Pakua TanzMED App?

Tohara kwa wanaume ni oparesheni inayohusu kuondolewa kwa sehemu ya ngozi au ngozi yote inayofunika kichwa cha uume, na imekuwa ikifanywa na baadhi ya watu katika makabila na dini mbalimbali kwa zaidi ya maelfu ya miaka.
Kwa sasa tohara kwa wanaume imeamsha mvuto mkubwa wa kisayansi na uchunguzi kwa sababu utafiti umethibitisha kuwa wanaume waliotahiriwa wana viwango vidogo vya maambukizo ya virusi vya ukimwi (VVU) kuliko wasiotahiriwa.

Aidha ueneaji wa VVU ni mdogo kwa jumla katika jamii zinazotahiri wanaume kuliko zile ambazo wanaume hawatahiriwi. Kiasi cha asilimia 20 cha wanaume duniani kote inasemekana kuwa wametahiriwa, iwe mara baada ya kuzaliwa
au wakati wa balehe, kwa kawaida kutokana na sababu za kiutamaduni, kiafya au dini. Si nchi zote Barani Afrika zenye takwimu, kuhusu ushauri wa tohara kwa wanaume, hata hivyo kwa kawaida inakadiriwa kuwa chini ya
asilimia 20 ya wanaume kusini mwa Jangwa la Sahara wametahiriwa, kati ya asilimia 50 na 80 katika sehemu nyingi za Afrika ya Mashariki, na zaidi ya asilimia 80 au zaidi katika Bara la Afrika.


Kinachofahamika ni Nini?

Utafiti wa majaribio wa mara ya tatu Afrika Mashariki na Kusini ambao umefanywa, miaka ya hivi karibuni kupima kwa njia ya utafiti uliodhibitiwa, manufaa ya tohara kwa wanaume katika kuzuia maambukizi ya VVU. Utafiti uliofanywa katika Jimbo la Gauteng,Afrika Kusini, ulisimamishwa mapema zaidi kuliko ulivyopangwa kwa sababu matokeo yamethibitisha kuwa tohara ilikuwa kinga dhidi ya maambukizi ya VVU na wachunguzi wamependekeza kuwa utaratibu huo uendelee kwa watu zaidi ya 3,274 wanaoshiriki.

 •  Wanaume waliotahiriwa waliofanyiwa utafiti wameonekana kuwa ni asilimia 60 pungufu ya uwezekano wa kuambukizwa VVU kuliko wasiotahiriwa.
 •  Iwapo utafiti wa majaribio unaoendelea nchini Kenya na Uganda unaowahusisha wanaume 8,000 utatoa matokeo sawa na yale ya Afrika Kusini, tohara kwa wanaume itaungana na zana kama vile Kondomu za kiume na za kike kama njia kuu za kuzuia maambukizi ya VVU.
 •  Tayari msingi wa shauku umeonekana nchini Botswana na Swaziland, nchi mbili miongoni mwa nchi zilizoathiriwa sana na VVU/UKIMWI.
 •  Zaidi ya asilimia 80 ya wanaume waliofanyiwa utafiti Botswana wamesema kuwa wangependa kutahiriwa iwapo utaratibu huo ni salama na wenye gharama nafuu.
 •  Nchini Swaziland zile hospitali ambazo hazikuwa zikitahiri, sasa zimekuwa zikitahiri watu 10-15 kwa juma na zina orodha ndefu ya watu wanaosubiri huduma hiyo

 Hivyo basi kutokana na faida hizi, wanamume wanashauriwa sana kufanyiwa tohara, kwa kufanya tohara siyo tuu watakuwa wamepunguza uwezekano wa kuambukizwa VVU, bali pia watakuwa wamepunguza uwezekano wa kuwaambukiza wengine kama wao wanaishi na virusi vya ukimwi.

Ikumbukwe pia, kufanya tohara pekee hakukuondolei uwezekano wa kuambukizwa VVU, hivyo unashauriwa kuendelea kutumia njia nyingine zilizo salama za kujikinga na maambukizi ya VVU.

 

Credit: www.nacp.go.tz

Ni muhimu kwa mzazi/ mlezi kufahamu aina ya chakula kimfaacho mtoto wake hususani yule aliye katika umri wa miezi tisa na nusu mpaka miaka  sita. Aina hizi za vyakula na jinsi ya uandaaji wake hutofautiana sana na zile anazokula mtoto mkubwa au mtu mzima. Leo, mtaalamu wetu wa  mapishi, Chef Issa anatuletelea ratiba ya chakula cha mtoto wa umri huo.

ratiba-ya-mlo-wa-mtoto

 

Kwa makala ya awali na majadiliano juu ya ratiba ya chakula kwa moto unaweza kusoma Ratiba ya Chakula cha Mtoto Kuanzia Miezi 9 Mpaka Miaka 6

Hakuna ubaya wowote kwa mtu kutaka kupendeza. Swala la kuonekana mzuri au kuwa mtanashati limekuwa sehemu muhimu ya maisha ya binadamu hususani upande wa dada zetu. Si kitu cha ajabu maana tangu enzi za mababu , tunasoma katika historia jinsi mwanamke alivyosifiwa kwa uzuri na urembo wake

