VVU/UKIMWI bado unaendelea kuwa janga katika jamii yote ya dunia ikiwa imeshasababisha vifo vya watu takribani millioni 33 mpaka sasa kulingana na taarifa ya WHO ya mwaka 2020.
Mpaka waka 2019 takribani ya watu million 38 walikuwa wanaishi na maambukizi ya VVU, Tanzania pekee ni watu millioni 1.6 wanaoishi na maambukizi hayo kwa taarifa ya mwaka 2018 pekee.
Hivyo taaarifa hizi zinaonyesha umuhimu wa kupima, kujua dalili na kujikinga na maambukizi ya VVU.
Hebu zifahamu dalili za ugonjwa wa VVU/UKIMWI
Moja kati ya changamoto kubwa kuhusu ugonjwa huu ni kuwa mara nyingi mtu mwenye maambukizi hatoonyesha dalili zozote hadi hapo baadae ugonjwa utakapo fika hatua mbaya zaidi. Sambamba na hilo dalili zake nyingi za awali hazina uhusika wa moja kwa moja na ugonjwa huu maana zinaweza sababishwa na magonjwa mengine.( non specific symptoms).
Na dalili hizi hutegemeana sana na hatua (stage) ya ugonjwa
Pindi mtu anapokuwa amepata maambukizi uanza na dalili zifuatizo katiki wiki chache za mwanzo (2-4) au kutokuwa na dalili kabisa. Dalili za awali na kama zifuatazo
- Homa
- Kichwa kuuma
- Miwasho au vipele
- Madonda ya koo (sore throat)
- Maumivu ya misuli na kuchoka
- Kuvimba matezi
- Kutoka jasho jingi
- Kukosa hamu ya kula
- kuharisha N.K
ukiona una dalili moja wapo kati ya hizi na umeshiriki tabia yoyote hatarishi ya ugonjwa wa VVU/UKIMWI unashauriwa ukifike kituo cha afya kwaajili ya kipimo cha VVU na kupata ushauri.
Kama nilivyoandika hapo awali unaweza usiwe na dalili yoyote hadi hapo baadae ambapo kinga yako imedhohofika kutokana na virusi hivi kushambulia chemechembe nyeupe dama (CD4) zinazo saidia kinga ya mwili.
Dalili zifuatazo na magongwa nyemelezi hutokea pindi unapo kuwa na usugu wa ugonjwa huu na kinga kushuka.
- Utando mweupe mdomoni
- Fungusi ukeni
- Malengelenge mdomoni na sehemu za siri (herpes simplex)
- Mkanda wa jeshi
- Vipele vyeusi mwili mzima (pruritic Papura Eruptions)
- Saratani mfano saratani ya shingo ya uzazi, saratani za ngozi (karposi sarcoma)
- Kifua kikuu
- Kupungua uzito
- Fangasi ya uti wa mgongo (criptococcal mengitis)
- Upungufu wa damu
- Gonjwa la akili utokanao na VVU/UKIMWI (HIV encephalopathy)
- Gonjwa la figo litokanalo na UKIMWI n.k
Ugojwa huu haina tiba wala chanjo lakini habari njema ni kwamba unaEPUKIKA! Aidha kabla ya kujua jinsi ya kujikinga ni muhimu kufahamu kwa sehemu jinsi ugongwa huu unavyosambaa.
Ugonjwa huu huambukizwa kwa kubadilishana majimaji na mtu aliyeathirika kama vile damu, maziwa, shahawa au majimaji kutoka kwenye uke. Pia huambukizwa kutoka kwa mama kuja kwa mtoto wakati wa ujauzito,kujifungua na kunyonyesha.
Zifuatazo na njia mbali mbali za kujikinga na VVU/UKIMWI.
Ile kujinga a ugonjwa wa VVU/UKIMWI ni muhimu kuondoa kabisa au kupunguza tabia hatarishi kwako.
Matumizi ya kondomu za kike na kiume
Ni vema kutumia kondomu pindi unapojamiana na mtu usiye jua hali yake au mwenye maambukizi ya VVU. Tafiti zinaonyesha kondomu huzuia maambukizi ya magonjwa ya zinaa ikiwemo ukimwi kwa Zaidi ya asilimia 85. Zingatia uvaaji sahihi wa kondomu.
Kuzuia maambukizi ya mama kwenda wa mtoto
Mtoto wa mama mwenye maambukizi huweza kupata maambukizi wakati wa ujauzito wakati wa kujifungua na kunyonyesha. Tafiti zinaonyesha kiwango cha maambukizi huanzia asilimia 15 hadi 45 bila kufanya harakati ya kuzuia maambukizi hayo.
Ili kuzua maambukizi mama mjamzito anapaswa kujua hali yake kabla na pindi unapokuwa mjamzito, na kama umeathirika anapaswa kuanza dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI mara. Pindi unapojifungua, mtoto huanzishiwa dawa maalum ya kumkinga na maambukizi kwa miezi sita huku akifanya vipimo kuthibitisha kama amepata maambukizi tiyari. Taarifa hizi na huduma za vipimo na madawa hutolea kliniki hivyo kuhudhuria kliniki ni muhimu sana.
Tohara kwa wanaume
Tohara imeonyesha kusaidia kupunguza maambukizi ya VVU kwa wanaume kwa asilimia 60 na sio kuzuia kama ilivyodhana potofu ya watu wengi. Hivyo hakikisha kwa hiari unafanyiwa tohara mapema ili kupumguza hatari ya kupata maambubikizi.
Kutokuchangia vitu vyenye uncha kali kama sindano, viwembe n.k. Kundi maalum hapa ni waathirika wa madawa ya kulevya maana hujidunga madawa kwa kuchangia mabomba ya sindano. Kundi hili ni muhimu kupata matibabu kuondoa ulevi wa madawa ili kuwalinda na maambukizi.
