Image

Wagonjwa wa Ukimwi huathiriwa sana na ugonjwa wa figo. Ugonjwa wa figo unaohusiana na Ukimwi (HIV-Associated Nephropathy au kwa kifupi HIVAN) unaweza kusababishwa na mashambulizi ya moja kwa moja ya VVU kwenye figo au madhara yanayotokana na matumizi ya madawa ya kurefusha maisha (ARVs).

Aidha wagonjwa wengi wa Ukimwi wapo katika hatari ya kupata magonjwa ya figo kwa sababu ya kupungukiwa na maji mwilini kutokana na kichefuchefu na kutapika mara kwa mara, kupoteza chumvi mwilini, au lishe duni.

Ukubwa wa Tatizo

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2010 na Msango, Leonard(1) na wenzake katika hospitali ya Bugando, Mwanza ilionekana kuwa zaidi ya asilimia 60 ya wagonjwa walioandikishwa kuanza ARVs hospitalini hapo walikuwa na matatizo ya figo yaliyotokana na VVU. Ilionekana pia kuwa HIVAN iliwaathiri zaidi wanawake kuliko wanaume, wenye uzito mdogo, na wale waliokuwa na CD4 chini ya 200.

Huko nchini Marekani, HIVAN ni maarufu zaidi miongoni mwa wamarekani weusi wenye asili ya Afrika ikilinganishwa na wale wa asili nyingine; na hushika nafasi ya tatu kwa kusababisha magonjwa sugu ya figo (CRF) miongoni mwa watu wa jamii hiyo wenye umri wa kati ya miaka 20-64(2). Kwa ujumla HIVAN huchangia karibu asilimia 1 ya wenye ugonjwa sugu wa figo (CRF) nchini humo kila mwaka.


Kwa ujumla takwimu za dunia zinaonesha kuwa HIVAN huathiri zaidi vijana weusi, na takribani nusu ya wagonjwa wa HIVAN ni watumiaji wa madawa ya kulevya ya kujidunga(3).

Wanaume huathirika zaidi kuliko wanawake katika uwiano wa 10:1, wakati wastani wa umri wa watu wenye HIVAN ni miaka 33(4) ingawa HIVAN huwapata pia watoto(5).

Nini hutokea? (Pathofiziolojia ya ugonjwa)

Watafiti wameonesha uhusiano wa mashambulizi ya moja kwa moja ya VVU-1 kwenye figo. Pia kuna uhusiano mkubwa wa vinasaba na vyanzo vya kimazingira vinavyochochea kutokea kwa tatizo hili, hususani kwa watu weusi zaidi kuliko watu wa asili nyingine.

VVU-1 hushambulia zaidi chujio (glomeruli) pamoja na seli za kuta (epithelium) za mirija yake (renal tubules) kuliko sehemu nyingine yeyote ya figo. Hali hii husababisha kuharibika kwa chujio pamoja na mirija na kufanya kazi ya uchujaji uchafu pamoja na utengenezaji wa mkojo kuvurugika. Matokeo yake mkojo huwa na kiwango kingi cha protini kuliko kawaida (protenuria), chujio huwa na makovu (glomerulosclerosis) hali kadhalika nayo mirija (tubulointerstitial scarring).

Uhusiano wa Vinasaba

Mpaka sasa, haijulikani sababu hasa inayowafanya watu weusi kuathirika zaidi na HIVAN kuliko watu wa asili nyingine. Ifahamike kuwa, kwa ujumla watu weusi wanaongoza kwa kupata magonjwa mengine ya figo kama vile ugonjwa wa figo unaotokana na kisukari (diabetic nephropathy) au unaotokana na mcharuko mwili (systemic lupus erythematosus); hivyo basi kuna uwezekano mkubwa pia wa vinasaba kuchangia katika kufanya watu weusi kupata HIVAN.

Dalili na muonekano wa mgonjwa

Pamoja na kuwa na dalili zote za magonjwa ya figo (rejea makala zilizopita za ARF na CRF), wagonjwa wa HIVAN huwa pia na tabia/dalili zifuatazo

