Image

Unyongovu Waweza Kusababisha Magonjwa ya Moyo kwa Vijana

Katika tafiti mpya zilizofanywa hivi karibuni zinaonyesha kuwa unyongovu na jaribio la kujiua ni viashiria hatari ambavyo huleteleza vijana kufa kwa magonjwa ya moyo.

Katika utafiti mkubwa uliohusisha washiriki zaidi ya 7000 walio chini ya miaka 40 ulionyesha kuwa kwa wale waliokuwa na historia ya unyongovu au jaribio la kujiua walikuwa na hatari kubwa zaidi ya kufa kutokana na magonjwa ya moyo hasa yale ambayo moyo hukosa oksijeni ya kutosha (ischemic heart disease) ukilinganisha na wale ambao hawakuwa na historia hiyo.

Ingawa jinsia zote zilikuwa kwenye hatari zaidi ya kufa kutokana na magonjwa ya moyo, lakini wanawake wenye unyongovu au waliofanya jaribio la kujiua walikuwa na hatari mara 14 zaidi ya kufa kwa magonjwa ya moyo yatokanayo na kukosa oksijeni ya kutosha (ischemic heart disease) kulinganisha na wale ambao hawakuwa na unyongovu au jaribio la kujiua.

Katika utafiti huu uliofanywa na Profesa Viola Vaccarino kutoka chuo kikuu cha Emory, Atlanta, Georgia aligundua jinsi matatizo ya kisaikolojia yanavyopelekea kuongeza hatari ya kufa mapema na magonjwa ya moyo katika idadi ya vijana.

Taarifa nyingi zilizopo za magonjwa ya moyo ambazo zilizokwisha tolewa huwa za umri wa kati na wazee, maana imekuwa ikizoeleka magonjwa haya huathiri zaidi rika hiyo, ambayo ni kweli kabisa hasa katika magonjwa yanao athiri zaidi mishipa ya damu ya moyo (CHD).

Kutokana na watatifi mkazo humewekwa zaidi kwa wazee ingawa magonjwa mengi ya moyo huanza katika kipindi cha ujanani.

Katika utafiti huu taarifa zilichukuliwa kutoka kwa washiriki 7641, wenye umri kati ya 17 hadi 34, kutoka mwaka 1988 hadi 1994.

Katika ratiba ya uchunguzi, tathmini ilikuwa kuhusu unyongovu na jaribio la kujiua , na matokeo baada ya ufuatiliaji yalikuwa kama ifuatavyo:  washiriki 51 walikufa kutokana na magonjwa ya moyo, na kati ya hao 28 walikufa kutokana na moyo hukosa oksijeni ya kutosha (ischemic heart disease).

Wagonjwa 538 walikutwa na historia ya unyongovu na 419 kuwa na jaribio la kujiua. Na 136 walikuwa na historia ya vyote viwili.

kubadilishwa athari ya uwiano (HR) kwa ajili ya hatari kwa CVD kifo 2.38 kwa ajili ya wagonjwa walio na unyogovu (95% ya muda kujiamini [CI], 0.93-6.08) na 3.21 kwa ajili ya wale walio na majaribio ya kujiua zamani (95% CI, 1.36-7.56)

Kuna mjadala mkubwa kuhusu madhara ya unyogovu na ugonjwa wa moyo na mishipa katika vifo vya wanawake kama ikilinganishwa na wanaume. Nadhani ushahidi kutoka kwa utafiti huu ni imara lakini masomo ya baadaye ni wazi kuwa ni muhimu.

Mmoja wa watafiti wengine Dr Scherrer alisema “kwa madaktari, anadhani matokeo ya jumla yanazidi kuongeza wasiwasi ni wakati gani hutambua unyongovu, ambapo ni kawaida kwa watu wenye umri mdogo, kuna uwezekano wa haja ya kuweka mkazo mkubwa katika kufuatilia afya yao ya moyo. Na kwamba sio kitu ambacho madaktari wengi  hufanya mara kwa mara kwa wagonjwa wenye umri mdogo sana.

Na hii huacha swali kubwa la kujiuliza:

Je inawezekana kuzuia magonjwa ya moyo yahusishwayo na unyongovu, kwa kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa mambo ya hatari yanayoweza kupelekea magonjwa ya moyo kwa kundi la vijana?

Imesomwa mara 7444 Imehaririwa Alhamisi, 29 Novemba 2018 08:59
Dr.Mayala

Dr.Henry A Mayala ni daktari bingwa Wa Tiba ya moyo katika taasisi ya Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI), ambaye kwasasa anasomea shahada ya uzamivu (PhD) ya Tiba ya Moyo katika Chuo Kikuu cha Tongji  nchini China.

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

Makala shabihana