Uaminifu hii pia jia ya kujikinga na maambukizi kwa kuwa mwaminifu kwa mpenzi mmoja hasa kwa wanandoa
Matumizi ya madawa ya kufubaza makali virusi vya UKIMWI- tafiti zinaonyesha kuwa mtu anayetumia madawa haya anakuwa hana huwezo mkubwa wa kuambukiza ukilinganisha na ambae hatumii kabisa au anayetumia kwa kusuasua.
Kinga baada ya kuwemo hatarini (post exposure prophylaxisis PEP)
Hizi na dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWIi zinazotolea kama kinga ndani ya masaa 72 pindi mtu anapokuwemo kwenye hatari ya maambukizi. Dawa hizi hutolewa kwa muda wa siku 28 pamoja na ushauri nasaa na vipimo.
USHAURI na Mazingatio
Pamoja na kujua dalili na jinsi ya kujinga na VVU/UKIMWI ni muhimu sana kujenga tabia ya kupima na kujua afya yako mara kwa mara na kuepuka tabia hatarishi. Usiogope maana hata ukigundulika na ugonjwa huu huo sio mwisho wa maisha. Sasa waweza ishi na kuwa na furaha hata kama umeathirika.
Nimekutana na jamii ya watu wengi kwenye utumishi wangu kama daktari ambao wanaamini kuwa ukigundulika una maaambukizi ya VVU/UKIMWI basi maisha yameishia hapo na hakuna tumaini tena.
Leo nimekuletea habari njema kuwa dhana ya kwamba hakuna maisha baada ya maambukizi ni uongo.
Wapo watu wengi sana wanaofurahia maisha pamoja na familia zao licha ya kwamba wanaishi na maambukizi ya VVU/UKIMWI.
Twende pamoja nami kwenye makala hii ili uweze kutambua mambo ya kuzingatia pindi unapogundulika kuwa umepata maambukizi ya VVU/UKIMWI.
HONGERA! Kwa kupima na kujua afya yako.
Jambo la kwanza la kufanya ukingundulika kuwa una maambukizi ni kukubali matokeo au hali halisi ya majibu ya vipimo. Na kupata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa mtoa huduma.
Mtoa huduma baada ya kukupa ushauri nasaha kulingana na miongozo ya matibabu ya VVU/UKIMWI atakuanzisha dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI.
Zingatia!!
Ni muhimu sana kujisajili na kuhudhuria katika kliniki za CTC zilizopo kwenye takribani vituo vyote vya afya ili taarifa zako na maendeleo yako yaweze kuafuatiliwa kwa ukaribu na wahudumu wa afya. Ukijisajili utapewa kadi ya CTC yenye namba yako ya usajili na inayoonyesha mahudhurio, dawa unazotumia, kiwango cha virusi mwilini (viral load) na wingi wa chembechembe nyeupe za damu zinazohusika na kinga ya mwili yaani CD4
Kuwa na mahudhurio mazuri kwenye kliniki za CTC kadri unavyoelekezwa na daktari ni jambo la msingi sana kwani wahudumu wa afya wataweza kufuatilia kwa karibu maendeleo ya afya yako, madhara yatokanayo na dawa za kufubaza virusi vya VVU/UKIMWI na kuangalia kama dawa ulizopewa zinakusaidia kupata nafuu au la nk.
Matumizi sahihi ya dawa ya kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI (ARV) -Dawa hizi mgonjwa humeza kila siku kulingana na maelekezo ya daktari.
Kama wewe ni msahaulifu ni vizuri kumtumia mtu wa karibu nawe (mwenza au ndugu katika familia au rafiki) kukusaidia kukukumbusha endapo umesahau kumeza dawa au utumie APP yetu ya Tanzmed ambayo inapatikana kwenye play store ambayo unaweza weka taarifa zako nayo ikakumbusha muda wa kumeza dawa.
Kumbuka kwamba dawa hizi hazitibu virusi vya VVU/UKIMWI bali hufubaza makali ya virusi hivyo, husaidia kuongezeka kwa kinga ya mwili wako, hupunguza au kuondoa kabisa magonjwa nyemelezi na kuboresha hali ya maisha ya mgonjwa. Ni muhimu sana kwa mgonjwa wa UKIMWI kuzingatia matumizi ya dawa hizi kwa kufuata maelekezo ya daktari bila kukosa.
Lishe na mazoezi
Madawa ya kufubaza virusi vya UKIMWI yana nguvu sana hivyo huhitaji lishe nzuri na mazoezi. Pia ugonjwa wa UKIMWI husababisha mwili kudhoofu kwa kupunguza kinga mwilini na hivyo basi kuongeza mahitaji ya nishati mwilini, hupunguza hamu ya kula chakula, na uduni wa kufyonza virutubisho kwenye mwili.
Hivyo unashauriwa ule mlo kamili wenye virutubisho vyote ile kusaidia kujenga mwili vizuri.
Lishe ya mgonjwa wa UKIMWI huzingatia umri wa muhusika, hali ya ujauzito au kama ananyonyesha.Pia lishe hutegemea kama mgonjwa wa UKIMWI ana magonjwa nyemelezi na hatua ya ugonjwa (stage) na wingi wa virusi vya VVU mwilini (viral load).
Lishe bora kwa wagonjwa wa UKIMWI inahusisha virutubisho kama wanga, protini,mafuta, vitamin na madini aina mbalimbali.