  • Muonekano wa mgonjwa: Hupoteza kiwango kingi cha protein katika mkojo (zaidi ya gramu 3.5 kwa siku). Hupoteza pia kiwango kingi cha albumin (aina nyingine muhimu sana ya protini). Aidha huwa na kiwango kingi cha mafuta mwilini (hyperlipidemia). Pamoja na kupoteza sana proteini, wagonjwa wengi wa HIVAN hawana hali ya kuvimba miguu (edema). Huwa na shinikizo la damu la kawaida (tofauti na wagonjwa wa ARF au CRF ambao huwa na ongezeko la shinikizo la damu). Huwa na mrundikano usio wa kawaida wa urea au mazao mengine machafu yanayotokana na Nitrogen katika damu (azotemia).
  • Muonekano wa figo katika Ultrasound au CT scan: Tofauti na wale wa CRF iliyosababishwa na vyanzo vingine ambao huwa na figo ndogo zilizosinyaa, wagonjwa wenye HIVAN huwa na figo zilizo na ukubwa wa kawaida au zilizovimba sana (kubwa kuliko kawaida).
  • Muonekano wa figo katika biopsy: Figo huwa na makovu makovu katika chujio zake (Focal segmental glomerulosclerosis (FSGS) yanayoonekana katika darubini tu.
  • Kiwango cha CD4+ T-cells cha mgonjwa: Kwa kawaida kiwango cha seli za CD4+ kwa wagonjwa wenye HIVAN huwa chini ya 200 cells/µL. Hata hivyo, HIVAN inaweza kutokea hata kwa mgonjwa mwenye kiwango cha juu cha CD4. Wagonjwa wenye CD4 chini ya 50 cells/µL wana hatari zaidi ya kufa mapema kutokana na HIVAN.

Wakati watafiti duniani wakiendelea kutafuta dawa itakayoweza kutibu tatizo la UKIMWI linalosababishwa na VVU, hivi karibuni imebainika kwamba kuna uwezekano mkubwa wa maambukizi ya VVU kupungua kwa mtoto mchanga anayenyonyeshwa zaidi ya miezi 6 kutoka kwa mama mwenye VVU anayetumia dawa. Hii ni kutokana na matokeo ya utafiti iliyofanywa na BAN (Breastfeeding, Antiretroviral and Nutrition) trial na kuchapwa katika mojawapo ya jarida kubwa la afya duniani la Lancet la mwezi Mei mwaka huu.

Hapo awali Shirika la Afya Duniani (WHO) na mashirika mengine ya afya yalipendekeza mama mwenye maambukizi ya VVU kunyonyesha mpaka mtoto atakapofika miezi 6 au chini ya hapo katika nchi maskini na familia zisizokuwa na kipato kikubwa ili kupunguza maambukizi ya VVU kutoka kwenye maziwa ya mama lakini vilevile kuepuka maambukizi ya magonjwa mengine ambayo yanaweza kumpata mtoto.

Faida mojawapo kubwa ya kunyonyesha mtoto ni kumpatia kinga imara kupitia katika maziwa ya mama ili kupambana na vimelea mbalimbali vya magonjwa. Ikumbukwe kwamba kinga ya mtoto mchanga dhidi ya vimelea vya magonjwa mbalimbali ni hafifu, na hii ndio inayosababisha kukawepo aina mbalimbali za chanjo kwa ajili ya watoto.

Hata hivyo, katika hii taarifa mpya ya BAN matokeo yanaonesha kwamba hatari ya maambukizi ya VVU huongezeka mara mtoto anapoacha kunyonya akiwa na miezi 6. Katika kukabiliana na hili, Shirika la Afya Duniani linapendekeza kwa mama mwenye maambukizi ya VVU kuendelea kumnyonyesha mtoto wake mpaka atakapofikisha mwaka 1.

Katika tafiti hii ambayo ilifanyika nchini Malawi katika kipindi cha miaka 7 toka mwaka 2004-2010, Dr. Denise J. Jamieson, kutoka kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa, (CDC) cha huko Atlanta, nchini Marekani na timu ya utafiti ya BAN walikuwa na makundi 3 ya akina mama pamoja na watoto wao wachanga [wajawazito ambao walikuwa kwenye dawa aina 3 za ARV, watoto wachanga waliokuwa kwenye dawa aina ya nevirapine na watoto wachanga ambao hawakuwa kwenye dawa ambao hawa waliitwa kundi thibiti au kwa lugha ya kitafiti control group].

Watoto wachanga walipimwa VVU wakati wa kuzaliwa, wakiwa na wiki 2, 12, 28, na wiki 48. Wale waliobainika kuwa na VVU katika wiki ya 2 walitibiwa na kuondolewa kwenye utafiti kwa vile hawa walishaonekana kuwa wameshapata maambukizi ya VVU kabla ya kuzaliwa na kunyonyeshwa. Akina mama waliambiwa kuanza kuwapatia watoto wao vyakula vya ziada kati ya wiki 24 na 28.

Katika wiki ya 32, wengi wa wanawake, karibu asilimia 96 kutoka katika kundi tafiti au kwa lugha ya kitafiti treatment group na karibu asilimia 88 ya kina mama kutoka kundi thibitiwa yaani control group waliripoti kuacha kunyonyesha.

