la mama wakati wa kunyonya,huingiza hewa ndani na hivyo kusababisha  kucheua
 • Kucheua hutokea baada tu ya mtoto kunyonya au saa 1-2 baada ya kunyonya
 • Watoto wachanga hadi kufikia umri wa miezi mitatu hucheua angalau mara moja kwa siku
 • Kucheua kwa watoto huongezeka mtoto anapofikisha umri wa miezi 2-4
 • Watoto wengi hupunguza kucheua wanapofikisha umri wa miezi 7-8 na
 • Huacha kabisa wanapofikisha umri wa mwaka mmoja

Vipimo vya Uchunguzi

Kama daktari wako atahisi mtoto wako ana tatizo zaidi kutokana na hali yake ya kucheua, baadhi ya vipimo ambavyo anaweza kumfanyia mtoto ni kama ifuatavyo

 • Ultrasound-Kipimo hiki kinaweza kuonyesha kuziba/kupungua kwa njia ya mrija wa chakula au kama mtoto ana pyloric stenosis kama nilivyoeleza hapo awali
 • Vipimo vya damu kama Complete blood Count ambacho huangalia wingi wa chembechembe za damu, maumbile yao, aina ya chembechembe hizo. Pia kipimo cha mkojo (urinalysis) ni muhimu kufanywa.
 • Eosophageal PH monitoring- Kipimo hiki husaidia kujua kama macheuo ya mtoto yana tindikali au la na hufanywa kwa daktari kuingiza mpira mwembamba kupitia pua au mdomo wa mtoto mojamoja kwenda kwenye mrija wa chakula, mbele ya mpira huu kuna kifaa maalum cha kupima PH ya mtoto wako kwa ndani.Kipimo hiki pia kitamsaidia mzazi kujua kama malalamiko, usingizi wa taabu anaopata mtoto (sleep disturbance) na mtoto kulia mara kwa mara (irritability) hutokana na tindikali au la.
 • X-rays za tumbo (Upper GI Series- Mtoto hupewa dawa kama chaki ya majimaji na kisha hupigwa picha za X-rays ambazo zitaonesha kama kwenye utumbo wa mtoto ana shida yoyote ile.
 • Upper endoscopy-Kipimo hiki ambacho hufanywa kwa kutumia mpira maalum wenye kamera kwa mbele ambao huingizwa kwenye mrija wa chakula (oesophagus) kupitia mdomoni mpaka kwenye sehemu ya kwanza ya utumbo mdogo na kwenye tumbo, husaidia kujua kama mrija wa chakula umeziba/kuwa mwembamba au umepata mcharuko wa maambukizi (oesophagitis).Kipimo hiki kwa watoto hufanywa kwa mtoto kupewa dawa ya usingizi au nusu kaputi.

Matibabu ya kucheua

Mara nyingi kucheua kwa mtoto hakuna madhara yoyote yale na husaidiwa kwa;

 • Kumpa mtoto milo midogo midogo mara nyingi (small frequent feedings)
 • Kukatisha chakula na kumweka mtoto begani
 • Kumweka/Kumshika mtoto akiwa wima wakati wa kunyonya au baada ya kunyonya
 • Hakikisha unamlaza mtoto chali na si kulala kifudifudi
 • Tiba inaweza kuwa ya dawa kama ambazo zinazozuia tindikali au ya upasuaji (fundalplication procedure) kwa wale wenye pyloric stenosis.

 

 

 

 

Kichwa maji au hydrocephalus (kwa lugha ya  kitaalamu) ni mkusanyiko usio wa kawaida wa maji yanayojulikana kitaalamu kama (cerebral spinal fluid) kwenye ventrikali (ventricles) au nafasi zilizo wazi (cavities) kwenye ubongo.