Tafiti zinasema kama una maambukizi na huna dalili yoyote unatakiwa kutumia lishe asilimia 10 zaidi ya mtu ambaye hana maambukizi, na kama una dalili inabidi kutumia lishe asilimia 20-30 ya mtu asiye na maambukizi wa rika moja, jinsia moja na shughuli za mwili zinazofanana. Endelea kuwa nasi kupata makala inayohusu lishe na UKIMWI.
Kujiepusha na tabia hatarishi za ugonjwa wa VVU/UKIMWI.
Kuna dhana mtaani kwamba kama nimepata maambukizi ya VVU/UKIMWI basi na mimi nastahili kuambukiza wengine. Dhana hii ni potofu sana.
Pindi unapogudulika na maambukizi ya VVU/UKIMWI inabidi uzigatie namna zote za kuzuia kueneza ugojwa huu hatari na kuwa msitari wa mbele kuelimisha na kulinda jamii inayokuzunguka.
Mfano wa tabia hatarishi ni;
Kushiriki ngono zembe bila kinga
Kuwa na wapenzi zaidi mmoja
Kuchangia vitu vyenye incha kali kama sindano, viwembe n.k na
Kutokutumia dawa za kufubaza virusi vya VVU/UKIMWI kama ulivyoelekezwa na dakari.n.k
kama ulikuwa na ulevi wa pombe unashauriwa kuacha mara moja kwani unywaji wa pombe kupindukia huongeza uwezekano wa kupata magojwa mbalimbali ikiwemo kifua kikuu,nimonia na homa ya ini na pia huongeza madhara kwenye ubungo kwa watu wenye maambukizi ya VVU/UKIMWI. Kama ni muathirika wa madawa ya kulevya hakikisha unaanza kliniki za methadone kwa ajili ya matibabu na kujiepusha kuchangia kujidunga sindano.
Mama mjauzito
Inawezekana ulikuwa unafikiri kama mimi ni mjamzito JE nafanyaje?
Nikupe hongera kwa sababu sasa unaweza pata mimba na kujifungua mtoto asiye na maambukizi kwa kufuata maelekezo kutoka kwa wahudumu wa afya ukiwa kliniki.
Jambo la kwanza ni kuanza kliniki mapema ambapo vipimo vitarudiwa tena na utaanzishiwa dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI (ARV) mara tu baada ya kukubali na kupata ushauri nasaha.
Mambo yote tajwa hapo juu ni muhimu kuyazingatia hata kama ni muathirika wa VVU/UKIMWI ni mjamzito. Matumizi ya madawa ni muhimu sana maana yatafubaza virusi na kupunguza uwezekano wa mtoto kupata maambukizi akiwa kwenye mfuko wa uzazi. Pamoja na hilo inabidi kuzingatia lishe bora kama ambavyo utaelekezwa na dakatri. Kwa maana mahitaji yako ya lishe yako tofauti na makundi mengine.
Pia inabidi kufanya mahudhurio mazuri kliniki na kuhakikisha unajifungulia kwenye kituo cha afya na sio nyumbani ili upate huduma sahihi na salama kwa mtoto wakati wa kujifungua ikiwemo dawa za kumkinga mtoto asipatae maambukizi ya virusi vya VVU/UKIMWI.
Ukizingatia hayo machache na mengi kutoka kwenye vituo vya afya basi utaweza kuishi maisha marefu yenye furaha na kuendelea na shughuli zako kama kawaida.
Moja kati ya vitu vya msingi vya kuzingatia ukiwa muathirika wa ugonjwa wa VVU/UKIMWI ni matumizi sahihi ya dawa.Watu wengi wamepotoshwa na taarifa za uongo kuwa dawa hizi hupunguza nguvu za kiume hivyo wagonjwa wengi wa UKIMWI hawatumii dawa hizi na badala yake hutumia mitishamba au kutokutumia dawa kabisa.
Tafiti nyingi zimefanyika na kuonyesha kwamba dawa hizi zina uwezo mkubwa wa kuzuia magonjwa yatokanayo na UKIMWI na kuzuia vifo. Aidha dawa hizi zimeonyosha uwezo mkubwa wa kupunguza maambukizi ya mama kwa mtoto.Matumizi ya dawa za kufubaza makali ya virusi vya VVU/UKIMWI kwa waathirika wa ugonjwa huu yanahusishwa na kupungua kwa hatari ya kueneza maambukizi ya virusi vya VVU/UKIMWI wakati wa kushiriki tendo la ndo kwa sababu ya uwezo wake wa kupunguza makali ya virusi vya UKIMWI.
KUKMBUKA dawa hizi sio tiba ya virusi vya VVU/UKIMWI.
Utaratibu wa Kuanza Dawa
Kulingana na miongozo ya matibabu ya VVU/UKIMWI anashauriwa kuanza dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI mara tu anapogundulika kuwa ni muathirika wa virusi vya VVU/UKIMWI na kupewa ushauri nasaha. Hii husaidia sana kupunguza makali ya virusi hivi.
Utaratibu wa kuanza dawa huambatana na kujisajili kwenye za kliniki za CTC ambazo zipo kwenye takribani vituo vyote vya afya nchini. Ukishajisajili utapewa namba pamoja na kadi ambayo itakuwa na taarifa zako zote muhimu kama muda au tarehe ya kumuona dakatri, aina na kiwango cha dawa unachotumia , wingi wa virusi vya VVU kwenye damu (viral load) na kiwango cha CD4.
Endapo uligundulika na virusi vya VVU/UKIMWI na umeshaanza kupata magonjwa nyemelezi, basi utaanza matibabu ya magonjwa hayo na kuanzishiwa dawa za kufubaza virusi vya ukimwi ndani ya wiki mbili.