Hatari ya kuongezeka kwa maambukizi ya VVU katika wiki ya 48 ilikuwa kubwa zaidi katika kundi thibitiwa [control group] kwa silimia 7 ukilinganisha na asilimia 4 katika kundi tafiti [treatment group]. Katika tathmini ya maambukizi ya VVU, asilimia 30 (%) ya maambukizi yalitokea baada ya wiki 28 mtoto alipoachishwa kunyonya maziwa ya mama, wakati asilimia tisa ya maambukizi ilitokea katika kundi la wakina mama wanaotumia ARV, asilimia 13 katika kundi la watoto wachanga wanatumia nevirapine, na asilimia 6 katika kundi thibitiwa [control group]. Aidha, matatizo mengine kama ya kuharisha, malaria, kifua kikuu, ukuaji mbaya na vifo yalijitokeza katika kipindi hiki.

Hitimisho katika tafiti hiyo ilikuwa kwamba kumuachisha mtoto kunyonya maziwa ya mama mapema siyo njia salama na sahihi katika mikakati ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa watoto wadogo.

Dawa za kufubaza makali ya ugonjwa wa ukimwi husababisha virusi hivyo visiendelee kuzaliana, na kama havitoendelea kuzaliana basi seli za kinga za mwanadamu zitaishi kwa mua mrefu na kusababisha mwili kutengeneza ilinzi thabiti kukukinga na magonjwa nyemelezi. Kimsingi virusi vya Ukimwi hushambulia seli hizi, hivyo uwingi wake huwa ni tishio kwa seli na hata husababisha mwili wa binadamu kupoteza uwezo wake wa kupambana na magonnjwa, na ndioyo sababu, mtu aliyeathirika na ukimwi na hatumii dawa za kufubaza makali, kunyemelewa na magonjwa ya mara kwa mara na hata kuzorotesha afya yake.

Matumizi bora ya dawa hizi husaidia kupunguza idadi ya virusi kwenye mwili (kwakuwa hawaendelei kuzaliana), hivyo hupunguzza sana uwezekano wa wewe kumuambukiza mtu mwingine. Kutokana na taarifa kutoka shirika la Afya duniani (WHO), mtu anayetumia dawa za ARV kwa ufasaha kama alivyoelekezwa na daktari huku akiishi maisha yenye kuzingata Afya bora (mazoezi na chakula bora), uwezekano wa kumuambikiza mtu mwingine ambaye hana virusi vya ukimwi unapunguzwa kwa asilimia 96%.

Hivyo, matumizi sahihi ya dawa hizi ni moja ya vitu muhimu ili kupambana na janga hili la ugonjwa wa ukimwi. Nenda kapime kujua hali ya afya yako na kama utagunulika umeambukizwa, uanze kutumia dawa mapema iwezekanavyo kwa afya bora na kuzuia maambukizi kwa umpendaye.

 

Picha kwa hisani ya: http://www.pedaids.org

Ukimwi ni ugonjwa unaosababishwa na ukosefu wa Kinga mwilini, ugonjwa huu husababishwa na virusi vya ukimwi(VVU). Njia kubwa inayopelekea maambukizi ya ugonjwa huu ni ngono, katika makala za awali, tuliangalia njia nyingine za maambukizi ya ugonnjwa huu pamoja na Njia Thabiti Ya Kujikinga Na Maambukizi Ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) .  Hadi sasa, bado hakuna tiba ya ugonjwa wa Ukimwi, lakini kuna dawa zinazotumika kupunguza makali ya ugonjwa huu (ARV), hivyo matumizi ya mapema ya ARV yatakuwezesha kuishi ukiwa na afya njema, na ndiyo sababu tunahimizwa sana kupima afya zetu ili kujitambua na kuchukua hatua mapema.

Ingawa maarifa ya ugonjwa huu ni mengi, ila bado kumeendelea kuwa ni changamoto kubwa katika jamii yetu na nchi nyingine zinazoendelea. MOja ya changamoto hizi ni imani potofu iliyojengeka katika jamii inayopelekea watu ama kuwanyanyapaa wagonjwa wa Ukimwi au kuogopa kupima kwakuwa wakishajulikana watanyanyapaiwa. Hii, hurudisha nyuma harakati za mapambano ya ugonjwa huu.

Leo hii tuangalie imani potofu juu ya ugonjwa wa ukimwi.

Hauwezi kuambukizwa au kumuambukiza mtu virusi vya ukimwi kwa njia zifuatazo

  • Kuumwa na mbu
  • Kwa jasho
  • Kuchangia vyoo, sauna, vifaa vya gym, bwawa la kuogelea
  • Kuchangia taulo
  • Kwenda shule pamoja au kuwa na rafiki mwenye virusi vya ukimwi
  • Kupiga chafya au kukohoa
  • Kushikana mikono, kukumbatia au kupigana busu kavu na mtu mwenye virusi vya ukimwi
  • Kuvuta hewa moja na mtu mwenye virusi vya ukimwi

Imani nyingine potofukatika jamii ni kama

Kupata maambukizi ya ukimwi ndiyo mwisho wa maisha, hii si kweli, kwa kupima na kujitambua mapema na kuanza ARV mapema, kutakupelekea kuishi maisha marefu yenye afya njema.

