Pakua TanzMED App?

Leo katika mahanjumati ya Eid, tunakuletea mapishi ya biriani ya nyama ya ngombe, biriani na sosi ya nyama ya mbuzi, mandi na nyama, makbuus dajaaj, maandazi, mchuzi wa kima na mayai, nyama ya kukaanga na pilipili manga, juisi ya tikiti maji na embe, juisi ya mabungo na juisi ya mapera na karakara. Wapikie familia yako vyakula vitamu wafurahie sikukuu vizuri.

Biriani Nyama ya Ngombe

Biriani nyama ngombe

 

 

 

 

 

 

 

Vipimo Vya Masala

Nyama vipande 3 lb (au Kilo moja na nusu)

Mtindi ½ Kopo

Thomu 1½ Kijiko cha supu

Tangawizi 1½ Kijiko cha supu

Nyanya 2

Pilipili mbichi Kiasi

Nyanya kopo 4 Vijiko vya supu

Vidonge supu (Curry cube) 2

Pilipili nyekundu paprika Kiasi

Bizari zote saga 2 Vijiko vya supu

Viazi 4

Mafuta 2 Mug

Samli ½ Kikombe

Vitunguu 6

Namna ya Kutayarisha na Kupika

Katika muendelezo wa makala ya mapishi ya futari sehemu ya pili, leo tunakuletea mapishi ya chapati, mbaazi kwa mchicha, mbaazi za nazi, uji wa kunde na juisi ya kuondoa sumu mwilini.

Chapati za Ngano

 

 

 

 

 

 

 

Vipimo

 • Vikombe vya unga wa ngano mweupe 
 • Vijiko vya kulia vya samli safi 
 • Vijiko vya chai vya chumvi 
 • Vikombe vya maji vuguvugu
 • Samli ya kupika chapati 

Namna ya Kutayarisha na Kupika

 • Mimina unga, samli na chumvi kwenye sinia au bakuli kubwa. Changanya pamoja.
 • Mimina maji kidogo kidogo huku unachanganya na ule mchanganyiko wa unga.
 • Mchanganyiko ukishashikana, kanda unga kwa mkono kiasi, kama dakika tano
 • Funika na uache mchanganyiko kwenye sinia kama dakika kumi hivi kwa   kuufunika ili hewa isiingie.
 • Gawanya ule mchanganyiko kwa kufanya madonge kama kumi na nne au kumi na sita kwa chapati ndogo.
 • Mimina unga kidogo mahali ambapo utasukuma chapati.
 • Sukuma donge moja mpaka liwe duwara jembamba.
 • Paka samli kama kijiko kimoja cha kulia, ukihakikisha umepaka duwara lote.
 • Kunja lile duwara kama mfano wa kamba, huku unazungusha kama kamba ili iwe ndefu kidogo.

Mapishi ya futari za Ramadhani hayakamiliki bila kupika vibibi, shurba ya nyama ya mbuzi, mkate wa mofa, bokoboko la kuku na mihogo.

Mkate wa Mofa (Yemen)

 

 

 

 

 

 

 

Vipimo

Unga wa mahindi 1 mug

Unga wa mtama 2 mugs

Kitunguu maji 1 Kikubwa

Chumvi 1 Kijiko cha chai (Kidogo)

Sukari 1 Kijiko cha chakula

Hamira 1 Kijiko cha chai

Maji 3 mugs

Namna ya Kutayarisha na Kupika

 • Upike unga wa mahindi kama uji kwa dakika kama tano na maji mug mbili.
 • Uache upoe tia unga wa mtama na vitu vyote vilivyobaki pamoja na ile mug moja ya maji iliyobaki.
 • Uache mpaka uumuke.
 • Fanya maduara duara halafu tandaza uchome kwa moto mdogo kama chapati bila ya mafuta kwenye kikaango (frying pan). Choma mmoja mmoja yote hadi umalize..
 • Lipange kwenye sahani tayari kwa kuliwa na mchuzi wa nazi wa samaki au kuku au vyovyote upendavyo.

