Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wanaume wawili ambao walikuwa na maambukizi ya ugonjwa wa HIV huko nchini Marekani wameweza kuacha kabisa kutumia dawa za kurefusha maisha yaani ARV’S ambazo hupewa wagonjwa wa HIV baada ya kufanyiwa upandikizaji wa uboho (bone marrow transplant) katika mifupa yao.
Wanaume hao ambao walikuwa na ugonjwa wa HIV kwa miaka 30, walikuwa wakipewa tiba ya upandikizaji wa uboho kutokana kuugua saratani ya damu (Leukemia). Mmoja wa wanaume hao ameacha kutumia dawa hizo za kurefusha maisha miezi minne iliyopita na mwingine ameacha kuzitumia wiki saba zilizopita.
Wanasanyansi katika chuo kikuu cha Saskatchewan cha nchini Canada wamesema ya kwamba manii(semen) yanayotolewa na mwanamume wakati wa kujamiana na mwanamke yanasaidia mwanamke kuwa na uwezo wa kushika mimba. Kulingana na utafiti mpya uliofanywa na watafiti wa kimataifa chini ya Gregg Adams na kuchapishwa katika jarida la proceedings of the National Academy of Sciences, umesema ya kwamba manii sio tu hubeba shahawa (sperm) za mwanamume kwenda kwa mwanamke bali pia huchochea mayai ya mwanamke (ovaries) kutoa mayai ya uzazi.
Protini inayopatikana katika shahawa inayojulikana kama Ovulation-Inducing Factor au IFO, ndio hasa huchochea sehemu ya ubongo inayojulikana kama hypothalamus kwenye ubongo wa mwanamke kutoa homoni ambazo hupelekwa moja kwa moja kwenye mfumo wa neva na kisha homoni hizo hupelekwa kwenye mfumo mwingine wa homoni unaojulikana kama endocrine system.
Homoni hufika kwenye mfumo huu wa endocrine system kupitia sehemu ya ubongo inayojulikana kama pitituary gland na hivyo kuingia kwenye mzunguko wa damu.Baada ya kufika wenye mzunguko wa damu, homoni hizi huenda moja kwa moja mpaka kwenye mayai ya mwanamke (ovary) na kuyachochea mayai haya kutoa mayai ya uzazi(ovum) katika hatua inayojulikana kama ovulation.
Tatizo la kuota matiti kwa wanaume na watoto limekuwa kubwa sana katika dunia ya leo. Inawezekana kabisa wakati unatembea njiani ukaona wanaume au watoto wadogo wa kiume wakiwa na matiti makubwa ambapo watu wengi huchukulia kama ni kawaida. Kitaalamu gynecomastia ni kukuwa kuliko kawaida yake kwa tishu ya kwenye titi inayojulikana kama glandular tissue. Tatizo hili huonekana sana kwa watoto wachanga na wanaume waliokatika umri wa kubaleghe, lakini pia huonekana kwa watu wazima na wazee.
Mrija wa mkojo (urethra) ni kiungo muhimu kinachotoa mkojo nje ya mwili kutoka kwenye kibofu. Mrija huu unaposinyaa au kuziba hufanya utokaji wa mkojo kuwa wa mashaka na maumivu makubwa. Kusinyaa/ Kuziba kwa mrija wa mkojo huitwa pia urethral stricture.
Visababishi na vihatarishi vya tatizo hili
Kusinyaa kwa mrija wa mkojo husababishwa na kovu linalotokea katika sehemu ya mrija baada ya mtu kuumia, kufanyiwa upasuaji au kupona magonjwa ya zinaa. Inaweza pia kusababishwa na uvimbe karibu na eneo la kinena unaokandamiza mrija.
Vihatarishi vya tatizo hili ni pamoja na
- Kuwa na historia ya kuugua magonjwa ya zinaa
- kuwahi kuwekewa mipira ya mkojo au vifaa vya namna hiyo (catheter au cystoscope)
- Kuvimba tezi dume (BPH) kwa wanaume
- kuwa na historia ya kuumia au kupata majeraha maeneo ya kinena. Hii hutokea sana kwa wale wanaopata ajali wakiendesha baiskeli
- Kupata maambukizi ya mara kwa mara ya mrija wa mkojo (urethritis)
Ni nadra sana kwa tatizo hili kutokea kwa wanawake. Aidha ni nadra pia kwa mtoto kuzaliwa akiwa na tatizo hili (congenital urethral stricture).
