Ugonjwa wa kaswende ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na bakteria aina ya Treponema pallidum. Ugonjwa wa huu ni kati ya magonjwa ya zinaa yanayoongoza kwa kusababisha madhara mengi.
Maambukizi ya kaswende wakati wa ujauzito huleta madhara mengi sana kama kujifungua kiumbe ambacho kimeshakufa, mtoto kuathirika na ugonjwa huu wakati wa kuzaliwa, mtoto kupata matatizo wakati wa ukuaji wake, degedege na kuongezeka kwa vifo vya watoto wachanga nchini.
Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa kaswende
- Kufanya ngono salama kwa kutumia kondomu, njia sahihi ni kuepuka kabisa ngono
- Wale walioathirika kuacha kufanya ngono na wenza wao hata kama wameanza tiba mpaka vidonda vipone
- Kwa wajawazito, kuhudhuria kliniki mapema ili kama ukigundulika kuwa na kaswende hivyo kupata tiba haraka.
- Epuka kugusana na majimaji yoyote yanayotoka kwa mtu aliyeathirika kwa ugonjwa huu.
Unaweza pia kusoma makala nzima ya kaswende Ugonjwa wa Kaswende (Syphilis) na Madhara yake