Malezi ya mtoto ni moja ya vitu muhimu vya kujifunza ukiwa kama mzazi, ni mara nyingi tumekuwa tukiona watoto wakilia bila kujua nini cha kufanya. Leo hii tudondoe njia moja wapo ya kumbembeleza mtoto.
Akiwa tumboni mwa mama, mara kwa mara mtoto alikuwa akisikia mapigo ya moyo ya mama. Hali hii ndiyo sababu kubwa ya watoto wengi kupendelea kubebwa na mama zao. Hata hivyo kuna aina nyingine za sauti zinazoweza pia kusaidia kumtuliza mtoto. Mzazi ama mlezi unaweza kujaribu kuweka muziki wa taratibu au kumuimbia mtoto nyimbo za kubembeleza kwa sauti ya chini sana. Unashauriwa kutokuweka miziki ya haraka au yenye sauti kubwa kwa sababu inaweza kumwondolea hali yake ya utulivu na hivyo kumfanya ashindwe kuacha kulia. Kwa makala iliyokamilika, nenda Hapa.
Je unataka kupokea dondoo za kila siku kwenye email yako, jiunge na mlisho wa habari kwa kwenda HAPA