Dalili
Mtu mwenye tatizo hili anaweza kuwa na dalili zifuatazo,
- Kutoa shahawa zilizochanganyika na damu
- Kukojoa mkojo mweusi au uliochanganyika na damu
- Kupungua kwa kiasi cha mkojo kinachotolewa
- Kukojoa kwa shida
- kutoa uchafu katika mrija wa mkojo
- kukojoa mara kwa mara
- Kushindwa kumaliza mkojo wote
- Kushindwa kuhimili kutoka kwa mkojo (mkojo kujitokea wenyewe/kujikojolea)
- Maumivu wakati wa kukojoa
- Maumivu chini ya tumbo
- Maumivu ya kinena
- Mtiririko dhaifu wa mkojo (hutokea taratibu au ghafla)
- Mkojo kutawanyika ovyo wakati wa kukojoa
- Kuvimba uume
Uchunguzi
Daktari atakufanyia uchunguzi wa mwili na namna unavyokojoa. Uchunguzi wa mwili unaweza kuonesha:
- Kupungua kwa mkondo wa mkojo
- Uchafu kutoka katika mrija wa mkojo
- Kibofu kilichojaa/kuvimba
- Kuvimba kwa mitoki ya maeneo ya kinena
- Tezi dume iliyovimba au yenye maumivu
- Kuhisi kitu kigumu chini ya uume
- Uume kuvimba au kuwa mwekundu
Hata hivyo, wakati mwingine uchunguzi unaweza usioneshe tatizo lolote lile.
Vipimo
Vipimo ni pamoja na
- Kipimo cha kuchunguza mrija pamoja na kibofu cha mkojo (cystoscopy)
- Kuangalia kiasi cha mkojo kinachobaki katika kibofu baada ya kukojo (Post-void residual (PVR) volume)
- X-ray ya mrija wa mkojo (Retrograde urethrogram)
- Vipimo vya magonjwa ya zinaa
- Uchun
Matibabu
Mrija unaweza kutanuliwa wakati wa kipimo cha cystoscopy na hiyo ikawa ndiyo mojawapo ya tiba.
Iwapo njia ya kutanua mrija haioneshi mafanikio sana, upasuaji unaweza kuhitajika. Upasuaji unategemea eneo lilipo tatizo na ukubwa wa tatizo. Kama tatizo ni dogo/fupi na lipo mbali na bawabu inayotenganisha mrija na kibofu cha mkojo, linaweza kutatuliwa kwa kukata kasehemu kalikoziba wakati wa kufanya cystoscopy au kwa kuweka kifaa maalum cha kuzibua na kutanua mrija.
Kama tatizo ni kubwa zaidi, upasuaji wa wazi wa eneo husika unaweza kufanyika. Upasuaji huu unajumisha kukata sehemu iliyoziba na kisha kukarabati sehemu hiyo.
Kwa mgonjwa ambaye amepata shida ya ghafla ya kushindwa kutoa mkojo (acute retention of urine), matibabu ya dharura ya kumuwekea catheter kupitia juu ya kinena (suprapubic catherization) hufanyika. Hii husaidia kibofu kutoa mkojo nje kupitia kwenye bomba lililowekwa chini ya tumbo.
Ifahamike kuwa mpaka sasa hakuna dawa ya tatizo hili zaidi ya njia za upasuaji na nyingine zilizoelezwa hapo juu.
Matarajio
Mara nyingi matibabu huleta matokeo mazuri na mgonjwa anaweza kuishi maisha yake kama kawaida. Hata hivyo wakati mwingine, mgonjwa anaweza kuhitaji matibabu ya mara kwa mara ili kuondoa sehemu ya kovu iliyopo katika mrija wa mkojo.
Madhara ya tatizo hili
Tatizo hili halina budi kutibiwa haraka maana kama likiachwa linaweza kusababisha kuziba kabisa kwa njia ya mkojo na kusababisha mkojo kujaa katika kibofu, hali ambayo, pamoja na kuleta maumivu makali kwa mgonjwa inaweza pia kusababisha figo kushindwa kufanya kazi (ARF).
