Image

Mambo ya kuyaepuka kwa mtu mwenye kisukari

Habari! Karibuni tena katika muendelezo wa makala zetu kuhusu Kisukari ambazo zinapatika katika tovuti pendwa ya TANZMED, Mara ya mwisho tulikumbushana kuwa wewe ndio tabibu ama daktari wa tatizo lako, wewe sio mgonjwa wewe ni mtu wenye kisukari, ama una ishi na kisukari, ni kitu cha kawaida sana kwa dunia ya sasa.

Sasa leo napenda kuwakumbusha ni vitu gani au ni mambo gani mtu wenye kisukari anatakiwa kuviepuka. Kama tujuavyo kuwa endapo Kisukari haitadhibitiwa ipasavyo basi inaweza kuleta madhara mengi kama kupata kiarusi,upofu, matatizo ya moyo, vidonda ndugu,matatizo ya figo na ini,kwa wanaume kukosa nguvu vya kiume, matatizo ya misuli na kadhalika. Sasa kwa sisi wenye kisukari tuishi vipi ama tufanye nini ili kuepuka haya yote?

  1. Jambo la kwanza ambalo mara nyingi napenda kuwakumbusha watu watu wenye kisukari kuwa ni muhimu sana kujikubali, hili ni jambo ya kwanza kwakuwa ukijikubali kuwa una tatizo la kisukari inakuwa rahisi sana kubadili mfumo wa maisha uliyokuwa unaishi kabla ya kupata tatizo  na mara nyingi nasisitiza umuhimu wa kumpatia ushauri nasaha kwa watu wenye kisukari.
  2. Jambo la pili ni kuepuka kabisa na kupunguza kutumia vitu ama vyakula vinavyoweza kupandisha sukari yako kwa haraka,vitu kama soda,juisi,keki,sukari,asali, Chokoleti na vitu vya kupunguza hasa hasa ni vyakula vya wanga na matunda,hapa nikisema matunda simaanishi kuwa matunda walisiwe hapana,ninachomaanisha hapa ni liliwe tunda na sio matunda na kwa muda, ima masaa mawili au lisaa limoja baada ya chakula.
  3. Jambo la tatu ni kuepuka kupata vidonda kwa kuwa kama hujaweza kudhibiti kisukari ni rahisi sana kidonda kuchelewa kupona kwa hiyo basi yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu ya kuizngatia;
  • Epuka kutembea bila viatu,yaani kutembea peku, kwa maana unaweza kujikata na kitu chenye ncha kali kama sindano, chumba, miiba nk
  • Epuka kutumia vitu vyenye ncha kali kutaka kucha kwa mfano usitumia wembe au mkasi kukata kucha ili kuepuka kupataka na kupata kidonda,pendelea sana kutumia nail taker.
  • Epuka kuvaa viatu na soksi za kubana, na pia hakikisha miguu yako ni mikavu kila muda, kwa hiyo basi utokapo kuoga ama kunawa miguu, hakikisha unaikausha vizuri hasa katikati ya vidole, kwa sababu kama ukiacha unyevunyevu ni rahisi kutengeneza lengelenge na pia endapo utapata lengelenge usitumbue, acha na likaule lenyewe
  • Kwa wanawake, epuka kuvaa viatu virefu kwa sababu vinazuia damu kufanya mvunguko wake wa kawaida (blood circulation)

Kwa kumalizia napenda kusisitiza tu kuwa kisukari sio mwisho wa maisha,na pia kumbuka kuwa watu wenye kisukari ni watu wanaoishi katika mfumo sahihi wa maisha.

Imesomwa mara 7554 Imehaririwa Jumanne, 29 Agosti 2017 10:22
Lucy Johnbosco

Diabetes Consciousness for Community is focusing on raising Diabetes awareness and healthy lifestyle

https://dicoco.or.tz | Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

Makala shabihana