Image

Magonjwa ya kinywa na meno husababisha harufu mbaya mdomoni

Takribani asilimia 85 ya watu wenye harufu mbaya kinywani huwa na magonjwa ya kinywa na meno,Ikiwa harufu mbaya kinywani inasababishwa na magonjwa kinywani, dawa za kusafisha kinywa (mouthwash) haziwezi kuondoa tatizo zaidi ya kulifunika kwa muda tu.

Hakuna sababu ya kuona haya kumwambia daktari wa meno kuhusu harufu mbaya kinywani inayokusumbua, kwa vile kumwambia na kujadili tatizo lako ni njia ya kuelekea kwenye tiba ya uhakika. Matumizi ya nyuzi-safishi (dental floss) kila siku, kusafisha meno na ulimi kwa mswaki walau mara mbili kwa siku yaweza kuondoa harufu mbaya kinywani kwa kiasi kikubwa.

Unaweza kusoma  Mambo 10 ambayo daktari wako wa meno angependa ufahamu

 

Imesomwa mara 5538 Imehaririwa Jumanne, 07 Agosti 2018 16:48
Dr. Augustine Rukoma

Dr Dr. Augustine Rukoma ni daktari na mtaalamu wa meno, anapenda kutumia muda wake wa ziada kuandika makala na kubadilishana mawazo juu ya afya ya kinywa na Meno.

rukomadentalanswers.blogspot.com | Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.