Muhogo, Samaki wa Kuchoma na Bamia

 

 

 

 

 

 

 

 

Vipimo

Mihogo (fresh) 3 - 4

Tui la kopo au (box) 1000 ml

Chumvi 1 kijiko cha chai

Kitunguu maji kilokatwakatwa 1

Nyanya mshumaa/tungule) 3-4

Pilipili mbichi ndefu 2-3

Pilipili boga 2

Namna ya Kutayrisha na Kupika

 • Menya mihogo kisha ikate kate vipande inchi tatu hadi nne, kila kipande kigawe kitoke vipanda vinne. Toa mzizi katikati.
 • Osha mihogo ipange kwenye sufuria ya nafasi na yenye mfuniko, ili upate nafasi ya kutia viungo unavyoona pichani na utokotaji wa tui wahitaji nafasi.
 • Panga/tandaza kitunguu, nyanya mshumaa/tungule, pilipili mbichi na pilipili boga juu ya mihogo, tia chumvi na tui lote.
 • Funika sufuria kisha weka jikoni moto wa kiasi kuchemsha tui lipande juu. Hakikisha tui halifuriki na kumwagika kwa kuchungulia au kufunika nusu mfuniko
 • Kwa muda wa nusu saa hivi ukiona sasa tui linatokota chini chini funika mfuniko na upunguze moto mdogo kabisa tui likauke kidogo na liwe zito.
 • Toa muhogo mmoja ubonyeze ukiona umeiva zima jiko na wacha sufuria hapo kwa muda wa dakika 10. Mihogo iko tayari kuliwa.

Kidokezo

Tui lote huwa chini baada ya mihogo kuiva unapopakuwa teka kutoka chini uweze kupata uzito wa tui umwagie juu.

Bamia/Mabenda

Vipimo

Bamia Robo kilo

Nyanya/Tungule 3

Kitunguu maji 1

Thomu ya unga au ilosagwa 1 Kijiko cha chai

Nyanya kopo (tomato paste) 1 Kijiko cha supu

Mafuta 150 ml

Chumvi 1 Kijiko cha chai

Pilipili boga 1

Namna ya Kutayarisha na Kupika

 • Kata vichwa vya bamia kisha zikate kate mara mbili zikiwa kubwa, ikiwa ni ndogo mno haina lazima kuzikata osha tu uweke kando.
 • Katika sufuria, katakata kitunguu, nyanya, pilipili boga tia ndani viungo hivi ongeza chumvi, mafuta, thomu na nyanya kopo
 • Washa moto mdogo mdogo huku umefunika sufuria kwa muda wa dakika 20 kisha ukiona mboga zimeshika kutokota ongeza bamia koroga.
 • Tia maji 200ml (glasi 2) wacha kwa muda wa dakika 15 kupikika tena, ukionja utamu wa mboga na chumvi, hakikisha bamia pia zimeiva. Hapa Bamia zipo tayari kuliwa.

Samaki wa Kuchoma

Vipimo

Samaki (dorado) au mikizi au tuna 2 Wakubwa (fresh)

Chumvi 1 Kijiko cha chai

Thomu ya unga au iliyosagwa 1 ½ cha chai

Tangawizi mbichi iliyosagwa 1 Kijiko cha supu

Namna ya Kutayrisha na Kuchoma

 • Safisha samaki vizuri mchane chane (slit) kwa ajili ya kuweka masala.
 • Changanya viungo vyote na chumvi, kisha paka katika samaki nje na ndani na sehemu ulizochanachana. Mloweke kwa muda wa robo saa hivi.
 • Weka karatasi ya jalbosi (foil paper) katika tray (treya) ya oveni. Muweke samaki kisha mpike (grill) kwa moto wa juu achomeke hadi samaki agueke rangi na aive.

Kidokezo

Kuweka karatasi ya jalbosi katika tray ya oveni kunasaidia kuhifadhi tray kuchafuka na tabu ya kusugua na kuiosha.