Kinga
Ni muhimu kujikinga dhidi ya magonjwa ya zinaa kwa kufanya ngono salama au kuacha kabisa kufanya ngono. Aidha kuwa makini na kazi au mambo ambayo yanaweza kukusababishia kuumia maeneo ya kinena.
Katika zama hizi za utandawazi na muingiliano baina ya tamaduni zetu za asili na tamaduni za kimagharibi, imekuwa ni kawaida kwa vijana wa rika tofauti na jinsia zote kutoga ulimi, mdomo, kitovu ama kivimbe cha nyusi kwa sababu tofauti tofauti sana.
Hivyo basi, ni muhimu sana kufahama ukweli kuhusu faida ama hasara za kutoga ulimi ama mdomo kabla hujatekeleza azma yako ya kutoga viungo hivi vya mwili.
Kutoga Ulimi ama Mdomo kunaweza kukusababishia madhara yasiyotarajiwa
Matokeo mazuri zaidi ya kutoga ulimi ama mdomo ni kutokutokea kwa kidonda ama kivimbe, wakati matokeo mabaya kutokea kwa baadhi ya watu ni pamoja na kuvunjika kwa meno/jino, kuvuja kiasi kikubwa cha damu, ama maambukuzi ya bakteria kwenye kidonda. Kutoga ulimi hujumuisha kutumika kwa sindano inayopenyezwa katikati ulimi ili kupitisha na kuhifadhi kipini, ama ndoana ama hereni ya urembo. Kazi hii ya kutoga ulimi mara nyingi ganzi huwa haitumiki. Baada ya kutoga, kuvimba kwa ulimi na maumivu ya muda hutokea.
Madhara ya kutoga Ulimi
- Kuvuja damu kiasi kidogo hutarajiwa, kuna hatari ya mishipa ya damu kuharibiwa wakati wa kutoga ulimi, hali inayoweza kusababisha kuvuja damu kwa kiasi kikubwa kuliko ilivyotarajiwa.
- Ingawa kuvimba kwa ulimi kunatarajiwa baada ya kitendo cha kutoga ulimi, wakati mwingine ulimi huvimba kwa kiasi cha kuziba kwa njia ya hewa. Kuziba kwa njia ya hewa kunaweza kusababisha kifo.
- Ikiwa fundi wako wa kutoga ulimi hana uzoefu wa kutosha kufanya kazi hiyo, anaweza kuharibu mishipa ya fahamu ya ulimi hivyo kuharibu uwezo wa ulimi kuhisi/kutambua hisia za joto,baridi ama ladha ya chakula na vinyaji, vile vile kuathiri mienendo ya viungo vya eneo la kinywa na uso. Kwani nyuma ya ulimi kuna mishipa ya fahamu,mishipa hii ikiharibiwa ulimi utapooza hivyo kusababisha ganzi la kudumu, kuathirika kwa uwezo kuongea na kushindwa kutambua ladha za chakula/vinywaji
- Vilevile kutoga ulimi kunakuweka kwenye hatari ya kupata maambukizi kwenye ulimi hasa ikiwa hutaweza kutunza hali ya usafi wa kinywa na meno kila wakati, hivyo kusababisha wadudu jamii ya bakteria kupenya na kuingia ndani ya ulimi na kusababisha maambuzi kwenye ulimi.
- Hali ya kutoga ulimi inapodumu kwa muda mrefu, inaweza kusababisha nyufa kwenye meno, ama kuvunjika kwa nyuso za jino/meno kwa sababu ya msuguano wa muda mrefu kati ya jino/meno na hereni/kipini ama ndoana ya chuma/plastiki iliyohifadhiwa kwenye ulimi kwa muda mrefu. Nyufa hizi kwenye meno, kwa kawaida husababisha maumivu makali ya jino/meno. Hivyo basi meno haya yenye nyufa yanaweza kutibiwa kwa kuvalishwa kofia “ dental crown”. Si kawaida kupata magonjwa ya fizi ama kuta za ndani za shavu ikiwa umetoga ulimi na unatunza afya ya kinywa na meno vizuri.
