Image

Ugonjwa wa pumu ni ugonjwa ambao huathiri sehemu ya kupitisha hewa kwenda kwenye mapafu ya binadamu zinazojulikana kitaalamu kama bronchioles.

Mtu mwenye pumu huwa na mcharuko mwili sugu (chronic Inflammation) kwenye mirija yake ya kupitishia hewa (bronchioles tubes) hali ambayo husababisha kuvimba kwa kuta za mirija hii, kujaa kwa ute mzito (mucus) na kupungua kwa njia ya kupitishia hewa, hali ambayo humfanya muathirika kushindwa kuvuta na kutoa hewa nje na hivyo kupumua kwa shida sana. Hali hii inaweza kudumu kwa muda mfupi au mrefu kiasi cha kuhitaji tiba ili kumuwezesha mgonjwa kupata nafuu.

Kutokana na  kuwepo kwa msuguano na uzuiaji wa kupitisha hewa wakati wa kupumua hwa nje, pumu hujulikana pia kama obstructive lung disease . Mtu aliye na pumu, huwa nayo kipindi chote cha maisha yake.  

Nini madhara ya pumu kwa mama wajawazito?

Tafiti kadhaa zimeonesha kuwa takribani theluthi moja ya wajawazito wenye pumu hupata nafuu kipindi cha ujauzito, theluthi  nyingine hupata matatizo kipindi hiki na theluthi iliyobakia huwa na hali ya kawaida kama kabla ya ujauzito. Kwa kawaida dalili za pumu hujirudia kama awali miezi mitatu baada ya kujifungua. 

Dalili za pumu kwa mjamzito zinaweza kuwa mbaya zaidi kuanzia wiki ya 24-36 (mwezi wa sita mpaka wa nane). Ni mara chache sana mjamzito anapata shambulizi la pumu wakati wa kujifungua. Inakisiwa kuwa, ni asilimia 10 tu ya wajawazito wenye pumu wanaopata shambulizi la pumu wakati wa kujifungua.

Baadhi ya dawa zinazotumika wakati wa ujauzito na baada ya kujifungua huongeza madhara ya pumu, hivyo ni vizuri  kumueleza daktari kwamba una pumu kabla ya kupewa dawa. Aidha  na si vyema kunywa dawa kwa mazoea.

Wanawake wenye pumu isiyoweza kuthibitiwa kipindi cha ujauzito hupata madhara ya kuzaa mtoto njiti (premature baby), kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo, kifafa cha mimba, shinikizo la damu (Hypertension), na iwapo atapata shambulizi hatari wakati wa ujauzito mtoto anaweza kufa kwa kukosa hewa ya oksijeni.

Soma hapa Ugonjwa wa Pumu (Bronchial Asthma), Chanzo, Dalili na Tiba kupata makala nzima kuhusu Pumu

Takribani asilimia 85 ya watu wenye harufu mbaya kinywani huwa na magonjwa ya kinywa na meno,Ikiwa harufu mbaya kinywani inasababishwa na magonjwa kinywani, dawa za kusafisha kinywa (mouthwash) haziwezi kuondoa tatizo zaidi ya kulifunika kwa muda tu.

Hakuna sababu ya kuona haya kumwambia daktari wa meno kuhusu harufu mbaya kinywani inayokusumbua, kwa vile kumwambia na kujadili tatizo lako ni njia ya kuelekea kwenye tiba ya uhakika. Matumizi ya nyuzi-safishi (dental floss) kila siku, kusafisha meno na ulimi kwa mswaki walau mara mbili kwa siku yaweza kuondoa harufu mbaya kinywani kwa kiasi kikubwa.

Unaweza kusoma  Mambo 10 ambayo daktari wako wa meno angependa ufahamu

 

kuosha-uso

Siku hizi watu wengi wanapenda kuonekana vijana, kuanzia kwa watu mashuhuri hadi kwa watu wasio mashuhuri, hakuna mtu anayetaka kuzeeka. Tafiti zinaonesha kuwa kuna baadhi ya matendo ambayo waweza kufanya au kuyaepuka huweza kukusaidia kupunguza au kukufanya uonekana mzee kabla ya muda.