Hariys - Bokoboko la Kuku

 

 

 

 

 

 

 

Vipimo

Ngano nzima (shayiri) 3 Vikombe

Kuku ½ (3 lb au kilo moja na nusu)

Thomu na tangawizi iliyosagwa 1 Kijko cha supu

Pilipili manga ya unga ½ Kijiko cha chai

Jiyrah (cumin/bizari ya pilau) ½ Kijiko cha chai

Chumvi Kiasi

Kidonge cha supu (Curry cube) 1

Samli ya moto ½ Kikombe

Namna ya Kutayarisha na Kupika

 • Loweka ngano (shayiri) tokea usiku au muda wa masaa.
 • Katakata kuku mtie katika sufuria, tia maji kiasi na viungo vyote. Mchemeshe aive na ibakie supu yake.
 • Toa kuku, toa mifupa na umchambue chambue vipande vidogo vidogo.
 • Chemsha ngano (shayiri) kwa kufunika sufuria hadi iive na kukauka maji.
 • Tia supu ya kuku katika ngano (shayiri), na kuku uliyemchambua. Tia kidonge cha supu (curry cube)
 • Tia samli nusu (bakisha nusu) kisha changanya mchanganyiko hadi uvurugike kuku na ngano (shayiri) vizuri.
 • Mimina katika sahani, mwagia samli ya moto iliyobakia ikiwa tayari.

Kidokezo

Ukipenda kulia na sukari

Shurba ya Nyama ya Mbuzi

 

 

 

 

 

 

 

Vipimo

Nyama ya mbuzi 2lb (Kilo moja)

Nyanya 1

Kitunguu maji 1

Kidonge cha supu (curry cube) 1

Maji 4 Mugs

Thomu 1 Kijiko cha supu

Bizari ya pilau (cumin) 1 Kijiko cha chai

Bizari ya manjano ½ Kijiko cha chai

Mdalasini 1 Kijiti

Shairi (oats) 5 Vijiko supu

Pilipili mbichi 2

Siki ya zabibu (Grape vinegar) 2 Vijiko vya supu

Chumvi Kiasi

Namna ya Kutayarisha na Kupika

 • Osha nyama vizuri tia kwenye sufuria.
 • Katakata kitunguu na nyanya, ikiwa hupendi maganda ya nyanya toa na ukate kate.
 • Tia kidonge cha supu, mdalasini, chumvi na maji funika uchemshe nyama mpaka iive.
 • Tia shairi (oats) kwenye bakuli na maji iache, nusu saa kisha isage kidogo tu, na mimina kwenye supu ya nyama.
 • Tia pilipili mbichi nzima, thomu, bizari zote na siki. Weka moto mdogo mdogo huku unakoroga kila baada ya muda.
 • Tazama uzito, na ongeza maji kidogo ikiwa nzito sana

Kidokezo

Ikiwa huna siki ya zabibu tia ndimu au limao au white vinegar.

Vibibi

 

 

 

 

 

 

 

Vipimo

Mchele 2 Vikombe

Tui la nazi 1 1/2 Kikombe

Mafuta 1 Kijiko cha supu

Hamira 2 Vijiko vya chai

Unga wa ngano 1 Kijiko cha supu

Hiliki Kiasi upendavyo

Sukari ¾ au 1 Kikombe

Namna ya Kupika na Kutayarisha

 • Osha na loweka mchele usiku mzima ndani ya maji baridi.
 • Mimina vifaa vyote isipokuwa sukari , ndani ya mashine ya kusagia (blender) na usage mpaka mchele uwe laini.
 • Mimina ndani ya bakuli na ufunike , kisha weka pahali penye joto ili mchanganyiko ufure/uvimbe.
 • Ukishafura , mimina sukari na changanya vizuri ; ukiona mchanganyiko ni mzito sana, ongeza maziwa kidogo.
 • Weka chuma kipate moto.
 • Paka mafuta au samli kidogo kwenye chuma kisha mimina mchanganyiko kiasi kuunda duara na ufunike.
 • Utazame ikishaiva upande mmoja , geuza upande wa pili mpaka iwe tayari.
 • Endelea Mpaka umalize mchanganyiko wote; panga kwenye sahani na tayari kuliwa.

Kidokezo

Unaweza kutumia chuma kisichoganda ( non stick ); nacho hakitaraji kutiwa mafuta.