Unaweza kumtambua muathirika kwa kumuangalia afya yake au muonekano wake kwa macho. Hauwezi kumtambua muathirika kwa kuangalia kwa macho, watu wengi hawana dalili yoyote ya maambukizi ya ukimwi kwa miaka ya awali. Hivyo, njia pekee na ya uhakika kujua kama mwenza wako ana maambukizi au la ni kupima. Na, sasa hivi upimaji wa HIV umerahisishwa zaidi na unatolewa bila gharama yoyote.

Tohara kwa wanaume inazuia kabisa maambukizi ya ukimwi: Ukweli ni kuwa, tohara inapunguza hatari ya maambukizi ya virusi ya ukimwi kwa kiasi kikubwa kama ilivyoandika hapa, lakini si kweli kwa inazuia maambukizi.

Ukimwi unatibika: Hadi sasa bado hakuna tiba ya ugonjwa wa Ukimwi.  ARV husaidia kupunguza makali ya virusi vya ukimwi. Hivyo , matumizi bora ya ARV hupelekea virusi kufubaa na kushindwa kuzaliana hivyo kumuwezesha mtu anayeishi na virusi vya ukimwi kuisha maisha marefu na yenye afya lakini si kweli kwamba zinatibu ugonjwa wa Ukimwi.

Nikiwa nina VVU/Ukimwi sitakiwi kubeba ujauzito: Unao uwezo wa kupata mtoto ili mradi viwango vya virusi (Viral load) ipo chini na imechungwa vyema ndani ya miezi sita. Wenza ambao mmoja wao ana maambukizi na mwingine hana, wanao uwezo wa kutumia njia ya tendo kwa ajili ya kupata ujauzito lakini wanatakiwa kuzingatia viwango vya virusi (viral load). Hivyo, unashauriwa kupima na kuongeza na washauri nasaa (Daktari) watakaofuatilia uwingi wa virudi na kukushauri muda muafaka wa kushika ujauzito.

Photo Credit: (David Bassey/MSU Reporter)  & Avert.org

 

Ugonjwa wa HIV/AIDS umekuwa janga kubwa sana duniani kwa sasa kutokana kuathiri watu wengi  na kukosekana kwa tiba ya ugonjwa huu. Maambukizi ya ugonjwa wa HIV/AIDS hufahamika kama maambukizi ya  VVU (Virusi vya Ukimwi). Mtu anapopata magonjwa nyemelezi (opportunistic infections) ndiyo huwa tunasema mtu amepata ugonjwa wa UKIMWI au AIDS.

Makala hii ni majibu ya swali la msomaji wetu mmoja aliyetaka kufahamu hatua za ugonjwa wa VVU/UKIMWI aliyesema “Ningependa kujua siteji 1-4 za vvu ukimwi na dalili zake zote”. Swali ambalo liliniweka kwenye wakati mgumu sana kwani hatua za ugonjwa huu zinajumuisha magonjwa mbalimbali ambayo mengine ni vigumu sana kuyaelezea kwa lugha yetu ya kiswahili. Natumai kwa kupitia makala hii tutakuwa tumetoa mwanga kidogo wa hatua za ugonjwa wa VVU.

Je ni kuna hatua ngapi za ugonjwa wa VVU/UKIMWI na dalili zake ni zipi?

Kwa mujibu wa uanishaji uliofanywa na wataalamu wa shirika la Afya Duniani yaani WHO, kuna hatua (stages) kuu nne za ugonjwa wa VVU/UKIMWI ambazo ni: 

Hatua ya kwanza [Primary HIV Infection]

Hatua hii huwa kwa muda wa wiki nne. Ni asilimia 20 tu ya watu wenye maambukizi ya VVU walio kwenye hatua hii ambao hupata dalili na viashiria vikali vya ugonjwa huu lakini mara nyingi  madaktari hushindwa kutambua kama mgonjwa amepata maambukizi ya VVU kutokana na dalili na viashiria vyake hapa kufanana sana na dalili za magonjwa mengine. Mgonjwa aliye katika hatua hii ya kwanza ya maambukizi ya VVU huweza kuonesha dalili na viashiria kama vile kuvimba tezi (swollen lymph glands), kupatwa na homa kali, kuumwa koo (sore throat), kujihisi mchovu, kujihisi maumivu sehemu mbalimbali mwilini (body aches), kutokwa na vipele mwilini (skin rash), na pia kutapika, kuharisha au kuumwa tumbo 

Mgonjwa anayepata dalili na viashiria hivi tunasema kwamba amepata “Acute HIV infection/Acute HIV retroviral infection au seroconversion illness.” Dalili hizi hutokana na mwili wa mtu mwenye maambukizi ya VVU kuanza kutengeneza kinga dhidhi ya VVU. 

