Saratani ya shingo ya kizazi ndio saratani ya kwanza kwa wanawake nchini Tanzania, na Saratani namba moja kwa wanawake walio kati ya umri wa miaka 15 hadi 44. Tanzania ina wanawake milioni 10.97 walio na umri wa miaka 15 na kuendelea, ambao wako kwenye hatari kubwa ya kupata saratani hii. Kwa afrika mashariki, asilimia 33.6 ya wanawake wote, wanasadikiwa kuwa na virusi aina ya human papilloma virus ambavyo ndio visababishi vya ugonjwa huu.
Je nini kinasababisha saratani ya shingo ya kizazi?
Maambukizi ya human papilloma virus ndio yanayosababisha saratani ya shingo ya kizazi.Virusi hivi huambukizwa kwa njia ya kujamiana au kugusana kwa ngozi ya mtu mmoja na mwengine, na huambukiza wanaume na wanawake.
Vihatarishi vya saratani ya shingo ya kizazi
- Kuanza kufanya ngono mapema – Wanawake wanaoanza kujamiana wakiwa na umri wa miaka 16 wako kwenye hatari baadae kupata saratani ya shingo ya kizazi.
- Kuwa na wapenzi wengi – Mwanamke mwenye wapenzi wengi au mwenye mwanamume mwenye wapenzi wengi yupo kwenye hatari ya kupata ugonjwa huu. Utumiaji wa kondomu hupunguza hatari ya kupata saratani hii, lakini ikumbukwe ya kwamba kondomu sio kinga ya ugonjwa huu.
- Maambukizi ya human papilloma virus
- Uvutaji sigara – Kemikali zilizopo kwenye sigara huchanganyikana na seli au chembechembe za shingo ya kizazi hivyo kuleta mabadiliko katika shingo ya kizazi hatimaye kusababisha saratani.
- Utumiaji wa vidonge vya kupanga uzazi kwa muda mrefu hasa wale wanaotumia kwa zaidi ya miaka mitano (miaka 5)
- Ugonjwa wa genital warts ( dalili ni matezi na muda mwingine vidonda katika sehemu ya siri ya mwanamke). Hii husababishwa na virusi vya human papilloma virus.
- Kuzaa watoto wengi – Wanawake ambao wamepata watoto zaidi ya watano wako kwenye hatari kubwa sana ya kupata saratani ya shingo ya kizazi. Ndio maana mama akishafikisha watoto watano anashauriwa kufunga kizazi.
Fuatilia hapa makala nzima Saratani ya Shingo ya Kizazi (Cervical Cancer)