Image

Tunashukuru kwa mtandao kwani habari zinasambaa haraka kama mwanga. Hata hivyo, uvumi, imani potofu vinasambaa kwa kasi ile ile pia. Hii inahusisha imani potofu kuhusu afya ya kinywa na meno. Kwa hiyo,

Nafikiri ni bora kuchukua muda kidogo kuweka baadhi mambo sawa kuhusu afya ya kinywa na meno.

Baadhi ya imani potofu ni kama ifuatavyo

POTOFU: Kupiga mswaki mara nyingi na kwa nguvu huzuia kuoza kwa meno

UKWELI: Si mara ngapi unapiga mswaki na nguvu gani inatumika, suala ni unapigaje mswaki. Kupiga mswaki mara nyingi na kwa maguvu kunaweza kupelekea kukwangua sehemu ngumu ya nje ya jino, kulifanya laini na hatimaye kuuma au hata kuvunjika. Kupiga mswaki mara mbili, taratibu na kwa njia sahihi ndicho kinachosaidia meno kuwa na afya

POTOFU: Huna haja ya kumuona tabibu wa meno kama hujaona au kuhisi una tatizo la meno.

UKWELI: Kila mtu anatakiwa kumuona tabibu wa meno angalau mara mbili kwa mwaka bila kujali meno yake yanaonekana vizuri au imara kiasi gani.Si meno yote yanayoonekana mazuri na imara ni mazima, mengine yanaweza kuwa yameoza katika maeneo usiyoweza ona kama chini ya fizi na kwenye mizizi, si hivyo tu hata uoto mpya (neoplasm) uweza kugundulika mapema kabla ya kufanya uaribifu mkubwa kama utachunguzwa na wataalamu. Kumbuka pia mangonjwa ya mifumo mingine kama ukimwi, kisukari na mengine mengi hujidhihirisha mapema kinywani kabla mgonjwa hajapata dalili zingine.

Neno syndrome humaanisha mkusanyiko wa dalili au magonjwa kadhaa ili kufanya ugonjwa mmoja.

Ugonjwa wa Nephrotic syndrome ni hali ya maradhi inayokumba figo na kusababisha kupoteza kiasi kingi cha protini kutoka kwenye damu kuingia kwenye mkojo. Kiasi cha protini kinachopotea ni wastani wa gram 3.5 kwa siku kwa kila mita za mraba 1.73 za mwili.

Chujio za figo (glomeruli) huwa na vitundu vidogo vidogo viitwavyo podocytes ambavyo hufanya kazi ya kuchuja uchafu na sumu nyingine kutoka mwilini na kuzitoa nje. Vitundu hivi vina uwezo wa kuzuia protini isichujwe kuingia kwenye mkojo. Hata hivyo, figo zenye Nephrotic syndrome huwa na podocytes kubwa kiasi cha kuweza kupitisha protini za ukubwa mbalimbali (zikiwepo albumin ambazo ni protini zenye kipenyo kikubwa zaidi). Pamoja na kuharibika huku kwa chujio, podocytes bado hazina ukubwa wa kuweza kupitisha seli nyekundu za damu ndiyo maana mkojo wa mgonjwa wa Nephrotic syndrome hauna damu ndani yake.

Ukubwa wa tatizo

Nephrotic syndrome huathiri karibu watu wa rika zote. Hata hivyo watoto walio katika umri wa miaka 2 mpaka sita ndiyo waathirika wakuu wa ugonjwa huu. Ugonjwa huu umeonekana kuwapata zaidi watoto wa kiume kuliko wa kike.

Visababishi vya Nephrotic syndrome

Visababishi vya Nephrotic syndrome vimegawanyika katika makundi mawili; yale yanayosababishwa na magonjwa yaliyo ndani ya figo zenyewe (primary nephrotic syndrome), au yale yanayosababishwa na magonjwa yaliyo nje ya figo (secondary nephotic syndrome).

Raia mmoja nchini Italia mwenye umri wa miaka 71 alipata mishtuko ya mioyo yake yote miwili na kupoteza fahamu kwa sekunde kadhaa lakini hatimaye aliweza kuokolewa maisha yake. Mtu huyo alikimbizwa katika hospitali ya Verona nchini Italia baada ya kupata maumivu ya kifua na mapigo ya mioyo yake kuwa si ya kawaida.

Taarifa kutoka jarida la American Emergency Medical Journal inaeleza kuwa mtu huyo aliwahi kufanyiwa upasuaji wa moyo na kupandikizwa moyo mwingine miaka kadhaa iliyopita katika upasuaji unaojulikana kama double heart transplant (heterotopic heart transplantation).