Vibibi vya Tui la Nazi

 

 

 

 

 

 

Vipimo

Mchele 2 Vikombe

Tui la nazi zito 2 Vikombe

Hamira 1 Kijiko Cha chai

Unga wa ngano 2 Vijiko vya supu

Iliki Kiasi upendavyo

Sukari Kiasi upendavyo

Yai 1

Vipimo vya Tui la Kupaka

Tui la nazi 2 Vikombe

Hiliki ya unga Kiasi upendacho

Sukari Kiasi upendacho

Unga wa ngano 1 Kijiko cha supu

Namna ya Kutayarisha na Kupika

 • Changanya vitu vyote vya tui la kupaka katika kisufuria kidogo.
 • Lipike tui huku walikoroga mpaka lichemke na liwe zito.
 • Osha na loweka mchele usiku mzima ndani ya maji baridi.
 • Mimina vifaa vyote isipokuwa yai na sukari , ndani ya mashine ya kusagia (blender) na usage mpaka mchele uwe laini.
 • Mimina sukari na yai usage kidogo tu kiasi cha kuchanganya.
 • Mimina ndani ya bakuli na ufinike , kisha weka pahali penye joto ili mchanganyiko ufure/uvimbe
 • Ukishafura, weka chuma kipate moto. (Ni bora kutumia kichuma kidogo)
 • Katika sahani ya kupakulia, paka tui kote.
 • Tia kijiko nusu cha chai cha mafuta au samli kwenye chuma kisha mimina mchanganyiko ukitumia upawa na ufunike.
 • Kibibi kikianza kuiva na kushikana upande mmoja , kigeuze upande wa pili mpaka kigeuke rangi na kuiva.
 • Panga kwenye sahani iliyopakwa tui.
 • Endelea Mpaka umalize mchanganyiko wote; kila ukiepua kibibi, panga juu ya mwenzake kama ilivyo kwenye picha na upake tui juu yake.

Usikose makala zifuatazo za mahanjumati ya Eid.

Shukrani kwa tovuti ya www.alhidaaya.com kwa makala hii.

Ni kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani. Ni kipindi cha mfungo kwa ndugu Waislam kote duniani. Kwa kulitambua hilo, wavuti yako ya TanzMED itakuwa ikikuletea makala mbalimbali kuhusu mapishi ya aina mbalimbali ya futari za mwezi huu wa Ramadhani. Vyakula hivi pia vinaweza kupikwa hata na wale ambao hawako kwenye mfungo wa mwezi wa Ramadhani, kwa wakristo wakati wa kwaresma au siku yoyote ile.

Pilau ya Sosi ya Soya na Mboga

 

 

 

 

 

Vipimo

Kuku (mkate vipande vipande) 1

Mchele wa Basmati (lowanisha) 3 magi (1 mug)

Mdalasini 1 mche mmoja

Vitunguu maji (vilivyokatwa vyembamba) 6

Mchanganyiko wa mboga za barafu 1 magi (1 mug)

(karoti, mahindi, njegere)

Kabichi (iliyokatwa katwa nyembamba) 1 magi (1 mug)

Pilipili mbichi (iliyosagwa) 3

Pilipili boga iliyokatwa vipande vidogo vidogo 1

Pilipili manga 1 kijiko cha chakula

Chumvi 1 kijiko cha chakula

Sosi ya soya (soy sauce) 5 vijiko vya chakula

Kotmiri iliyokatwa katwa 1 magi (1 mug)

Leo katika makala hii, chef Issa anawaletea jinsi ya kuandaa chapati (pancake) za unga wa mchele na choroko, namna ya kupamba chakula na kukifanya kuwa cha mvuto kwa mlaji,

jinsi ya kupika viazi vya kukaanga na mchanganyiko wa mboga za majani, na jinsi ya kutengeneza halwa ya karoti.

Habari njema kwa wale wasiotumia nafaka aina ya ngano na wale wasiotumia mayai na wangependa sana kula chapati hizi za maji.

