Image

Jinsi ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU)

VVU/UKIMWI bado unaendelea kuwa janga katika jamii yote ya dunia ikiwa imeshasababisha vifo vya watu takribani millioni 33 mpaka sasa kulingana na taarifa ya WHO ya mwaka 2020.

Mpaka waka 2019 takribani ya watu million 38 walikuwa  wanaishi na maambukizi ya VVU, Tanzania pekee ni watu millioni 1.6 wanaoishi na maambukizi hayo kwa taarifa ya mwaka 2018 pekee.

Hivyo taaarifa hizi zinaonyesha umuhimu wa kujikinga na maambukizi ya VVU. 

Zifuatazo na njia mbali mbali za kujikinga na VVU/UKIMWI.

Ile kujikinga a ugonjwa wa VVU/UKIMWI ni muhimu kuondoa kabisa au kupunguza tabia harishi kwako.

Matumizi ya kondomu za kike na kiume

Ni vema kutumia kondomu pindi unapojamiana na mtu usiye jua hali yake au mwenye maambukizi ya VVU. Tafiti zinaonyesha kondomu huzuia maambukizi ya magonjwa ya zinaa ikiwemo ukimwi kwa Zaidi ya asilimia 85. Zingatia uvaaji sahihi wa kondomu.

Tohara kwa wanaume

Tohara imeonyesha kusaidia kupunguza maambukizi ya VVU kwa wanaume kwa asilimia 60 na sio kuzuia kama ilivyodhana potofu ya watu wengi. Hivyo hakikisha kwa hiari unafanyiwa tohara mapema ili kupumguza hatari ya kupata maambubikizi.

Kutokuchangia vitu vyenye uncha kali kama sindano, viwembe mikasi  n.k. Kundi maalum hapa ni waathirika wa madawa ya kulevya maana hujidunga madawa kwa kuchangia mabomba ya sindano. Pia kundi ni muhimu pia kupata matibabu  ili kuondoa ulevi wa madawa ili kuwalinda na maambukizi.

Uaminifu hii pia jia ya kujikinga na maambukizi kwa kuwa mwaminifu kwa mpenzi mmoja hasa kwa wanandoa

Matumizi ya madawa ya kufubaza virusi vya UKIMWI- tafiti zinaonyesha kuwa mtu anayetumia madawa haya anakuwa hana huwezo mkubwa wa kuambukiza ukilinganisha na ambae hatumii kabis au anayetumia kwa kusuasua.

Kinga baada ya kuwemo hatarini (post exposure prophylaxisis PEP)

Hizi na dawa za kufubaza kirusi vya ukimwi zinazotolea kama kinga ndani ya masaa 72 pind mtu anapokuwemo kwenye hatari ya maambukizi. Dawa hizi hutolewa kwa muda wa siku 28 pamoja na ushauri nasaa na vipimo.

Hakikisha pindi unapoongezewa dama kwasababu yoyote ile hiyo damu iwe imepimwa na haina virusi vya ukimwi.

kujiepusha na kutibiwa magonjwa ya zinaa. Tafati zinaoyoonyesha magaonjwa ya zinaa yanaongeza uwezekano mkubwa wa maambukizwa ugonjwa wa VVU/UKIMWI

Kuzuia maambukizi ya mama kwenda wa mtoto

Mtoto wa mama mwenye maambukizi huweza kupata maambukizi wakati wa ujauzito wakati wa kujifungua na kunyonyesha. Tafiti zinaonyesha kiwango cha maambukizi huanzia asilimia 15 hadi 45 bila kufanya harakati ya kuzuia maambukizi hayo.

Ili kuzua maambukizi mama mjamzito anapaswa kujua hali yake kabla na pindi unapokuwa mjamzito, na kama umeathirika anapaswa kuanza dawa za kufubaza vurusi vya VVU mara. Pindi unapojifungua mtoto huanzishiwa dawa maalum ya kumkinga na maambukizi kwa miezi sita huku akifanya vipimo kuthibitisha kama amepata maambukizi tiyari. Taarifa hizi na huduma za vipimo na madawa hutolea kliniki hivyo kuhudhuria kliniki ni muhimu sana.

USHAURI

Pamoja na kujua dalili na jinsi ya kujinga na VVU/UKIMWI ni muhimu sana kujenga tabia ya kupima na kujua afya yako mara kwa mara na kuepuka tabia hatarishi. Usiogope maana hata ukigundulika na ugonjwa huu huo sio mwisho wa maisha. Sasa waweza ishi na kuwa na furaha hata kama umeathirika.

 

 

 

 

Imesomwa mara 7741 Imehaririwa Jumapili, 08 Agosti 2021 22:21
TanzMED Admin

TanzMED ni mjumuiko wa wataalamu wa fani mbalimbali za Afya na IT wa kitanzania ambao wamejitoa katika kuhakikisha kuwa jamii ya kitanzania na Afrika kwa ujumla inafaidika kwa kupata habari na ushauri juu ya masuala ya afya yanayozunguka jamii hizo.

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.