Kuna baadhi ya magonjwa ikiwemo kifua kikuu (PTB) pamoja na ugonjwa wa kukakamaa shingo (Cryptococcoal Meningitis) huwa kuanza kutumia dawa haraka sio vizuri kwani inaongeza hatari ya kupata mchafuko wa kinga ya mwili (Immune Reconstitution Inflammatory Syndrome- IRIS) ambayo huzidisha dalili za magonjwa nyemelezi.
Hali hii hutokea kwa sababu madawa ya kufubaza virusi vya UKIMWI husaidia kuongeza kinga ya mwili na hivyo mwili huanza vita na magonjwa nyemelezi ambayo mwanzo mwili ulikuwa hauna uwezo wa kuyadhiti hii huleta mchafuko wa kinga ya mwili na kuzidisha dalili zilizopo au kusababisha dalili mpya za magonjwa nyemelezi.
Matumizi Sahihi ya Dawa za Kufubaza Makali ya Virusi vya VVU/UKIMWI (ARV)
Matumizi sahihi ya dawa za kufubaza makali ya virusi vya VVU/UKIMWI ni muhimu sana kwani usipofanya hivyo unaweza kupata madhara makubwa zaidi ikiwemo ugonjwa wa UKIMWI kuja kwa kasi zaidi, hali hii huchangia sana mgonjwa kupoteza maisha. Hivyo hakikisha unapata maelekezo yote kuhusu utumiaji wa dawa kutoka kwa daktari wako.
Dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI zipo kwenye makundi mbalimbali. Tafiti tofauti pamoja na miongozo ya matibabu ya VVU/UKIMWI zimependekeza matumizi ya dawa zifuatazo; Tenofovir disoproxil fumarate(TDF), Lamuvidine(3TC), Dultegravir(DTG) kama dawa za kwanza dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI (first line treatment).
Yapo makundi mbalimbali ya mchanganyiko wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya VVU/UKIMWI ambayo yanaweza kutumika kulingana na kundi analotoka mgonjwa mfano watoto wadogo, mama mjamzito au kulingana na jinsi ambavyo dawa hizi hufanya kazi kwa mtu binafsi n.k
Dawa hizi za mchanganyiko hupatikana kama dawa moja ambayo humezwa kila siku. Dawa hii ya mchanganyiko wa madawa mbalimbali ina nguvu sana hivyo unashauriwa kula lishe bora wakati wote ili kupunguza maudhi madogo madogo yanayotokana na dawa hizi.
Hata hivyo,imeripotiwa kuwa baadhi ya waathirika hupata madhara kutokana na matumizi ya dawa hizi zilizochanganywa kwa pamoja, endapo mgonjwa atapata madhara ya dawa hizi, basi anashauriwa kumuona daktari haraka iwezekanavyo kwa ajili ya uchunguzi wa kina ili kugundua ni aina gani ya dawa inayomsababishia mgonjwa madhara.
Pindi unapougua epuka kununua madawa na kutumia bila kumuona daktari wako. Hii ni kwa sababu kuna baadhi ya dawa huingiliana na dawa za kufubaza makali ya virusi vya UKIMWI katika utendaji kazi hivyo hupelekea kupungua kwa nguvu ya dawa au dawa kubaki mwilini kwa muda mrefu sana (toxicity). Mambo yote hayo tajwa yana madhara kwa mtumiaji.
Pia unashauriwa kupunguza na kuacha unywaji wa pombe.
Muhimu: Hakikisha unameza dawa kwa kufuata maelekezo ya daktari na epuka kuruka ruka kumeza dawa au utoro wa kuhurudhia kliniki ili kuepuka madhara zaidi.
VVU/UKIMWI bado unaendelea kuwa janga katika jamii yote ya dunia ikiwa imeshasababisha vifo vya watu takribani millioni 33 mpaka sasa kulingana na taarifa ya WHO ya mwaka 2020.
Mpaka waka 2019 takribani ya watu million 38 walikuwa wanaishi na maambukizi ya VVU, Tanzania pekee ni watu millioni 1.6 wanaoishi na maambukizi hayo kwa taarifa ya mwaka 2018 pekee.
Hivyo taaarifa hizi zinaonyesha umuhimu wa kujikinga na maambukizi ya VVU.
Zifuatazo na njia mbali mbali za kujikinga na VVU/UKIMWI.
Ile kujikinga a ugonjwa wa VVU/UKIMWI ni muhimu kuondoa kabisa au kupunguza tabia harishi kwako.
Matumizi ya kondomu za kike na kiume
Ni vema kutumia kondomu pindi unapojamiana na mtu usiye jua hali yake au mwenye maambukizi ya VVU. Tafiti zinaonyesha kondomu huzuia maambukizi ya magonjwa ya zinaa ikiwemo ukimwi kwa Zaidi ya asilimia 85. Zingatia uvaaji sahihi wa kondomu.
Tohara kwa wanaume
Tohara imeonyesha kusaidia kupunguza maambukizi ya VVU kwa wanaume kwa asilimia 60 na sio kuzuia kama ilivyodhana potofu ya watu wengi. Hivyo hakikisha kwa hiari unafanyiwa tohara mapema ili kupumguza hatari ya kupata maambubikizi.
Kutokuchangia vitu vyenye uncha kali kama sindano, viwembe mikasi n.k. Kundi maalum hapa ni waathirika wa madawa ya kulevya maana hujidunga madawa kwa kuchangia mabomba ya sindano. Pia kundi ni muhimu pia kupata matibabu ili kuondoa ulevi wa madawa ili kuwalinda na maambukizi.
Uaminifu hii pia jia ya kujikinga na maambukizi kwa kuwa mwaminifu kwa mpenzi mmoja hasa kwa wanandoa
Matumizi ya madawa ya kufubaza virusi vya UKIMWI- tafiti zinaonyesha kuwa mtu anayetumia madawa haya anakuwa hana huwezo mkubwa wa kuambukiza ukilinganisha na ambae hatumii kabis au anayetumia kwa kusuasua.