Hii ni aina ya upasuaji ambapo moyo hupandikizwa na kufanya kazi sambamba na moyo wa awali (wa mgonjwa mwenyewe) ambao huwa umeadhirika kutokana na maradhi. Chemba za damu za kwenye mioyo hiyo huunganishwa ili moyo uliopandikizwa uweze kusaidia moyo wa mgonjwa.

Ripoti zinasema kuwa moyo mmoja ulianza kuwa na nguvu zaidi kuliko mwingine na hivyo kusababisha mapigo yake kutofautiana na mwingine. Madaktari walijaribu kurekebisha mapigo ya mioyo hiyo ili yaendane sawa kwa kutumia dawa lakini mioyo hiyo iliacha kupiga kabisa na mtu huyo kuacha kupumua.

Hata hivyo, waliweza kumrejesha katika hali ya kupumua kwa kutumia kifaa maalum cha Defibrillator kabla ya kumfanyia upasuaji na kubadilisha kifaa kinachosaidia kuweka sawa mapigo ya moyo kinachojulikana kama pacemaker.

Huu ni ugonjwa unaoathiri zaidi ndege wa jamii mbalimbali. Hata hivyo virusi wanaosababisha ugonjwa huu, wana uwezo wa kujibadilisha umbo na tabia zake (mutation) na kisha kumuathiri mwanadamu. Mabadiliko haya ya kimaumbile na kitabia husababisha kutokea kwa milipuko (epidemic) ya mafua ya ndege sehemu mbalimbali duniani hali ambayo isipothibitiwa inaweza kusambaa na kuathiri sehemu kubwa ya dunia kwa wakati mmoja (pandemic).

Visababishi vya mafua ya ndege

Mafua ya ndege husababishwa na jamii ya virus wajulikanao kama Avian Influenza virus. Virusi vya kwanza kabisa kumuathiri binadamu na kumsababishia mafua ya ndege vilihusishwa na kuku na viligunduliwa mwaka 1997 huko nchini Hong Kong na kupewa jina la avian influenza A (H5N1). Huu ulikuwa ni mlipuko wa kwanza wa ugonjwa huu kuwahi kuripotiwa. Kuna matukio machache sana ya maambukizi kutoka kwa binadamu kwenda binadamu yaliyowahi kuripotiwa mpaka sasa.

Influenza virus ni nini?

Kuna aina kuu tatu za virusi wa influenza, A, B na C. Mafua ya ndege husababishwa na jamii ya influenza A ambao wana uwezo wa kuingia na kuishi katika seli za ndege. Umbo la kinasaba la virusi hawa wa influenza A limeundwa na kamba nane za protein aina ya RNA.

Aidha virus wa Influenza wanaweza pia kuainishwa kulingana na aina ya protein inayounda maumbo yao. Protini hizo zipo katika aina mbili nazo ni hemagglutinin (H) pamoja na neuraminidase (N). Protini hizi zina kazi mbalimbali katika umbo la virusi. Kadhalika protini hizi nao pia zimeganyika katika aina mbali, ambapo virusi hatari wa mafua ya ndege wanaundwa na aina ya 5 ya protin ya hemagglutinin na aina ya 1 ya protini ya neuraminidase na hivyo ndiyo maana hujulikana kama H5N1 influenza A virus.

Hii ni aina ya saratani inayokumba tezi ya thyroid. Ikumbukwe kuwa tezi ya thyroid ipo sehemu ya mbele ya shingo ya mwanadamu ikiwa na sehemu mbili (lobes) moja kila upande wa shingo.

Visababishi na ukubwa tatizo

Saratani ya thyroid huwapata watu wa umri mbalimbali, kuanzia watoto mpaka watu wazima. Watu waliowahi kupigwa mionzi sehemu ya mbele ya shingo wapo katika hatari kubwa ya kupata aina hii ya saratani. Kadhalika watu wazima ambao waliwahi kupigwa mionzi kipindi cha utotoni nao pia wana hatari kubwa zaidi ya kupata saratani ya thyroid hata kama hawakuwahi kupata tatizo hilo wakati wanakua.

Tiba ya mionzi maeneo ya shingoni ilikuwa ikitumika sana zamani kwenye miaka ya 50 mpaka 60 kwa ajili ya matibabu ya uvimbe wa tezi ya thymus, mafindofindo (tonsils), au baadhi ya magonjwa ya ngozi. Hata hivyo ni nadra sana kwa tiba hii kutumika katika zama hizi.