Hatua ya Pili (Clinically Asymptomatic Stage)

Katika hatua hii ambayo inaweza kudumu kwa muda wa miaka kumi, mgonjwa anakuwa haonyeshi dalili/viashiria vyovyote vile isipokuwa anaweza kuwa na tezi zilizovimba [swollen lymph nodes]. Kiwango cha VVU kwenye damu hupungua sana lakini mgonjwa anaweza kuambukiza mtu mwingine yoyote na vipimo vya VVU vina uwezo wa kutambua uwepo wa maambukizi y VVU katika damu. 

Tafiti mablimbali zimeonesha kwamba VVU katika mwili huwa bado zinazaliana [active] na hukimbilia/hujificha kwenye tezi [lymph nodes]. Kutokana na kujificha kwake katika hatua hii, kipimo cha kupima wingi wa virusi vya ukimwi (Viral load test) katika mwili hutumiwa sana ili kuweza kutambua uwepo wa VVU. Kipimo hiki pia husaidia katika kumpangia mgonjwa tiba yake.

 

Hatua ya Tatu [Symptomatic HIV infection]

Kutokana na kuongezeka kwa wingi wa VVU katika mwili, kinga ya mwili huzidi kudhoofika na  hii husababishwa na;

  • Tezi na tishu zilizoathiriwa na VVU huharibika kutokana na maambukizi ya muda mrefu

  • VVU hubadilika badilika na kuwa na uwezo zaidi wa kuathiri tishu na sehemu mbalimbali za mwili na hata kuziua/kuziharibu seli zinazokinga mwili kutokana na maambukizi zinazojulikana kama T helper cell

  • Mwili hushindwa kumudu uharibifu wa T helper cell na kushindwa kuzalisha seli nyingine mpya. 

Dawa za kuvubaisha VVU au Antiretroviral therapy huanza kutumiwa wakati seli aina ya CD4 zinapopungua na kuwa kiwango cha chini sana. Kupungua kwa seli hizi za CD4 ni kielelezo cha kinga ya mwili kuwa dhaifu. Matumizi ya dawa hizi huboresha kinga ya mwili na kumfanya mgonjwa kuishi kwa muda mrefu bila kuonyesha dalili au viashiria vyovyote vile [yaani kumrudisha mgonjwa katika hatua ya pili]. 

Kama mgonjwa wa VVU hatumii dawa za kuvubaisha VVU au anatumia ARV's ambazo hazimsaidii au hazifanyi kazi vizuri mwilini mwake, basi mgonjwa ataendelea kuingia kwenye hatua ya nne ya Ukosefu wa Kinga Mwilini (Ukimwi) au AIDS. 

Katika ulimwengu wa leo, kuna njia nyingi za kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU). Njia mojawapo ni kwa wapenzi kufuata maadili ya dini na kuacha kushiriki tendo la ndoa nje ya ndoa.

Kama umeshindwa, basi unashauriwa kupunguza idadi ya washirika wa mapenzi na kuzingatia njia za kujikinga na maambukizi ya magonjwa ya zinaa ikiwemo Ukimwi. Njia moja inayoshauriwa ni matumizi ya mipira ya kiume (Condom), matumizi sahihi ya mipira hii huweza kukukinga na maambukizi ya magonjwa ya zinaa ikiwemo virusi vya ukimwi na magonnjwa mengine. Pia, husaidia kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa mengine yanayosambazwa kupitia tendo la kujamiina kama Zika au Ebola, bila kusahau mimba zisizo tarajiwa, hivyo matumizi ya kondomu yana faida kubwa sana kwa mwanamume.

Leo hii tutaangalia vitu vya msingi vya kuzingatia unapotumia mipira hii;

1. Hakikisha unatumia condom kila wakati unapofanya ngono, usiwe na machaguo ya kwa nani utatumia na kwa nani hautumiaa au kumuamini mtu kwa fikira. Jenga kuwa matumizi ya kondomu ni moja ya sehemu muhimu ya tendo lako la ndoa.

2. Hakikisha unatumia condom kabla ya kuanza ngono. Kuna baadhi ya watu huanza kwanza ngono bila kutumia condom na huvaa baadae wakiwa wanakaribia kumaliza. Kwa kufanya hivi, kunakuweka katika hatari ya kupata maambukizi ya ya magonjwa ya zinaa ikiwemo virusi vya VVU kwa sababu, viusi vya magonjwa haya havina mua maarumu, maambukizi hutokea pale tuu kunapokuwa na mazingira yanayowezesha muingiliano wao, kama machubuko ambayo si rahisi kuiona kwa macho.