Baadhi ya matendo yanayoweza kukufanya usionekane mzee harraka ni kama; kulala chali, kula kwa wingi samaki wa jamii ya salmoni, kujiupusha na mionzi ya moja kwa moja ya jua, kutovuta sigara na mengineyo. Lakini je unafahamu kuwa kuosha sana sura yako hukufanya uonekane mzee?

Visababishi vya amenorrhea vyaweza kugawanywa katika makundi makuu matatu, vile vinavyohusisha matatizo katika mfumo wa homoni, vile vinavyohusisha matatizo ya kimaumbile katika njia ya uzazi ya mwanamke na vile vinavyohusisha mabadiliko katika mwili wa mwanamke.

Matatizo katika mfumo wa homoni: Matatizo katika mfumo wa homoni yanaweza kuwa katika tezi za hypothalamus, pituitary au ovary.

Matatizo katika Hypothalamus

Matatizo katika hypothalamus yanayoweza kusababisha mwanamke kukosa hedhi ni pamoja na

 • Uvimbe katika ubongo karibu na tezi ya pituitary
 • Ukosefu au upungufu wa homoni zinazochochea kukua na kufanya kazi kwa via vya uzazi. Ugonjwa huu hujulikana kama Kallmann syndrome
 • Lishe duni na utapia mlo
 • Uzito mdogo kuliko kawaida (kukonda kwa kupitiliza)

Matatizo katika tezi ya Pituitary

Vyanzo vinavyohusisha tezi ya pituitary ni pamoja na

 • Kuwepo kwa kiwango kikubwa cha homoni ya prolactin katika damu au kwa kitaalamu Prolactinemia. Prolactin ni homoni inayochochea uzalishaji wa maziwa wakati wa kunyonyesha. Hali ya kuwa na prolactin nyingi katika damu inaweza kutokea iwapo kuna uvimbe unaoitwa (prolactinoma) katika tezi ya pituitary.
 • Kuwepo kwa uvimbe mwingine wowote katika tezi ya pituitary.
 • Pituitary kushindwa kufanya kazi baada ya seli zake kufa, hususani iwapo mama alipoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.
 • Kuharibika kwa tezi ya pituitary baada ya seli zake kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili.
 • Kuwa na historia ya kupata tiba ya mionzi inayohusisha tezi ya pituitary.

Matatizo katika ovary

Vyanzo vinavyohusisha matatizo katika viwanda vya kuzalisha mayai ya kike yaani ovaries ni pamoja na

 • Kutozalishwa kabisa kwa mayai (Anovulation)
 • Kuwepo kwa kiwango kingi cha homoni za kiume katika damu (Hyperandrogenemia)
 • Ovary kuwa na vifukovifuko (Polycystic ovarian syndrome) na kushindwa kufanya kazi zake vizuri. Haya ni matatizo ya homoni ambayo huwapata baadhi ya wanawake walio katika umri wa kuzaa
 • Kufa na kushindwa kufanya kazi kwa ovary kabla ya muda wake
 • Ugonjwa wa kuzaliwa unaoitwa Turner syndrome ambao humbatana na kukosekana kwa ovary au ovary kuwa changa kuliko kawaida, msichana kushindwa kuvunja ungo na msichana kuwa na kimo kifupi kuliko kawaida. Ugonjwa huu hutokana na matatizo ya kijenitikia (genetic disease)
 • Ukosefu wa kimaumbile wa ovary ambao hutokea wakati wa ukuaji
 • Kufa kwa ovary baada ya seli zake kushambuliwa na mfumo wa kinga ya mwili
 • Historia ya kuwahi kupata tiba ya mionzi au madawa yanaathiri ovary
 • Ugonjwa wa kurithi wa Galactosemia unaoambatana na kuwa na kiwango cha juu cha sukari aina ya galactose katika damu.