 

 

 

 

 

 

MAHITAJI

180 gram za mchele uliochemshwa

180 gram za mchele uwe wenye mbegu fupi nene

120 gram za choroko zilizotolewa ngozi

1/2 kijiko cha chai Fenugreek seeds (angalia chini hapo katika picha)

1-1/2 kijiko kidogo cha chai chumvi

Jinsi ya kuandaa fuatilia mafunzo hapa chini

 

 

 

 

 

 

Loweka choroko pamoja na fenugreek katika bakuli moja kisha loweka mchele katika bakuli jingine kwa masaa matatu tu.

 

 

 

 

 

 

Na huu ndio muonekano wa mbegu za fenugreek

 

 

 

 

 

 

 

Huu ni muonekano wa choroko

 

 

 

 

 

 

Unaweza tumia blenda au ukalowanisha grinder kusaga mchanganyiko wako. Kama unavyoona katika picha hapo mimi natumia grinder ndogo naiweka juu ya meza na huwa natumia kusagia vitu vingi kwa urahisi zaidi.

Kwa sasa weka mchele na maji kisha washa mashine iendelee kusaga au blenda.

 

 

 

 

 

 

Saga mpaka upate uji mzito. Hata baada ya kusaga kwa muda mrefu unaweza ona chenga chenga usikate tamaa ni kawaida na mchanganyiko wako uko safi kabisa. Mimina mchanganyiko wako katika bakuli pembeni.

 

 

 

 

 

 

Kisha usioshe blenda yako au mashine ya kusagia weka choroko na mbegu za fenugreek katika grinder pamoja na maji kiasi.

 

 

 

 

 

 

Saga tena upate mchanganyiko mzuri na mzito.

 

 

 

 

 

 

Kisha chukua mchanganyiko huo na changanya katika ule mchanganyiko wa mchele uliosagwa pia.

 

 

 

 

 

 

Hakikisha mikono yako ni safi na salama weka chumvi katika mchangayiko na changanya vizuri kwa kutumia mikono yako.

Sio lazima kutumia mikono unaweza tumia mwiko pia, lakini kumbuka joto la kwenye mikono yako linasaidia kufanya unga uchachuke vizuri pale unapouacha usiku mzima kabla ya kupika.

 

 

 

 

 

 

Weka mchangayiko wako katika bakuli safi kwa usiku mzima. Kama unaishi nchi au miji yenye joto unaacha tu nje itaumuka na kuchachuka safi sana ila kama unakaa nchi za baridi basi iwashe oven yako na kisha izime ipoe kiasi chukua unga wako na uweke humo ukae usiku mzima hakikisha oven imezimwa na joto ni dogo sana.

 

 

 

 

 

 

Siku inayofuata, changanya mchanganyiko wako safi. Kisha changanya vizuri tena mchanganyiko wako. Weka kikaango chako katika moto na kisha paka mafuta kiasi.

Huwa natumia kitunguu kilichokatwa kuenezea mafuta katika kikaango hii husaidia mchangayiko wako wa unga usigandie wakati unakaanga.

 

 

 

 

 

 

Chukua upawa na chota mchanganyiko anza kumimina kati kati ya kikaango.

 

 

 

 

 

 

Baada ya kumimina kiasi hakikisha unasambaza kwanza uone kama inatosha au uongeze.

 

 

 

 

 

 

Kiwango ni iwe nyembemba ili iweze kuiva kwa haraka

 

 

 

 

 

 

Acha iive kwa dakika 3 au mpaka uone mwisho mwa chapati kunajikunja na kuacha kikaango na kua na rangi ya kahawia. Hapo itakua rahisi kugeuza na kuivisha upande mwingine.

 

 

 

 

 

 

Geuza na pika tena kwa dakika 2.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Huu ndio muonekano saafi wa chapati yako ya maji na mchanganyiko wa mchele na choroko.

 

 

 

 

 

 

 

Baada ya kuiva ikunje nusu na mpatie mlaji ikiwa ya moto.Inakua na ubora wake endapo utampatia mlaji mara tu baada ya kuiva. Furahia chapati yako na Coconut Chutney, Tomato Chutney, Onion Chutney, Jam ya ladha yeyote au asali.

