Image

Je unafahamu inakadiriwa kuwa, mwanamke hupata hedhi wastani wa mara 400 katika maisha yake? Pia, neno linalotumika sana kuwakilisha hedhi ni "period", neno hili lilianza kutumika kwa mara ya kwanza kwenye miaka ya 1822 likimaanisha tukio linalotokea ndani ya muda fulani au linalojirudia baada ya muda fulani. Leo hii tuangalie mambo mengine 5 muhimu kuyajua kuhusiana na hedhi.

1. Kwa wastani, mwanamke huanza kupata hedhi yake ya kwanza kabisa akiwa na umri wa miaka 12.

2. Mzunguko wa siku za hedhi huwa kati ya siku 21 hadi 35. Ingawa wengi huwa na mzunguko wa siku 28, lakini kuzidi wiki moja au kuwahi kwa wiki moja ni kitu cha kawaida.

3. Mwanamke huzaliwa na mayai milioni 1 hadi 2. Mayai haya, mengi hufa jinsi mwanamke anavyoendelea kuishi na ni mayai 400 tu ndiyo hukadiriwa kufika hatua ya ukomavu tayari kwa uchavushwaji.

4. Msichana anaweza kupata ujauzito kabla ya kuanza hedhi yake ya kwanza. Hii ni kwa sababu, yai huanza kukomaa kabla ya kuona hedhi yake ya kwanza, hivyo kama atashiriki tendo bila kinga, kuna uwezekano wa kupata ujauzito.

5. Wanawake wengi hufikia ukomo wa kupoata hedhi (menopause) wakiwa na umri wa miaka 48 hadi 55.

Utafiti uliofanyika nchini Uingereza kwa kuhusisha wanawake 46,000 umesema ya kwamba matumizi ya dawa za uzazi wa mpango hupunguza hatari ya kupata saratani ya mayai ya mwanamke (ovarian cancer), saratani ya mfuko wa kizazi (uterine cancer) na ya utumbo mpana wa chakula (bowel cancer).Watafiti hao wamesema kinga anayopata mwanamke dhidi ya saratani hizi kutokana na matumizi ya dawa hizi za uzazi wa mpango ni ya muda mrefu mpaka miaka 35 baada ya mwanamke huyo kuacha kutumia dawa hizi za uzazi wa mpango.

Katika utafiti huu, wanawake wa Uingereza walitumia dawa hizi za uzazi wa mpango kwa wastani wa miaka mitatu na nusu wakati wakiwa na umri kati ya miaka 20 mpaka miaka 30.Kinga dhidi ya saratani kwa wanawake hawa waliotumia dawa hizi za uzazi wa mpango kipindi cha ujana wao ilionekana kuwepo mpaka walipotimiza miaka 50, 60 na 70, umri ambao wanawake wanakuwa kwenye hatari kubwa ya kupata saratani.

Watafiti hawa kutoka chuo kikuu cha Aberdeen nchini Uingereza,waliendelea kusema ya kwamba  wanawake waliotumia dawa za uzazi wa mpango walikuwa na hatari pungufu ya  theluthi moja kupata saratani ya mayai ya mwanamke au saratani ya ukuta wa mfuko wa kizazi cha mwanamke (endometrial cancer).Pia wanawake hawa waligundulika kuwa na hatari pungufu ya moja ya tano kupata saratani  zozote zile ikilinganishwa na wanawake ambao hawakutumia dawa hizi za uzazi wa mpango.

Karibia wanawake milioni 3.5 nchini Uingereza hutumia njia hii ya uzazi wa mpango kama njia rahisi kwao. Utafiti huu uliochapishwa katika jarida la American Journal of Obstetrics and Gynaecology utabadilisha mtazamo wa watu kuhusu athari na faida za dawa hizi za uzazi wa mpango.

Mara nyingi wanawake wameambiwa ya kwamba dawa za uzazi wa mpango zinawaweka kwenye hatari ya kupata saratani ya matiti au ya shingo ya kizazi  (cervical cancer) lakini utafiti huu umeonyesha hatari hii huondoka kabisa ndani ya miaka mitano baada ya mwanamke kuacha kutumia dawa hizi za uzazi wa mpango.Wakati mwanamke anapotimiza umri wa kukoma kupata hedhi, kipindi ambacho kwa kawaida huongeza hatari ya kupata saratani za aina tofauti tofauti, lakini kwa wale ambao walitumia dawa za uzazi wa mpango hapo awali hawako kwenye hatari yoyote ile ya ziada ya kupata saratani, walisema watafiti hao kutoka nchini Uingereza.