Hali hii huweza kusababisha kuongezeka kwa shinikizo katika fuvu (increased intracranial pressure).  Hydrocephalus limetokana na lugha ya kigiriki ambalo humaanisha: Hudro - Maji , na Kephalos - Kichwa

Kwa kawaida kwa kila mtu huwa na maji yanayoitwa kitaalamu cerebral spinal fluid kifupi CSF ambayo huzunguka ndani ya ventrikali za ubongo, nje na ndani ya ubongo na kuelekea kwenye uti wa mgongo (spinal cord) ambapo hufyonzwa na kurudi kwenye damu. Kichwa maji husababishwa na uzuiwaji wa mzunguko wa CSF, au kufyonzwa kwake au uzalishwaji wa CSF kwa wingi kupita kiasi kama kwenye papilloma of choroid plexus. Ikumbukwe ya kwamba kichwa maji huweza hata kusababisha kifo.

Kuna aina mbili za kichwa maji ambazo ni

Communicating hydrocephalus (Non obstructive hydrocephalus)

Aina hii husababishwa na kutokufyonzwa kwa maji ya CSF ingawa hakuna uzuiwaji wake wa mzunguko baina ya ventrikali na nafasi iliyopo kwenye ubongo inayojulikana kama Subarachnoid space. Hii inaweza kuleta madhara kama uvujaji wa damu baina ya ventrikali au kwenye Subarachnoid space, ugonjwa wa uti wa mgongo (meningitis) nk. Aina hii ya kichwa maji nayo imegawanyika katika sehemu mbili, ambazo ni

 • Normal Pressure Hydrocephalus (NPH) – Katika aina hii ventrikali za kwenye ubongo zimeongezeka ukubwa na kuongeza pressure ya CSF.
 • Hydrocephalus ex vacuo – Katika aina hii, pia kuna kuongezeka ukubwa kwa vetrikali za ubongo na subarachnoid space kutokana na kusinyaa kwa ubongo ambapo kunaweza kusababishwa na ugonjwa wa dementia, baada ya kupata ajali ya kichwa au matatizo ya akili kama Schizophrenia.

Non communicating hydrocephalus (Obstructive hydrocephalus)

Aina hii husababishwa na uzuiwaji wa mzunguko wa CSF kwenda kwenye Subarachnoid space kutokana na uvimbe wa kwenye ventrikali.
Kwa hiyo mtu anaweza kuwa na kichwa maji kutokana na kuzaliwa nacho (congenital) au akakipata baadae maishani (acquired) baada ya kupata maradhi kwenye mfumo wa neva mwilini (CNS infections), ugonjwa wa uti wa mgongo (meningitis), uvimbe kwenye ubongo, ajali ya kichwa, kuvuja damu kwenye ventrikali nk. Kichwa maji anachopata mtu baadae maishani huwa kinaambatana na maumivu makali sana.

Kwa nini watoto wachanga wanalia?

Ni kawaida kwa watoto kulia. Hata watoto wanaozaliwa na afya njema kabisa wanaweza kulia kwa jumla ya wastani wa kati ya saa moja mpaka matatu kwa siku. Kwa vile watoto hawawezi kujifanyia chochote wao wenyewe zaidi ya kutegemea wazazi, walezi ama watu wengine wanaowazunguka katika kuwapatia chakula, joto, na faraja, kilio ni njia ya mtoto ya kuwasilisha moja ya mahitaji hayo.

Kama mzazi mpya, wakati mwingine inakuwa vigumu kutambua mtoto wako anahitaji nini anapolia. Mzazi anaweza kuwa na maswali kadhaa kichwani mwake, je, mtoto ana njaa, anasikia baridi, ana kiu, anaumwa ama amechoka? Katika siku za mwanzo, hali ya namna hii inawawia vigumu wazazi wengi, wasijue nini la kufanya. Hata hivyo, kwa kadiri siku zinavyopita mzazi mpya ataweza kutambua kuwa kilio cha mtoto wake kinamaanisha anahitaji nini kutokana na mfumo wake wa kulia.

No Internet Connection