Matatizo ya kimaumbile katika njia ya uzazi

Matatizo ya kimaumbile katika njia ya mfumo wa uzazi wa mwanamke yanayoweza kusababisha ukosefu wa hedhi ni pamoja na

 • Mwanamke/msichana kuzaliwa bila kuwa na uke, shingo ya uzazi au mji wa mimba (uterus)
 • Kuta za uterus zinazotazamana kujishikiza pamoja
 • Utando unaozunguka uke (hymen) kuziba kabisa na kukosekana kwa tundu la kupitishia damu ya hedhi (imperforate hymen)
 • Kuwepo kwa utando unaokatiza katika uke unaozuia damu ya hedhi kushindwa kutoka.

Mabadiliko katika mwili wa mwanamke

Mambo yanayoweza kuathiri mwili wa mwanamke na kumfanya ashindwe kupata hedhi ni pamoja na

 • Kula kiasi kidogo sana cha chakula kuliko kawaida au kula kupita kiasi
 • Unene uliopitiliza au kupungua uzito/kukonda isivyo kawaida
 • Uwepo wa magonjwa sugu kama kifua kikuu
 • Utapiamlo
 • Msongo wa mawazo
 • Matumizi ya madawa ya kulevya
 • Matumizi ya baadhi ya madawa hususani baadhi ya dawa za kutibu magonjwa ya akili
 • Kuwa na hofu iliyopitiliza
 • Kufanya mazoezi ya mwili kupita kiasi

Dalili za Amenorrhea ni zipi?

Kukosa hedhi siyo ugonjwa bali ni dalili ya kuwepo kwa tatizo au ugonjwa fulani katika mwili. Kulingana na ugonjwa unaosababisha tatizo hili, kukosa hedhi kunaweza kuambatana pia na

 • Matiti kutoa maziwa wakati mwanamke si mjamzito na wala hanyonyeshi, maumivu ya kichwa na matatizo katika kuona vitu ambavyo kwa pamoja vinaweza kuashiria uwepo wa uvimbe katika ubongo
 • Mwanamke kuwa na nywele na vinyweleo vingi mwilini na kuota ndevu kama mwanaume hali inayoashiria kuwepo kwa wingi kwa homoni za kiume za androgen
 • Ukavu katika uke, kutoka jasho sana wakati wa usiku, au mabadiliko katika kupata usingizi vinaweza kuashiria matatizo katika ovary
 • Kuongezeka uzito kupita kiasi au kupungua kwa uzito isivyo kawaida
 • Mwanamke kuwa na mhemko kuliko kawaida yaweza kuashiria kuwepo kwa matatizo ya kiakili na kisaikolojia

Uchunguzi na vipimo

Msichana yeyote aliyefikia umri wa kubalehe na kuvunja ungo na ambaye bado hajaanza kupata mabadiliko yeyote ya kubalehe katika mwili wake hana budi kumuona daktari kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Aidha msichana aliyefikia umri wa miaka 16 na ambaye bado hajaanza kupata hedhi anatakiwa pia kumuona daktari kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Kwa wanawake waliokuwa wakipata hedhi kama kawaida lakini ghafla wakaacha kupata kwa muda wa miezi mitatu mfululizo au zaidi nao pia hawana budi kumuona daktari kwa ajili ya uchunguzi wa tatizo hili.

Vipimo vifuatavyo vinaweza kufanywa kuchunguza sababu za kukosa hedhi kwa mwanamke:

 • Kupima damu kwa ajili ya kuchunguza kiwango cha homoni za FSH, LH, TSH na prolactin ambazo uzalishwaji wake unachochewa na tezi ya pituitary, na pia kupima kiwango cha homoni ya estrogen inayozalishwa na ovary.
 • Kipimo cha ultrasound ya nyonga kwa ajili ya kuchunguza uwepo wa matatizo katika njia ya uzazi na pia kuchunguza hali ya ovary.
 • CT scan au MRI ya kichwa kwa ajili ya kuchunguza uwepo wa matatizo kwenye tezi ya pituitary au hypothalamus.
 • Vipimo vya kufahamu ufanyaji kazi wa tezi ya thyroid
 • Kupima damu ili kufahamu kiwango cha homoni ya prolactin katika damu
 • Kuchunguza uterus kwa kutumia aina ya X-ray inayoitwa Hysterosalpingogram na kipimo kingine kiitwacho Hysteroscopy ambacho huchunguza chumba cha uterus.