Mazoezi yanayokuza na kuyapa makalio na nyonga muonekano mzuri

Zoezi muhimu kuliko yote, ambalo kwa bahati mbaya kinadada wengi hulikwepa, ni zoezi lijulikanalo kitaalamu kama ’’squarts’’ yaani kuchuchumaa kwa kiswahili rahisi. Kufanya squarts, waweza tumia uzito au waweza fanya squarts bila kutumia uzito wowote. Unachukua uzito unaoweza kuhimili, na kuuweka mabegani (kumbuka uzito huu unatakiwa uwe umewekwa pande zote kwa uwiano sawa ukiunganishwa na bomba ambalo ndiyo unaliweka mabegani).

Simama wima miguu yako ikiwa imetengana kiasi, halafu chuchumaa taratibu, na kunyanyuka taratibu. Rudia mzunguko huu mara 6 mpaka 8, kwa kila seti, na ni vema kufanya seti tatu mpaka tano. Kumbuka waweza fanya squarts bila kuwa na uzito wowote, cha muhimu ni kuikutanisha mikono yako pamoja nyuma ya kichwa wakati wote unapokuwa unachuchumaa na kusimama.

                                                                                 

Kwa maelezo zaidi, soma : Nyonga na Umbo lililojengeka la Ndoto Yako

 

 

 

 

 

 

 

Dengue ni moja kati ya homa kali inayodhoofisha na  kuambatana na maumivu makali. Kwa sasa hakuna kinga ya homa ya dengue, njia pekee ya kuepuka ugonjwa huu ni kuzuia kuumwa na mbu anayesambaza homa ya dengue.

Dalili za ugonjwa huu ni

•Homa kali ya ghafla

•Maumivu makali ya kichwa

•Macho kuuma

•Maumivu ya viungo

•Kichefuchefu

•Kutapika

•Vipele ambavyo hutokea siku nne baada ya homa kuanza

•Kutoka damu puani, kwenye fizi na kuchubuka kirahisi

Mara nyingi dalili huwa sio kali na wengi hudhania ni homa ya mafua au maambikizi mengine ya virusi. Dalili hizi huanza kutokea baada ya wiki mbili, lakini kwa wengi huchukua wiki moja ya kwanza na tayari utaanza kuona dalili za dengue.

Kwa maelezo zaidi, kuhusu vipimo vyake na matibabu, tafadhali soma hapa Ufahamu ugonjwa wa Homa Ya Dengue

Katika dunia ya leo, wengi wetu tumekuwa tukifanya kazi kwa muda mwingi, hata kutufanya tukose muda wa kufanya mazoezi. Siku hizi, wengi wa wafanyakazi wamekuwa kwenye magari, ofisini kwenye kiti kurudi tena kwenye gari na kulala, hivyo hukosa hata muda wa kupasha / kunyoosha viungo.

Leo, tutakufahamisha moja ya mazoezi yenye matokeo mazuri kwa viungo vya binadamu tena bila ya kutumia kifaa chochote. Na hii si nyingine bali ni Push up. Push up ni moja ya mazoezi yanayojenga afya njema kwani push up zinasaidia kuimarisha kifua, mabega misuli ya mikono.

Jinsi ya kufanya push up: Uso wako ukiwa unatizama chini, weka mikono yako kwenye sakafu, itanue izidi kidogo mabega yako (kama inavyoonekana kwenye picha).

Hakikisha vidole vyako vya miguu vipo sakafuni, kama hii ni ngumu, basi unaweza kuanza kwa kuweka magoti yako chini. Hakikisha mwili wako umenyooka kuanzia vidoleni hani kichwani. Kunja mabega yako mpaka uwe kama unagusa sakafu. Rudi juu kwa kujinyanyua kwa kutumia mabega, hakikisha mwili wako umenyooka mwanzo hadi mwisho. Fanya hivi mara kadhaa ukiwa unaongeza idadi siku hadi siku.

Hauna haja ya Gym, hauna haja ya kununua kifa chochote, unaweza kufanya zoezi hili hata ukiwa ofisini. Na hii ndio dondoo yako ya leo. 

mtoto-akilia

Malezi ya mtoto ni moja ya vitu muhimu vya kujifunza ukiwa kama mzazi, ni mara nyingi tumekuwa tukiona watoto wakilia bila kujua nini cha kufanya. Leo hii tudondoe njia moja wapo ya kumbembeleza mtoto.

Akiwa tumboni mwa mama, mara kwa mara mtoto alikuwa akisikia mapigo ya moyo ya mama. Hali hii ndiyo sababu kubwa ya watoto wengi kupendelea kubebwa na mama zao. Hata hivyo kuna aina nyingine za sauti zinazoweza pia kusaidia kumtuliza mtoto. Mzazi ama mlezi unaweza kujaribu kuweka muziki wa taratibu au kumuimbia mtoto nyimbo za kubembeleza kwa sauti ya chini sana. Unashauriwa kutokuweka miziki ya haraka au yenye sauti kubwa kwa sababu inaweza kumwondolea hali yake ya utulivu na hivyo kumfanya ashindwe kuacha kulia. Kwa makala iliyokamilika, nenda Hapa.

