Image

Kwa kawaida, meno ya mtoto ya utotoni (meno ya awali) huanza kutoka kuanzia miaka 6. Kwa baadhi ya watoto, huweza kuchelewa kuanza kutoka meno ya utotoni hadi wanapoanza mwaka wA 7.

Meno ya kwanza yanayoanza kutoka ni yale mawili ya chini ya kati (lower central incisors) na hufuatiwa na yale ya juu ya kati (upper central incisors) (. Baada ya hapo, hufuatiwa na meno ya kutafunia ya kwanza na ya pili.

Kwa kawaida, meno ya ya awali hukaa bila kutoka mpaka pale meno ya kudumu yanapotaka kuanza kuchomoza, hivyo hulisukuma jino la utoto na kusababisha kutoka. Endapo mtoto atatoka meno mapema au jino litatoka kwa sababu ya ajali au kuoza, basi jino la kudumu litaziba pengo hilo baada ya muda kufika. Hii inaweza kusababisha meno kutokuwa na mpangilio mzuri kwakuwa wakati linachomoza kulikuwa na meno mengine ya utotoni, hivyo unashauri kuwasiliana na daktari wa kinywa na meno kwa ushauri zaidi.

Pale mtoto anapoanza kutoka meno, tafadhali zingatia kanuni bora za Afya ya kinywa na meno kama ;

  • Kuhakikisha anasubua meno angalau mara mbili kwa siku. Mkazanie kwa sababu umakini unahitajika.
  • Msaidie mtoto kusugua meno kila siku
  • Hakikisha anakula chakula bora na kupunguza matumizi ya vyakula vitamu
  • Weka miadi na daktari wa kinywa nameno

Kwa mazingatio haya, utaweza kuhakikisha afya bora ya kinywa na meno ya mtoto wako. Pia, unaweza kusoma makala zaidi juu ya Afya ya kinywa na meno wakati wa makuzi ya mtoto

Afya bora ya kinywa na meno kwa mtoto ni muhimu sana na ina uhususiano wa moja kwa moja na afya yake kwa ujumla. Humuepusha mtoto kupata maumivu, uwezekano wa uambukizo, kumfanya aweze kutafuna vizuri ili kupata virutubisho muhimu kwa ajili ya kujenga kinga dhidi ya magonjwa, na kusaidia ukuaji. Afya nzuri ya kinywa na meno pia itamfanya mtoto aweze kuhudhuria masomo ipasavyo na hivyo kupata matokeo mazuri.

Umuhimu wa meno ya utoto

Wazazi /walezi wengi hujiuliza kwanini wahangaike kutunza meno ya utoto ambayo yanatarajiwa kung’oka na kuota ya ukubwa. Meno ya utoto ni muhimu kutokana na sababu zifuatazo:
Humsadia mtoto kutafuna na hivyo kumwezesha kupata virutubisho muhimu
Hutunza nafasi kwa ajili ya meno ya ukubwa
Hali ya afya ya meno ya utoto huathiri hali ya afya ya meno ya ukubwani
Husadia uumbaji wa maneno (kuongea)

Kama mzazi / mlezi unatakiwa kuwa mstari wa mbele kutunza meno ya mtoto wako kwani, watoto hupenda kujifunza kutokana na mfano wa wazazi.

Zifuatazo ni dondoo muhimu kwa wazazi/walezi kwa ajili ya kutunza afya bora ya mtoto:

Umri wa kuzaliwa mpaka miezi 6

  • Mnyonyeshe mtoto maziwa ya mama pekee hadi umri wa miezi sita.
  • Maziwa ya mama ni muhimu sana kwa ukuaji na kinga dhidi ya magonjwa.