3. Hakikisha condom unayotumia haijapita muda wake. Kwa kutumia kondomu iliyopita muda wake kunaweza kusababisha kupasuka ukiwa kwenye tendo na kukuweka katika hali ya hatari kupata maambukizi kwa sababu ni wachache sana hubaini kama kondomu imepasuka au kuwa na nguvu ya kuacha na kubadili kondomu pindi wanapoanza na kutokea upasukaji.

4. Hakikisha condom ipo kwenye hali yake ya uimara. Matumizi ya condom iliyoanza kupasuka au yenye vitobo huweza kupelekea kupasuka inapowamba na kukuweka kwenye hatari zaii.

5. Hifadhi kwenye hali inayotakiwa; Kuhifadhi conom kwenye mazingira yenye joto zaidi huathiri ubora wake

Unaweza kununua kondomu kutoka katika duka la dawa lolote lililo karibu yako, unaweza kutumia TanzMED App kutafuta duka lililo karibu nawe au kwenda moja kwa moja kwenye orodha ya maduka hapa https://tanzmed.co.tz/directory/pharmacies,5.html 

 

Madhara ya ugonjwa wa kaswende katika mfumo wa mishipa ya  fahamu hutokea  miaka 10-20 baada ya mtu kuugua ugonjwa wa kaswende na ambaye hakupata tiba yoyote hapo awali. Madhara haya huonekana kwenye uti wa mgongo na kwenye ubongo.
Kuna aina nne ya neurosyphilis kama ifuatavyo:
1.Asymptomatic – Katika aina hii mgonjwa anakuwa hana dalili zozote. Aina hii ndio huonekana sana kwa wagonjwa ambao hawakupata tiba hapo awali.
2.General paresis
3.Meningovascular
4.Tabes dorsalis
General paresis hutokana na kuathirika kwa ubongo na hivyo kuleta upungufu katika ufanyaji kazi wa ubongo (impairement of mental function). Aina hii pia huweza kutokea kwa wagonjwa wa kisonono (gonorrhoea).
 
Dalili za general paresis
•Kupungua uwezo wa kuzungumza (aphasia)
•Kupungua uwezo wa kufanya maamuzi (impaired judgement)
•Kutokuwa na uwezo wa kuhesabu kitu chochote
•Kupungua kuhamasishika (impaired motivation)
•Kutokuwa na kumbukumbu ya vitu vilivyopita muda mrefu (loss of long term memory)
•Kutokuwa na kumbukumbu ya vitu vilivyopita karibuni/muda mfupi (loss of short term memory or recent events)
•Degedege
•Kushindwa kutembea au kutumia miguu, mikono na viungo vyengine vya mwili
•Personality changes  kama 
a.Delusions, kuona au kusikia vitu ambavyo visivyokuwepo (hallucinations)
b. Kukasirika kwa haraka (irritability)
c.Inappropiate moods
d.Low mood
 
Viashiria vya general paresis
•Mboni za jicho kuwa katika umbile ambalo si la kawaida
•Mboni kushindwa kupepesuka  (changes in pupil response)
•Loss of sense of vibration or position
•Kushindwa kusimama wakati mtu amefunga macho (romberg test)
•Kushindwa kutembea vizuri
•Viungo vya mwili kuwa dhoofu
•Matatizo ya kusahau
 
Vipimo vya uchunguzi
•FTA- ABS – Kipimo cha damu kinachofanya kuangalia antibodies za bakteria aina ya Treponema Pallidum  wanaosababisha kaswende
•RPR  (Rapid Plasma Reagin) – Kipimo hiki pia huangalia antibodies za Treponema Pallidum katika damu ya  wagonjwa wa kaswende
•VDRL (Veneral Disease Research Laboratory)- Kipimo cha kuangalia antibodies za  Treponema Pallidum, kipimo hiki kimeshahabiana sana na kipimo cha RPR.
•Lumbar Puncture – Kipimo cha kuchukua maji ya uti wa mgongo ili kuangalia kiwango cha sukari katika maji hayo, presha yake, protini, chembechembe nyekundu na nyeupe za damu, rangi yake, madini ya chloride. Kipimo hiki ni muhimu sana kwani husaidia kutambua kama kuna magonjwa mengine kama ugonjwa wa uti wa mgongo, multiple sclerosis, hypoglycemia, kiharusi, saratani, jipu nk.
•Cranial CT na MRI – CT Scan ya kichwa pamoja na kipimo cha MRI ili kuangalia kama kuna magonjwa mengine mbali na kaswende na kuangalia sehemu ipi ya ubongo iliyoathirika.
•Nerve conduction test – Kipimo cha neva za mwilini
•Vipimo vya macho
 
Dalili za meningovascular ni;
•Mboni kuwa ndogo
•Kupooza kutokana na kuathirika kwa neva mbalimbali
•Kuharibika mishipa ya damu mwilini
•Kupooza upande mmoja wa mwili
•Matatizo ya kumeza chakula – Kumeza chakula kwa shida
•Degedege
•Kupooza neva ya jicho (optic neuropathy)
•Chorioretinitis
•Kiziwi
•Vertigo nk.
 