Vihatarishi vingine vya saratani ya tezi ya thyroid ni pamoja na kuwepo kwa historia ya tatizo hili miongoni mwa wanafamilia na kuwa na goita iliyodumu muda mrefu bila kutibiwa.

Aina za saratani ya tezi ya thyroid

Kulingana na aina ya seli zinazounda tezi ya thyroid zinazoshambuliwa, saratani ya thyroid inaweza kugawanywa katika aina zifuatazo

Gauti (Gout) ni aina ya ugonjwa unaoathiri viungo vya mwili unaosababishwa na kuwepo kwa kiasi kikubwa kuliko kawaida cha tindikali ya Urea (uric acid) katika damu.

Ongezeko la uric acid husababisha madhara katika jointi (joint) (joint ni sehemu ya mwili inapokutana/ inapoungana mifupa miwili). Gauti inaweza kutokea ghafla (acute gout) au ikawa sugu (chronic gout). Gauti inayotokea ghafla huwa na maumivu makali na mara nyingi huathiri jointi moja tu wakati gauti sugu inaweza kuathiri jointi zaidi ya moja na huambatana na hali ya kujirudia ya maumivu na uvimbe kwenye jointi.

Visababishi

Gauti husababishwa na kuwepo kwa kiwango kikubwa kuliko kawaida cha uric acid katika damu. Hali hutokea iwapo mwili  wa mgonjwa unatengeneza uric acid nyingi kuliko kawaida au unashindwa kutoa uric acid mwilini kama inavyotakiwa.

Ongezeko hili husababisha mrundikano wa uric acid katika maji maji yanayozunguka jointi yanayoitwa synovial fluid na hatimaye kutengeneza vijiwe vidogo vidogo vya tindikali ya urea yaani uric acid crystals ambavyo husababisha jointi kuvimba na hatimaye kuathirika.

Vihatarishi (risk factors)

Ingawa chanzo hakieleweki vema, ugonjwa wa gauti hutokea kuwapata baadhi ya watu walio katika familia moja. Wanaume huathiriwa zaidi kuliko wanawake ingawa wanawake waliokoma kupata hedhi huathiriwa zaidi kuliko wale wanaoendelea kupata hedhi.

Aidha unywaji pombe unachangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa ugonjwa huu pamoja na matumizi ya baadhi ya madawa kama vile dawa za kutoa maji mwilini ambazo kwa ujumla husababisha ongezeko la kiwango cha uric acid katika damu.

Vihatarishi vingine vya gauti ni pamoja na kuwa na ugonjwa wa kisukari, magonjwa ya figo, unene uliopitiliza, ugonjwa wa sickle cell anemia au aina nyingine za upungufu wa damu, pamoja na saratani ya damu (leukemia).

Hali kadhalika, gauti inaweza kusababishwa na matumizi ya dawa ambazo utendaji wake kazi huingiliana na utoaji wa uric acid mwilini.

Dalili

 • Dalili za gauti kwa kawaida uhusisha jointi moja au joint chache. Jointi zinazoathiriwa zaidi ni pamoja na kidole kikubwa ha mguuni, magoti, au kiwiko cha mguu.
 • Wagonjwa huwa na maumivu yanayoanza kwa ghafla hususani nyakati za usiku. Mara nyingi mgonjwa hudai anasikia maumivu makali kama kitu kinachokata, kupwita au mifupa inayosagana.
 • Jointi hubadilika na kuwa na joto, kuvimba na kuwa na nyekundu (hujionesha zaidi kwa watu wenye ngozi nyeupe). Kwa kawaida mgonjwa hulalamika maumivu makali ikiwa ataguswa kwenye jointi yenye matatizo.
 • Shambulio linaweza kudumu kwa siku kadhaa kabla mgonjwa hajapata nafuu, lakini pia laweza kujirudia mara kwa mara.
 • Pia mgonjwa anaweza kujihisi homa.

Baadhi ya wagonjwa hupata gauti sugu ambayo huwaletea madhara sugu katika jointi (chronic arthritis) hali ambayo husababisha mgonjwa kujihisi maumivu na muda mwingi kushindwa vizuri kutumia jointi zake. Wagonjwa wenye gauti kwa muda mrefu huwa pia na vinundu chini ya ngozi inayozunguka jointi zilizoathirika. Vinundu hivi kwa kitaalamu huitwa trophy na ni ishara ya muhimu kwa madaktari.