Kinga baada ya kuwemo hatarini (post exposure prophylaxisis PEP)
Hizi na dawa za kufubaza kirusi vya ukimwi zinazotolea kama kinga ndani ya masaa 72 pind mtu anapokuwemo kwenye hatari ya maambukizi. Dawa hizi hutolewa kwa muda wa siku 28 pamoja na ushauri nasaa na vipimo.
Hakikisha pindi unapoongezewa dama kwasababu yoyote ile hiyo damu iwe imepimwa na haina virusi vya ukimwi.
kujiepusha na kutibiwa magonjwa ya zinaa. Tafati zinaoyoonyesha magaonjwa ya zinaa yanaongeza uwezekano mkubwa wa maambukizwa ugonjwa wa VVU/UKIMWI
Kuzuia maambukizi ya mama kwenda wa mtoto
Mtoto wa mama mwenye maambukizi huweza kupata maambukizi wakati wa ujauzito wakati wa kujifungua na kunyonyesha. Tafiti zinaonyesha kiwango cha maambukizi huanzia asilimia 15 hadi 45 bila kufanya harakati ya kuzuia maambukizi hayo.
Ili kuzua maambukizi mama mjamzito anapaswa kujua hali yake kabla na pindi unapokuwa mjamzito, na kama umeathirika anapaswa kuanza dawa za kufubaza vurusi vya VVU mara. Pindi unapojifungua mtoto huanzishiwa dawa maalum ya kumkinga na maambukizi kwa miezi sita huku akifanya vipimo kuthibitisha kama amepata maambukizi tiyari. Taarifa hizi na huduma za vipimo na madawa hutolea kliniki hivyo kuhudhuria kliniki ni muhimu sana.
USHAURI
Pamoja na kujua dalili na jinsi ya kujinga na VVU/UKIMWI ni muhimu sana kujenga tabia ya kupima na kujua afya yako mara kwa mara na kuepuka tabia hatarishi. Usiogope maana hata ukigundulika na ugonjwa huu huo sio mwisho wa maisha. Sasa waweza ishi na kuwa na furaha hata kama umeathirika.
Utangulizi
Neno ukimwi ni kifupisho cha maneno “Upungufu wa Kinga Mwilini”. Ugonjwa huu usabishwa na virusi ambavyo hushambulia chembe chembe za kinga na kuufanya mwili ushindwe kujilinda dhidi ya maradhi ipasavyo au hata kushindwa kupambana na maradhi yaliyoingia tayari.
Ukimwi huambukizwa kwa njia mbali mbali kama
- kuingia damu ya mtu mwenye ukimwi kwa hasiye nao-hapo ndo kuna vitu kama kuchangia nyembe, sindano, kuwekewa damu isiyo salama n.k.
- Kujamiiana- wadudu wa ukimwi wameonekana kuwemo kwenye majimaji ya sehemu za sili, hivyo kama kuna michubuko mtu akafanya tendo hili na mhadhilika kuna nafasi ya kuambukizwa.
- Mama mjamzito kumuambukiza kiumbe kilichopo kwenye mfuko wakewa uzazi.
Tohara kwa wanaume ni oparesheni inayohusu kuondolewa kwa sehemu ya ngozi au ngozi yote inayofunika kichwa cha uume, na imekuwa ikifanywa na baadhi ya watu katika makabila na dini mbalimbali kwa zaidi ya maelfu ya miaka.
Kwa sasa tohara kwa wanaume imeamsha mvuto mkubwa wa kisayansi na uchunguzi kwa sababu utafiti umethibitisha kuwa wanaume waliotahiriwa wana viwango vidogo vya maambukizo ya virusi vya ukimwi (VVU) kuliko wasiotahiriwa.
Aidha ueneaji wa VVU ni mdogo kwa jumla katika jamii zinazotahiri wanaume kuliko zile ambazo wanaume hawatahiriwi. Kiasi cha asilimia 20 cha wanaume duniani kote inasemekana kuwa wametahiriwa, iwe mara baada ya kuzaliwa
au wakati wa balehe, kwa kawaida kutokana na sababu za kiutamaduni, kiafya au dini. Si nchi zote Barani Afrika zenye takwimu, kuhusu ushauri wa tohara kwa wanaume, hata hivyo kwa kawaida inakadiriwa kuwa chini ya
asilimia 20 ya wanaume kusini mwa Jangwa la Sahara wametahiriwa, kati ya asilimia 50 na 80 katika sehemu nyingi za Afrika ya Mashariki, na zaidi ya asilimia 80 au zaidi katika Bara la Afrika.
Kinachofahamika ni Nini?
Utafiti wa majaribio wa mara ya tatu Afrika Mashariki na Kusini ambao umefanywa, miaka ya hivi karibuni kupima kwa njia ya utafiti uliodhibitiwa, manufaa ya tohara kwa wanaume katika kuzuia maambukizi ya VVU. Utafiti uliofanywa katika Jimbo la Gauteng,Afrika Kusini, ulisimamishwa mapema zaidi kuliko ulivyopangwa kwa sababu matokeo yamethibitisha kuwa tohara ilikuwa kinga dhidi ya maambukizi ya VVU na wachunguzi wamependekeza kuwa utaratibu huo uendelee kwa watu zaidi ya 3,274 wanaoshiriki.
- Wanaume waliotahiriwa waliofanyiwa utafiti wameonekana kuwa ni asilimia 60 pungufu ya uwezekano wa kuambukizwa VVU kuliko wasiotahiriwa.
