Image

Zijue njia salama za kulala kwa mama mjamzito

 Tabia hii ya kulala chali wakati wa ujauzito inaweza kuepukika kwa kuwashauri kina mama wajawazito madhara yanayopatikana kwa kulala chali.

Matokeo ya utafiti huu yanaonyesha ya kwamba zaidi ya robo ya idadi ya watoto wanaozaliwa wafu inaweza kuepukika kwa kubadilisha staili ya kulala tu kwa wanawake wajawazito.

Siku zote madaktari wanashauri kina mama wajawazito kulala ubavu mmoja hasa upande wa kushoto ili kuepuka kuzaa mtoto mfu au mtoto mwenye uzito mdogo kwa sababu mwanamke mjazito anapolalia ubavu wake wa kushoto huongeza mzunguko wa damu kwa kiumbe kilichomo ndani yake.

Mlalo hatari kwa mama mjamzito

Mlalo salama kwa mama mjamzito

Kwa maelezo zaidi, soma   Kulala Chali kwa Mjazito ni Hatari kwa Mtoto?

 

 

 

Imesomwa mara 22296 Imehaririwa Jumanne, 08 Januari 2019 13:06
Dr Khamis

Dr. Khamis H.Bakari (MD PhD) ni daktari bingwa,mhadhiri katika chuo cha afya cha Chuo  Kikuu cha Dodoma,mtaalamu wa Tiba na Uchunguzi kwa kutumia mionzi ya nyuklia (Nuclear medicine).

This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.