Vipimo

Vipimo vya gauti hujumuisha

 • Kiwango cha uric acid katika damu. Hata hivyo, si kila aliye na kiwango kikubwa cha uric acid katika damu huwa na gauti.
 • Kiwango cha uric acid katika mkojo
 • Uchunguzi wa maji maji yanayozunguka jointi (synovial fluid) kuchunguza vijiwe katika jointi
 • X ray ya jointi iliyoathirika
 • Uchunguzi wa utando unaozunguka jointi (synovial biopsy)

Matibabu

Matibabu ya gauti hujumuisha matumizi ya dawa, lishe pamoja na mabadiliko katika mfumowa maisha wa mgonjwa.
Dawa hutumika mara tu mgonjwa anapopata shambulio la ghafla. Dawa hizo ni pamoja na

 • Dawa za kutuliza maumivu kama vile codeine, paracetamol
 • Dawa za kutuliza mcharuko mwili (nonsteroidal anti-inflammatory drugs (NSAIDs) kama vile ibuprofen (brufen), indomethacin (indocid), diclofenac n.k. Pia ni muhimu mgonjwa kumfahamisha daktari wake iwapo ana matatizo yasiyoendana na matumizi ya dawa hizi kama vile vidonda  vya tumbo au mzio.

Dawa hizo husaidia kupunguza maumivu, uvimbe, na mcharuko mwili (inflammation). Baadhi ya madaktari huchoma sindano dawa ya corticosteroids kwenye jointi iliyoathirika kwa ajili ya kupunguza maumivu na uvimbe. Kwa kawaida maumivu huondoka saa 12 baada ya kuanza matibabu, na mgonjwa hupata nafuu kamili baada ya saa angalau 48.

Ili kupunguza kiwango cha uric acid katika damu, mgonjwa hupewa dawa za allopurinol au probenecid kila siku. Wagonjwa wanaotumia dawa hizi ni wale ambao hupata mashambulizi ya mara kwa mara ndani ya mwaka au wale ambao hupata mashambulia makali, wagonjwa waliopata madhara mkubwa kwenye jointi, wagonjwa walio na vinundu (trophy) au wagonjwa wenye vijiwe vya uric katika figo.

Lishe na mabadiliko katika mfumo wa maisha husaidia pia kuthibiti na kumuepusha mgonjwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya gauti. Njia hizi ni pamoja na:

 • Kuacha kunywa pombe
 • Kupunguza ulaji wa vyakula vyenye viasili vya purine (aina ya protini) kama vile nyama ya mbuzi, samaki jamii ya sardines na herring, nyama ya maini au figo, mkate mtamu, maharage yaliyokaushwa, njegere, baadhi ya aina za uyoga, spinachi, n.k.
 • Thibiti pia ulaji wa nyama kwa kila mlo unaokula
 • Jiepushe na matumizi ya vyakula vya mafuta kama vile ice creams, mayonise au vyakula vya kuokwa
 • Kula kiasi kikubwa cha wanga
 • Iwapo utaamua kupunguza uzito, hakikisha unapunguza kidogo kidogo kwa sababu upunguzaji wa kasi unaweza kusababisha vijiwe vya uric kujitengeneza katika figo

Matarajio

Wagonjwa wanaofuata masharti na ushauri wa daktari huweza kuishi maisha ya kawaida. Hata hivyo, ni vema kufahamu kuwa mara nyingi gauti ya ghafla hatimaye huwa gauti sugu.

Madhara ya gauti

 • Gauti inaweza kusababisha matatizo sugu kwenye jointi (chronic gouty arthritis)
 • Vijiwe katika figo
 • Mrundikano wa uric acid unaoweza kusababisha ugonjwa sugu wa figo

Kinga

Kwa kawaida gauti haizuiliki, hata hivyo mgonjwa anashauriwa sana kujiepusha na vitu vinavyoweza kuchochea shambulizi na dalili za ugonjwa huu (rejea lishe na mabadiliko katika mfumo wa maisha hapo juu).

Leukemia ni saratani inayoshambulia tishu za mwili zinazohusika na utengenezaji wa damu zikiwemo supu ya mifupa (bone marrow) na mfumo wa lymph (lyphatic system). Kwa maneno rahisi, leukemia humaanisha saratani ya damu. Kuna aina mbalimbali za leukemia, nyingine zikiathiri watoto na nyingine zikiathiri zaidi watu wazima.