- Iwapo utafiti wa majaribio unaoendelea nchini Kenya na Uganda unaowahusisha wanaume 8,000 utatoa matokeo sawa na yale ya Afrika Kusini, tohara kwa wanaume itaungana na zana kama vile Kondomu za kiume na za kike kama njia kuu za kuzuia maambukizi ya VVU.
- Tayari msingi wa shauku umeonekana nchini Botswana na Swaziland, nchi mbili miongoni mwa nchi zilizoathiriwa sana na VVU/UKIMWI.
- Zaidi ya asilimia 80 ya wanaume waliofanyiwa utafiti Botswana wamesema kuwa wangependa kutahiriwa iwapo utaratibu huo ni salama na wenye gharama nafuu.
- Nchini Swaziland zile hospitali ambazo hazikuwa zikitahiri, sasa zimekuwa zikitahiri watu 10-15 kwa juma na zina orodha ndefu ya watu wanaosubiri huduma hiyo
Hivyo basi kutokana na faida hizi, wanamume wanashauriwa sana kufanyiwa tohara, kwa kufanya tohara siyo tuu watakuwa wamepunguza uwezekano wa kuambukizwa VVU, bali pia watakuwa wamepunguza uwezekano wa kuwaambukiza wengine kama wao wanaishi na virusi vya ukimwi.
Ikumbukwe pia, kufanya tohara pekee hakukuondolei uwezekano wa kuambukizwa VVU, hivyo unashauriwa kuendelea kutumia njia nyingine zilizo salama za kujikinga na maambukizi ya VVU.
Credit: www.nacp.go.tz
VVU/Ukimwi umeenelea kuwa ni moja kati ya changamoto kubwa katika sekta ya Afya duniani haswa kwa nchi zinazoendelea. Kutokana na Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), inakadiriwa kuwa, kuna watu milioni 36.9 wanaishi na virusi vya ukimwi duniani kote.
Kwa siku za karibuni, kumekuwa na matokeo chanya kwenye mapambano na ugonjwa wa ukimwi, sasa hivi watu wenye virusi vya ukimwi (VVU) wanaishi maisha yenye afya njema na kwa muda mrefu kwa msaada wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya ukimwi (antiretroviral therapy (ART)), pia matumizi sahihi ya dawa hizi husaidia kupunguza muendeleo wa uabukizaji kwa wengine.
Kazi kubwa pia imefanyika ili kuzuia na hata kumaliza kabisa maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua.
Ingawa kuna matokeo yote hayo chanya, lakini bado kuna sehemu kubwa ya jamii bao haina uelewa juu ya ugonjwa huu, hivyo TanzMED itakuwa inakuletea dondoo chache juu ya ugonjwa huu;
1. VVU vinaweza kuambukizwa kwa njia mbalimbali kama;
- Kuambukizwa kwa mtoto mchanga wakati akiwa tumboni, wakati wa kuzaliwa au kwa kunyonyeshwa na mama anayeishi na virusi vya ukimwi. Hivyo, kabla na baada ya kuanza kubeba ujauzito, inashauriwa kupima Afya na kuhudhuria vyema kliniki kwa ajili ya vipimo na ushauri juu na njia za kuondoa maambukizi haya.
- Kujamiiana bila ya kinga na mtu mwenye virusi vya ukimwi
- Kuwekewa damu yenye virusi vya ukimwi
- Kushare vitu vyenye incha kali (sindano, viwembe, masjine za kuchorea tattoo, mikasi nk) vilivyo na virusi vya ukimwi. Watumiaji wa madawa ya kulevya wapo kwenye hatari ya kuambukizana kwakuwa wengi hutumia sindano kwa pamoja
- Matumizi ya vifaa vya upasuaji ambavyo havijafanyiwa usafi wa kuua virusi
2. Jinsi ya kujikinga au kuzuia maambukizi ya virusi vya ukiwmi (VVU) kwa wengine
- Hakikisha unatumia zana pindi unapofanya ngono
- Nenda kapime na upate tiba ya magonjwa mengine ya zinaa kwani kuwa na magonjwa ya zinaa kuna uwezekano mkubwa wa kuambukizwa virusi vya ukimwi, pia kupima na kujijua mapema, kunasaiia kulinda afya yako na kuzuia kuwaambukiza wengine
- Hakikisha damuunayowekewa imepimwa na haina virusi vya ukimwi
- Kutahiriwa kwa wanamume kunasaidia kupunguza maambukizi (soma makala juu ya faida za tohara hapa)
- Matumizi ya mapema na yaliyobora ya dawa za kufubama makali ya virusi vya ukimwi (ARV) husaidia kukufanya uishi na afya bora pia kupunguza maambukizi kwa wengine
- Kuishi maisha yanayompendeza mungu kwa kuacha kuzini kabla na nje ya ndoa
Tangu kuingia kwa dawa za kuvubaza VVU (ARVs) kumeripotiwa kuwepo kwa mafanikio makubwa katika kuboresha afya za watu wanaoishi na VVU kwa kusaidia kupunguza idadi ya VVU na kuongeza idadi ya chembe nyeupe za CD4 zinazosaidia mwili kujilinda na maradhi. Lakini ARVs ni nini? Kuna makundi mangapi ya dawa hizi, zinafanyaje kazi, je zina madhara (side effects) yeyote katika mwili wa binadamu? Katika kujibu maswali haya, mwandishi wako Dk. Fabian P. Mghanga anatuletea makala ifuatayo.
Dk. Robert Kisanga aliegesha gari yake katika eneo la kuegesha magari la kituo kinachojishughulisha na huduma kwa waathirika wa ugonjwa wa UKIMWI kilichopo wilaya moja ya jiji la Dar es Salaam. Kama ilivyo kawaida ya kazi zake za kila siku, ratiba ya shughuli zake za leo inaonesha ana jukumu la kutoa mada kwa baadhi ya wateja wapya walioandikishwa kwa ajili ya kuanza matibabu ya dawa za kurefusha maisha kwa waathirika kwa ugonjwa wa Ukimwi maarufu kama ARVs.