VIAZI VYA KUKAANGA NA MCHANGANYIKO WA MBOGA MAJANI

Viazi ulaya (Irish potato) oka kwenye oven pamoja na chumvi na mafuta kiasi na kitunguu swaumu.

Pili chukua pili pili hoho pamoja na nyanya mbivu pia oka kwenye oven lakini hakikisha zinaiva wastahi tu zisipondeke au kuiva sana pia kumbuka kuziwekea chumvi na mafuta kabla ya kuzioka.

Kisha kata kata kitunguu maji slice, majani ya kitunguu mabichi changanya katika viazi mchangayiko wote huo wa mboga majani hizi mbichi na zile za kuoka pia.

Kumbuka kuweka pili pili manga na tomato ketchup kidogo.

Hapa mlo kamili unakua umekamilika kwa wale wasio tumia nyama na pia kwa wanaotumia nyama chakula hiki unaweza kula nanyama ya samaki, kuku au mbuzi na ng'ombe pia.

Badilisha muonekano bora wa chakula nyumbani kwako familia ifurahie mapishi bora na chakula kitamu.

JIFUNZE KUPAMBA CHAKULA ILI KUONGEZA MVUTO KWA WALAJI

Muonekano wa chakula ni kivutio tosha kwa mlaji. Jitahidi kupamba chakula katika sahani ili kivutie walaji kwani mtu anaanza kula kwa macho hata kama chakula si kitamu lakini macho yakishapenda mlaji ataridhika na mapishi yako. Kupamba chakula si hotelini tu hata nyumbani unaweza pamba chakula chako na kikavutia sana.

WALI NYAMA, YAI LA KUKAANGA NA SALSA

 

 

 

 

 

 

 

Huu ni muonekano wa chakula safi sana na kwa muonekano wa macho na hata kwa ladha ni safi sana

Pika wali wako saafi kisha kaanga yai kwa pembeni jicho la ng'ombe (fried egg sun side up) kisha tengeneza salsa ya embe, nyanya na kitunguu weka pilipili manga, chumvi, limao na pilipili mbuzi kiasi sio lazima.

Kupamba katika sahani, chukua kibakuli au kikombe cha chupa ya chai kisha weka wali humo na kandamiza vizuri kisha geuza na weka katika sahani pembeni kama picha inavyoonyesha. Kisha weka salsa pembeni na yai la kukaanga.

Juu ya wali weka nyama au, kuku wa mchuzi mzito au samaki kisha juu yake unatupia karanga zilizookwa au korosho.

Chakula hiki kitakua na muonekano safi sana na mlaji atafurahia mchanganyiko wa ladha.

JIFUNZE KUANDAA CARROT HALWA

Kuandaa ni dakika30

Kupika ni dakika 30

Idadi ya watu kula ni 2

MAHITAJI

480 gram ya karoti ya kukwaruzwa (grated)

240 gram ya maziwa

1240 gram ya fresh cream

120 gram ya samli (ghee)

240 gram ya sukari

1 kijiko kidogo cha chai unga wa hiliki (cardamom powder)

1 kijiko kikubwa cha korosho zivunje vunje

Jinsi ya kuandaa fuatilia picha hapa chini

 

 

 

 

 

 

Pasha kikaango katika moto, kisha weka samli iyeyuke na weka karoti, kaanga mpaka upate harufu nzuri ya kuiva (distinct aroma).

 

 

 

 

 

 

Kisha weka maziwa pamoja na cream pika kwa dakika 10 mpaka maziwa na cream yakaukie kwenye karoti (absorbed).

 

 

 

 

 

 

Kisha weka sukari pamoja na hiliki pika mpaka ishikane kabisa.

 

 

 

 

 

 

Kisha chukua chombo chochote au kikombe na weka halwa yako kisha mimina katika sahani juu yake weka zile korosho zilizo kaangwa au kuokwa kama pambo kwa juu na pamoja kuongeza ladha. Pia unaweza tumia zabibu kavu (raisins) na zinapendeza sana.

 

 

 

 

 

 

Huu ni muonekano wa halwa ikiwa katika sahani tayari kwa kuliwa. Watengenezee familia yako wafurahie.

No Internet Connection