Fibroids ni moja ya matatizo yanayowasumbua wanawake wengi , kwa lugha ya kawaida, Fibroids maana yake ni uvimbe wa msuli wa kifuko cha uzazi. Uvimbe huu unaweza kuwa na ukubwa tofauti kuanzia kama punje ya harage mpaka ukubwa wa nazi. Wakati mwingine unaweza kudhani ni ujauzito!

Sio kila mwenye fibroids anakuwa na matatizo kiafya. Zinaweza kuwepo miaka mingi bila matatizo yoyote. Hata hivyo inashauriwa kila mwenye fibroids awe anapimwa na daktari angalau mara moja kwa mwaka ili kuona jinsi zinavyoendelea na kuhakikisha kuwa hazikui kwa kasi au kuhatarisha kuwa kansa.

Kwa wale zinaowaletea matatizo, fibroids husababisha kutokwa na damu nyingi za hedhi, maumivu ya tumbo, mimba kuharibika zikiwa changa, kuzaa watoto njiti na fibroid kukandamiza viungo vingine kama kibofu cha mkojo na kusababisha kukojoa mara kwa mara au matatizo ya haja kubwa.

Njia ya kugundua uwepo wa fibroid ni kupimwa na daktari na kufanyiwa ultrasound.

Matibabu yake yapo ya aina kuu tatu:

1. Kunywa dawa. Hata hivyo dawa zilizopo sasa hazina matokeo mazuri kuondoa fibroids ila husaidia kupunguza ukuaji wake.

2. Kuiondoa fibroid kwa operation. Ziko aina nyingi za operation kupitia kwenye tumbo au kupitia ndani ya kifuko cha uzazi. Aina ya operation hutegemea mahali ilipo fibroid.

3. Kuondoa kifuko cha uzazi. Njia hii huwafaa wale ambao hawana mpango wa kupata mtoto.

Kuna nadharia mbalimbali juu ya vitu vinavyosababisha fibroids lakini hakuna kitu kilichothibitika moja kwa moja kuwa chanzo cha fibroids. Kwa wale wenye uzito mkubwa inashauriwa kupunguza mwili kunaweza kupunguza uwezekano wa kupata fibroids.


Zipo tafiti zinazoonyesha kuwa matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango vinapunguza uwezekano wa kupata fibroids.

Kunyonyesha kuna faida nyingi sana kwa mtoto mchanga pia na kwa mama. Na mara nyingi hili huwa ni umamuzi wa mtu binafsi ila ushauri wa msisitizo unatolewa na chama cha madaktari wa watoto na chama cha madaktari wa magonjwa ya wakina mama vyote vya marekani.

Faida kwa Mtoto

  • Virutubisho vilivyomo kwenye maziwa ya mama ni muhimu kwa mtoto mchanga , maana maziwa ya mama huwa uwiano mzuri wa vitamin, protini, na mafuta mazuri na kumuwezesha mtoto kukuwa vizuri
  • Vilevile maziwa ya mama huwa na virutubisho vyenye uwezo wa kumkinga mtoto kupata magonjwa kitaalamu antibodies, ambavyo humkinga mtoto mchanga dhidi ya vimelea (bakteria na virusi)
  • Maziwa ya mama hupunguza uwezekano wa mtoto mchanga kupata pumu au aleji
  • Na vilevile watoto wakinyonyeshwa kwa miezi sita mfululizo bila kuchanganyiwa na vyakula vingine hupunguza hatari ya kupata maambukizi ya masikio, mfumo wa hewa na magonjwa ya kuharisha
  • Kuna tafiti ambazo zinaonyesha maziwa ya mama yanaongeza upeo wa kufikiri wa mtoto atakapo kua

Maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke kwa kitaalamu Pelvic Inflamatory Diseases au kwa kifupi PID, ni moja ya matatizo ambayo huwaathiri sana wanawake. Kwa kawaida maambukizi haya huusisha shingo ya uzazi (cervix) hali ambayo hujulikana kama cervicitis, nyama ya mfuko wa uzazi (endometrium) ambayo kitaalamu huitwa endometritis, na mirija ya uzazi (fallopian tubes) hali ijulikanayo kitabibu kama salpingitis.