Katika umri wake wa miaka ya mwanzo ya thelathini, Dk. Kisanga amejipatia umaarufu sana miongoni mwa wateja wake kwa sababu ya upole, ucheshi, utu na uchapakazi wake. Ni aghalabu kumkuta akiwa amekunja uso au kutoa maneno yasiyofaa na yenye maudhi kwa wale wanaomzunguka. Sifa na tabia hizi zimemfanya awe kipenzi hata kwa wafanyakazi wenzake.
Baada ya kumaliza taratibu nyingine za kikazi asubuhi ile, alielekea chumba cha mkutano, eneo ambalo lilikuwa na wateja wapya takribani thelathini wakimsubiri kwa hamu. Somo la leo lilihusu dawa za ARVs, aina, namna zinavyofanya kazi, faida na athari zake.
Wagonjwa wa Ukimwi huathiriwa sana na ugonjwa wa figo. Ugonjwa wa figo unaohusiana na Ukimwi (HIV-Associated Nephropathy au kwa kifupi HIVAN) unaweza kusababishwa na mashambulizi ya moja kwa moja ya VVU kwenye figo au madhara yanayotokana na matumizi ya madawa ya kurefusha maisha (ARVs).
Aidha wagonjwa wengi wa Ukimwi wapo katika hatari ya kupata magonjwa ya figo kwa sababu ya kupungukiwa na maji mwilini kutokana na kichefuchefu na kutapika mara kwa mara, kupoteza chumvi mwilini, au lishe duni.
Ukubwa wa Tatizo
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa mwaka 2010 na Msango, Leonard(1) na wenzake katika hospitali ya Bugando, Mwanza ilionekana kuwa zaidi ya asilimia 60 ya wagonjwa walioandikishwa kuanza ARVs hospitalini hapo walikuwa na matatizo ya figo yaliyotokana na VVU. Ilionekana pia kuwa HIVAN iliwaathiri zaidi wanawake kuliko wanaume, wenye uzito mdogo, na wale waliokuwa na CD4 chini ya 200.
Huko nchini Marekani, HIVAN ni maarufu zaidi miongoni mwa wamarekani weusi wenye asili ya Afrika ikilinganishwa na wale wa asili nyingine; na hushika nafasi ya tatu kwa kusababisha magonjwa sugu ya figo (CRF) miongoni mwa watu wa jamii hiyo wenye umri wa kati ya miaka 20-64(2). Kwa ujumla HIVAN huchangia karibu asilimia 1 ya wenye ugonjwa sugu wa figo (CRF) nchini humo kila mwaka.
Kwa ujumla takwimu za dunia zinaonesha kuwa HIVAN huathiri zaidi vijana weusi, na takribani nusu ya wagonjwa wa HIVAN ni watumiaji wa madawa ya kulevya ya kujidunga(3).
Wanaume huathirika zaidi kuliko wanawake katika uwiano wa 10:1, wakati wastani wa umri wa watu wenye HIVAN ni miaka 33(4) ingawa HIVAN huwapata pia watoto(5).
Nini hutokea? (Pathofiziolojia ya ugonjwa)
Watafiti wameonesha uhusiano wa mashambulizi ya moja kwa moja ya VVU-1 kwenye figo. Pia kuna uhusiano mkubwa wa vinasaba na vyanzo vya kimazingira vinavyochochea kutokea kwa tatizo hili, hususani kwa watu weusi zaidi kuliko watu wa asili nyingine.
VVU-1 hushambulia zaidi chujio (glomeruli) pamoja na seli za kuta (epithelium) za mirija yake (renal tubules) kuliko sehemu nyingine yeyote ya figo. Hali hii husababisha kuharibika kwa chujio pamoja na mirija na kufanya kazi ya uchujaji uchafu pamoja na utengenezaji wa mkojo kuvurugika. Matokeo yake mkojo huwa na kiwango kingi cha protini kuliko kawaida (protenuria), chujio huwa na makovu (glomerulosclerosis) hali kadhalika nayo mirija (tubulointerstitial scarring).
Uhusiano wa Vinasaba
Mpaka sasa, haijulikani sababu hasa inayowafanya watu weusi kuathirika zaidi na HIVAN kuliko watu wa asili nyingine. Ifahamike kuwa, kwa ujumla watu weusi wanaongoza kwa kupata magonjwa mengine ya figo kama vile ugonjwa wa figo unaotokana na kisukari (diabetic nephropathy) au unaotokana na mcharuko mwili (systemic lupus erythematosus); hivyo basi kuna uwezekano mkubwa pia wa vinasaba kuchangia katika kufanya watu weusi kupata HIVAN.
Dalili na muonekano wa mgonjwa
Pamoja na kuwa na dalili zote za magonjwa ya figo (rejea makala zilizopita za ARF na CRF), wagonjwa wa HIVAN huwa pia na tabia/dalili zifuatazo
- Muonekano wa mgonjwa: Hupoteza kiwango kingi cha protein katika mkojo (zaidi ya gramu 3.5 kwa siku). Hupoteza pia kiwango kingi cha albumin (aina nyingine muhimu sana ya protini). Aidha huwa na kiwango kingi cha mafuta mwilini (hyperlipidemia). Pamoja na kupoteza sana proteini, wagonjwa wengi wa HIVAN hawana hali ya kuvimba miguu (edema). Huwa na shinikizo la damu la kawaida (tofauti na wagonjwa wa ARF au CRF ambao huwa na ongezeko la shinikizo la damu). Huwa na mrundikano usio wa kawaida wa urea au mazao mengine machafu yanayotokana na Nitrogen katika damu (azotemia).