Kwa kawaida leukemia huanzia kwenye chembe nyeupe za damu yaani white blood cells, ambapo mwili huzalisha kiwango kikubwa cha seli zenye maumbo mabaya ambazo hazina uwezo wa kufanya kazi zake sawasawa. Kazi ya chembe nyeupe za damu ni kulinda mwili dhidi ya vimelea waletao maradhi mbalimbali.

Leukemia husababishwa na nini?

Kama zilizo kwa aina nyingi za saratani, mpaka sasa chanzo halisi cha leukemia hakijulikani. Hata hivyo, wanasayansi wanadai kuwa leukemia hutokea kutokana na mkusanyiko wa vyanzo mbalimbali vikiwemo vinavyohusu sababu za kinasaba (genetic factors) na kimazingira.

Kwa ujumla, leukemia hutokea pindi chembe nyeupe za damu zinapobadilika muundo wake wa kinasaba yaani viasili vyake vya DNA, ambavyo kwa kawaida hubeba maelekezo yanayoifanya seli yeyote ya kiumbe hai iweze kuishi, kutenda kazi zake, kujizaa na hata kufa, vinapobadilika maumbile na muundo wake kutokana na sababu mbalimbali. Kitendo cha kubadilika kwa maumbile na muundo wa DNA hujulikana kama mutation. Ndiyo kusema basi, seli yeyote iliyopatwa na tatizo hili huwa na tabia ya kukua kwa haraka na kujizaa (kujigawa) kwa kasi zaidi kuliko kawaida, na pindi inapofikia muda wake wa kufa seli hiyo hugoma kufa badala yake huendelea kujizaa zaidi hatimaye kusambaa kwa wingi katika mfumo mzima wa damu, hali inayosababisha saratani ya damu.

Je, kuna vihatarishi vya leukemia?

Malaria is known to be the largest single  component of the burden of diseases in Tanzania for both morbidity and mortality especially for under fives and pregnant women. In Dodoma region, the prevalence of malaria among underfives is 12.5% while, in Bahi District Council, about 60,000 people of all ages suffer from malaria every year.

Malaria diagnosis is first suspected on defined features and then confirmed by laboratory tests mainly through microscope; however in the year 2010, the cheapest and easiest laboratory test was introduced in Bahi District Council namely Malaria Rapid Diagnostic Test (m-RDTs).

Malaria Rapid Diagnostic Test (m-RDT) is a test that assists in the diagnosis of malaria by providing evidence of presence of malaria parasites in the human blood within a very short period of time and it’s considered to be user friendly as it doesn’t need one to have advanced lab training.

The prevalence of malaria in our district council was reported to be higher prior to introduction of m-RDTs, and malaria was always ranked number one in the district’s top ten diseases. However, after the introduction of  m-RDTs in the year 2010 there has been changes on the trend of the top ten diseases as the number of malaria cases is  currently on the decline compared to the same period of time before the use  this rapid test. The aim of this study was to determine the success obtained after introduction of m-RDT as a tool for diagnosis of malaria in Bahi District Council.

The study design was descriptive comparative study, in which District Health Information System data base gathered from Health facility reports were used. The information obtained was organized and computerized in a soft ware. Analyses were based on descriptive and comparisons between two periods of January – June 2011 and the same time period of the year 2010. All tests were done using relevant statistical tests.

The findings reported a high number of malaria cases between January and June 2010 when both microscope and clinical diagnosis for malaria were still used in the diagnosis of malaria, compared to the same six months-period of January to June, 2011 when we started using malaria rapid diagnostic tests (m-RDTs) as an adjuvant doagnostic modality for malaria. In overall malaria case diagnosis was reduced by 65% for under fives, 58% for above five years and 63% for patients of all ages. This difference was found to be statistically significant. In the year 2010 malaria was leading among the district’s top ten diseases reporting 39,295 cases followed by Acute Respiratory Tract Infection (ARI) which had 17,126 cases. On the contrary, until June 2011, ARI was reportedly leading with 21,244 cases followed by malaria with 17,126 cases.

Microscope remains the gold standard for malaria diagnosis, however due to reasons such as lack of skilled laboratory personnel and unavailability of microscopes and reagents, the best diagnostic modality at the moment would be malaria rapid diagnostic tests which can help in the over- and/or mis-diagnosis of malaria and patients’ mismanagement who actually have other diseases than malaria.

From our findings we recommend that, it is time now we review our malaria treatment guidelines including its testing algorithms  in order to improve the quality of health care delivery through proper management of malaria cases by use of m-RDT especially for the developing countries.

The author declares no conflicts of interest.


