Image

Nafasi ya Tendo la ndoa katika kudhibiti kisukari

Karibuni tena katika kijiwe chetu,leo kwenye muendelezo wa makala zetu kuhusu udhibiti wa kisukari  tunaangalia umuhimu wa tendo la ndoa katika kusaidia kupunguza kiwango cha juu ya sukari.

Kwa upande moja ama mwingine tendo la ndoa ni moja ya zoezi la mwili kama mazoezi mengine kama kukimbia na mazoezi mengine ya viungo na pia tendo hili linasaidia sana kushuka kiwango cha sukari, Moja ya tafiti iliyowahi kufanya na  American Journal of Medicine inasema kuwa mtu akifanya tendo la ndoa mara tatu au nne kwa wiki anajiweka kwenye nafasi ya kutopata matatizo ya msongo wa mawazo ambayo unaweza kuleta matatizo kama ya Kisukari na Presha.

 Moja ya tafiti iliyofanywa na Taasisi ya Kisukari Marekani (ADA) zinaonesha kuwa kufanya tendo la ndoa husaidia kuyeyusha mafuta na sukari mwilini kwakuwa ni moja ya mazoezi ya viungo.Tafiti zingine zinaonesha kuwa endapo mtu ukifanya tendo la ndoa mara tatu au nne kwa siku husaidia kupunguza kiasi cha mafuta mwilini.

Tendo la ndoa husaidia kupunguza ama kutoa msongo wa mawazo, na kama tunavyojua kuwa msongo wa mawazo huchangia kupandisha sukari kwa mtu mwenye Kisukari na pia hutoa au hupunguza hatari ya kupata shinikizo la damu,kasi ya mapigo ya  moyo wakati wa tendo la inaweza kupunguza hatari ya kupata shinikizo la dawa na kupanda kwa sukari,wataalamu wanasema sio tu kwa mtu mwenye tatizo la kisukari ila hii ni kwa kila mtu,kufanya tendo la ndoa.

Majibu ya tafiti iliyofanya na chuo kikuu cha Yale huku nchini Marekani, ulionesha kuwa watu wenye tatizo la Kisukari hupata shida kupata usingizi,uchovu wa akili, na pia husahau mara kwa mara, Tendo la ndoa hasa kwa wenye Kisukari linasaidia kumpatia mtu amani, utulivu wa mwili na akili na pia huboresha afya ya akili.

Kwa kumalizia basi, kwa yeyote kwenye tatizo ya Sukari, asiogope kufanya tendo la ndoa kwa kuhofia labda unaweza kupata tatizo, kama nilivyosema mwanzoni kuwa tendo la ndoa  hupunguza presha kwenye damu, husaidia kuchoma mafua au kuyeyusha mafuta mwilini,husaidia kuboresha afya ya mwili na akili, huondoa msongo wa mawazo na  uchovu,huongeza furaha katika maisha na vyote hivyo zinasaidia kudhibiti kiwango cha sukari.

 

 

 

 

Imesomwa mara 8871 Imehaririwa Ijumaa, 04 Mai 2018 20:48
Lucy Johnbosco

Diabetes Consciousness for Community is focusing on raising Diabetes awareness and healthy lifestyle

https://dicoco.or.tz | Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.