Vipimo vya uchunguzi vya meningovascular
A.Vipimo vya hepatitis
B.ELISA for HIV – Kipimo cha ugonjwa wa ukimwi
C.PCR (Polymerase Chain Reaction) – Kipimo cha kuangalia vina saba vya bakteria mbalimbali kama Chlamydia trachomatis, Trichomonas vaginalis nk.
D.Urinalysis (urine test) – Vipimo vya mkojo
Tabes Dorsalis husababisha kudhoofika kwa viungo vya mwili kutokana na kuathirika kwa uti wa mgongo pamoja na mishipa ya fahamu. Hali hii ni hatari sana kwani ina kawaida ya kuwa endelevu na huweza kusababisha kifo kwa mgonjwa.
 
Dalili za Tabes Dorsalis
•Kutembea kwa shida
•Mgonjwa kutembea huku ametanua miguu sana (wide based gait)
•Kudhoofika viungo vya mwili
•Loss of coordination
•Abnormal sensation (lightening pains)
•Loss of reflexes
 
Vipimo vya uchunguzi vya Tabes Dorsalis
•CBC (Complete Blood Count) – Kipimo cha wingi wa damu, kuangalia aina za chembechembe za damu nk.
•Urinalysis – Kipimo cha mkojo
•Lumbar Puncture for CSF – Kipimo cha kuangalia maji ya uti wa mgongo kama nilivyoeleza hapo juu.
•CT Scan – Kipimo cha CT Scan ya kichwa, uti wa mgongo, moyo, mishipa ya damu.
•MRI ya kichwa
•VDRL, RPR, FTS-ABS, MHA-TP – Vipimo vya kuangalia antibodies za bakteria aina ya Treponema Pallidum kama nilivyowahi kueleza.
 
Tiba ya Neurosyphilis
Tiba ya aina zote za neurosyphilis huusisha kwanza kutibu ugonjwa wa kaswende kwa kutumia dawa za antibiotics aina ya penicillin G au doxycyline kwa wale wanaopata madhara ya penicillin. Hata hivyo kwa wale wenye matatizo na penicillin ni bora kumueleza Daktari mapema ili achukue hatua zinazostahili.
Kwa wale wagonjwa wasioweza kula, kuvaa nguo, wale waliopooza viungo, wasioweza kuzungumza, watahitaji tiba mbalimbali kama rehabilitation therapy, physical therapy, occupation therapy, speech therapy nk.
Dawa za maumivu na  degedege zinaweza kutumika kwa wale wenye kupata maumivu na degedege. Kwa wale viziwi, watahitaji vifaa maalum vya kuwasaidia kusikia (hearing aids) baada ya kuonana na Daktari wa masikio, pua na koo.

 

Madhara ya ugonjwa wa kaswende katika mfumo wa mishipa ya  fahamu hutokea  miaka 10-20 baada ya mtu kuugua ugonjwa wa kaswende na ambaye hakupata tiba yoyote hapo awali. Madhara haya huonekana kwenye uti wa mgongo na kwenye ubongo.
Kuna aina nne ya neurosyphilis kama ifuatavyo:
1.Asymptomatic – Katika aina hii mgonjwa anakuwa hana dalili zozote. Aina hii ndio huonekana sana kwa wagonjwa ambao hawakupata tiba hapo awali.
2.General paresis
3.Meningovascular
4.Tabes dorsalis
General paresis hutokana na kuathirika kwa ubongo na hivyo kuleta upungufu katika ufanyaji kazi wa ubongo (impairement of mental function). Aina hii pia huweza kutokea kwa wagonjwa wa kisonono (gonorrhoea).
 
Dalili za general paresis
•Kupungua uwezo wa kuzungumza (aphasia)
•Kupungua uwezo wa kufanya maamuzi (impaired judgement)
•Kutokuwa na uwezo wa kuhesabu kitu chochote
•Kupungua kuhamasishika (impaired motivation)
•Kutokuwa na kumbukumbu ya vitu vilivyopita muda mrefu (loss of long term memory)
•Kutokuwa na kumbukumbu ya vitu vilivyopita karibuni/muda mfupi (loss of short term memory or recent events)
•Degedege
•Kushindwa kutembea au kutumia miguu, mikono na viungo vyengine vya mwili
•Personality changes  kama 
a.Delusions, kuona au kusikia vitu ambavyo visivyokuwepo (hallucinations)
b. Kukasirika kwa haraka (irritability)
c.Inappropiate moods
d.Low mood
 