Matibabu ya kukosa hedhi

Matibabu ya kukosa hedhi yanaweza kufanyika nyumbani bila kuhitaji dawa, ingawa pia, kutegemeana na chanzo cha tatizo, yanaweza kuhitaji dawa na hata upasuaji wakati mwingine.

Matibabu yasiyohitaji dawa

 • Baadhi ya wanawake wanaopata tatizo la kukosa hedhi kwa sababu ya kujinyima kula (wanaofanya dieting) na hivyo kupata upungufu wa virutubisho mwilini, wanashauriwa kula lishe bora.
 • Baadhi ya wanawake wanaopata tatizo hili la kukosa hedhi kwa sababu ya kuongezeka uzito kupitiliza, wanashauriwa kuwa makini katika aina ya vyakula wanavyokula ili kuwa na uzito unaotakiwa.
 • Wanawake wanaokosa hedhi kwa sababu ya kufanya mazoezi ya mwili kupita kiasi wanashauriwa kujiwekea kiasi katika ufanyaji wao wa mazoezi.
 • Iwapo kukosa hedhi kumesababishwa na msongo wa mawazo, ni jambo jema kutafuta njia za kushughulikia matatizo hayo na kuyatatua ili kuondoa msongo wa mawazo
 • Inashauriwa kutokuvuta sigara na kuacha kunywa kunywa pombe.

Matibabu yanayohitaji dawa

Matibabu ya kukosa hedhi hutegemea chanzo cha tatizo. Matibabu huelekezwa katika kutibu chanzo, na iwapo chanzo cha tatizo ni matatizo ya kimaumbile, upasuaji unaweza kufanyika.

Kwa wanawake wenye matatizo ya kuwa na kiwango kingi cha prolactin, daktari anaweza kushauri matumizi ya dawa aina ya bromocriptine au pergolide.

Kwa wanawake wenye upungufu wa homoni ya estrogen au wale wenye matatizo katika ovary zao, dawa zenye kurejesha homoni hiyo zaweza pia kutumika. Wakati mwingine dawa za uzazi wa mpango zaweza kutumika kurejesha mzunguko wa hedhi na pia kusaidia kuongeza kiwango cha homoni ya estrogen mwilini.

Upasuaji

Upasuaji unaweza kufanywa iwapo kuna

 • Uvimbe katika ubongo unaoathiri tezi ya pituitary na hypothalamus
 • Matatizo katika njia ya uzazi ya mwanamke

Je kukosa hedhi kunaweza kusababisha nisipate mtoto?

Ikumbukwe kuwa, kukosa hedhi si ugonjwa bali ni dalili ya kuwepo tatizo hivyo basi iwapo tatizo hilo lina uhusiano na kutunga mimba na kupata mtoto, uwezekano wa kupata mtoto utakuwa mdogo ikiwa tatizo hilo halitashughulikiwa. Matatizo kwenye tezi za pituitary, hypothalamus pamoja na ovary ambayo yana uhusiano mkubwa na kukosa hedhi, husababisha pia tatizo la ugumba. Iwapo matatizo hayo yatashughulikiwa ipasavyo, uwezekano wa kupata kupata hedhi na hatimaye kupata mimba huwa mkubwa.

Vijiwe hivi  hutokana na  madini chumvi au tindikali mbalimbali zinazotolewa mwilini.

Vijiwe katika figo husababishwa na nini?

Kwa kiasi kikubwa, vijiwe husababishwa na kukosekana kwa usawa wa maji, madini na tindikali mwilini yaani electrolyte imbalance.