- Muonekano wa figo katika Ultrasound au CT scan: Tofauti na wale wa CRF iliyosababishwa na vyanzo vingine ambao huwa na figo ndogo zilizosinyaa, wagonjwa wenye HIVAN huwa na figo zilizo na ukubwa wa kawaida au zilizovimba sana (kubwa kuliko kawaida).
- Muonekano wa figo katika biopsy: Figo huwa na makovu makovu katika chujio zake (Focal segmental glomerulosclerosis (FSGS) yanayoonekana katika darubini tu.
- Kiwango cha CD4+ T-cells cha mgonjwa: Kwa kawaida kiwango cha seli za CD4+ kwa wagonjwa wenye HIVAN huwa chini ya 200 cells/µL. Hata hivyo, HIVAN inaweza kutokea hata kwa mgonjwa mwenye kiwango cha juu cha CD4. Wagonjwa wenye CD4 chini ya 50 cells/µL wana hatari zaidi ya kufa mapema kutokana na HIVAN.
Wakati watafiti duniani wakiendelea kutafuta dawa itakayoweza kutibu tatizo la UKIMWI linalosababishwa na VVU, hivi karibuni imebainika kwamba kuna uwezekano mkubwa wa maambukizi ya VVU kupungua kwa mtoto mchanga anayenyonyeshwa zaidi ya miezi 6 kutoka kwa mama mwenye VVU anayetumia dawa. Hii ni kutokana na matokeo ya utafiti iliyofanywa na BAN (Breastfeeding, Antiretroviral and Nutrition) trial na kuchapwa katika mojawapo ya jarida kubwa la afya duniani la Lancet la mwezi Mei mwaka huu.
Hapo awali Shirika la Afya Duniani (WHO) na mashirika mengine ya afya yalipendekeza mama mwenye maambukizi ya VVU kunyonyesha mpaka mtoto atakapofika miezi 6 au chini ya hapo katika nchi maskini na familia zisizokuwa na kipato kikubwa ili kupunguza maambukizi ya VVU kutoka kwenye maziwa ya mama lakini vilevile kuepuka maambukizi ya magonjwa mengine ambayo yanaweza kumpata mtoto.
Faida mojawapo kubwa ya kunyonyesha mtoto ni kumpatia kinga imara kupitia katika maziwa ya mama ili kupambana na vimelea mbalimbali vya magonjwa. Ikumbukwe kwamba kinga ya mtoto mchanga dhidi ya vimelea vya magonjwa mbalimbali ni hafifu, na hii ndio inayosababisha kukawepo aina mbalimbali za chanjo kwa ajili ya watoto.
Hata hivyo, katika hii taarifa mpya ya BAN matokeo yanaonesha kwamba hatari ya maambukizi ya VVU huongezeka mara mtoto anapoacha kunyonya akiwa na miezi 6. Katika kukabiliana na hili, Shirika la Afya Duniani linapendekeza kwa mama mwenye maambukizi ya VVU kuendelea kumnyonyesha mtoto wake mpaka atakapofikisha mwaka 1.
Katika tafiti hii ambayo ilifanyika nchini Malawi katika kipindi cha miaka 7 toka mwaka 2004-2010, Dr. Denise J. Jamieson, kutoka kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa, (CDC) cha huko Atlanta, nchini Marekani na timu ya utafiti ya BAN walikuwa na makundi 3 ya akina mama pamoja na watoto wao wachanga [wajawazito ambao walikuwa kwenye dawa aina 3 za ARV, watoto wachanga waliokuwa kwenye dawa aina ya nevirapine na watoto wachanga ambao hawakuwa kwenye dawa ambao hawa waliitwa kundi thibiti au kwa lugha ya kitafiti control group].
Watoto wachanga walipimwa VVU wakati wa kuzaliwa, wakiwa na wiki 2, 12, 28, na wiki 48. Wale waliobainika kuwa na VVU katika wiki ya 2 walitibiwa na kuondolewa kwenye utafiti kwa vile hawa walishaonekana kuwa wameshapata maambukizi ya VVU kabla ya kuzaliwa na kunyonyeshwa. Akina mama waliambiwa kuanza kuwapatia watoto wao vyakula vya ziada kati ya wiki 24 na 28.
Katika wiki ya 32, wengi wa wanawake, karibu asilimia 96 kutoka katika kundi tafiti au kwa lugha ya kitafiti treatment group na karibu asilimia 88 ya kina mama kutoka kundi thibitiwa yaani control group waliripoti kuacha kunyonyesha.
Hatari ya kuongezeka kwa maambukizi ya VVU katika wiki ya 48 ilikuwa kubwa zaidi katika kundi thibitiwa [control group] kwa silimia 7 ukilinganisha na asilimia 4 katika kundi tafiti [treatment group]. Katika tathmini ya maambukizi ya VVU, asilimia 30 (%) ya maambukizi yalitokea baada ya wiki 28 mtoto alipoachishwa kunyonya maziwa ya mama, wakati asilimia tisa ya maambukizi ilitokea katika kundi la wakina mama wanaotumia ARV, asilimia 13 katika kundi la watoto wachanga wanatumia nevirapine, na asilimia 6 katika kundi thibitiwa [control group]. Aidha, matatizo mengine kama ya kuharisha, malaria, kifua kikuu, ukuaji mbaya na vifo yalijitokeza katika kipindi hiki.
Hitimisho katika tafiti hiyo ilikuwa kwamba kumuachisha mtoto kunyonya maziwa ya mama mapema siyo njia salama na sahihi katika mikakati ya kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa watoto wadogo.