Image

Sababu za kutokea vijiwe katika Figo

Vijiwe hivi  hutokana na  madini chumvi au tindikali mbalimbali zinazotolewa mwilini.

Vijiwe katika figo husababishwa na nini?

Kwa kiasi kikubwa, vijiwe husababishwa na kukosekana kwa usawa wa maji, madini na tindikali mwilini yaani electrolyte imbalance.

Aidha, kuna magonjwa kadhaa ambayo hupelekea kwa kiasi kikubwa kutokea kwa hali hii kama ugonjwa wa utindikali kwenye mirija ya figo (renal tubular acidosis) ugonjwa wa Dent, matatizo kwenye tezi za parathyroid (hyperparathyroidism), kukojoa chumvi chumvi za oxalate kupita kiasi (primary hyperoxaluria) na hali ya nyama za figo kuwa tepetepe (medulary sponge kidney).

Fualitlia makala hii hapa Mawe katika Figo (Kidney Stones)

Imesomwa mara 2598 Imehaririwa Jumatatu, 12 Machi 2018 12:24
Sophia Mangapi

Web Developer

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.