Image

Bawasiri (Hemorrhoids)

Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.

Kuna aina mbili za Bawasiri

Nje

Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.

Ndani

Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili. Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo
Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.

Je bawasiri husababishwa na nini?

Bawasiri husababishwa na

 • Tatizo sugu la kuharisha
 • Kupata kinyesi kigumu
 • Ujauzito
 • Uzito kupita kiasi (obesity)
 • Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
 • Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.
 • Umri mkubwa

Dalili za bawasiri

 • Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
 • Maumivu au usumbufu
 • Kinyesi kuvuja
 • Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
 • Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
 • Kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa

Matatizo yanayoweza kutokana na Bawasiri

 • Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
 • Strangulated hemorrhoids

Vipimo na uchunguzi

 • Digital rectal examination
 • Kipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)
 • Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)

Matibabu

Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri

 • Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
 • Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
 • Coagulation (infrared, laser and bipolar)
 • Upasuaji
  • Hemorrhoidectomy
  • Stapled hemorrhoidopexy
 •  kutibu chanzo cha bawasiri

 

Njia za kuzuia Bawasiri

 • High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
 • Kunywa maji mengi kwa siku (glasi sita had nane kwa siku)
 • Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa.
Imesomwa mara 13069 Imehaririwa Jumatatu, 18 Januari 2021 01:38
Dr.Mayala

Dr.Henry A Mayala ni daktari bingwa Wa Tiba ya moyo katika taasisi ya Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI), ambaye kwasasa anasomea shahada ya uzamivu (PhD) ya Tiba ya Moyo katika Chuo Kikuu cha Tongji  nchini China.

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

Makala shabihana