Aidha, kuna magonjwa kadhaa ambayo hupelekea kwa kiasi kikubwa kutokea kwa hali hii kama ugonjwa wa utindikali kwenye mirija ya figo (renal tubular acidosis) ugonjwa wa Dent, matatizo kwenye tezi za parathyroid (hyperparathyroidism), kukojoa chumvi chumvi za oxalate kupita kiasi (primary hyperoxaluria) na hali ya nyama za figo kuwa tepetepe (medulary sponge kidney).

Fualitlia makala hii hapa Mawe katika Figo (Kidney Stones)

Wagonjwa wa Ukimwi huathiriwa sana na ugonjwa wa figo. Ugonjwa wa figo unaohusiana na Ukimwi (HIV-Associated Nephropathy au kwa kifupi HIVAN) unaweza kusababishwa na mashambulizi ya moja kwa moja ya VVU kwenye figo au madhara yanayotokana na matumizi ya madawa ya kurefusha maisha (ARVs).

Aidha wagonjwa wengi wa Ukimwi wapo katika hatari ya kupata magonjwa ya figo kwa sababu ya kupungukiwa na maji mwilini kutokana na kichefuchefu na kutapika mara kwa mara, kupoteza chumvi mwilini, au lishe duni.

Ukubwa wa Tatizo

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2010 na Msango, Leonard(1) na wenzake katika hospitali ya Bugando, Mwanza ilionekana kuwa zaidi ya asilimia 60 ya wagonjwa walioandikishwa kuanza ARVs hospitalini hapo walikuwa na matatizo ya figo yaliyotokana na VVU. Ilionekana pia kuwa HIVAN iliwaathiri zaidi wanawake kuliko wanaume, wenye uzito mdogo, na wale waliokuwa na CD4 chini ya 200.

Huko nchini Marekani, HIVAN ni maarufu zaidi miongoni mwa wamarekani weusi wenye asili ya Afrika ikilinganishwa na wale wa asili nyingine; na hushika nafasi ya tatu kwa kusababisha magonjwa sugu ya figo (CRF) miongoni mwa watu wa jamii hiyo wenye umri wa kati ya miaka 20-64(2). Kwa ujumla HIVAN huchangia karibu asilimia 1 ya wenye ugonjwa sugu wa figo (CRF) nchini humo kila mwaka.


Kwa ujumla takwimu za dunia zinaonesha kuwa HIVAN huathiri zaidi vijana weusi, na takribani nusu ya wagonjwa wa HIVAN ni watumiaji wa madawa ya kulevya ya kujidunga(3).

Wanaume huathirika zaidi kuliko wanawake katika uwiano wa 10:1, wakati wastani wa umri wa watu wenye HIVAN ni miaka 33(4) ingawa HIVAN huwapata pia watoto(5).

Nini hutokea? (Pathofiziolojia ya ugonjwa)

Watafiti wameonesha uhusiano wa mashambulizi ya moja kwa moja ya VVU-1 kwenye figo. Pia kuna uhusiano mkubwa wa vinasaba na vyanzo vya kimazingira vinavyochochea kutokea kwa tatizo hili, hususani kwa watu weusi zaidi kuliko watu wa asili nyingine.

VVU-1 hushambulia zaidi chujio (glomeruli) pamoja na seli za kuta (epithelium) za mirija yake (renal tubules) kuliko sehemu nyingine yeyote ya figo. Hali hii husababisha kuharibika kwa chujio pamoja na mirija na kufanya kazi ya uchujaji uchafu pamoja na utengenezaji wa mkojo kuvurugika. Matokeo yake mkojo huwa na kiwango kingi cha protini kuliko kawaida (protenuria), chujio huwa na makovu (glomerulosclerosis) hali kadhalika nayo mirija (tubulointerstitial scarring).

Uhusiano wa Vinasaba

Mpaka sasa, haijulikani sababu hasa inayowafanya watu weusi kuathirika zaidi na HIVAN kuliko watu wa asili nyingine. Ifahamike kuwa, kwa ujumla watu weusi wanaongoza kwa kupata magonjwa mengine ya figo kama vile ugonjwa wa figo unaotokana na kisukari (diabetic nephropathy) au unaotokana na mcharuko mwili (systemic lupus erythematosus); hivyo basi kuna uwezekano mkubwa pia wa vinasaba kuchangia katika kufanya watu weusi kupata HIVAN.

