Image
08 Mach 2023
Inasikitisha sana unapokuta mtoto anakosa heshima kwa dada anayemlea na kukaa naye nyumbani pale wazazi wanapokuwa kazini. Na mara nyingine mzazi anaona ni sawa tu na wala hamkemei mtoto wake kwa tabia hizo.
Unakuta mtoto anamuona dada wa kazi kama mtu asiye na thamani na wa kudharaulika tu. Akiamka asubuhi wala hamsalimii, anatupatupa vitu ovyo akijua kuna mtu wa kuviokota, akila anaacha vyombo hapo hapo mezani na kumuamuru msichana wa kazi avitoe na anaongea naye kwa lugha ya dharau na kuamrisha.
 
Yaani mtoto mdogo anaweza kumgombeza dada wa kazi kama wamelingana vile, hali hii ikiachwa kuendelea inafika wakati wakiwa na umri mkubwa kidogo wanaanza kuwapiga wadada wa kazi.
Mtoto akiachwa kuendelea na dharau kwa msichana wa kazi ambaye anakaa naye kila siku na kumlea atajenga tabia ya kudharau mtu yeyote aliye chini yake na hii itampelekea kuwa na mahusiano mabaya kuanzia shuleni, kazini hadi kwenye ndoa yake.
Ni vizuri mtoto tangu akiwa na umri mdogo akafahamu kuwa watu wote ni sawa na hakuna mtu bora zaidi ya mwingine. Atambue kuwa dada wa kazi yupo pale kama msaidizi na sio mtumwa.
 
Dharau hii ya mtoto kwa dada wa kazi mara nyingi huchangiwa na jinsi mzazi anavyomtendea msichana wake wa kazi. Onyesha mfano mzuri kwa mtoto wako kwa kukaa vizuri na kwa upendo na msaidizi wa kazi na utamsaidia mtoto wako aweze kujifunza heshima kwa watu wote wanaomzunguka.
Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116, ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini.

Je unafahamu inakadiriwa kuwa, mwanamke hupata hedhi wastani wa mara 400 katika maisha yake? Pia, neno linalotumika sana kuwakilisha hedhi ni "period", neno hili lilianza kutumika kwa mara ya kwanza kwenye miaka ya 1822 likimaanisha tukio linalotokea ndani ya muda fulani au linalojirudia baada ya muda fulani. Leo hii tuangalie mambo mengine 5 muhimu kuyajua kuhusiana na hedhi.

1. Kwa wastani, mwanamke huanza kupata hedhi yake ya kwanza kabisa akiwa na umri wa miaka 12.

2. Mzunguko wa siku za hedhi huwa kati ya siku 21 hadi 35. Ingawa wengi huwa na mzunguko wa siku 28, lakini kuzidi wiki moja au kuwahi kwa wiki moja ni kitu cha kawaida.

3. Mwanamke huzaliwa na mayai milioni 1 hadi 2. Mayai haya, mengi hufa jinsi mwanamke anavyoendelea kuishi na ni mayai 400 tu ndiyo hukadiriwa kufika hatua ya ukomavu tayari kwa uchavushwaji.

4. Msichana anaweza kupata ujauzito kabla ya kuanza hedhi yake ya kwanza. Hii ni kwa sababu, yai huanza kukomaa kabla ya kuona hedhi yake ya kwanza, hivyo kama atashiriki tendo bila kinga, kuna uwezekano wa kupata ujauzito.

5. Wanawake wengi hufikia ukomo wa kupoata hedhi (menopause) wakiwa na umri wa miaka 48 hadi 55.

Kuongezeka ukubwa wa matiti kwa wanaume hutokana na kuharibika kwa mfumo wa vichocheo unaojulikana kama estrogen-androgen balance na hivyo kusababisha estrogen kutolewa kwa wingi ama kuongezeka kwa msisimko (sensitivity) wa matiti kwa kiwango cha zaidi ya kawaida kwa kichocheo aina ya estrogen kilicho kwenye mzunguko wa damu. Tatizo hili huonekana sana kwa watoto wachanga na  wanaume waliokatika umri wa kubaleghe, lakini pia huonekana kwa watu wazima na wazee.

Ni nani aliyekatika hatari ya kupata tatizo hili?

.Wanaume walio na umri zaidi ya miaka 50.

.Wenye uzito uliopitiliza (Obesity)

.Unywaji pombe kupindukia

.Magonjwa sugu ya figo au ya Ini

.Kuwepo kwa historia ya tatizo hili katika familia.

.Soma hapa kupata maarifa zaidi Tatizo la Kuota Matiti kwa Wanaume na Watoto (Gynecomastia)

Kujikubali ni jambo  muhimu sana, kutayarisha akili yako na kuikubali hali hiyo ya kuwa na  ugonjwa wa kisukari,na kuiambia akili yako kuwa ugonjwa huu hauponi ni hali ambayo itakuwepo katika umri wa maisha yako yote na kuwa tayari kubadili mfumo wako mzima wa maisha.Hii ni sawa na mtu aliyezaliwa upya.

 

Kusoma makala nzima juu ya umuhimu wa kujukubali nena hapa

Ukurasa 1 ya 5