Je unataka kupokea dondoo za kila siku kwenye email yako, jiunge na mlisho wa habari kwa kwenda HAPA

Tendo la ndoa husaidia kupunguza ama kutoa msongo wa mawazo, na kama tunavyojua kuwa msongo wa mawazo huchangia kupandisha sukari kwa mtu mwenye Kisukari na pia hutoa au hupunguza hatari ya kupata shinikizo la damu,kasi ya mapigo ya  moyo wakati wa tendo la inaweza kupunguza hatari ya kupata shinikizo la dawa na kupanda kwa sukari,wataalamu wanasema sio tu kwa mtu mwenye tatizo la kisukari ila hii ni kwa kila mtu,kufanya tendo la ndoa.

Kwa makala zaidi juu ya umuhimu wa tendo la noa kwa watu wenye kisukari temmbelea hapa .

ndoa-kuishi-sana

Tafiti nyingi zinaonesha kuwa watu wengi walio funga ndoa wamewapiku wale wasio funga ndoa kwenye umri wa kuishi. Watafiti hawa wamebainisha kuwa mfumo wa maisha wa mtu aliye kwenye ndoa huchangia mabadiriko yake kifikira na hata kiuchumi hivyo kwa njia moja au nyingine ndio sababu ya wale walio kwenye ndoa kuishi kwa muda mrefu.

Wakati ndoa huchangia kuongea muda wa kuishi na faida nyingine nyingi kwenye afya ya binadamu, tafiti zinaonesha kuwa wale walio achika / tengana au wajane umri wao wa kuishi huwa mfupi kuliko wale wasioolewa /oa kabisa.

Zipo njia nyingi ya kutibia maumivu ya hedhi.

Mojawapo ni kuweka chupa au mfuko wenye maji ya moto kwenye sehemu ya chini ya tumbo (isiwe moto mkali wa kuunguza ngozi).


Dawa za kutuliza maumivu kama ibuprofen, mefenamic acid, naproxen.


Matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango pia husaidia kupunguza maumivu ya hedhi. Kama ilivyo kwa dawa nyingine, ni muhimu kupata ushauri wa kitaalam kabla ya kuanza kutumia dawa hizi. 

Iwapo njia hizi hazifanikiwi kutuliza maumivu ya hedhi, vipimo zaidi vinahitajika ili kugundua chanzo cha maumivu hayo.

Miongoni mwa vipimo vinavyohitajika ni vipimo vya magonjwa ya infection ya njia ya uzazi pamoja na upasuaji ili kuona uwepo wa endometriosis na kuiondoa (picha zinaonyesha jinsi upasuaji huo unavyofanyika kwa matundu madogo na kamera bila kafungua tumbo).

Iwapo maumivu ni makali sana na hayatibiki kwa dawa, mgonjwa asiyekuwa na mpango wa kupata mtoto hushauriwa kuondoa kifuko cha uzazi.

Tezi dume ni sehemu mojawapo ya mfumo wa uzazi wa kiume. Mojawapo ya kazi za tezi dume ni kutoa majimaji yanayochanganyika na mbegu za kiume (sperms) wakati wa kilele cha tendo la ngono. Mchanganyiko huu wa mbegu pamoja na majimaji hayo hufanya shahawa (semen). Mchanganyiko huu wa mbegu pamoja na majimaji hayo hufanya shahawa (semen). Aidha majimaji hayo husaidia kuzipa mbegu za kiume nguvu ya kusafiri kwenye uke mpaka kufikia kwenye mirija ya fallopian tayari kwa utungisho na yai la kike.

Kwa kadiri mwanaume anavyozeeka, ni jambo la kawaida pia kwa tezi dume kuongezeka ukubwa na kuvimba. Hali hii kitabibu huitwa Benign Prostate Hyperplasia.(BPH)

Pichani, ni muonekano wa tezi dume ya kawaida(normal prostate) na tezi dume iliyovimba(enlarged prostate) zinavyokuwa

Madhara ya BPH

BPH kama ilivyo saratani ya tezi dume, inaweza kumletea mgonjwa madhara (complications) kadhaa. Madhara hayo ni pamoja na

 • Mkojo kushindwa kutoka (retention of urine)
 • Mgandamizo kwenye kibofu cha mkojo
 • Vijiwe kwenye kibofu cha mkojo
 • Uambukizi katika njia ya mkojo (UTI)
 • Madhara katika figo au kibofu
 • Shinikizo la damu
 • Kushindwa kutoa shahawa kwenye uume (retrograde ejaculation)
 • Maambukizi mbalimbali
 • Nimonia (Pneumonia)
 • Damu kuganda
 • Uhanithi

Kuhusu dalili zake, vipimo,uchunguzi na matibabu fuatilia hapo Kuvimba kwa Tezi Dume (Benign Prostate Hyperplasia BPH)

Ukurasa 1 ya 4
No Internet Connection