Dalili na muonekano wa mgonjwa

Pamoja na kuwa na dalili zote za magonjwa ya figo (rejea makala zilizopita za ARF na CRF), wagonjwa wa HIVAN huwa pia na tabia/dalili zifuatazo

 • Muonekano wa mgonjwa: Hupoteza kiwango kingi cha protein katika mkojo (zaidi ya gramu 3.5 kwa siku). Hupoteza pia kiwango kingi cha albumin (aina nyingine muhimu sana ya protini). Aidha huwa na kiwango kingi cha mafuta mwilini (hyperlipidemia). Pamoja na kupoteza sana proteini, wagonjwa wengi wa HIVAN hawana hali ya kuvimba miguu (edema). Huwa na shinikizo la damu la kawaida (tofauti na wagonjwa wa ARF au CRF ambao huwa na ongezeko la shinikizo la damu). Huwa na mrundikano usio wa kawaida wa urea au mazao mengine machafu yanayotokana na Nitrogen katika damu (azotemia).
 • Muonekano wa figo katika Ultrasound au CT scan: Tofauti na wale wa CRF iliyosababishwa na vyanzo vingine ambao huwa na figo ndogo zilizosinyaa, wagonjwa wenye HIVAN huwa na figo zilizo na ukubwa wa kawaida au zilizovimba sana (kubwa kuliko kawaida).
 • Muonekano wa figo katika biopsy: Figo huwa na makovu makovu katika chujio zake (Focal segmental glomerulosclerosis (FSGS) yanayoonekana katika darubini tu.
 • Kiwango cha CD4+ T-cells cha mgonjwa: Kwa kawaida kiwango cha seli za CD4+ kwa wagonjwa wenye HIVAN huwa chini ya 200 cells/µL. Hata hivyo, HIVAN inaweza kutokea hata kwa mgonjwa mwenye kiwango cha juu cha CD4. Wagonjwa wenye CD4 chini ya 50 cells/µL wana hatari zaidi ya kufa mapema kutokana na HIVAN.

Ikumbukwe kuwa, kukosa hedhi si ugonjwa bali ni dalili ya kuwepo tatizo hivyo basi iwapo tatizo hilo lina uhusiano na kutunga mimba na kupata mtoto, uwezekano wa kupata mtoto utakuwa mdogo ikiwa tatizo hilo halitashughulikiwa. Matatizo kwenye tezi za pituitary, hypothalamus pamoja na ovary ambayo yana uhusiano mkubwa na kukosa hedhi, husababisha pia tatizo la ugumba. Iwapo matatizo hayo yatashughulikiwa ipasavyo, uwezekano wa kupata kupata hedhi na hatimaye kupata mimba huwa mkubwa.

Tatizo la kukosa hedhi ni jambo ambalo linawakumba wanawake wengi waliovunja ungo.Aidha suala hili limekuwa likiwaletea usumbufu mwingi wa kisaikolojia wanawake wengi waliowahi kukumbana nalo.
Tatizo la kukosa hedhi au amenorrhea linaweza kutokea awali kabisa (primary) au baadaye kabisa maishani (secondary)...... Kwa maelezo zaidi soma hapa Tatizo la kukosa Hedhi (Amenorrhea)

 

Ugonjwa wa matende ni aina ya ugonjwa unaosababisha ngozi na  tishu zilizo chini ya ngozi ya  mwanadamu kuwa nene (thickening of skin and underlying tissue).Ugonjwa huu  huathiri  miguu, mikono, figo,  korodani  na kusababisha korodani  kuvimba na kuwa kubwa sana.Inakisiwa watu milioni 120 duniani wana maambukizi ya ugonjwa huu ambapo kati yao milioni 40 wamepata madhara makubwa kutokana na ugonjwa huu

Kinga ya ugonjwa wa matende?