 PID husababishwa na nini? 

Pamoja na aina kadhaa za vimelea kuhusishwa na PID, vimelea vya jamii ya Neisseria Gonorrhoeae pamoja na Chlamydia trachomatis ndivyo vinavyoongoza kwa umaarufu zaidi katika kusababisha PID kwa akina mama.

Je mwanamke huambukizwaje PID?

Kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza kuambukizwa PID. Njia hizo ni pamoja na

  • Kufanya ngono isiyo salama
  • Maambukizi ya njia ya uzazi hasa kipindi mara baada ya kujifungua (au postpartum period)
  • Maambukizi ya njia ya uzazi mara baada ya kutoa mimba kwa njia zisizo salama (post abortion) au mara baada ya mimba kutoka (miscarriage)
  • Kutumia vipandikizi vya ndani ya mfuko wa uzazi (IUCD) kama njia mojawapo ya uzazi wa mpango, na
  • Kuambukizwa kupitia damu iliyo na vimelea vya PID.

Dalili za PID ni zipi?

Zipo dalili kadhaa za ugonjwa huu wa PID. Miongoni mwa dalili hizi ni

Tunaendelea na mfululizo wa makala juu ya hali za dharura kipindi cha ujauzito. Leo tunazungumzia placenta previa. 

Placenta previa ni miongoni mwa hali za hatari na dharura inayowapata baadhi ya mama wajawazito ambapo kondo la nyuma hujipachika katika sehemu ya chini ya mfuko wa uzazi, kukua na kisha kufunika sehemu ndogo au kubwa ya njia ya uzazi inayoelekea kwenye shingo ya uzazi na hivyo kuzuia kabisa uwezekano wa mtoto kuzaliwa kwa njia ya kawaida.

Chanzo chake ni nini?

Wakati wa ujauzito, kondo huongezeka ukubwa na kutanuka kadiri jinsi mfuko wa uzazi unavyotanuka na kukua. Kipindi cha awali cha ujazito, ni jambo la kawaida kwa kondo kuwa maeneo ya chini ya mfuko wa uzazi (low-lying palcenta). Lakini, kadiri mimba inavyokua ndivyo mfuko wa uzazi unavyopaswa pia kulivuta kondo kutoka sehemu za chini na kulipandisha sehemu za juu za kuta zake. Mpaka ifikapo theluthi ya tatu ya ujauzito, kondo linapaswa kuwa karibu kabisa na juu ya mfuko wa uzazi ili kufanya njia ya uzazi kuwa wazi kwa ajili ya kurahisisha utokaji wa mtoto.

Masundosundo au vigwaru au Genital warts ni vinyama laini vidogo vinavyoota kwenye ngozi au utando laini unaozunguka maeneo ya siri. Vinaweza kutokea kwenye uume, uke, mrija wa mkojo [urethra], vulva, shingo ya kizazi [cervix], au maeneo ya kuzunguka njia ya haja kubwa au ndani yake.

Huu ni ugonjwa unaoenezwa kwa njia ya kujamiiana [sexually transmitted infection (STI)].

Visababishi

Ugonjwa wa masundosundo husababishwa na jamii ya virusi wanaoitwa Human papilloma virus (HPV). Kuna zaidi ya aina 70 tofauti za virusi wa HPV ingawa si wote wanaosababisha masundosundo kwenye maeneo ya siri [genital warts]. Baadhi ya aina nyingine za HPV husababisha masundosundo kwenye ngozi inayozunguka sehemu nyngine za mwili kama vile kwenye mikono au miguu. 

Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa baadhi ya aina za virusi wa HPV pia husababisha saratani ya shingo ya kizazi [carcinoma of the cervix] kwa wanawake au saratani ya njia ya haja kubwa [anal cancer] kwa jinsia zote mbili. Aina hii ya virusi hujulikana pia kama high-risk HPV.

