Madhara yanayoletwa na Cocaine
Cocaine huathiri mfumo wa mishipa ya fahamu (sympathetic nervous system) kwa kuzuia ufyonyaji upya wa homoni ya katekolamine na kuongeza kazi yake ambayo ni kuongeza mapigo ya moyo, kuongeza shinikizo la damu,kuongeza kazi ya misuli ya moyo kupiga zaidi hivyo kusababisha mahitaji ya oxijeni kuongezeka, vile vile mkazo (spasms) au mbano kwenye mishipa ya damu ya moyo hupunguza usambazaji wa oxijeni, vyote hivi hupelekea misuli ya moyo kuumia napengine kufa (ischemia-infarction)
Cocaine pia huzuia njia za usafirishaji madini(Ion) ya sodium kwenye moyo, na kusababisha moyo kupiga bila mpangilio
Zifuatazo ni athari zinazoweza kusababishwa na Cocaine:
- Mshtuko wa moyo (heart attack)
- Moyo kushindwa kufanya kazi vizuri (heart failure)
- Shida au magonjwa ya misuli ya moyo (cardiomyopathies)
- Kuchanika kwa mshipa mkubwa wa damu (aortic dissection)
- Maambukizi ya misuli ya ndani ya moyo (endocarditis)
- Moyo kupiga bila mpangilio
Dalili kuu ya mgonjwa anayekuja na matatizo ya moyo kwasababu ya matumizi ya cocain:
- Maumivu ya kifua, kifua kinakuwa kizito na huambatana na kushindwa kupumua vizuri na kutokwa jasho sana
Dalili nyingine ni:
- Kichefuchefu
- Kuhisi mapigo yako ya moyo
- Na kutapika
Athari zinazoletwa na heroin ni:
- Maambukizi kwenye bitana ya moyo
- Maambukizi kwenye milango ya moyo
Vipimo mbali mbali vya moyo ambavyo hufanyika ni:
- Electrocardiogram- kuangalia hali ya mapigo ya moyo na kuweza kugundua shida ya mishipa ya damu ya moyo, Maambukizi kwenye bitana ya moyo
- Echocardiogram- kuangalia uwezo wa myo kufanya kazi na kama kuna shida kwenye misuli ya moyo, milango ya moyo au maambukizi kwenye milango ya moyo
- Cardiac Biomakers- hasa Troponin kuangalia kama kuna shida kwenye mishipa damu ya moyo
Matitabu ya maumivu makali ya kifua na mshtuko wa Moyo
- Dawa za junior Aspirin na Benzodiazepines
- Na kwa wenye mshtuko wa moyo watahitaji kupata matibabu zaidi ikiwemo ya kuzibua mishipa hiyo (PCI)
- Kutibu kila ugonjwa kutokana na ushauri wa daktari
NB: ni muhimu kupata matibabu hospitali na kamwe usijitibu mwenyewe
Ushauri nasaha
- Wa kuacha matumizi ya madawa ya kulevya cocain na heroin na kuanza mpango wa detoxification