Image

Vyakula vya mafuta ni chanzo cha kukukosesha usingizi

baga

Tumekuwa tukipokea maoni toka kwa watu wengi juu ya matatizo ya kukosa usingizi, ingawa kuna sababu nyingi zinazoweza kukufanya ukose usingizi kama magonjwa nk, ila mlo nao ni moja ya sababu hizo.Na moja ya vyakula hivi ni vile vyenye  mafuta (fat) mengi kama burger, chipsi nk. Tafiti zinaonesha kuwa, vyakula hivi sio tu hukufanya uongezeke uzito bali pia huabiri mfumo wa kulala.

Tafiti zinaendelea kuwa, vyakula hivi vizito huamsha mfumo wa usagaji vyakula (digestion system) na kuifanya ianze kufanya kazi, hii hukupelekea mwili wako kuwa hai na pia hukufanya mara nyingi kujisikia kwenda haja hivyo kukukosesha
usingizi.

Hivyo basi epuka kula mlo wenye wanga mwingi wakati wa usiku au angalau kwa masaa mawili kabla ya kwenda kulala.

Imesomwa mara 3856 Imehaririwa Jumatano, 31 Oktoba 2018 16:12
Mkata Nyoni

Mkata Nyoni ni mtaalamu wa masuala ya Uchumi na Biashara ya Teknohama. (Information Economics & IT Management). Ni muanzilishi na mkurugenzi wa kampuni ya Dudumizi Technologies LTD inayojishughulisha na masuala yautengenezaji wa Website, Web Systems na Applications za simu.

https://www.dudumizi.com | This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.