Pamoja na kwamba ugonjwa wa masundosundo kwenye maeneo ya siri umejitokeza kwa kasi kubwa hasa baada ya kuwepo kwa janga la UKIMWI, watu wengi waliopatwa na ugonjwa huu huwa hawaoneshi dalili zozote zile. Kwa mfano, kwa wanawake, virusi wa HPV wana uwezo wa kusambaa mpaka maeneo ya ndani kabisa ya kuta za uke au shingo ya kizazi [cervix] bila kuonekana wala kuhisiwa kwa urahisi. 

Kama tulivyotangulia kueleza hapo awali, maambukizi ya HPV husambaa kutoka kwa mtu mmoja mpaka mwingine kwa njia ya kujamiiana kunakohusisha njia ya haja kubwa, uke au ngono ya mdomoni. Mara baada ya kuambukizwa, huweza kuchukua mpaka muda wa wiki sita hadi miezi 6 kwa masundosundo kuwa dhahiri, ingawa baadhi ya wagonjwa wanaweza kukaa hata miaka kadhaa bila kuwa na dalili yeyote ile. Aidha imeonekana pia kuwa si kila mtu anayejamiina na aliye na maambukizi ya HPV au mwenye masundosundo anaweza naye kupata ugonjwa huu. 

Siku hizi, kumekuwa na taarifa nyingi juu ya masuala ya uzazi. Taarifa hizi hutokana na imani tofauti zilizopo kwenye jamii. Na, nyingi ya imani hizi hazina uhakika wa kitaalamu. Moja ya imani ni kutokukojoa kwa mwanamke baada ya tendo la ndoa ili kuzuia mbegu za kiume kutoka.

Kukojoa baada ya kufanya tendo la ndoa ni njia mojawapo inayotumiwa na wengi kusaidia kupunguza uwezekano wa kupata maambukizi ya njia ya mkojo (UTI).  Na inashauriwa sana kukojoa punde baada ya tendo la ndoa ili kujikinga na uwezekano wa kuambukizwa ugonjwa wa UTI kama anavyoelezea Dr. Leah Millheiser . Hivyo, kama na wewe ni mmoja wapo, basi unaweza kuendelea. Kukojoa baada ya tendo la ndoa hakuwezi kupunguza uwezekano wako wa kupata ujauzito.

Wakati wa tendo la ndoa, kuna mbegu kati ya milioni 20 hadi 400 hutotelwa na mwanamume kwenye manii (semen) kwa pamoja , na inakadiriwa kuwa mpaka 65% ya mbegu hufanikiwa kutoka kwenye bao na kuingia kwenye mlango wa uke ikisaidiwa na majimaji ya ukeni yanayotoka wakati wa tendo la ndoa (vaginal discharge) au kwa kitaalamu cervical mucus.

Asilimia kubwa ya mbegu hizi hupenya kwenye lango la uzazi wa mwanamke na kuacha sehemu kubwa ya manii ikiwa na maji maji mengine ambayo yana kiasi kidogo sana cha mbegu za kiume /shahawa (kumbuka manii za mwanamume zinajumuisha vitu vingi vingine zaidi ya shahawa  kama protini , ute wa kusaidia shahawa kuelea au kwa kitaalamu  Seminal fluid nk). Kwenye kila manii (bao) moja la mwanamume (manii yote unayoiona), inakadiriwa  kuwa ni 1% tuu ndiyo shahawa / mbegu za mwanamume, hivyo unapoona kama manii zinamwagika, sehemu kubwa siyo mbegu bali ni majimaji mengine yanayotumika kwenye kuhifadhi mbegu za mwanamume.

Kumbuka: Shahawa(sperms) ni sehemu ya manii (semen ) inayotoka wakati mwanamume akifika kilele. Shahawa huelea kwa kutumia kimiminika kiitwacho Seminal fluid  inayopatikana kwenye manii, Hivyo, siyo maji yote ya kwenye manii ni shahawa.

Kimsingi, mpaka muda anaenda kukojoa, mbegu huwa zimeshafika kwenye lango la uzazi, (cervix) hivyo kiasi kidogo sana cha mbegu zilizoshindwa kutoka kwenye manii ndiyo huendelea kubaki kwenye majimaji ambayo yatatoka dakika au masaa kadhaa baada ya tendo la ndoa.

