Image

Jinsi ya kula kwa watu wenye Kisukari

Ugonjwa wa kisukari ni tatizo ambalo siku hizi husababishwa na mfumo wa maisha tunayoishi hasa vijana, tafiti zilizowahi kufanywa zinaonesha kuwa vijana wapo kwenye hatari kubwa ya kupata kisukari kwa sababu ya mfumo usio sahihi wa maisha wanayoishi vijana.

Kutokufanya mazoezi, kukosa muda wa kupumzika na kutokula mlo sahihi,unywaji wa pombe na uvutaji sigara wa kupitiliza, hizi ni sababu chache zinazochangia vijana kuishi katika mfumo wa maisha hatarishi wa kupata maradhi ya kisukari.

Leo tunaangalia suala zima la chakula kwa watu mwenye maradhi ya kisukari,madaktari wapo wengi sana kwenye hospitali zetu pamoja na majumbani mwetu lakini wewe mwenye ugonjwa wa  kisukari ndiyo daktari namba moja katika kutibu afya yako.

Kitu muhimu kwa mgonjwa wa kisukari ni  kufahamu ya kwamba  ana uwanja mpana  sana wa vyakula anavyoruhusiwa kula tofauti na  na mazoea yaliyojengeka miongoni mwetu kuwa mtu anayeuugua maradhi haya basi ana  vyakula vyake vya kipekee kabisa. Maisha ya mtu mwenye kisukari yanatakiwa kuendelea kama kawaida, na unaruhusiwa kula aina zote za vyakula isipokuwa tu vile venye sukari.

Unakula kile kilichopo na kinachokuwepo  na usijiulize ule nini ila jiulize  ule vipi hicho chakula kilichopo,kwa mfano, nyumbani kuna pilau, usipoteze muda na kusema mimi nina  kisukari kwa hiyo siwezi kula pilau,la hasha. Kitu unachotakiwa kujua ni ule vipi hiyo pilau. Pilau ni chakula chenye wanga,na kwa kuwa vyakula vya wanga kazi yake ni kutengeneza nishati mwilini kwa maana hiyo wanga utengeneza sukari, na tayari wewe una kisukari, basi hautakiwi ule wanga mwingi, sasa hapa cha kufanya ni kula kiasi kidogo cha pilau ili kuepuka utengenezwaji mwingi wa sukari mwilini.

Upawa mmoja tu wa pilau,nyama kidogo  na mboga za majani au kachumbari kwa wingi na hivyo ndiyo unavyotakiwa kula kila mlo wako, hakikisha unakula kiasi kidogo cha wanga, na kiasi kikubwa au kingi cha mboga za majani.

Mpangilio wa vyakula anaotakiwa kufuata mtu mwenye kisukari

Mfano wa ulaji unaofaa kwa mgonjwa wa kisukari. Kiasi cha ugali ni kidogo na mboga za majani ni nyingi

Imesomwa mara 25151 Imehaririwa Jumatatu, 28 Januari 2019 08:25
Lucy Johnbosco

Diabetes Consciousness for Community is focusing on raising Diabetes awareness and healthy lifestyle

https://dicoco.or.tz | Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

Makala shabihana