Viashiria vya general paresis
•Mboni za jicho kuwa katika umbile ambalo si la kawaida
•Mboni kushindwa kupepesuka  (changes in pupil response)
•Loss of sense of vibration or position
•Kushindwa kusimama wakati mtu amefunga macho (romberg test)
•Kushindwa kutembea vizuri
•Viungo vya mwili kuwa dhoofu
•Matatizo ya kusahau
 
Vipimo vya uchunguzi
•FTA- ABS – Kipimo cha damu kinachofanya kuangalia antibodies za bakteria aina ya Treponema Pallidum  wanaosababisha kaswende
•RPR  (Rapid Plasma Reagin) – Kipimo hiki pia huangalia antibodies za Treponema Pallidum katika damu ya  wagonjwa wa kaswende
•VDRL (Veneral Disease Research Laboratory)- Kipimo cha kuangalia antibodies za  Treponema Pallidum, kipimo hiki kimeshahabiana sana na kipimo cha RPR.
•Lumbar Puncture – Kipimo cha kuchukua maji ya uti wa mgongo ili kuangalia kiwango cha sukari katika maji hayo, presha yake, protini, chembechembe nyekundu na nyeupe za damu, rangi yake, madini ya chloride. Kipimo hiki ni muhimu sana kwani husaidia kutambua kama kuna magonjwa mengine kama ugonjwa wa uti wa mgongo, multiple sclerosis, hypoglycemia, kiharusi, saratani, jipu nk.
•Cranial CT na MRI – CT Scan ya kichwa pamoja na kipimo cha MRI ili kuangalia kama kuna magonjwa mengine mbali na kaswende na kuangalia sehemu ipi ya ubongo iliyoathirika.
•Nerve conduction test – Kipimo cha neva za mwilini
•Vipimo vya macho
 
Dalili za meningovascular ni;
•Mboni kuwa ndogo
•Kupooza kutokana na kuathirika kwa neva mbalimbali
•Kuharibika mishipa ya damu mwilini
•Kupooza upande mmoja wa mwili
•Matatizo ya kumeza chakula – Kumeza chakula kwa shida
•Degedege
•Kupooza neva ya jicho (optic neuropathy)
•Chorioretinitis
•Kiziwi
•Vertigo nk.
 
Vipimo vya uchunguzi vya meningovascular
A.Vipimo vya hepatitis
B.ELISA for HIV – Kipimo cha ugonjwa wa ukimwi
C.PCR (Polymerase Chain Reaction) – Kipimo cha kuangalia vina saba vya bakteria mbalimbali kama Chlamydia trachomatis, Trichomonas vaginalis nk.
D.Urinalysis (urine test) – Vipimo vya mkojo
Tabes Dorsalis husababisha kudhoofika kwa viungo vya mwili kutokana na kuathirika kwa uti wa mgongo pamoja na mishipa ya fahamu. Hali hii ni hatari sana kwani ina kawaida ya kuwa endelevu na huweza kusababisha kifo kwa mgonjwa.
 
Dalili za Tabes Dorsalis
•Kutembea kwa shida
•Mgonjwa kutembea huku ametanua miguu sana (wide based gait)
•Kudhoofika viungo vya mwili
•Loss of coordination
•Abnormal sensation (lightening pains)
•Loss of reflexes
 
Vipimo vya uchunguzi vya Tabes Dorsalis
•CBC (Complete Blood Count) – Kipimo cha wingi wa damu, kuangalia aina za chembechembe za damu nk.
•Urinalysis – Kipimo cha mkojo
•Lumbar Puncture for CSF – Kipimo cha kuangalia maji ya uti wa mgongo kama nilivyoeleza hapo juu.
•CT Scan – Kipimo cha CT Scan ya kichwa, uti wa mgongo, moyo, mishipa ya damu.
•MRI ya kichwa
•VDRL, RPR, FTS-ABS, MHA-TP – Vipimo vya kuangalia antibodies za bakteria aina ya Treponema Pallidum kama nilivyowahi kueleza.
 
Tiba ya Neurosyphilis
Tiba ya aina zote za neurosyphilis huusisha kwanza kutibu ugonjwa wa kaswende kwa kutumia dawa za antibiotics aina ya penicillin G au doxycyline kwa wale wanaopata madhara ya penicillin. Hata hivyo kwa wale wenye matatizo na penicillin ni bora kumueleza Daktari mapema ili achukue hatua zinazostahili.
Kwa wale wagonjwa wasioweza kula, kuvaa nguo, wale waliopooza viungo, wasioweza kuzungumza, watahitaji tiba mbalimbali kama rehabilitation therapy, physical therapy, occupation therapy, speech therapy nk.
Dawa za maumivu na  degedege zinaweza kutumika kwa wale wenye kupata maumivu na degedege. Kwa wale viziwi, watahitaji vifaa maalum vya kuwasaidia kusikia (hearing aids) baada ya kuonana na Daktari wa masikio, pua na koo.
Ukurasa 2 ya 2