Image

Njia thabiti ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU)

VVU/Ukimwi umeenelea kuwa ni moja kati ya changamoto kubwa katika sekta ya Afya duniani haswa kwa nchi zinazoendelea. Kutokana na Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), inakadiriwa kuwa, kuna watu milioni 36.9 wanaishi na virusi vya ukimwi duniani kote.

Kwa siku za karibuni, kumekuwa na matokeo chanya kwenye mapambano na ugonjwa wa ukimwi, sasa hivi watu wenye virusi vya ukimwi (VVU) wanaishi maisha yenye afya njema na kwa muda mrefu kwa msaada wa dawa za kufubaza makali ya virusi vya ukimwi (antiretroviral therapy (ART)), pia matumizi sahihi ya dawa hizi husaidia kupunguza muendeleo wa uabukizaji kwa wengine.

Kazi kubwa pia imefanyika ili kuzuia na hata kumaliza kabisa maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kujifungua.

Ingawa kuna matokeo yote hayo chanya, lakini bado kuna sehemu kubwa ya jamii bao haina uelewa juu ya ugonjwa huu, hivyo TanzMED itakuwa inakuletea dondoo chache juu ya ugonjwa huu;

1. VVU vinaweza kuambukizwa kwa njia mbalimbali kama;

  • Kuambukizwa kwa mtoto mchanga wakati akiwa tumboni, wakati wa kuzaliwa au kwa kunyonyeshwa na mama anayeishi na virusi vya ukimwi. Hivyo, kabla na baada ya kuanza kubeba ujauzito, inashauriwa kupima Afya na kuhudhuria vyema kliniki kwa ajili ya vipimo na ushauri juu na njia za kuondoa maambukizi haya.
  • Kujamiiana bila ya kinga na mtu mwenye virusi vya ukimwi
  • Kuwekewa damu yenye virusi vya ukimwi
  • Kushare vitu vyenye incha kali (sindano, viwembe, masjine za kuchorea tattoo, mikasi nk) vilivyo na virusi vya ukimwi. Watumiaji wa madawa ya kulevya wapo kwenye hatari ya kuambukizana kwakuwa wengi hutumia sindano kwa pamoja
  • Matumizi ya vifaa vya upasuaji ambavyo havijafanyiwa usafi wa kuua virusi

2. Jinsi ya kujikinga au kuzuia maambukizi ya virusi vya ukiwmi (VVU) kwa wengine

  • Hakikisha unatumia zana pindi unapofanya ngono
  • Nenda kapime na upate tiba ya magonjwa mengine ya zinaa kwani kuwa na magonjwa ya zinaa kuna uwezekano mkubwa wa kuambukizwa virusi vya ukimwi, pia kupima na kujijua mapema, kunasaiia kulinda afya yako na kuzuia kuwaambukiza wengine
  • Hakikisha damuunayowekewa imepimwa na haina virusi vya ukimwi
  • Kutahiriwa kwa wanamume kunasaidia kupunguza maambukizi (soma makala juu ya faida za tohara hapa)
  • Matumizi ya mapema na yaliyobora ya dawa za kufubama makali ya virusi vya ukimwi (ARV) husaidia kukufanya uishi na afya bora pia kupunguza maambukizi kwa wengine
  • Kuishi maisha yanayompendeza mungu kwa kuacha kuzini kabla na nje ya ndoa
Imesomwa mara 13701 Imehaririwa Jumapili, 06 Septemba 2020 00:00
TanzMED Admin

TanzMED ni mjumuiko wa wataalamu wa fani mbalimbali za Afya na IT wa kitanzania ambao wamejitoa katika kuhakikisha kuwa jamii ya kitanzania na Afrika kwa ujumla inafaidika kwa kupata habari na ushauri juu ya masuala ya afya yanayozunguka jamii hizo.

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.