The author is Public Health Specialist, and a District Medical Officer (DMO) for Bahi District Council in Dodoma, Tanzania.


 

Photo Credit: NMCP

Ugonjwa sugu wa figo hutokea pale figo zinazopoteza uwezo wa kutenda kazi unaotokea taratibu na kudumu baada ya kitambo fulani. Hali hii hutokea taratibu, na huchukua muda wa takribani miezi kadhaa hata miaka. Ugonjwa sugu wa figo umegawanywa katika hatua kuu tano, kulingana na ukubwa wa tatizo.

Figo linapopoteza uwezo wake wa kutenda kazi, kusanyiko na limbikizo la maji, uchafu na sumu hutokea mwilini mwa mgonjwa. Aidha kushindwa kufanya kazi kwa figo husababisha pia kutokea kwa maradhi mengine kama vile upungufu wa damu mwilini (anemia), shinikizo la damu (hypertension), ongezeko la tindikali kwenye damu (acidosis), ongezeko la lehemu na mafuta kwenye damu, na magonjwa ya mifupa.

Hatua ya tano ya ugonjwa sugu wa figo hujulikana pia kama kushindwa kufanya kazi sugu kwa figo (chronic kidney disease au end-stage-renal disease).

Tofauti ya Ugonjwa sugu wa figo na kushindwa kufanya kazi kwa figo kwa ghafla (AKI) ni kwamba AKI hutokea ghafla, huchukua muda mfupi kati ya siku hadi wiki kadhaa kuwa tatizo kubwa zaidi. Tofauti nyingine ni kuwa AKI hutokana na tatizo linaloathiri figo moja kwa moja, mishipa yake ya damu au mtiririko wa mkojo unaotoka kwenye figo. Aidha ARF mara nyingi huweza kurekebishwa na mgonjwa akapona kabisa, ingawa kwa baadhi ya wagonjwa sehemu fulani ya figo inaweza isipate nafuu na ikaendelea kudorora kiutendaji kazi.

Hatua za Ugonjwa Sugu wa Figo

Hatua hizi zimegawanywa kulingana na kiwango cha GFR kilichofikiwa na figo husika. GFR kwa kirefu Glomerular Filtration Rate ni kiwango kinachoonesha uwezo wa utendaji kazi wa figo. GFR hupima uwezo wa glomeruli (chujio) la figo katika kuchuja uchafu, maji pamoja na sumu nyingine kwa kila dakika moja kwa mtu mwenye wastani wa urefu wa mita za mraba 1.73. Kadiri jinsi GFR inavyopungua, ndivyo inavyoashiria ukubwa wa tatizo katika figo.

Katika muendelezo wa magonjwa ya moyo ya kuzaliwa nayo, leo nitagusia kuhusu Tundu katika kuta za juu za moyo (atrial walls) au kwa kitaalamu Atrial septal defect (ASD).

Wakati kijusi (fetus) kinapo endelea kukua, kuta kati ya atria mbili za moyo nayo hukua (kitaalamu interatrial septum) ili kutenganisha chemba ya kulia na kushoto. Lakini katika kipindi hiki huwa kuna tundu kati ya kuta hizi kitaalamu huitwa foramen ovale.

Tundu hili ni la kawaida kwa kipindi hiki cha kijusi, tundu hili husababisha damu yenye oksijeni  kutoka kwenye kondo la mama (placenta) kutokwenda kwenye mapafu amabayo hayaja komaa na kuelekea sehemu nyingine za mwili hasa kichwani. Kipande cha tishu kinachoitwa kitaalamu septum primum hufanya kazi kama valvu katika tundu hili. Mara tu mtoto anapozaliwa, shinikizo katika mishipa ya damu ya mapafu (pulmonary circulatory system) hushuka na kusababisha tundu hili (foramen ovale) kufunga kabisa.

Tundu hili huwa halifungi kabisa kwenye karibu asilimia ishirini na tano ya watu wazima, hivyo pindi shinikizo likiongezeka katika mishipa ya damu ya mapafu (hali inayoweza kutokea kwa sababu ya kuwepo kwa shinikizo la damu kwenye mapafu (pulmonary hypertension) kutokana na sababu mbalimbali, au kuwa na matatizo ya kikohozi cha muda mrefu), husababisha tundu la foramen ovale kutofunga na kubaki wazi. Hali hii kitaalamu huitwa patent foramen ovale (PFO).

Aina za tundu katika kuta za juu za moyo

Mpaka sasa, zipo aina kuu sita za tundu katika kuta za juu za moyo, ambazo ni