Umri wa miezi 7 hadi miezi 18

  • Usimlaze mtoto akiwa na chuchu ya maziwa au chuchu ya mama mdomoni ili kuzuia ugonjwa wa kuoza kwa meno (rampant caries)
  • Mpatie mtoto maji badala ya juisi akiwa na kiu.
  • Iwapo utampa mtoto juisi ya boksi unashauriwa kuongeza kiwango cha maji sawa na kile cha juisi ili kupunguza kiasi cha sukari kilichomo ndani ya juisi.
  • Ukitengeneza juisi nyumbani kwa ajili ya mtoto, jiepushe kuiongezea sukari.
  • Jino la kwanza litakapoota, anza kusafisha kinywa cha mtoto kutumia kitambaa laini kilicholoweshwa kwenye maji safi au mswaki laini bila dawa.
  • Panga miadi ya kwanza ya kumwona daktari wa meno (first appointment) wakati mwanao hana maumivu au shida yoyote ili kujenga mahusiano mazuri kati ya mtoto na daktari

Umri wa miezi 18 hadi miaka 6

  • Dhibiti ulaji wa vyakula vyenye sukari na zingatia ulaji wa vyakula vinavyojenga afya ya mtoto kama matunda, mboga mboga, karanga, maziwa na samaki.
  • Safisha meno ya mtoto kutumia maji safi na mswaki laini na dawa ya meno (zingatia kiwango cha dawa: kiasi cha mbegu ya kunde) asubuhi na jioni kila siku.
  • Mtoto asukutue mdomoni ili kupunguza kiwango cha dawa itakayobaki.
  • Chunguza mara kwa mara meno ya mtoto ili kugundua dalili za mwanzo za ugonjwa wa kuoza kwa meno (rangi kuwa nyeupe au kahawia zaidi katika eneo husika baada ya kukausha) na pia matatizo mengine kama uvimbe, vijipu au kutoka damu kwenye fizi.
  • Mpeleke mtoto kwa daktari wa meno angalau mara moja kwa mwaka na mara unapogundua tatizo lolote kinywani mwake.

Umri wa miaka 6 hadi 12

  • Msimamie mtoto kusafisha kinywa na meno mara mbili kwa siku.
  • Mtoto ateme dawa itakayobaki ila asisukutue na maji baada ya kupiga mswaki.
  • Mjengee mtoto tabia ya kusukutua na maji kila baada ya kula vyakula vyenye sukari kama keki, chokoleti au juisi.
  • Chunguza mara kwa mara meno ya mtoto ili kugundua dalili za mwanzo za ugonjwa wa kuoza kwa meno na matatizo mengine kinywani.
  • Mpeleke mtoto kwa daktari wa meno angalau mara moja kwa mwaka na mara unapogundua tatizo lolote kinywani mwake.

Umri wa miaka 12 na zaidi

  • Mtoto anaweza kuanza kusafisha kinywa na meno bila ya usimamizi.
  • Dhibiti ulaji wa vyakula vyenye sukari na zingatia ulaji wa vyakula vinavyojenga afya ya mtoto kama matunda, mboga mboga, karanga, maziwa na samaki.
  • Mpeleke mtoto kwa daktari wa meno angalau mara moja kwa mwaka na mara unapogundua tatizo lolote kinywani mwake.

CREDIT: Muhimbili University of Health and Allied Sciences (MUHAS)

Watoto ambao hula chakula cha usiku pamoja na familia yao wanakuwa na afya njema kiakili na kimwili na wana uwezekano mdogo wa kupenda kunywa soda na vyakula hatarishi kwa afya (fast food)

Watafiti kutoka nchini Canada wanasema, watoto ambao mara kwa mara hula chakula pamoja na familia zao wanakuwa na afya njema ya kiakili na kimwili ukilinganisha na watoto ambao hawapati nafasi ya kula chakula pamoja na familia zao.

Watafiti hao wamegundua ya kwamba watoto hao wanapofikisha umri wa miaka 10 wanakuwa na afya njema kiakili, wachangamfu na uwezekano mdogo sana wakunywa vinywaji vyenye sukari kama soda ikiwa watakula chakula mara kwa mara pamoja na wazazi, ndugu au walezi wao.

Utafiti huu ulifanyika kwa muda wa miaka 10, na ulihusisha kuwafuatilia watoto tokea wakiwa wachanga mpaka walipotimiza umri wa miaka 10.

Watafiti hao wanasema,matokeo yao yanathibitisha  ile dhana ya kwamba,kula chakula kwa pamoja kama familia ni muhimu sana kwa binadamu na huleta manufaa mbalimbali kwa sababu  hujumuisha vipengele  vyote muhimu sana vya  mfumo  wetu maisha pamoja na afya za wazazi wetu.