Kutoga Mdomo
Kutoga mdomo ni pale pete ya urembo inapovalishwa ama kuhifadhiwa ndani ya mdomo. Majeraha ya kutoga mdomo hupona haraka zaidi, hata hivyo unapaswa kutunza kidonda cha jeraha hili kwa umakini mkubwa wakati wa kupona. Vyakula, vinywaji na moshi wa sigara vinapofikia kidonda hiki, vinaongeza hatari ya kupata maambukizi kwenye kidonda.
Kishikizo vishikizo vya pete hii ya urembo kinaweza kusababisha vidonda kwenye fizi ama kuharibu jino. Kwa baadhi ya watu, tiba ya kupandikiza fizi hutumika kurejesha fizi zilizoathirika. Kama ilivyo kwa kutoga ulimi, kutoga mdomo pia kunaweza kuathiri mshipa wa fahamu hivyo kuathiri mienendo ya misuli ya kwenye eneo la kinywa na mdomo.
Je, una mpango wa kutoga Ulimi ama Mdomo?
Ikiwa unapanga kutoga viungo hivi vya mwili, unashauriwa ufanye mambo yafuatayo yatakayo kuwezesha kupata huduma ambayo haita athiri afya yako:
- Hakikisha ngariba mtoga ulimi ama mdomo sio tu ana uzoefu wa kutosha kwenye kazi anayofanya, bali pia anazingatia usafi kufanya kazi zake.
- Nenda hospitali kupata ushauri tiba mara tu unapoona ama maumivu ni makali sana, kuvimba kwa ulimi ama damu zinavuja kwa muda mrefu (zaidi ya dakika 30) ama ikiwa jeraha linapata maambukizi ya bakteria.
- Unapokuwa na hereni, pete ama ndoana ya urembo kwenye ulimi ama mdomoni, unashauriwa kumwona daktari wa kinywa na meno kila baada ya miezi sita (6). Daktari wa meno atafanya kazi ya kuhakiki ikiwa kidude kilichovalishwa kina madhara kwenye meno ama fizi, hivyo kudhibiti athari zinazoweza kutokea kwa kutoga ulimi ama mdomo.
- Wana michezo wanashauriwa kutovaa hereni, pete ama ndoana ya urembo iliyopo kwenye ulimi ama mdomoni wanapokuwa mchezoni, kwani vyombo hivi vya urembo vinaweza kunasa kwenye ngozi bila kutarajia hivyo kusababisha madhara yasiyotarajiwa.
Utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha State University cha Jijini New York nchini Marekani umesema ya kwamba manii ni nzuri kwa wanawake kwani huwaondolea msongo wa mawazo.Pia watafiti hao wamesema wanawake wanaofanya tendo la ndoa mara kwa mara bila kutumia kinga (mapenzi salama) wanakuwa na kiwango idogo cha msongo wa mawazo na hufanya vizuri katika vipimo vya akili.
Maambukizi ya tete kuwanga hupatikana vipi?
Dalili na viashiria vya Tete kuwanga
Dalili za kwanza ni
Vipimo vya uchunguzi
- Utambuzi wa ugonjwa huu hufanywa kwa kuangalia dalili na viashiria vya ugonjwa huu(Kichefuchefu, kupungua kwa hamu ya kula,maumivu ya kichwa,maumivu ya misuli, kuumwa tumbo na vipele)
- Kupima majimaji ya ndani ya vipele kwa kutumia direct immunoflorescent test
- Kipimo cha damu kuangalia wingi wa Immunglobin M (IgM), ambapo kiwango chake huongezeka panapotokea maambukizi mapya au kuangalia uwepo wa Immunoglobulin G (IgG) ili kuthibitisha kuwepo kwa maambukizi hapo awali.
- Kipimo cha ultrasound kwa wanawake wajawazito ili kuangalia dalili za kuwepo kwa maambukizi ya ugonjwa huu kwa kiumbe kilichomo tumboni (Fetal Varicella Infection).Inashauriwa kuchelewesha kipimo hiki kwa wiki 5 toka mama apate maambukizi ya tete kuwanga ili kuweza kutambua kama mtoto ameathirika au la.