Kati ya mambo ambayo watu wengi hawatilii maanani sana ni unywaji wa pombe wakati wa ujauzito. Nimekuwa nikiwaona akina mama wajawazito wengi wakinywa pombe kwenye sehemu za starehe na sherehe mbalimbali. Hata hivyo si nia ya makala hii kuwazuia kunywa pombe bali kuwapa elimu sahihi juu ya unywaji wa pombe wakati wa ujauzito.

Watafiti wa magonjwa wanadai kuwa msongo mkali wa mawazo wakati wa ujauzito unaweza kusababisha hitilafu katika uumbaji wa mtoto na hatimaye mtoto kuzaliwa akiwa mlemavu.


Ripoti ya watafiti hao inazidi kuthibitisha matokeo ya tafiti zilizopita kuwa mama mwenye msongo wa mawazo wakati wa ujauzito kutokana na mambo kama kufukuzwa au kuachishwa kazi, kutengana na mwenza wake au kufiwa ana hatari ya kuzaa mtoto mwenye ulemavu kama vile midomo sungura (cleft lip na cleft palate) au matatizo kwenye uti wa mgongo (spina bifida).

Jopo la watafiti wa kidenmark likiongozwa na Dr Dorthe Hansen walifanya uchunguzi ili kuthibiitisha ukweli na uhakika wa  dhana hii. 

Wakitumia rikodi za taarifa za kitabibu za kipindi cha miaka 12 kutoka 1980 mpaka 1992 kutoka masjala ya Taifa ya kitabibu,  watafiti hao waliweza kuwatambua wajawazito wote waliokumbwa na matatizo makubwa ya kimaisha wakati wa ujauzito na hata miezi 16 kabla ya kupata ujauzito. Matatizo makubwa ya kimaisha yaliyochunguzwa yalikuwa kukumbwa na msiba wa ndugu au jamaa wa karibu, ndugu au jamaa wa karibu kulazwa hospitali kwa mara ya kwanza baada ya kugundulika kuwa na kansa ya aina yeyote au ndugu au jamaa wa karibu kupatwa na ugonjwa wa mshtuko wa moyo. Mambo haya yalichunguzwa kwa kigezo kuwa, mjamzito yeyote aliyewahi kukumbana nayo ana hatari kubwa ya kuwa katika msongo wa mawazo bila kujali tabia yake, kama ana watu wa kumfariji au uwezo wake wa kukabiliana nayo.

Jopo hilo lilichunguza maendeleo ya mimba kwa wajawazito 3,560 ambao walikumbana na matukio hayo kwa kulinganisha na  wajawazito wengine 20,299 ambao hawakukumbana na hali yeyote ambayo ingewasababishia kupata msongo wa mawazo wakati waujauzito.


Matokeo ya uchunguzi wao yalionesha kuwa ulemavu na hitilafu za viungo kwa watoto waliozaliwa ulikuwa mara mbili miongoni mwa  kundi la wajawazito waliokumbwa na msongo mkali wa mawazo ikilinganishwa na kundi la kinamama ambao hawakuwa na hali hiyo. 

Kadhalika ilionekana kuwa wanawake waliowahi kukumbwa na hali kama hiyo katika ujauzito mbili mfululizo za nyuma walikuwa katika hatari kubwa zaidi ya kuzaa watoto wenye ulemavu wa viungo tofauti na wale waliowahi kupatwa na hali hiyo mara moja tu au wale ambao hawakupatwa kabisa.

Ilionekana pia kuwa tukio lililoongeza uwezekano wa mtoto kuzaliwa akiwa na ulemavu wa viungo ilikuwa ni iwapo mjamzito atafiwa na mtoto wake mwingine mkubwa wakati akiwa katika miezi mitatu ya mwanzo wa ujauzito wake huu wa sasa. Hatari ya kuzaa mtoto mlemavu iliongezeka iwapo kifo cha mtoto huyo mkubwa kingetokea bila kutarajiwa kwa mfano kwa ajali.

Ukurasa 1 ya 3