Uwepo wa wazazi wakati wa kula chakula huwapatia nafasi muhimu sana watoto ya kujifunza kujumuika na wengine, kujadiliana kuhusu mambo mbalimbali ya kijamii na kutoa duku duku zao za kila siku na ni fursa adhimu ya kujifunza mijumuiko ya kifamilia kwenye mazingira wanayoyafahamu na salama kiakili’’ alisema Professor Linda Pagani, mtaalamu wa wa elimu ya kiakili kutoka Chuo Kikuu cha Montreal, Canada.

Ni muhimu kwa mzazi/ mlezi kufahamu aina ya chakula kimfaacho mtoto wake hususani yule aliye katika umri wa miezi tisa na nusu mpaka miaka sita. Aina hizi za vyakula na jinsi ya uandaaji wake hutofautiana sana na zile anazokula mtoto mkubwa au mtu mzima. Leo, mtaalamu wetu wa mapishi, Chef Issa anatuletelea ratiba ya chakula cha mtoto wa umri huo.

Kwa nini watoto wachanga wanalia? 

Ni kawaida kwa watoto kulia. Hata watoto wanaozaliwa na afya njema kabisa wanaweza kulia kwa jumla ya wastani wa kati ya saa moja mpaka matatu kwa siku. Kwa vile watoto hawawezi kujifanyia chochote wao wenyewe zaidi ya kutegemea wazazi, walezi ama watu wengine wanaowazunguka katika kuwapatia chakula, joto, na faraja, kilio ni njia ya mtoto ya kuwasilisha moja ya mahitaji hayo. 

Kama mzazi mpya, wakati mwingine inakuwa vigumu kutambua mtoto wako anahitaji nini anapolia. Mzazi anaweza kuwa na maswali kadhaa kichwani mwake, je, mtoto ana njaa, anasikia baridi, ana kiu, anaumwa ama amechoka? Katika siku za mwanzo, hali ya namna hii inawawia vigumu wazazi wengi, wasijue nini la kufanya. Hata hivyo, kwa kadiri siku zinavyopita mzazi mpya ataweza kutambua kuwa kilio cha mtoto wake kinamaanisha anahitaji nini kutokana na mfumo wake wa kulia. 

Kadiri watoto wanavyokua npyo ambavyo hujifunza hatua mbalimbali za kuwasiliana na wazazi ama walezi wao. Wanakuwa na namna nzuri ya kuwasiliana kwa mfano kwa macho, na kutoa sauti, na hata kutabasamu ambavyo vyote kwa pamoja hupunguza haja ya kulia.

 

Sababu zinazofanya watoto kulia 

Tuangalie sababu kadhaa zinazosababisha mtoto kulia na nini anachotakiwa mzazi ama mlezi kufanya pindi mtoto anapolia. 

1. Hitaji la chakula 

Njaa ni mmoja ya sababu kubwa inayowafanya watoto wengi kulia. Uwezekano wa mtoto kulia unaendana sana na umri wa mtoto. Kadiri jinsi mtoto alivyo mdogo zaidi npyo uwezekano wa kulia sana pindi anapohisi njaa unavyokuwa mkubwa, isipokuwa katika siku mbili za mwanzo baada ya kuzaliwa ambapo watoto hula kwa kiasi kidogo sana. Kwa kawaida katika siku mbili za mwanzo tangu mtoto kuzaliwa, maziwa ya kujilimbikizia mapema sana yaani ‘colostrum’ huwa ni kidogo sana kwa mama walio wengi na huanza kuongezeka kuanzia siku ya tatu baada ya kujifungua.

Pia tumbo la mtoto katika kipindi hiki huwa bado dogo sana na hivyo uwezo wake wa kuhifadhi maziwa anayonyonya huwa bado mdogo hali ambayo humfanya mtoto kujisikia njaa. Hivyo kama mtoto wako analia, uwezekano mkubwa ni kuwa ana njaa na hivyo mzazi unashauriwa kumnyonyesha. Inawezekana mtoto asiache kulia mara moja, lakini mama unashauriwa kuendelea kumnyonyesha taratibu na mtoto anaweza kuacha kulia kwa kadiri anavyoburudika na chakula na kuanza kushiba. Iwapo mama unadhani mtoto wako ameshiba lakini bado anaendelea kulia, inawezekana kuna sababu nyingine zaidi.