• Shirika la afya duniani (WHO) limeanzisha jitihada za kutokomeza ugonjwa huu wa matende ifikapo mwaka 2020.
• Matumizi ya  dawa aina ya albendazole kwa wale walio katika hatari kupata ugonjwa wa matende unaosababishwa na vimelea.
• Kuvaa viatu wakati wa kutembea nje ili kujikinga kupata maambukizi ya aina ya podoconiosis.
• Kuosha miguu na mikono kwa kutumia maji na sabuni
• Kuosha miguu kila siku kwa kutumia antiseptic (bleach).
Kwa muda mrefu sana wanawake wamekuwa wakitumia parachichi kama nyenzo mojawapo ya urembo ima kwa kupaka kwenye uso au  nywele bila kuwa na uhakika kama kweli parachichi husaidia katika kurutubisha nywele na ngozi ya kwenye uso, swali ni je ni wangapi wanajua faida za parachichi kiafya, hususani faida ya kuukinga mwili dhidi ya kemikali hatari pamoja na kumfanya mtu kuonekana kijana?
 
Wanasayansi wa chuo kikuu cha Michoacana de San Nicolas de Hidalgo cha nchini Mexico wamesema ya kwamba parachichi husaidia katika kuukinga mwili dhidhi ya kemikali hatari (free radicals) na hivyo kuweka kinga dhidhi ya magonjwa mengi pamoja na kumfanya mtu kuonekana kijana (fight against ageing). Wanasayansi hao wamesema kwamba mafuta yanayopatikana katika parachichi yanauwezo wa kupenya hadi ndani ya injini inayotengeneza nishati mwilini inayopatikana katika seli inayojulikana kama mitochondria.
 
Free radicals ni kemikali zinazosababisha magonjwa mengi yakiwemo baadhi ya saratani, huharibu mishipa ya damu ya ateri (arteries), pamoja na kumfanya mtu kuzeeka haraka. Mafuta yanayopatikana katika baadhi ya mboga za majani, matunda na nyanya/tungule (tomatoes) yanauwezo wa kupambana na kemikali hizi hatari lakini mafuta haya hushindwa kuingia ndani ya mitochondria ambapo ndio kuna kemikali hizi hatari kwa wingi.
 

Dawa za kufubaza makali ya ugonjwa wa ukimwi husababisha virusi hivyo visiendelee kuzaliana, na kama havitoendelea kuzaliana basi seli za kinga za mwanadamu zitaishi kwa mua mrefu na kusababisha mwili kutengeneza ilinzi thabiti kukukinga na magonjwa nyemelezi. Kimsingi virusi vya Ukimwi hushambulia seli hizi, hivyo uwingi wake huwa ni tishio kwa seli na hata husababisha mwili wa binadamu kupoteza uwezo wake wa kupambana na magonnjwa, na ndioyo sababu, mtu aliyeathirika na ukimwi na hatumii dawa za kufubaza makali, kunyemelewa na magonjwa ya mara kwa mara na hata kuzorotesha afya yake.

Matumizi bora ya dawa hizi husaidia kupunguza idadi ya virusi kwenye mwili (kwakuwa hawaendelei kuzaliana), hivyo hupunguzza sana uwezekano wa wewe kumuambukiza mtu mwingine. Kutokana na taarifa kutoka shirika la Afya duniani (WHO), mtu anayetumia dawa za ARV kwa ufasaha kama alivyoelekezwa na daktari huku akiishi maisha yenye kuzingata Afya bora (mazoezi na chakula bora), uwezekano wa kumuambikiza mtu mwingine ambaye hana virusi vya ukimwi unapunguzwa kwa asilimia 96%.

Hivyo, matumizi sahihi ya dawa hizi ni moja ya vitu muhimu ili kupambana na janga hili la ugonjwa wa ukimwi. Nenda kapime kujua hali ya afya yako na kama utagunulika umeambukizwa, uanze kutumia dawa mapema iwezekanavyo kwa afya bora na kuzuia maambukizi kwa umpendaye.

 

Picha kwa hisani ya: http://www.pedaids.org

Page 3 of 4