- Kipimo cha kuangalia vina saba (DNA) ya virusi vya Varicella zoster virus kwa mama wajawazito kwa kuchukua maji kwenye chupa ya uzazi ya mama (amniotic fluid). Kipimo hiki kina madhara kama kusababisha mimba kutoka au mtoto kupata Fetal Varicella Syndrome
Matibabu
- Kuwakata watoto kucha ili kuepusha kujikuna na hatimaye kukata vipele hivyo kuongeza kutokea kwa vipele mwilini
- Dawa za maumivu kama paracetamol n.k
- Antihistamines-Dawa za kupunguza kuwashwa mwili
- Calamine lotion ingawa hakuna tafiti zilizofanyika kuthibitisha ubora wa matumizi yake dhidhi ya ugonjwa huu.Dawa hii ni salama
- Kuongeza kiwango cha usafi wa mwili, kuosha mwili kwa maji ya uvuguvugu
- Kukaa sehemu zenye baridi ili kupunguza kuwashwa mwili
- Kuepuka kujikuna vipele
- Dawa dhidhi ya virusi (antiviral medication) kama acyclovir au valacyclovir ambazo hutolewa saa 24-48 baada ya vipele kuanza,dawa hizi hupunguza kusambaa kwa virusi lakini haziui virusi hao.Dawa hizi hutolewa kwa wale ambao wana upungufu wa kinga mwilini na kwa wanawake wajawazito.Watoto chini ya miaka 12 au wale wenye umri wa zaidi ya mwezi mmoja hawaruhusiwi kutumia dawa hizi kama hawana tatizo la upungufu wa kinga mwilini ili kuwaepusha na madhara wanayoweza kupata kutokana na matumizi ya madawa haya.
Madhara ya tete kuwanga kwa wajawazito
- Madhara kwenye ubongo wa mtoto-Kichwa maji (hydrocephalus), kichwa kuwa kidogo, maambukizi ya ubongo (encephalitis),aplasia of brain
- Madhara ya macho kama mtoto wa jicho (cataract), optic cup, optic stalk,microphthalmia, cataracts, chorioretinitis, optic atrophy n.k.
- Madhara ya mishipa ya fahamu
- Madhara ya kibofu cha mkojo, miguu, njia ya haja kubwa,vidole kutoota vizuri n.k.
- Matatizo ya ngozi kama hypopigmentation na n.k.
Zamani ilikuwa ni kawaida kuona wanawake wanatoboa masikio, pua, ili kuvaa aina mbalimbali za herini na shemeri. Siku hizi si ajabu kuona wanaume na wanawake wakijitoboa au kuchorwa alama (tattoo) sehemu mbalimbali za miili yao kama kwenye pua, mdomo, ulimi, tumbo, masikio, mikono, miguu, kwenye kichwa, mapaja, mgongo na hata sehemu za siri yote haya kwa ajili ya urembo, miila au desturi zao, kutaka kujinasibu na tabaka fulani au kutaka kuonyesha ubunifu wao (artistic expression).
Ni mambo gani ya kuzingatia kabla ya kutoboa/kuchorwa mwili wako?
- Unatakiwa kujua uwezekano wako wa kupata maambukizi - Kama tayari una maambukizi au una kidonda kilichowazi, ni bora ukaacha kutoboa/kuchorwa mwili mpaka utakapopona na kuwa na afya njema. Hatari ya kupata maambukizi ni kubwa kama utatobolewa/kuchorwa na mtu ambaye si mtaalamu na hana ujuzi wa kufanya kazi hii. Hakikisha anayekufanyia hivi awe anafahamu masuala ya kukinga wateja wake na maambukizi ambayo ni pamoja na kusafisha vifaa vyake kila baada ya kazi, kuvichemsha vifaa hivyo au kuhakikisha vipo salama na havina bakteria wowote kwa kutumia kemikali za kusafishia, kuvifunika vifaa hivyo baada ya kuvisafisha na yeye mwenyewe kuvaa gloves salama (surgical gloves) wakati wa kufanya kazi yake hiyo ili hata kama ana magonjwa ya kuambukiza asiweze kukuambukiza wewe kwani zipo taarifa ambazo watu wameambukizwa ugonjwa wa ukimwi au wamepata ugonjwa wa tetanus wakati wa kutobolewa/kuchorwa miili yao.
- Hakikisha huna maradhi yoyote sugu - Kama una maradhi ya kisukari, ni bora ukaepuka kutoboa/kuchorwa mwili kwani kidonda chake kinaweza kisipone haraka na hatari ya maambukizi kwa wagonjwa wa sukari iko juu kupitia kwenye vidonda.
- Fahamu kuhusu uwezo wako wa kupona - Unatakiwa uwe na ufahamu juu ya uwezo wa mwili wako katika kupona (healing tendencies) kidonda chochote kile. Kuna watu wengine wanapopata mchubuko au kukatika ngozi zao hupona kwa ngozi ile kufanya kama baka na uvimbe unaojulikana kama keloids. Kama wewe ni mmoja wa watu wa aina hii basi unahitaji kuepuka kufanya kitendo hiki cha kutoboa/kuchora mwili wako. Sehemu ambazo huchukua muda mrefu kupona baada ya kutoboa/kuchora mwili ni pamoja na kwenye maeneo ya tumboni, kwenye chuchu na hata sehemu za siri kwa wanawake.
Taarifa iliyotolewa na shirika la habari la Uingereza BBC, Julai 8 kuhusu utafiti uliofanyika nchini Uingereza uliowahusisha watoto 11,000 wakifuatiliwa kuhusu ratiba zao za kulala na kupima uwezo wa bongo zao.
Watafiti hao walisema ya kwamba wale watoto waliolala baada ya saa tatu usiku na waliokuwa hawana ratiba maalumu walikuwa na alama za chini kwenye hisabati na uwezo wa kusoma.
Na vilevile waliripoti kuwa ni vigumu ubongo kujifunza vitu vipya kutokana na ukosefu wa usingizi. Walichukua watoto wa kati ya miaka 3, 5 na 7 wakifuatilia uwezo wao wa kujifunza ukilinganisha na ratiba zao za kulala. Ratiba ilikuwa mbaya zaidi kwa watoto wa miaka 3. Na mpaka wanapofika miaka saba huwa na ratiba inayoeleweka kati ya saa moja na nusu usiku na saa mbili na nusu usiku.
Kwa takribani miongo mitatu sasa, tumeshuhudia ongezeko kubwa la mlipuko wa ugonjwa wa mkanda wa jeshi linaloendana na ongezeko la hususani ugonjwa wa UKIMWI. Hali hii imefanya baadhi ya watu kuamini kuwa, ugonjwa huu ni dalili ya wazi kabisa ya mtu kuwa na VVU, imani ambayo kwa kiasi kikubwa ina ukweli ndani yake ingawa si kwa wote wanaopatwa nao.
Mkanda wa jeshi au shingles au herpes zoster kwa majina ya kitabibu ni ugonjwa unaosababishwa na virus wa aina ya Varicella-zoster ambao pia husababisha ugonjwa wa tetekuwanga au chickenpox. Ugonjwa huu huathiri ngozi ambapo huambatana na vipele na michubuko kama ya kuungua yenye kuambatana na maumivu makali.
Visababishi
Kama tulivyokwisha tangulia kueleza hapo juu, ugonjwa huu husababishwa na virus aina ya Varicella-zoster ambao pia husababisha ugonjwa wa tetekuwanga. Baada ya mtu kupatwa na tetekuwanga, virus hawa hubaki katika hali ya kupooza/kutokuwa na madhara (dormant) katika neva fulani za mwili. Baada ya miaka kadhaa, iwapo itatokea kinga ya mwili ikashuka kwa sababu yoyote ile, virus hawa hupata tena nguvu/kuwa na madhara (active), kuibuka na kusababisha ugonjwa wa mkanda wa jeshi.
Kwa kawaida shambulio la mkanda wa jeshi hutokea mara moja maishani ingawa laweza kujirudia.
Vihatarishi
Mkanda wa jeshi unaweza kumpata mtu wa umri wowote ule ingawa watu walio katika makundi haya wapo katika hatari kubwa zaidi:
• Wenye umri wa zaidi ya miaka 60
• Mtu aliyewahi kuugua ugonjwa wa tetekuwanga kabla ya umri wa mwaka mmoja
• Watu ambao kinga yao ya mwili imepungua kwa sababu mbalimbali kama vile matumizi ya aina fulan za dawa, magonjwa kama vile maambukizi ya VVU (HIV/AIDS), saratani na utapiamlo.